Nyie wanaume nyie sio kabisa

Nyie wanaume nyie sio kabisa

hapo kwenye bold mmmh,,,,waambie na ww watakusikia wanadai hakuna penzi la mkopo siku hizi.

wanaume mzuri ni yule anaemjali mpenz wake kwa kidogo alichonacho,mwanamke pia asitake kuweka njaa/shida zake mbele as if mwanaume aliyempata ndio mwokozi wake..kwani kabla ya kukutana na mimi ulikuwa unaishije? I dont think swala la mausiano yamekuwa siku hizi ni trade..mtu hata haujaspend nae tayari ashakupiga mzinga wa laki au hamsa..je siku mkispend si atakuletea invoice ya kufa mtu...mwanaume anaejitambua ni yule anayejua kwamba mwenzangu akisuka style hii ananimaliza kabisa,akipulizia marashi haya nazimia kabisaa,akivaa hivi nakuwa hoi,then inakuwa ni jukumu lake kumwezesha mwenzi wake kupendeza anavyotaka...ogopa sana mwanaume ambaye ukiwa nae sehemu mmechill yeye ni story za mizigo yake bandarini,mara mwezi ujao napandishwa cheo,mara hammer yangu ni ni old fashioned,kutwa kubrag tuu.
 
ni fikra zako tu ambazo haziwezi kubadilishwa na mtu yeyote kwa sababu zimeshakuwa mgando,hunijui,sikujui ya nini kung'ang'ania mambo,,,,,,,mi kama mgonjwa kifikra we ni marehemu kifikra.

Let the world check me here Home and decide for themselves between the two of us which one is manifestly sick; let them judge from the words we speak you curse, i bless the verdict is theirs
 
Mla vya wenzake naye vyake huliwa,kwanini ukomae na waume za wenzio na kuwakosesha amani.hiyo ndio tiba ya watu kama hao
 
Kaz kwel kwel..
Hiyo inafaa kabsaaa

Kuna ma chatu mjini yanasubir waume walotoka kimaisha wapunzike pamoja
 
Habari zenu wana jamvi,natumaini mko salama salimini kwa kudra za muumba wetu.
kuna baadhi ya wanaume mishipa ya aibu ilishakatika kabisa ikabakia kwenye dushelele zao tu,kuna bi shostito mmoja kaingizwa mkenge na mwanaume mchana kweupeeee wakati alikuwa akijitapa yeye ni mtoto wa mjini hakuna mwanaume anayeweza kumtapeli loh hebu tupate habari kamili.

Binti kapata mume wa mtu,kama mjuavyo wakishikwa wanashikamana hela ya kodi,mafuta,saloon,shopping n.k si haba kutolewa,kasheshe ikaja kama ifuatavyo ktk marafiki zake shostito kuna mmoja alikuwa anamfahamu yule baba kwa sababu walikuwa wakiishi mtaa mmoja, kumbe yule baba kapanga hana nyumba wala nini maisha yake ya kawaida sana lakini kamdanganya yule bi dada anaishi kwake kampeleka kumwonyesha nyumba ya watu mtaa mwingine kabisa.

bi dada bila hiyana akamuamini ukizingatia anapiga simu za kuzuga kuulizia mizigo yake bandarini n.k kubwa kuliko kamwambia bi shost anamtafutia nyumba ya kumpangishia ili asipate tabu hehehehehehe hapo ndo kasheshe ilipoanzia,dada kapelekwa kuonyeshwa nyumba,alivyo mbea kawachukua mashost wake kuwapeleka kupaona na kuwalingishia,yule best anayemjua yule bwana akatulia zake aone mwisho wa ngoma utakavyokuwa.

La haula ikaandikwa cheque sijui iliokotwa wapi, eti ndo ikipokelewa benki wampatie pesa aje kumlipia bi dada kodi yote,mmmmh katafuta na mkataba wa kughushi kaupeleka stationary wautype kumbe yule dada wa stationary na yeye anamjua akatype akaprint akampa huku nyuma akabaki anacheka eti mtoto wa kike kaingizwa mjini na mara kibao huwa anapeleka mikataba ya uongo pale ili mwanamke aliye nae ajue kweli kapata bwana kumbe hamna kitu,huwezi amini hadi muda huu ninavyoandika mwanaume kaishia mitini yule bestito kafyata mkia kwa mabest zake kawa mdogo kama piriton wenzake mbavu hawana,matambo yote yameisha dah nyie wanaume baadhi yenu hamfai kabisa

Kawaida tu Asnam, jamaa ametumia maneno ambayo mdada anapenda kuyasikia.
 
Asnam... Labda mie sijaelewa hizo lawama za mwanaume kukosa mishipa ya aibu imetoka wapi nikitumia kigezo cha hii story umetoa.


  1. Dada anatoka na mume wa mtu, kumuonyesha hiyo nyumba yeye inamuhusu nini hadi asimulie shosti zake kuwa huyo mwanaume anajenga hadi kwenda kuonyesha mashosti wake hiyo nyumba (Asnam huyo dada hana mshipa wa aibu kukusanya wenzie kuwaonyesha hiyo nyumba?)
  2. Wanawake tuwe makini saana sometimes... Unaringishia nyumba ambayo anaishi mtu mwingine na wala hata huishi wala hutarajii kuishi hapo? Heshima kitu cha bure, na ulimbukeni ndicho huwaponza wengi in such circumstances.
  3. Analipiwa nyumba, anahudumiwa kila kitu; hayo mengine kwa kweli hayamuhusu hadi pale mwanaume mwenyewe aamue (kwa sababu zake mwenyewe iwe/zisiwe za msingi). Kitendo cha kumdanganya na kwenda kumuonyesha nyumba mtaa mwingine ni wazi kuwa yawezekana bi dada ndiye alikuwa aking'ang'ania kujua anako kaa huyu mwanaume OR kisha someka kuwa ni limbukeni na hushoboka kwa material things kuweza kufanyiwa lolote lile mwili wake.

Huyo mwanaume ni typical mwanaume wa mjini ambae atafanya lolote lile kumpata mwanamke anaye mtaka. Hiyo si kwa huyu baba tu; ni wengi saana.

BTW kuna kitu watu wanasahau... Haijalishi kaka/dada ni wa mjini vipi, kuna kiboko yake tu! Nina msemo "Kila mbabe ana mbabe wake".

Ni kweli kabisa kosa lipo kwa huyo dada, kukosa kujitambua.

Kwenye green hapo ninaweza nikam spare huyo dada. Nilikuwa na rafiki yangu ambaye ni tapeli wa wadada sijapata kuona. Yeye alikuwa hasubiri mwanamke aulize, yeye mwenyewe anaanzisha ishu na anamshawishi mdada wakatembelee site zake fake au biashara zake fake(anakuwa tayari keshapanga mchoro), tena wakati mwingine mdada hataki yeye atafanya bidii mpaka mdada anaenda kuona, na mara nyingine anamchukua tu mdada amsindikize matembezi ya kawaida halafu anampitisha kwenye hizo shughuli zake fake.

AshaDii wewe acha tu kuna matapeli wanaijua kazi yao usipime. Wana mbinu nyingi na ni wabunifu kila kukicha, yaani kama hizo mbinu zingekuwa zina apply kwenye kutafuta pesa basi wangekuwa mabilionea.
 
nikajua chamaana kumbe adith za kwe sani,,mbaaaav
 
Back
Top Bottom