Nyie wanaume nyie sio kabisa

Nyie wanaume nyie sio kabisa

Nimeelewa. Asante kwa ufafanuzi Asnam... Kwa misingi hiyo alikuwa na haki ya kuwapeleka rafikize kupaona kupata ushauri.

kwa bahati mbaya amegeuka kituko mbele ya best zake.
 
best kumbe ni wewe,ujue nimeona avatar nikajua ni dume loh kusoma Id ngastuka kidogo....hawa wenzetu wanapenda vya bwelele bila kutoa jasho matokeo yake yanawakuta ya firauni loh
Just thinking loudly, hivi hapo huyo bidada ilibidi atoe jasho kivipi..??
 
Just thinking loudly, hivi hapo huyo bidada ilibidi atoe jasho kivipi..??

apambane kwa njia halali kuvipata hivyo anavyoviota ndotoni mwake,na sio kusubiria kula majasho ya watu
 
asingetegemea hela za mwanaume. Angefanya opposite mambo yasingemwia hivi...
 
ila mwanamke ndiye hamnazo.

Matamshi haya hapa chini yanatosha kabisa kugundua kati ya hao wawili nani ni mjanja...

kuna bi shostito mmoja kaingizwa mkenge na mwanaume mchana kweupeeee wakati alikuwa akijitapa yeye ni mtoto wa mjini hakuna mwanaume anayeweza kumtapeli
 
Habari zenu wana jamvi,natumaini mko salama salimini kwa kudra za muumba wetu.
kuna baadhi ya wanaume mishipa ya aibu ilishakatika kabisa ikabakia kwenye dushelele zao tu,kuna bi shostito mmoja kaingizwa mkenge na mwanaume mchana kweupeeee wakati alikuwa akijitapa yeye ni mtoto wa mjini hakuna mwanaume anayeweza kumtapeli loh hebu tupate habari kamili.

Binti kapata mume wa mtu,kama mjuavyo wakishikwa wanashikamana hela ya kodi,mafuta,saloon,shopping n.k si haba kutolewa,kasheshe ikaja kama ifuatavyo ktk marafiki zake shostito kuna mmoja alikuwa anamfahamu yule baba kwa sababu walikuwa wakiishi mtaa mmoja, kumbe yule baba kapanga hana nyumba wala nini maisha yake ya kawaida sana lakini kamdanganya yule bi dada anaishi kwake kampeleka kumwonyesha nyumba ya watu mtaa mwingine kabisa.

bi dada bila hiyana akamuamini ukizingatia anapiga simu za kuzuga kuulizia mizigo yake bandarini n.k kubwa kuliko kamwambia bi shost anamtafutia nyumba ya kumpangishia ili asipate tabu hehehehehehe hapo ndo kasheshe ilipoanzia,dada kapelekwa kuonyeshwa nyumba,alivyo mbea kawachukua mashost wake kuwapeleka kupaona na kuwalingishia,yule best anayemjua yule bwana akatulia zake aone mwisho wa ngoma utakavyokuwa.

La haula ikaandikwa cheque sijui iliokotwa wapi, eti ndo ikipokelewa benki wampatie pesa aje kumlipia bi dada kodi yote,mmmmh katafuta na mkataba wa kughushi kaupeleka stationary wautype kumbe yule dada wa stationary na yeye anamjua akatype akaprint akampa huku nyuma akabaki anacheka eti mtoto wa kike kaingizwa mjini na mara kibao huwa anapeleka mikataba ya uongo pale ili mwanamke aliye nae ajue kweli kapata bwana kumbe hamna kitu,huwezi amini hadi muda huu ninavyoandika mwanaume kaishia mitini yule bestito kafyata mkia kwa mabest zake kawa mdogo kama piriton wenzake mbavu hawana,matambo yote yameisha dah nyie wanaume baadhi yenu hamfai kabisa
Alithamini vya mwlini ulitegemea apewe vya rohoni? hakuna mwanamke ambaye haingizwi mkenge hapa duniani hata wewe mwenyewe ushaingizwa mara kibaaao; msipobadilika na kutafuta roho ya mtu ikoje kabla hamjajitosa mnapapatikia fahari ya macho mustachi mzuri, tabasam mwanana, kifua kipana, mpunga kwa wingi, mkoko wa maana, nk kwa hayo mkae mkao wa maumivu tuuuuu
 
Hapo ubaya wa huyo mwanaume uko wapi?

1. Kama ni saloon alikuwa akipelekwa.
2. Hela ya mafuta, kodi shopping anapewa kama kawaida.

Huyo msichana mwenyewe tapeli mshobokea vitu kuliko mapenzi ya kweli amekutana na tapeli la mjini mla K za warembo washobokaji kama huyo.

Namuunga mkono huyo baba kwa kuwa anatoa somo zuri sana kwa dada zetu wenye tamaa. Ndiyo maana huwa wanashobokea wazungu wanaishia kufanyishwa ngono ya mtungo au na Mbwa.
 
Sasa celew hii stor imekaaje mala dada katapeliwa wakat mwenyewe uroho wake mala mshkaj kazoe mala umecheka duuu jifunze kuandka script itafanya inoge.
 
dawa ya wanaoishi kwa kutegemea wanaume mujini ndio hiyo. natamani kama hako kaugonjwa ka huyo baba awaambukize wanaume wote, ndio wadada watatia akili kua maisha ya mteremko hayapo. Well done mbaba, nimekukubali, endeleza libeneke ili wapenda kupewa wapate akili ya kutafuta vyao wasitegemee papuchi kuishi mjini....
kadungwa na kodi ya nyumba hakupata, kazi mnayo.
 
nilisema ni ngumu kutenganisha pesa na mapenzi watu wakataka kunitoa roho, wakati kila siku yanajidhihirisha
 
^^
Bora mimi masikini nawaambiaga sina kitu,,mapemaaa!
Aamue mwenyewe.
^^


Mkuu utakula sana mabek3 kama umetahiriwa bure vile,,,hao classic bila kuwadanganya(usizidi tu) utawaangalia hivyohivyo kwa wenzako.

Mwanamke anaamini uongo kuliko ukweli.
 
mbona hapo kwenye bold ni rahisi sana siku hizi kuliko unavyofikiria ndg, mzee akichezewa sharubu siku mbili ya tatu analipia kodi ya mwaka mzima.
Note kwamba kachezewa sharubu tayari, huko kuhangaika huko,
 
Back
Top Bottom