Nyie wanaume nyie sio kabisa

Nyie wanaume nyie sio kabisa

Asnam

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2012
Posts
4,256
Reaction score
2,949
Habari zenu wana jamvi,natumaini mko salama salimini kwa kudra za muumba wetu.
kuna baadhi ya wanaume mishipa ya aibu ilishakatika kabisa ikabakia kwenye dushelele zao tu,kuna bi shostito mmoja kaingizwa mkenge na mwanaume mchana kweupeeee wakati alikuwa akijitapa yeye ni mtoto wa mjini hakuna mwanaume anayeweza kumtapeli loh hebu tupate habari kamili.

Binti kapata mume wa mtu,kama mjuavyo wakishikwa wanashikamana hela ya kodi,mafuta,saloon,shopping n.k si haba kutolewa,kasheshe ikaja kama ifuatavyo ktk marafiki zake shostito kuna mmoja alikuwa anamfahamu yule baba kwa sababu walikuwa wakiishi mtaa mmoja, kumbe yule baba kapanga hana nyumba wala nini maisha yake ya kawaida sana lakini kamdanganya yule bi dada anaishi kwake kampeleka kumwonyesha nyumba ya watu mtaa mwingine kabisa.

bi dada bila hiyana akamuamini ukizingatia anapiga simu za kuzuga kuulizia mizigo yake bandarini n.k kubwa kuliko kamwambia bi shost anamtafutia nyumba ya kumpangishia ili asipate tabu hehehehehehe hapo ndo kasheshe ilipoanzia,dada kapelekwa kuonyeshwa nyumba,alivyo mbea kawachukua mashost wake kuwapeleka kupaona na kuwalingishia,yule best anayemjua yule bwana akatulia zake aone mwisho wa ngoma utakavyokuwa.

La haula ikaandikwa cheque sijui iliokotwa wapi, eti ndo ikipokelewa benki wampatie pesa aje kumlipia bi dada kodi yote,mmmmh katafuta na mkataba wa kughushi kaupeleka stationary wautype kumbe yule dada wa stationary na yeye anamjua akatype akaprint akampa huku nyuma akabaki anacheka eti mtoto wa kike kaingizwa mjini na mara kibao huwa anapeleka mikataba ya uongo pale ili mwanamke aliye nae ajue kweli kapata bwana kumbe hamna kitu,huwezi amini hadi muda huu ninavyoandika mwanaume kaishia mitini yule bestito kafyata mkia kwa mabest zake kawa mdogo kama piriton wenzake mbavu hawana,matambo yote yameisha dah nyie wanaume baadhi yenu hamfai kabisa
 
:A S-key:mwambie aje kuchukua ufunguo, haahahahaha...........maisha ya siku hizi bana mnajuana wenyewe tu
 
Hahaha, huyo jamaa anastahili kufanya mishe zake kwenye Institutions kama CIA vile, ana akili sana, huyo binti naye hajisomi, we unadhani mambo ya mjini ni rahisi rahisi tu, unapewa nyumba hata hujahangaikia? chizi
 
Mjini shule alidhani hapa shamba nguvu? Tatizo wadada ulimbukeni baadhi yenu umewajaa ndio maana mnaishiwa kuchezewa tu,,,sasa hivi ule ujanja wa wanaume kuwapeleka driving na kuwapa gari kwa maneno huku kadi ya gari anayo jamaa mmeanza kushtuka.
 
Asnam... Labda mie sijaelewa hizo lawama za mwanaume kukosa mishipa ya aibu imetoka wapi nikitumia kigezo cha hii story umetoa.

  1. Dada anatoka na mume wa mtu, kumuonyesha hiyo nyumba yeye inamuhusu nini hadi asimulie shosti zake kuwa huyo mwanaume anajenga hadi kwenda kuonyesha mashosti wake hiyo nyumba (Asnam huyo dada hana mshipa wa aibu kukusanya wenzie kuwaonyesha hiyo nyumba?)
  2. Wanawake tuwe makini saana sometimes... Unaringishia nyumba ambayo anaishi mtu mwingine na wala hata huishi wala hutarajii kuishi hapo? Heshima kitu cha bure, na ulimbukeni ndicho huwaponza wengi in such circumstances.
  3. Analipiwa nyumba, anahudumiwa kila kitu; hayo mengine kwa kweli hayamuhusu hadi pale mwanaume mwenyewe aamue (kwa sababu zake mwenyewe iwe/zisiwe za msingi). Kitendo cha kumdanganya na kwenda kumuonyesha nyumba mtaa mwingine ni wazi kuwa yawezekana bi dada ndiye alikuwa aking'ang'ania kujua anako kaa huyu mwanaume OR kisha someka kuwa ni limbukeni na hushoboka kwa material things kuweza kufanyiwa lolote lile mwili wake.

Huyo mwanaume ni typical mwanaume wa mjini ambae atafanya lolote lile kumpata mwanamke anaye mtaka. Hiyo si kwa huyu baba tu; ni wengi saana.

BTW kuna kitu watu wanasahau... Haijalishi kaka/dada ni wa mjini vipi, kuna kiboko yake tu! Nina msemo "Kila mbabe ana mbabe wake".
 
Mwanamke ukitanguliza pesa kwenye mapenzi, kwa wanaume wasio na uwezo na wanahitaji huduma ya huyo dada kuna uwezekano mkubwa wa kukumbwa na hali kama hii! Nampa pole na aaache hizo tabia!
 
tatizo mabinti wakileo wanashobokea waume zawatu sana, yaani wakiwa nao wanaona sifa kweli nakutambishiana alijua ndio keshampata bonge la bwana eee? Ishakula kwake huyo
 
Habari zenu wana jamvi,natumaini mko salama salimini kwa kudra za muumba wetu.
kuna baadhi ya wanaume mishipa ya aibu ilishakatika kabisa ikabakia kwenye dushelele zao tu,kuna bi shostito mmoja kaingizwa mkenge na mwanaume mchana kweupeeee wakati alikuwa akijitapa yeye ni mtoto wa mjini hakuna mwanaume anayeweza kumtapeli loh hebu tupate habari kamili.

Binti kapata mume wa mtu,kama mjuavyo wakishikwa wanashikamana hela ya kodi,mafuta,saloon,shopping n.k si haba kutolewa,kasheshe ikaja kama ifuatavyo ktk marafiki zake shostito kuna mmoja alikuwa anamfahamu yule baba kwa sababu walikuwa wakiishi mtaa mmoja, kumbe yule baba kapanga hana nyumba wala nini maisha yake ya kawaida sana lakini kamdanganya yule bi dada anaishi kwake kampeleka kumwonyesha nyumba ya watu mtaa mwingine kabisa.

bi dada bila hiyana akamuamini ukizingatia anapiga simu za kuzuga kuulizia mizigo yake bandarini n.k kubwa kuliko kamwambia bi shost anamtafutia nyumba ya kumpangishia ili asipate tabu hehehehehehe hapo ndo kasheshe ilipoanzia,dada kapelekwa kuonyeshwa nyumba,alivyo mbea kawachukua mashost wake kuwapeleka kupaona na kuwalingishia,yule best anayemjua yule bwana akatulia zake aone mwisho wa ngoma utakavyokuwa.

La haula ikaandikwa cheque sijui iliokotwa wapi, eti ndo ikipokelewa benki wampatie pesa aje kumlipia bi dada kodi yote,mmmmh katafuta na mkataba wa kughushi kaupeleka stationary wautype kumbe yule dada wa stationary na yeye anamjua akatype akaprint akampa huku nyuma akabaki anacheka eti mtoto wa kike kaingizwa mjini na mara kibao huwa anapeleka mikataba ya uongo pale ili mwanamke aliye nae ajue kweli kapata bwana kumbe hamna kitu,huwezi amini hadi muda huu ninavyoandika mwanaume kaishia mitini yule bestito kafyata mkia kwa mabest zake kawa mdogo kama piriton wenzake mbavu hawana,matambo yote yameisha dah nyie wanaume baadhi yenu hamfai kabisa
We Asnam, mi nilidhani sisi wanaume wote ndo tumemtapeli huyo bidada, kumbe katapeliwa na mmoja tu...??? TENA KWA TAMAA ZAKE ZA KUTAKA MAISHA MAZURI... TUONDOKEE HAPA, SIYE WENGINE HATUPO HIVYO.

Asnam... Labda mie sijaelewa hizo lawama za mwanaume kukosa mishipa ya aibu imetoka wapi nikitumia kigezo cha hii story umetoa.

  1. Dada anatoka na mume wa mtu, kumuonyesha hiyo nyumba yeye inamuhusu nini hadi asimulie shosti zake kuwa huyo mwanaume anajenga hadi kwenda kuonyesha mashosti wake hiyo nyumba (Asnam huyo dada hana mshipa wa aibu kukusanya wenzie kuwaonyesha hiyo nyumba?)
  2. Wanawake tuwe makini saana sometimes... Unaringishia nyumba ambayo anaishi mtu mwingine na wala hata huishi wala hutarajii kuishi hapo? Heshima kitu cha bure, na ulimbukeni ndicho huwaponza wengi in such circumstances.
  3. Analipiwa nyumba, anahudumiwa kila kitu; hayo mengine kwa kweli hayamuhusu hadi pale mwanaume mwenyewe aamue (kwa sababu zake mwenyewe iwe/zisiwe za msingi). Kitendo cha kumdanganya na kwenda kumuonyesha nyumba mtaa mwingine ni wazi kuwa yawezekana bi dada ndiye alikuwa aking'ang'ania kujua anako kaa huyu mwanaume OR kisha someka kuwa ni limbukeni na hushoboka kwa material things kuweza kufanyiwa lolote lile mwili wake.

Huyo mwanaume ni typical mwanaume wa mjini ambae atafanya lolote lile kumpata mwanamke anaye mtaka. Hiyo si kwa huyu baba tu; ni wengi saana.

BTW kuna kitu watu wanasahau... Haijalishi kaka/dada ni wa mjini vipi, kuna kiboko yake tu! Nina msemo "Kila mbabe ana mbabe wake".
a.k.a NDEGE MJANJA HUNASA KWENYE TUNDU BOVU...
 
Back
Top Bottom