Asnam... Labda mie sijaelewa hizo lawama za mwanaume kukosa mishipa ya aibu imetoka wapi nikitumia kigezo cha hii story umetoa.
- Dada anatoka na mume wa mtu, kumuonyesha hiyo nyumba yeye inamuhusu nini hadi asimulie shosti zake kuwa huyo mwanaume anajenga hadi kwenda kuonyesha mashosti wake hiyo nyumba (Asnam huyo dada hana mshipa wa aibu kukusanya wenzie kuwaonyesha hiyo nyumba?)
- Wanawake tuwe makini saana sometimes... Unaringishia nyumba ambayo anaishi mtu mwingine na wala hata huishi wala hutarajii kuishi hapo? Heshima kitu cha bure, na ulimbukeni ndicho huwaponza wengi in such circumstances.
- Analipiwa nyumba, anahudumiwa kila kitu; hayo mengine kwa kweli hayamuhusu hadi pale mwanaume mwenyewe aamue (kwa sababu zake mwenyewe iwe/zisiwe za msingi). Kitendo cha kumdanganya na kwenda kumuonyesha nyumba mtaa mwingine ni wazi kuwa yawezekana bi dada ndiye alikuwa aking'ang'ania kujua anako kaa huyu mwanaume OR kisha someka kuwa ni limbukeni na hushoboka kwa material things kuweza kufanyiwa lolote lile mwili wake.
Huyo mwanaume ni typical mwanaume wa mjini ambae atafanya lolote lile kumpata mwanamke anaye mtaka. Hiyo si kwa huyu baba tu; ni wengi saana.
BTW kuna kitu watu wanasahau... Haijalishi kaka/dada ni wa mjini vipi, kuna kiboko yake tu! Nina msemo "Kila mbabe ana mbabe wake".