Nyimbo za Diamond ni chanzo kikubwa cha mmomonyoko wa maadili

Mtu mwenyewe Diamond! Mtoto wa mtaani japo alikuwa na wazazi! Kalelewa mitaa ya kariakoo na kukulia tandale! Kwenye fikra zake mambo yote ya hovyo yasiyokuwa na staha kwake anaona ni fasheni na kwenda na wakati huku akitafuta kitu wanaita "kick". Sasa kaanzisha kituo cha TV "wasafi TV" ndo anasambaza upotovu kwa vijana! Fuatilia mahojiano kwenye wasafi TV wanaongelea mambo ya ngono! Tatizo watu wenye uwezo wa kutenda mema hawajitokezi na kutoa mwanya kwa waovu kuvuma!
Uko sahihi kabisa.

Hata kama ana ukwasi lkn ukweli lazima aambiwe, kama yeye tayari ameharibika asituharibie kizazi chetu kwa kutunga Miziki ya ovyo iliyo jaa maneno ya ngono
 
Unayo ongea ni kweli, sema sio yeye tuu wapo wasanii wengi wanaimba matusi, wataje wote, ukimtaja diamond tuu watasema unaona wivu
Siwezi kumuinea wivu hata kidogo, aliye Pewa kapewa, mimi hapa nalia na maadili ya watoto wa kitanzania kuharibiwa na miziki ya daimondi inayo hamasisha na kuchochea ngono.

Hili halipaswi kunyamaziwa na mtanzania yeyote mwwnye kujali maadili ya watoto na vijana wa taifa letu.

Daimondi na jopo lake waache kuharibu maadili ya jamii badala yake watunge nyimbo zenye kujenga maadili na zenye kuelimisha jamii.
 
Asa shekele
Mwendo wa kandanda
Ndani ya nangwanda
Sa nisongeze
Leta msambwanda
Nikazie ngangangaaa

(Chiii!) Kananivuta ghetto
Nkapinge bunduki (high bunduki)
Ile naogopa central
Michezo ya Amber Rutty (Amber Rutty)

Eeh nyege nyege
Kwetu mwanza nyegezi
Hmmm nyege nyege
Nishushe mwanza Nyegezi
Ushenzi mtupu!!

halafu tunachekelea kabisa jinsi anavyo haribu jamii yetu!!! hii ni hatari kubwa sana, yatupasa sote kama watanzania tukemee nyimbo za ovyo kama hizo.
 
Kupitia watu wengine na haswa watoto wadogo.
Lawama mnawatupia wasanii ila wazazi ndiyo chanzo cha momonyoko wa maadili.
Angalia malezi ya familia ya sasa hivi yalivyo, nimefanya uchunguzi ila nimegundua tatizo ni wazazi.
1. Mtoto / watoto wengi hawawezi kusalimia. Mtoto utakuta ana miaka 3 lkn hawezi kukusalimia na wazazi wake wapo wanachekacheka. Utasikia, msalimie fulani wazazi wanajichekesha, zamani ni viboko kwa kwenda mbele
2. Mtoto anatumwa kitu anasema amechoka na mzazi anasema sikununulii pipi. Mtoto anaenda. Zamani ukitumwa ukigoma ni viboko na kila huli
3. Watoto wanasimuliana wanavyofanya mapenzi wazazi wao. Wazazi wanafanya ngono watoto wao wanawaona. Zamani huwezi kuhisi kama wazazi wanashiriki
4. Wazazi wa sasa wanaangalia video au kusikiliza nyimbo za 18+ na watoto wao. Mtoto anauwezo wa kununua TV au radio? Kama mzazi lazima ujue ni video au nyimbo gani za kusikiliza na watoto wenu
5. Wazazi wa sasa, mtoto ni wa kwako. Leo mtoto anaweza kukutukana, sasa mchape uone wazazi wake wanavyokuja juu. Ni ugomvi ila zamani mtoto ni wa wote. Ukizingua jamii inakuchapa na ukifika nyumbani unachapwa.
 
Ushenzi mtupu!!

halafu tunachekelea kabisa jinsi anavyo haribu jamii yetu!!! hii ni hatari kubwa sana, yatupasa sote kama watanzania tukemee nyimbo za ovyo kama hizo.
Mtoto hana radio wala hana tv. Amesikia wapi kama wazazi ndiyo wanasikiliza?
Chanzo ni wazazi
 
Akiwa kama mwanamuziki maarufu na anayekubalika zaidi, nyimbo zake nyingi anahamasisha mambo yasiyofaa kwenye maadili, nyimbo zake nyingi zinabomoa zaidi jamii kuliko kujenga jamii.

