Nyimbo kwa Waliopita JKT

Manumbu

JF-Expert Member
Oct 28, 2009
1,746
1,282
Ghafla nimezikumbuka nyimbo za jeshini, enzi zileee

"safari ya mamaa naiombea baraka, safari ya mamaa naiombea baraka,
nilimwambia mama, kwa heri nakwenda, kulijenga taifa langu la leo,
hiyooo mamaaa
kwa heri mamaaa nakwenda zangu yoyoyooo kwa heri mamaa nakwenda zangu mbali sana,
nakwenda Mlale
kwa heri mamaa nakwenda zangu mbali sana
nakwendaa Ruvu
kwa heri mamaa nakwenda zangu mbali sana"

Wadau mnakumbuka nyimbo zipi za majeshi?
 
He he pole sana uliukosa uhondo weye!.

Uhundo gani alioukosa? Mi binafsi naona JKT ulikuwa ujinga mtupu. Sikujifunza chochote zaidi ya kujuana na marafiki wapya. That's it. Nilipoteza mwaka wangu bure pasipo na sababu za msingi.
JKT was just a crap!! I'm glad hakuna hou ujinga tena
 
kidume wakati nyimbo hizo zinaimbwa ulikuwa unanyamaza kwa sababu ni girlish?
Sema hivi yeye kipindi hicho alikuwa akisema nasikia kukojoa anaambiwa kakojoe pale,!!hadharani anamwaga kojo!!!!hivyo hawezikuona nini maanayake na faida zake!!
 
Jua lile literemke mama!
Haiya iya iya iya mama!

Hapa mnaambiwa muimbe mpaka jua lishuke chini.
 
Uhundo gani alioukosa? Mi binafsi naona JKT ulikuwa ujinga mtupu. Sikujifunza chochote zaidi ya kujuana na marafiki wapya. That's it. Nilipoteza mwaka wangu bure pasipo na sababu za msingi.
JKT was just a crap!! I'm glad hakuna hou ujinga tena

selule!
 
Nani anakumbuka Operation Tumaini; Afande Londo Na Kayuya Ruvu!

Kinate kinanguruma; Kinate kinanguruma; Oyee oyee Kinate kinanguruma.
 
Hilo jeshi mambo yake, vitendo vyake sawasawa!

Kula yao sawasawa
Vaa yao sawasawa

Hilo jeshi mambo yake, vitendo vyake sawasawa!
Temba yao sawasawa
Imba yao sawasawa
 
Ghafla nimezikumbuka nyimbo za jeshini, enzi zileee

"safari ya mamaa naiombea baraka, safari ya mamaa naiombea baraka,
nilimwambia mama, kwa heri nakwenda, kulijenga taifa langu la leo,
hiyooo mamaaa
kwa heri mamaaa nakwenda zangu yoyoyooo kwa heri mamaa nakwenda zangu mbali sana,
nakwenda Mlale
kwa heri mamaa nakwenda zangu mbali sana
nakwendaa Ruvu
kwa heri mamaa nakwenda zangu mbali sana"

Wadau mnakumbuka nyimbo zipi za majeshi?

Poa kinona hapo ndipo watanzania tulikuwa tunajenga umoja. Mchakamchaka
 
Nani anakumbuka Operation Tumaini; Afande Londo Na Kayuya Ruvu!

Kinate kinanguruma; Kinate kinanguruma; Oyee oyee Kinate kinanguruma.

Operation Tumaini 1972 JK akiwa ndani A Coy ya Afande Mirudi au siyo? .
 
Uhundo gani alioukosa? Mi binafsi naona JKT ulikuwa ujinga mtupu. Sikujifunza chochote zaidi ya kujuana na marafiki wapya. That's it. Nilipoteza mwaka wangu bure pasipo na sababu za msingi.
JKT was just a crap!! I'm glad hakuna hou ujinga tena

Mbona wengi waliopita jkt wanasema ilikuwa very interesting na walijfunza ukakamavu na uzalendo? we mwenzetu ulipitia jeshi la nchi gani?
Mmh! ngoja nisikulaumu sana maana naskia kuna wengine walifanywa kitu mbaya walipokuwa jkt na huenda nawe ulikuwa ni mmojawapo kwani waswahili wanasema, AISIFUYE MVUA,IMEMNYEA!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu, lilikuwa kosa lako. Kujifunza kuna pande mbili, anayefundisha na anayefundishwa. Inaelekea wakati waliokuwa wanafundisha wanafanya kazi yao, wewe uligoma kujifunza na mwaka ukakatyika hivihiiv bila kujifunza kitu kwa sababu akili yako iligoma kujifunza. Inashangaza sana kusema kuwa JKT ulikuwa ujinga mtupu. kwa sababu pamoja na mapungufu yake, lakini tuliokuwa tumeweka akili zetu pale tulitoka na kitu
 
Mbona wengi waliopita jkt wanasema ilikuwa very interesting na walijfunza ukakamavu na uzalendo? we mwenzetu ulipitia jeshi la nchi gani?
Mmh! ngoja nisikulaumu sana maana naskia kuna wengine walifanywa kitu mbaya walipokuwa jkt na huenda nawe ulikuwa ni mmojawapo kwani waswahili wanasema, AISIFUYE MVUA,IMEMNYEA!!!!!!!!!!!!

Ni kweli jeshini kulikuwepo na suluba za hapa na pale, sometimes maonevu kwa baadhi ya watu. Lakini kwa vijana wagumu na wavumilivu walichukulia hizo kama changamoto tu ambazo mtu ulitakiwa uzishinde.

Yalikuwepo mengi ya kujifunza. Tulifundishwa ujanja wa porini (field crafts) kama vile camouflage and concealment, platoon drill, kutumia na kusafisha bunduki, kulenga shabaha (range), ukakamavu kwa ujumla na mengineyo. Ni jeshini ndipo niliweza kuona mhindi na mwarabu nao wemeshika majembe wanashughulikia miraba yao. Tulijengwa umoja na tulikuwa tunaonana kama ndugu. Hivyo si kweli kuwa jeshi halikuwa na faida kabisa. Faida zilikuwepo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom