Nyimbo kwa Waliopita JKT

Nde nde nde mama ndeee nde mama
nilikwenda Dodoma walitaka kuniua
niliacha begi langu na butii main gate
yooo Amini amekiona cha motoo!

Kulikuwa na faida nyingi sana jeshini na sio kweli kuwa tulipoteza mwaka mzima pale.
 
Mi ninaukumbuka sana wimbo huu: "Silaha yangu naipenda mama wee ukiichezea nitakupiga singeeee!"
Na mwingine:
Nimpeleleze nani habari za kuruta, nimpeleleze nani habari za majeshi; afande ndiyee wa kumpeleleza, afande ndiyee wa kumpelelezaaaa!
 
Da! mmenikumbusha mbali kweli kweli....

Hao wanaoona kuwa JKT ilikuwa ujinga hakika ni watu wa ajabu kweli, kulikuwa mafunzo sana pale na ile tu peke yake ya kukaa pamoja kwa shida ilifundisha uvumilivu na umoja sana. Wengi walijifunza ukakamavu na kuthubutu. Iliwaweka watu wote sawa, mtoto wa mkuu wa mkoa, mtoto wa waziri, mtoto wa mkulima wote tulitafuta kuni pamoja, miraba tulikata pamoja na tuliamka saa 11 kasoro pamoja!

Hivi hakuna utaratibu pakafanyika mradi wa kuimba hizi nyimbo katika ala za muziki na kufanya album kweli? Mbona nyimbo za watoto zimefanyiwa huu mpango? Ninaamini yoyote atakaefanya hivi atapata soko sana, ni wengi tunazihitaji hizi nyimbo
 
Mselele mselelee kajua kagenda mselele !
JKT limetufunza mengi mbali na umoja, kukubali kuwa binadamu wote ni sawa nk, lakini nilipenda somo la mbinu za medani-nilizozitumia kupata ugali kabla ya kuruta wengine.
 
Uhundo gani alioukosa? Mi binafsi naona JKT ulikuwa ujinga mtupu. Sikujifunza chochote zaidi ya kujuana na marafiki wapya. That's it. Nilipoteza mwaka wangu bure pasipo na sababu za msingi.
JKT was just a crap!! I'm glad hakuna hou ujinga tena

Inawezekana ni selule,wagonjwa wa aina mbili tu ndio walio julikana na ni selule na C ya Matron,JKT ilikuwa na maana sana ni sera ya kujitegemea na ukakamavu mafisadi walivyoanza kuingia katika siasa wakauwa JKT,unasoma bure STD 1 mpaka form six kisha unaenda kuzalisha kidogo,ukakamavu,na jinsi ya kukabili maisha(kujitegemea)
 
Ukiona hivyo huyo alikuwa dogi mkubwa. Mi binafsi nilienjoy sana maana raha yake akili ilikuwa haina cha kufikiri unategemea kuamrishwa tu ingawa mchakamchaka wa asubuhi ndo ulikuwa unaniacha hoi. Maana ilikuwa mnahesabu namba kabla ya kukimbia then nabana mahali nasubiri wakirudi kumbe kule walikofika walihesabu namba nyingine. Kimbembe kinakuja wakati wa kwenda kunywa chai mnaitwa kwa namba...so ikitajwa mnajikuta mko wawili....ikifika hapo utarijua riafande mzee.
 
...Ukimkumbuka baba na mama naona uchungu..we mama hahaha ha aha wee baba naona uchungu
One day afande akasikia alisema Weeee achaaaaaa hiyooooooo.!!!
 
Embakasy!!
Masange jkt na majaruba!! Na disco la usiku sitawasahau hawa afande Sijali,Afande Msakatti,Afande Msabaha!!Ila afande Sijali alikuwa mwisho!!
 
Mkuu, lilikuwa kosa lako. Kujifunza kuna pande mbili, anayefundisha na anayefundishwa. Inaelekea wakati waliokuwa wanafundisha wanafanya kazi yao, wewe uligoma kujifunza na mwaka ukakatyika hivihiiv bila kujifunza kitu kwa sababu akili yako iligoma kujifunza. Inashangaza sana kusema kuwa JKT ulikuwa ujinga mtupu. kwa sababu pamoja na mapungufu yake, lakini tuliokuwa tumeweka akili zetu pale tulitoka na kitu

inaelekea jamaa alijiaandaa kutoelewa ndo maana alitoka mweupe au ni Bongofleva generation kizaz cha masoseji.
 
Da! mmenikumbusha mbali kweli kweli....

Hao wanaoona kuwa JKT ilikuwa ujinga hakika ni watu wa ajabu kweli, kulikuwa mafunzo sana pale na ile tu peke yake ya kukaa pamoja kwa shida ilifundisha uvumilivu na umoja sana. Wengi walijifunza ukakamavu na kuthubutu. Iliwaweka watu wote sawa, mtoto wa mkuu wa mkoa, mtoto wa waziri, mtoto wa mkulima wote tulitafuta kuni pamoja, miraba tulikata pamoja na tuliamka saa 11 kasoro pamoja!