Ombi kwake na kwa viongozi wake, sisi kama wananchi tunafahamu anafanya biashara ya muziki lakini tunamtaka ajikite kuelimisha na kujenga zaidi jamii kuliko kuporomoa.

Narudia tena kusema nyimbo zake zinaporomoa maadili zaidi kuliko kujenga, yeye na timu yake wanachojali ni kutengeneza pesa tu hawajali kama wanabomoa maadili.
Na Basata wala hawahangaki naye, wanahangaika na wasanii wadogo tu!!!
 
Lawama mnawatupia wasanii ila wazazi ndiyo chanzo cha momonyoko wa maadili.
Angalia malezi ya familia ya sasa hivi yalivyo, nimefanya uchunguzi ila nimegundua tatizo ni wazazi.
1. Mtoto / watoto wengi hawawezi kusalimia. Mtoto utakuta ana miaka 3 lkn hawezi kukusalimia na wazazi wake wapo wanachekacheka. Utasikia, msalimie fulani wazazi wanajichekesha, zamani ni viboko kwa kwenda mbele
2. Mtoto anatumwa kitu anasema amechoka na mzazi anasema sikununulii pipi. Mtoto anaenda. Zamani ukitumwa ukigoma ni viboko na kila huli
3. Watoto wanasimuliana wanavyofanya mapenzi wazazi wao. Wazazi wanafanya ngono watoto wao wanawaona. Zamani huwezi kuhisi kama wazazi wanashiriki
4. Wazazi wa sasa wanaangalia video au kusikiliza nyimbo za 18+ na watoto wao. Mtoto anauwezo wa kununua TV au radio? Kama mzazi lazima ujue ni video au nyimbo gani za kusikiliza na watoto wenu
5. Wazazi wa sasa, mtoto ni wa kwako. Leo mtoto anaweza kukutukana, sasa mchape uone wazazi wake wanavyokuja juu. Ni ugomvi ila zamani mtoto ni wa wote. Ukizingua jamii inakuchapa na ukifika nyumbani unachapwa.
Nakubaliana nawe kwa kiasi lakini pia miziki ya daimondi yenye maudhui ya kingono inawahatibu sana vijana.
Kumbuka daimondi ni msanii mkubwa anaye kubalika kwenye jamii, hivyo chochote anacho kifanya kinafuatwa na kuigwa na jamii haswa vijana na watoto wadogo.
 
Katika maisha yako lazima ujue
1. Kuna nyimbo za watu wazima
2. Nyimbo za watoto
Shida ya wazazi wa siku wanaangalia ilimradi tu hawajui. Kuna nyimbo za watoto zipo na za dini wawekee watotot.
Mimi siwezi kumlaumu Diamond ila nawalaumu wazazi. Kumbuka tupo kwenye ulimwengu utandawazi kila kitu kipo wazi ni wewe na chaguo lako. Huyu mtoto hana hela ya kununua radio au tv amesikia wapi?
Kuna nyimbo za wazungu wanacheza nusu uchi, mbona huweki ukaangalia na watoto?
Wazazi wanasikiliza nyimbo na watoto zao za 18+ halafu wanasingizia wasanii.
Muwe mnaona aibu ndugu
 
Daimondi lazima abebe lawama kwa asilimia 60%.
nyimbo zake zenye maudhui ya kingono zinaharibu sana kizazi hiki.

40% lawama kwa wazazi wasio jielewa.

Msanii ni kio cha jamii. Jamii inajifunza kwa asilimia kubwa kutoka kwa wasanii, hivyo wasanii lazima wafahamu wanalo jukumu la kuijenga na kuielimisha familia.
 
Mziki saivi umekuwa hovyo kote tu.

Nilisikia Kuna tribute ya kutoa heshima Kwa miaka 50 ya hip hop kwenye tuzo za MTV.. Bhas ni kasema niangalie ni uozo mtupu.

Wasanii wa kike wanashindana kufanya performance wakiwa utupu.. Hovyo sana
 
Ni familia yako na wala siyo yake. Ni jukumu lako na siyo lake Endelea kumlaumu Diamond huku yeye anatengeneza hela. Hizo nyimbo za matusi ndizo zinapendwa sana, kwanini asiimbe?

Shida ya waafrika hamuishi kwa machaguo, kila kitu mnataka msikilize, ukisikia kuna mtu karekodi video ya ngono, mnataka muangalie.

Kuna nyimbo za dini zipo nyingi sana ila mnamsikiliza diamond.
Tafuta video ya Anaconda ya Nick Minaj uangalie.

Kama unaona Diamond anajukumu la kukulelea mwanao sawa. Mlaumu
Unataka diamond awe anaimba unachopenda wewe.
 
Mziki saivi umekuwa hovyo kote tu.

Nilisikia Kuna tribute ya kutoa heshima Kwa miaka 50 ya hip hop kwenye tuzo za MTV.. Bhas ni kasema niangalie ni uozo mtupu.

Wasanii wa kike wanashindana kufanya performance wakiwa utupu.. Hovyo sana
Dunia ya sasa tunaishi kwa machaguo.
Kuna series ukiangalia nyingi kuna ngono, usagaji, ufiraji n.k lakini ndizo zinazopendwa. Kama game of throne
Kaangalie nyimbo ya Anaconda ya Nick Minaj
Nyimbo ili uuze lazima usifie ngono na pombe ndiyo uuze bila hivyo watu hawasikilizi.
Diamond ndiyo msaani mwenye hela kuliko waimba nyimbo za dini halafu tunamlaumu.
Leo unaenda kwa rafiki yako katoto kanakuangalia tu, ukichukua remote kanasema acha tv yetu. Ukikachapa mzazi wake anakuja juu.
 
Sio nyimbo za diamond tu nyimbo nyingi za bongo fleva ni za hovyo
Zinaamasisha ulevi, umalaya, ushoga na zinatweza utu wa mwanamke
 
Dunia ya sasa tunaishi kwa machaguo.
Kuna series ukiangalia nyingi kuna ngono, usagaji, ufiraji n.k lakini ndizo zinazopendwa. Kama game of throne
Kaangalie nyimbo ya Anaconda ya Nick Minaj
Nyimbo ili uuze lazima usifie ngono na pombe ndiyo uuze bila hivyo watu hawasikilizi.
Diamond ndiyo msaani mwenye hela kuliko waimba nyimbo za dini halafu tunamlaumu.
Leo unaenda kwa rafiki yako katoto kanakuangalia tu, ukichukua remote kanasema acha tv yetu. Ukikachapa mzazi wake anakuja juu.

Huyo na nyimbo zake hizo kutwa mwalikwa kwa mama na hafla za chama na serekale.

Na wanazipenda kweli kweli hizo nyimbo zake. Hapo napo wawaonaje wanaomwalika ndugu?
 
Akiwa kama mwanamuziki maarufu na anayekubalika zaidi, nyimbo zake nyingi anahamasisha mambo yasiyofaa kwenye maadili, nyimbo zake nyingi zinabomoa zaidi jamii kuliko kujenga jamii.

Ombi kwake na kwa viongozi wake, sisi kama wananchi tunafahamu anafanya biashara ya muziki lakini tunamtaka ajikite kuelimisha na kujenga zaidi jamii kuliko kuporomoa.

Narudia tena kusema nyimbo zake zinaporomoa maadili zaidi kuliko kujenga, yeye na timu yake wanachojali ni kutengeneza pesa tu hawajali kama wanabomoa maadili.
Huyu Jamaa wakiendelea kumhendekeza ataleta impact mbaya sana kwenye jamii.

Kwani lazima aimbe mambo yasiyofaa?
 
Hili jambo haliwezi kufanikiwa kwakuwa kuna watu wakubwa wanaonufaika nalo, ila kiukweli waathirika wakubwa wasiojua damage ya hiyo miziki ni watoto wa shule wanaoona hiyo miziki runingani
Yaani zinahubiri Starehe tu na Kula bata mwisho wa siku watoto wa kiume na wa kike wamekuwa wote wanajiuza ili kuishi maisha yanayosemwa na wasanii hao.

Hatuoni wakihimiza elimu, kilimo, umoja na uchapa kazi.

Wao kila kukicha ".....Itemee mate iteleze kama nyoka pangoni....."

"".......Inamaa nikuwekee Tango Mtaroni......"

Hii ni promotion ya Ushoga.
 
Back
Top Bottom