Kukosekana kwa Malezi ya Pamoja kwenye Jamii (Collective Parenting) Chanzo kikubwa cha Matatizo ya Mmomonyoko wa Maadili

mocoservices

Member
Feb 24, 2023
45
144
Wanajukwaa nawasalimu, Salamu zangu hizi nazitoa kutoka upande wa Nyanda za Juu Kusini.

Siku za hivi karibuni, nimejikuta nimekuwa na hasira sana, nachukizwa na mambo mengi yanayotokea kwenye jamii yetu ya sasa (nipewe pole jamani, hata kama unawaza kuwa hayanihusu).

Nianze kwa kusema hivi, ukiona jambo linazungumziwa sana katika jamii yako maana yake ni kwamba jambo hilo lipo na linafanyika na linafanywa na wengi katika jamii husika.

Ukipita kwenye mitandao ya kijamii hivi sasa, ukipitia pages 50 kuna pages 3 au 4 zinaongelea "ushoga" aidha kwa kuuponda au kwa kuuona ni sawa. Kwangu tafsiri yake ni kwamba tumefika pabaya na ndiyo maana tunadiliki kujadili kuwa ni sawa au si sawa, maana huwezi jadili kitu ambacho hakipo.

Tunakubaliana kwamba kila kitu kina mwanzo, mwanzo huo unaweza kufahamika au usifahamike na watu wakaona matokeo tu ya mambo husika. Chanzo cha mambo mengi yanayotusumbua kwenye jamii yetu ni kuacha ustaarabu wetu wa asili na kuvamia ustaarabu wa watu wengine wa asili tofauti na sisi.

Sio siri kwamba watu wa asili tofauti na sisi nia yao tangia miaka ile haijawahi kuwa njema kwetu hata kidogo, wanaleta vitu ili kupenyeza agenda zao. Huenda wao hawana kosa, kosa ni letu sisi ambayo tumeshindwa kuchambua cha kuchukua na kuachana nacho.

Malezi ya sisi (waafrika) kwa kiasi kikubwa yalikuwa malezi ya kushirikiana, mtoto alikuwa halelewi na familia tu ya baba na mama bali alikuwa analelewa na jamii nzima. Mimi si mtu mzima saana, nimezaliwa miaka ya 90, kuna tukio moja nalikumbuka, natamani malezi yale yajirudie katika maisha ya sasa.

Ilikuwa hivi; siku moja mimi na mwenzangu tulitoraka shule, kilikuwa kipindi cha maembe kule Kyela basi tukawa tumepanda juu ya mti tukila maembe porini. Tukakutwa na mbaba (hatukuwahi kumfahamu) ila alitushika na akatucharaza bakora za kutosha na akatupeleka nyumbani nako tukachezea bakora za kutosha. Huo ulikuwa mwaka 2002 tu, tulikuwa darasa la 4.

Kwa siku hizi, nawaza nani anawezafanya hivyo? Nani anaweza thubutu kuadhibu mwana asiyewake? Tumepoteza "Society Collective Parenting" ukimuona mtoto wa jirani anafanya kitu cha ajabu hujihangaishi, maana kichwani kwako unasema hayakuhusu, maana mtoto si wako.

Siku hizi ukiadhibu mtoto wa mtu ni kesi kubwa...nani anapenda kupata kesi ya shambulio na kujeruhi? Siku hizi mtoto wa mwenzio si wako. Jamii imepotoka.

Katika kukua kwangu kote, sijawahi msikia mama yangu au baba yangu akisema "usile kwa watu"...tafsiri yake kwangu ni kwamba wana jamii walikuwa wanashirikiana mwa ukaribu kwenye vitu vinavyohusu jamii.

Kauli hiyo hiyo ni maarufu siku hizi, mama au baba atamwambia mwanae "usile kwa watu" kumwambia hivyo mwanao, kwa tafsiri ya juujuu unamwambia siwaamini watu hao (majirani).

Jamii imegeuka, jirani ni adui, jirani haaminiki na ndo maana siku hizi kila nyumba inayojengwa inaukuta mrefu, huo ni ubinfsi na ni utumwa kwa nini ujiwekee uzio kama "ng'ombe". Huo si ustaarabu wetu sisi.

Ndugu zangu, vita hii ni kali na tushashindwa mapema, maana wenye agenda zao walishapigana vita mezani muda mrefu sana, sasa wametuachia sisi tubishane na kukosoana sisi kwa sisi. Hawa watu, walitumia akili katika mambo mawili.

1. Kuua malezi ya pamoja ya watoto ya kiafrica

2. Kuua ushirikiano na mshikamano wa viongozi wa familia (baba na mama) kwa kuleta agenda ya "haki sawa".

Hoja ya kwanza nimeizungumzia, hapa kidogo nitagusia hoja ya pili.

Najiuliza ni nani alisema "haki sawa?" Haki sawa ni kugawa watu, haki sawa ni kugombanisha watu, panye usawa hakuna utulivu hata siku moja, hata Mungu anajua na ndiyo maana shetani alipoyaka kuleta ujuaji akamtupilia mbali. Ukiweka usawa maanake unaweka ugomvi.

Sasa iko hivi, wewe unataka "equal access to education" kati ya mtoto wa kiume na wa kike, sawa. Sasa je nani atamtawala mwenzie? Sisi waafrica, miaka hiyo elimu tuliigawa kulingana na "roles" za mtu katika jamii.

Mwanaume kazi yake ilkuwa ni kuwa kuongoza, kulinda familia na jamii, kuleta usitawi wa uchumi na chakula katika familia, basi ilipaswa lazima mwanaume ufundishwe vitu vinavyofanya asimame imara kwenye nafasi yake. Come on! Wewe mwanamke hutunzi familia unataka kazi upate hela, hela za nini wakati huna jukumu hilo?

Kila kitu katika ustaarabu wetu kilikuwa na mpangilio mzuri, mtu mwingine atasema sasa itakuwaje mwanaume akifa? Kwetu unyakyusani ilikuwa kuna urithishaji, haikuwa lazima ila kama hutaki kurithiwa uondoke, yes uondoke.

Huenda unashangaa kwamba ni ustaarabu gani huu wa hovyo . Maana yake ilikuwa ni hivi, moja kutunza mali kwenye ukoo husika, maana ukifiwa na mume na usirithiwe, ukileta mwanaume mwingine pale ni lazima uondoke. Maana ya pili ilikuwa ni kuweka uzao pamoja na kudumisha ukoo.

Kuna vitu haviko sawa kwenye ustaarabu tuliochukua kwa watu wengine, wewe mwanaume kumbuka; ikitokea leo wanaume wote wakabaki nyumbani wasitafute hela, jua sio wanaume wote watakula ila wanaume wakienda kutafuta hela jua kuwa wanawake wote watakula. Ni kanuni ndogo tu hiyo.

Turudi sasa, nimesoma sehemu kwamba serikali imefuta "boarding" kwa watoto nursery hadi darasa la tano. Napongeza hatua hii. Lakini tuende mbali zaidi kwa kuelimisha jamii nzima maana mtoto kutokaa boarding si njia ya kutatua tatizo la malezi moja kwa moja.

Familia ziangalie na kuwekea mkazo vitu ambavyo watoto wanaona kwenye luninga, nyimbo wanazosikiliza, na vyakula wanavyokula. Tujaribu kurudi kwenye malezi ya kushirikiana, malezi ya kushirikiana kijamii yatatatua changamoto nyingi sana.

Familia kuwa na roles za kueleweka, haiingii akilini baba yuko busy na mama yuko busy, kwangu si sawa. Kama ni sawa basi kuna kitu hakipo na ndiyo maana sasa mtoto analelewa na msaidizi wa kazi au mtoto ana shinda matunzo ya siku (day care).

Kwa kuhitimisha, niseme hayo ni maoni yangu binafsi, ukijibu jibu hoja, hii ni jamii yetu lazima tushirikiane. Pili, kama ambavyo suala la Haki Sawa lilivyoanza ndivyo ambavyo suala la ushoga lilivyoanza, tuiangalie jamii yetu na kuilinda kwa nguvu zote.
 
Hili suala la ushoga mnalikuza sana hii itafanya watu waanze kulifuatiria na kuanza kujaribu,

Pia tambua muingiliano wa jamii ambao hauwezi zuilika
 
Upo sahih mkuu ila changamot wa aya matatizo uanzia sehem tunayoishi yaan ni majumban kwetu sisi wenyew mzazi ana habar na mtot je mtot unategemea atakuwa vp lazma atabadirika na yeye

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mzazi anapaswa kutimiza jukumu lake nyumbani, kiukweli kulea mtoto peke yako bila jamii ni kazi sana. Mtoto hawi na mzazi muda wote ila ni ukweli usiopingika kuwa mtoto huwa na jamii muda wote.
 
Hili suala la ushoga mnalikuza sana hii itafanya watu waanze kulifuatiria na kuanza kujaribu,

Pia tambua muingiliano wa jamii ambao hauwezi zuilika
Nimekiri kwenya andiko langu kuwa, ukiona jambo linajadiliwa maana yake lipo. Sasa, tufanye nini kupunguza kasi hii? Sisi ndo jamii.
 
Back
Top Bottom