Hivi hakuna utaratibu pakafanyika mradi wa kuimba hizi nyimbo katika ala za muziki na kufanya album kweli? Mbona nyimbo za watoto zimefanyiwa huu mpango? Ninaamini yoyote atakaefanya hivi atapata soko sana, ni wengi tunazihitaji hizi nyimbo

Jiulize ni kwanini JKT ilifutwa kama sio mzigo kwa serikali ambao ulikuwa hauna maana?
Mafunzo gani hayo ya kulimishana miraba ya mahindi kwa jembe la mkono?
Mafunzo gani hayo ya kwenda range na kujifunza silaha za mwaka 47?
 
Nasikitika sana sikukuta jeshi, labda sasa hivi ningekuwa kwenye ulimwengu tofauti na huu. Unajua wengi wataona ni mambo ya kitoto ila aliyeondoa jeshi ndiye aliyeleta hawa vibaka. Vinginevyo wote weangekuwa wako fiti mambo ya kuwa mario kupenda bwerere hakuna. Sasa hivi unakkuta mtu liko slake ni kubwa zima.

What I can say watu waliopita jeshini wote wengi ninaowajua wako responsible, serious fitcally, hata thinking capacity yao ni tofauti. Mtapinga lakini ukweli ndiyo huo.

Kwa kheri!
 
Binafsi nilikuwa kuruta kwa mwaka mmoja. Kuna faida za JKT na mapungufu yake. Faida: nilikutana na marafiki wengi ambao tumeendela kuwa karibu hadi leo, uvumilivu, ukakamavu wa mwili na fikra, nk

Hasara zake: dada zetu wengi waliambukizwa HIV kwa kuwa walilazimishwa kuwa na mahusiano na makamanda pale kikosini na wengine walibakwa. Mwaka mmoja ulipotea huko JKT, then tukawa tunasubiri another year kwenda UDSM. Ukiangalia hiyo miaka 2 iliopotea na hayo tuliyojifunza huko JKT naona ilikuwa ni kutupotezea muda tu. Na mengineyo mengi
 
Jeshi lilikuwa tamu bwana. Tulijifunza mambo mengi sana, uvumilivu,ujasiri, ukakamavu, kutumia silaha (kuweza kuilinda nchi wakati wa vita), umoja na mbinu mbalimbali za kukabiliana na magumu mbalimbali....
Nilikuwa operation miaka 20 ya Azimio la Arusha (1986-7) Ruvu JKT
A-Coy
Nilikuwa najulikana kama General Marwa
(Nawakumbuka maafande: Sungura, Nyundo, Maganga, Nyoka, Kidongo chekundu....)
Servicemen/women: Kichemuli, Madawili, Alitabu Kinyongo, Ajibu, Getrude Mrema, Husna Omar, Mujigwa....
Nyimbo:
Malela, malela namtafuta....

Sijambo la ajabu kumwona afande anaruka ruka kama kuruta.....

Zaina, zaina......

Kanadiani ee, ya A-coy ee, yapanda mlima ee, na Marwa yupo ee.....

Binafsi nilikuwa kuruta kwa mwaka mmoja. Kuna faida za JKT na mapungufu yake. Faida: nilikutana na marafiki wengi ambao tumeendela kuwa karibu hadi leo, uvumilivu, ukakamavu wa mwili na fikra, nk

Hasara zake: dada zetu wengi waliambukizwa HIV kwa kuwa walilazimishwa kuwa na mahusiano na makamanda pale kikosini na wengine walibakwa. Na mengineyo mengi
JKT kwa mujibu wa sheria Ukuruta ilikuwa ni miezi sita tu, miezi mingie sita ulikuwa unabandikwa cheo kingine!.
 
Mbona wengi waliopita jkt wanasema ilikuwa very interesting na walijfunza ukakamavu na uzalendo? we mwenzetu ulipitia jeshi la nchi gani?
Mmh! ngoja nisikulaumu sana maana naskia kuna wengine walifanywa kitu mbaya walipokuwa jkt na huenda nawe ulikuwa ni mmojawapo kwani waswahili wanasema, AISIFUYE MVUA,IMEMNYEA!!!!!!!!!!!!

Ilikuwa bomba, maselule ndo wanaiponda. Kuhusu wimbo, nakumbuka ''iyena iyena, iyena iyeena. Siku hizi inaimbwa hata kwenye harusi (tarumbeta)
 
Nasikitika sana sikukuta jeshi, labda sasa hivi ningekuwa kwenye ulimwengu tofauti na huu. Unajua wengi wataona ni mambo ya kitoto ila aliyeondoa jeshi ndiye aliyeleta hawa vibaka. Vinginevyo wote weangekuwa wako fiti mambo ya kuwa mario kupenda bwerere hakuna. Sasa hivi unakkuta mtu liko slake ni kubwa zima.

What I can say watu waliopita jeshini wote wengi ninaowajua wako responsible, serious fitcally, hata thinking capacity yao ni tofauti. Mtapinga lakini ukweli ndiyo huo.

Kwa kheri!

Kwani kila kilichofutwa kilikuwa mzigo kwa serikali? Vipi Azimio lz Arusha?
 
JKT kwa mujibu wa sheria Ukuruta ilikuwa ni miezi sita tu, miezi mingie sita ulikuwa unabandikwa cheo kingine!.

ahsante kwa masahihisho, manake nimeshasahau hata hizo ranks uchwara tulivyokuwa tukiitwa. yeah nilikuwa recruit for 6 months then nikawa sijui service man....... don't even wanna remember. Sikuwa selule ila basi hiyo kero ya kupoteza 2 years kabla ya kujoin Udsm ndio hadi leo inanikera sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom