Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

.

Hata ukiangalia ilani za chaguzi za vyama vya CCM na CHADEMA ambavyo ndio vikubwa, havina tofauti za msingi, kilicho bayana ni ushindani wa kukimbilia Ikulu kwenda kuwa watekelezaji bora (kuliko chama kingine) wa matakwa ya IMF, WorldBank na wakubwa wa nchi za OECD bila ya kuyahoji, matakwa ambayo Mwalimu alipingana nayo kwa miaka karibia mitano (1980 – 1985).


Ahsante sana Mchambuzi,
Nilichopenda sana kwenye andiko lako ni kwamba umeweka masuala mengi sana yakimsingi ya taifa letu chini ya mwamvuli wa Baba wa Taifa.
Binafsi suala la Baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere sio suala la kujadili na mtu, wala siwezi kuhoji ubaba wake kwa kadiri ninavyoelewa yeye alishakuwa na yake ya kutenda, katika usimamizi wa jamii kwa nyakati zile na mazingira inalazimu kuhalalisha aina zote za mapungufu aliyopitia. Nadhani mbaya zaidi inakuwa pale tunapokwama kwenye mapungufu yaleyale ya enzi zile, hii inadhihirisha ombwe la kifikra katika kizazi hiki chetu.
Napenda sana kujielekeza kule tunakoelekea hasa kwa kupokea tokea pale alipotuachia Mwalimu na fikra zake na mwanzo wa anguko letu........
Hii imenifanya nimege nukuu hii kwenye maandishi yako.
Huko ndio tunapoelekea.
Tupo katikati ya nyakati hizi mgogoro wa kisiasa katika kujenga mustakabali wa Taifa letu, 2015 ni kipenga..!
Ni lazima turejeshe tafakari hapa juu ya aina za siasa katika vyama vinavyoamua muelekeo wetu, hasa katika kudaka pale alipoishia Baba wa Taifa.
Ni wazi kuwa CCM imeshashindwa!!
Vipi kuhusu CDM??
Ni vipi kinabeba ndoto ile ya Baba wa Taifa??
Uchumi wa mchanganyiko ni siasa za kimalaya/ siasa koko zisizo na sura ya kueleweka katika kusimamia maslahi ya masikini wa vijijini.
Ifike sehemu tuchore mstari uliowazi kwa chama chenye uelekeo wa kushika dora (CDM) juu ya tathmini mpya juu ya Itikadi na Mlengo wa kati haufai katika kulivusha taifa hili na kurudisha uchumi kwa UMMA.
Na hiyo ndio ilikuwa ndoto ya Baba wa Taifa.
 
Topical, hakuna mtu anayekubembeleza aisee, hapo unakosea. Wewe kama hukubali asemayo mtoa mada huo ni muangalio wako na kwa upande wangu sina tatizo na hilo. Tunaishi kwenye zama za fikra huria, kwa hiyo unao uhuru wa kuwafundisha watoto wako kile unachokiona ni sahihi.

Kitu kimoja tukubaliane kama waTanzania, nacho ni kwamba mfarakano utokanao na tofauti za kidini hauna tija kwa taifa!

Sawa kabisa mfarakano wa kidini hauna tija kwa Taifa na Tanzania lakini ..ni haki kwa dini zetu zote kutoka kwa serikalini ndio itakayoondoa hiyo kuliko kupendelea na kugawa hela za tanzania kwa dini moja ..hapo kutakuwa tu na matatizo..lol

Hilo la nyerere sawa sawa mimi siwezi kumuita baba, wala watoto wangu na ukoo wangu niko huru..sijaona la maana alilonifanyia kama familia (zaidi ya kunyang'anya mashamba yetu na kuweka kijiji) wakati tumeng'oa magogo wenyewe tukaishia kufungwa kwa kudai haki)...na kwa taifa langu naona alikuwa anajichekesha chekesha radio akifikiri uchumi unaongozwa na siasa..lol

I beg to differ BIG TIME enjoy
 
Sawa kabisa mfarakano wa kidini hauna tija kwa Taifa na Tanzania lakini ..ni haki kwa dini zetu zote kutoka kwa serikalini ndio itakayoondoa hiyo kuliko kupendelea na kugawa hela za tanzania kwa dini moja ..hapo kutakuwa tu na matatizo..lol

Hilo la nyerere sawa sawa mimi siwezi kumuita baba, wala watoto wangu na ukoo wangu niko huru..sijaona la maana alilonifanyia kama familia (zaidi ya kunyang'anya mashamba yetu na kuweka kijiji) wakati tumeng'oa magogo wenyewe tukaishia kufungwa kwa kudai haki)...na kwa taifa langu naona alikuwa anajichekesha chekesha radio akifikiri uchumi unaongozwa na siasa..lol

I beg to differ BIG TIME enjoy
That's your democratic right as well as mine. Na kama unafikiria unaweza kuwazuia watoto wako kuwa na mawazo huria basi unajidanganya. Unaweza ukawafundisha kutokumuita Nyerere "Baba wa Taifa" lakini hiyo inategemea na wao wenyewe watakavyoamua. Trust me!
 
Hilo la nyerere sawa sawa mimi siwezi kumuita baba, wala watoto wangu na ukoo wangu niko huru..sijaona la maana alilonifanyia kama familia (zaidi ya kunyang'anya mashamba yetu na kuweka kijiji) wakati tumeng'oa magogo wenyewe tukaishia kufungwa kwa kudai haki)...na kwa taifa langu naona alikuwa anajichekesha chekesha radio akifikiri uchumi unaongozwa na siasa..lol

I beg to differ BIG TIME enjoy

Topica acha kujichanganya kuwa eti nyerere hawezi kuwa baba kwa kuwa hujaona la maana alililokufanyia wewe kama mtanzania au Tanzania.

Wewe umesema baba au mama ni kwako ni wale tu wa kbailojia. Kigezo cha na nyerere au Abdul Sykes kufanya au kutofanya chochote cha maana kwako kimeanza saa ngapi ????? au umebadilikaka sa ngapi? Acha kuyumba yumba..........

Umeanza kwa nguvu zote kupinga concept ya mtu kuitwa baba. May be ulipinga sababu kulikuwa kuna Jina la Julius. Ukapewa mfano wapo wengi wanaitwa baba ( mfano A.Sykes) ukabadilika kuwa kwani Nyerere aifanya nini? Ukaanza kumuhusiaha na wizi. Unaona ulivyo mtata.

Ukiwa na principles na kuangalia hoja huwezi kuyumba yumba lakini ukitaka kuponda au kusifia mtu kwa misingi ya jina la abdallah au James utaonekana kituko..........

Sio tu suala la kudiffer na kufurahia kudffer kumsifia au kumponda Julius na wengineo . Lets do it critically with strong and sound argument.
 
That's your democratic right as well as mine. Na kama unafikiria unaweza kuwazuia watoto wako kuwa na mawazo huria basi unajidanganya. Unaweza ukawafundisha kutokumuita Nyerere "Baba wa Taifa" lakini hiyo inategemea na wao wenyewe watakavyoamua. Trust me!
Sawasawa mimi kama mzazi nawajibika kuwafundisha niaminivyo mimi kama alivyonifundisha baba yangu if mtoto ataamua baada na kuona vingine that's him/her, I have no problem as long nimetimiza wajibu wangu kama baba..

Kwani mimi nani alinizuia nobody lakini siwezi kumuita nyerere baba wala ha -qualify kuwa baba kwangu na kwa watoto wangu na ukoo wangu...that will be our teachings..kama tulimpinga tangu zamani kwa sera zake za kijinga na ubaguzi wake wa kidini nini kitabadilisha generation yetu kuamini hivyo..that's our right..
 
Hilo la nyerere sawa sawa mimi siwezi kumuita baba, wala watoto wangu na ukoo wangu niko huru..sijaona la maana alilonifanyia kama familia (zaidi ya kunyang'anya mashamba yetu na kuweka kijiji) wakati tumeng'oa magogo wenyewe tukaishia kufungwa kwa kudai haki)...na kwa taifa langu naona alikuwa anajichekesha chekesha radio akifikiri uchumi unaongozwa na siasa..lol

I beg to differ BIG TIME enjoy

Masikini Topical, you are such an idiot and a baby ! Huo Ubaba wa Taifa is there to stay and as long as wewe ni Mtanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndiye Baba wa Taifa lako upende usipende. Njia iliyopo kwako na ukoo wako pamoja na watoto wako kukwepa kumwita Baba wa Taifa ni kuukana Uraia wa Tanzania na kulowea labda Uarabuni kama alivyofanya Barubaru. Lakini hili la kuapa kutomtambua Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama Baba wa Taifa wakati wewe ni Mtanzania, huo kama si upumbavu ni utoto, uwezo huo huna.
 
Topica acha kujichanganya kuwa eti nyerere hawezi kuwa baba kwa uwa hujaona la maana alilikufanyia kama mtanzania au Tanzania.

Wewe umesema baba au mama ni kwako ni wale tu wa kbailojia. Kigezo cha na nyerere au Abdul Sykes kufanya au kutofanya chochote cha maana kwako kimeanza saa ngapi ????? au umebadilikaka sa ngapi? Acha kuyumba yumba

Umeanza kwa nguvu zote kupinga concet ya mtu kuitwa baba. May be ulipinga sababu kulikuwa kuna Jina la Julius. Ukapewa mfano wapo wengi wanaitwa baba ( mfano A.Sykes) ukabadilikaa kuwa kwani Nyerere aifanya nini . Ukaanzakumuhusiaha na wizi. Unaona uivyo mtata.

Ukiwa na principles na kuangalia hoja huwezi kuyumba yumba lakini ukitaka kuponda au kusifia mtu kwa misingi ya jina la abdallah au James utaonekana kituko.

Sio tu suala la kudffer na kufurahia kudffer kumusifia au kumponda Julius na wengine . Let do it critically with strong and sound argument.

Mkuu kwangu mimi mtu anakuwa baba for biological reason, fine ukaanza kuleta story za utamaduni ukanieleza kuwa kwa utamaduni wa kiafrika mtu anakuwa baba kwa heshima fulani fulani, jirani mwema, etc fair enough??

Sasa mimi nyerere kwangu kwa familia yetu hakuwa jirani mwema, wala hakuwa rais mwema (kiongozi mwema) hizo sifa nitaanza kumpa nitakuwa mnafiki nami siwezi kufanya unafiki huo hana nafasi kwangu, kwa watoto wangu hata kwa ukoo wangu...ok

Sasa nyie mmefaida lecture zake, uchumi wake, elimu yake fair muiteni hata mungu who cares?? lakini mimi namwona binadamu fulani katili, lihuni, mbaguzi, na mnafiki..hawezi kuwa baba bana mbona..period ..
 
Masikini Topical, you are such an idiot and a baby ! Huo Ubaba wa Taifa is there to stay and as long as wewe ni Mtanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndiye Baba wa Taifa lako upende usipende. Njia iliyopo kwako na ukoo wako pamoja na watoto wako kukwepa kumwita Baba wa Taifa ni kuukana Uraia wa Tanzania na kulowea labda Uarabuni kama alivyofanya Barubaru. Lakini hili la kuapa kutomtambua Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama Baba wa Taifa wakati wewe ni Mtanzania, huo kama si upumbavu ni utoto, uwezo huo huna.

Mbona niko Tanzania, nakaa mbezi sijawahi, siwezi na sinta muita baba wa taifa..namuita Rais wa kwanza wa Tanzania

Siyo utoto ni choice ok
 
@mag3

Nyerere hatoi uraia wa Tanzania bana, yeye alikuwa raia kama mimi period
 
Baba wa Taifa wa Zaire (DRC), Patrice Lumumba, ambae alifariki miaka michache sana baada ya kuikomboa Zaire, na ambae alikuwa mshirika mkubwa wa Nyerere, Je amelifanyia nini Taifa la Zaire kitakwimu mpaka aitwe baba wa taifa? Tusisahau kwamba aliuwawa kikatili na mabepari wa nje wakati anajaribu kufanya uchumi wa Zaire uwe wa wote kama Nyerere.

Mkuu Mchambuzi,

Tuweke rekodi sawa, DRC ilipata uhuru wake June 30, 1960 na Mwanamapinduzi Patrice E. Lumumba aliuawa January 17, 1961. Serikali yake nadhani ilidumu kwa miezi miwili na nusu [June 30 - September 14]. Kwa hiyo haikuwa miaka michache sana baada ya Uhuru, bali ilikuwa ni miezi miwili na nusu tu baada ya uhuru.

Dhambi ya baadhi ya wa-Congoman ya kumsaliti Lumumba inaendelea kuwatesa mpaka leo hii. Uroho wa madaraka na ubinafsi ndio ambavyo vinaendelea kututafuna Afrika mpaka leo. Tunataka kuendelea kugawana sehemu ili kila mmoja apate authority.

Mobutu Sese seko ambaye ni mmoja wa wasaliti wa Lumumba, mwaka 1966 alitambua rasmi mchango wa Lumumba wa kudai uhuru na kutaka kujenga DRC moja iliyoungana na siyo kila jimbo lijitawale kivyake. Baada ya hapo alianza kutumia kauli zile zile za Lumumba katika kuhamasisha watu ili aweze kupata support ya wananchi, lakini kwa bahati mbaya hakuweza kupata support ya kutosha na hivyo kuishia kutawala kimabavu na ndio maana wapinzani walikuwa wamesambaa kwenye nchi zote za jirani zinazoizunguka DRC.

Leo hii hapa Tanzania kuna watu wanabeza mchango wa Mwalimu Nyerere katika kudai uhuru na wakati huo huo wakitaka kupata support wanakuwa wa kwanza kutumia nukuu za Mwalimu ili kuhamasisha wa-Tanzania waweze kuwaona kwamba wana nia njema juu ya maisha yao na kumbe ni chui waliojivisha ngozi ya kondoo ili kuwa-fool wananchi.

Hata kwenye swala la ubora wa marais, bado ninampa consideration kubwa sana Mwalimu Nyerere. Marais waliofuata baada ya uongozi wa Nyerere, kama wao ndio wangekuwa ni viongozi wakati huo, nina hakika kwamba wangetuuza hata sisi wenyewe maana sijawahi kuona uongozi ambao umejaa ubinafsi na kujali maslahi yao wenyewe kama wa awamu ya Mkapa na JK. Kila wanachofanya wanaangalia kwanza hapa nita-gain nini, akishashikishwa chake ndipo anaanza kuja kwa nguvu na kufoka mpaka povu linamtoka. Kila siku nikikumbuka jinsi Mkapa alivyokuwa anatokwa na povu kutetea ununuzi wa radar na baadaye inakuja kugundulika kwamba ni "dili", na jinsi alivyowaingia NetGroup Solution kwa kutumia mtutu wa FFU na kumbe ni dili la shemeji yake na madudu mengine kibao.

Kosa la Mwalimu Nyerere ni moja, hakujua kuwa alikuwa amezungukwa mafisadi. Mkapa [Mr. Clean] ambaye tulijua ni chaguo la Mwalimu kumbe alikuwa ni fisadi aliyeficha makucha yake. Hawa akina Lowassa na JK ndo walikuwa vijana wa chama, wasomi waliotoka Mlimani na kwenda kukitumikia chama na walifundwa ipasavyo pale Chuo Kikuu Cha Chama Kivukoni. Alitakiwa kuzinduka mwaka 1992 alipowaambia kwamba upepo wa mageuzi unaokuja hamtasalimika, kubalini kuingia kwenye mfumo wa siasa za vyama vingi. Wapo waliombeza kwa kusema kwamba Mzee huyu amekula amemaliza, inafika zamu yetu ndo anakuja kutuambia habari za kukubali vyama vingi. In a way ilikuwa ni msaada mkubwa sana maana wangeingizwa ghafla na kwa nguvu, wasingeweza kupata nafasi ya kujiandaa yangewakuta yaliyomkuta Babu yangu Ken Kaunda.

Nyerere alikuwa yuko well informed kuliko hawa viongozi wetu wa siku hizi ambao hawasomi wanasubiri kupewa briefing then wanaanguka sahihi zao hata bila kusoma kilicho kwenye makaratasi aliyosaini. Viongozi wetu wa sasa wanachofikiria ni namna gani ya kuongeza utajiri wao na ndiyo maana wanashindwa kujenga hoja kutetea misimamo yao, wanaishia kusema hata Nyerere, Mwinyi na Mkapa walifanya hivyo. Je, kama wao walifanya hivyo kimakosa, ndo na Rais wa sasa anataka kutuingiza kwenye mkenge huo huo? Mazingira ya utawala wa Mwinyi, Nyerere na Mkapa, JK na kwa hiyo kati yao hakuna ambaye anatakiwa kumtumia mwenzake kama justification ya kufanya kitu fulani, unless kiwe ni kitu cha kikatiba. Na kama ni kitu cha kikatiba hakuna ambaye ata-question kwa kuwa Katiba inamlinda Rais kufanya kile anachokifanya.

Wapo waliomwita HAAMBILIKI, tatizo ni kwamba unapokuwa kiongozi kuna vitu ambavyo unasimamia na sidhani kama mtu akija na hoja tofauti unaweza kukubaliana naye kirahisi bila kukupa hoja yenye mashiko. Anakuja mshauri wa Uchumi anakushauri hiki, lakini ukikiangalia kwa makini unakuta kiko kinyume na kile unachokisimamia, ni ngumu sana kuweza kukubaliana nacho kirahisi. Kwa hiyo swala la kwamba alikuwa HAAMBILIKI au hakubaliani na washauri wake au wasaidizi wake, ni swala ambalo liko kwa kila binadam, ni sehemu ya mapungufu yetu kusimamia kile ambacho tunachokiamini.

Sasa yupi ambaye haambiliki kati ya hawa? Mkapa aliyetokwa na povu kununua radar? au JK aliyekubaliana na Lowassa kutuletea Richmond na Dowans na huku magazeti yakipiga kelele sana? Katika zama za utawala wa Mkapa na JK, information kuhusu mambo mbali mbali zimekuwa zikitoka na magazeti/wanaharakati wamekuwa mstari wa mbele kupiga kelele zao kwa nguvu zote, lakini kelele hizo hazikufika popote. Baada ya madudu kuwa wazi, JK anasema ajali ya kisiasa, Lowassa anasema Rais alijua kila kitu. JK anasema mwacheni mzee wetu apumzike, ebooo yaani afisadi mali ya walala hoi halafu aachwe apumzike then watu wanakuja kusema ni Rais Bora!
 
Asante mkuu, Sasa kwa nini watu wanajaribu kudanganya kuwa JKN hakuwachukulia hatua wazembe?! Nina maswali zaidi ya nyongeza! Kenya kama ilivyo Tanganyika kuna maeneo hadi sasa
watu wanaliwa na simba, haya malalamiko kuwa watu walipelekwa maporini, walikuwa mijini wakaondolewa au ilikuwaje? Na tangu enzi waafrika wamejua kwa kiasi kikubwa kujikinga/kupambana na wanyama wakali, hawa 'wengi' walioliwa walitolewa dunia gani?! Kwa nini wakati wa ukoloni watu waliobahatika kusoma (tunaambiwa wengi walilazimika kutembea km nyingi sana kwenda shule) hawakuliwa na simba?! Ni nani alikuwa anaamua kijiji A kiwe eneo fulani ni Nyerere au watendaji wa ngazi za chini na je hawakuwashirikisha wananchi kuangalia faida na hasara za maeneo husika?

Mwaka 1961 wakati nchi inapata uhuru, Tanzania ilikuwa na population ya watu milioni tisa whereby 95% ilikuwa ni vijiji, na 5% miji. Hii ina maana kwamba kati ya watu milioni 9, watu milioni 8,500,000 walikuwa vijijini, na watu elfu 50,000 tu ndio walikuwa katika miji mbali mbali. Kwa maana hii ni rahisi kuelewa kwanini kulikuwa na mapori mengi karibia na makazi ya watu, hususan ukizingatia kwamba hii nchi, mbali ya kujaliwa na Mungu kuwa na madini kuanzia mashariki hadi magharibi, na kaskazini hadi kusini, pia imejaliwa na misitu yenye wanyama wa kila aina karibia nchi yote; na ndio maana ni kitovu cha vivutio vya wanyama wa porini dunia nzima; kwahiyo kutokana na asili, makazi ya binadamu na makazi ya wanyama hayakuwa yametengena kiasi hicho by 1961;

Hata miaka michache baadae, Mzazi wangu amewahi kuniambia kwamba wakati wanasoma Chuo kikii (UD) miaka ya mwisho ya sitini (mid to late 1960s), kulikuwa na Simba wengi sana SINZA na MAKONGO, na walikuwa wanawasikia wakinguruma usiku wakati wamelala; Na safari ya kutoka chuo kwenda mjini ilikuwa ya uangalifu wakati wote; sasa watu wanaomlaumu Mwalimu kwamba vijiji vya ujamaa vilipelekea watu kuliwa na simba wanakuwa wavivu kidogo kuelewa uhalisia wa Tanzania kama nchi ya nyika; Miaka ile hata ungehamishia watu Masaki wangeliwa na Simba, nadhani unafahamu masaki mwisho kulikuwa na Simba na Chui; Watu wenye mawazo ya namna hii wanaweza kabisa kujenga hoja kwamba yule Simba alieuawa Mbagala Mwisho Mwaka jana kwenye makazi ya watu, kuna mkono wa Mwalimu na vijiji vya ujamaa;
 
Kwanza umekosea, Marekani haina "Baba" as singular bali ina plural "Fathers" Marekani kuna Founding Fathers. Naomba urekebishe hiyo ili uweze kuweka hiyo point unayojaribu kuweka.
 
Kwanza umekosea, Marekani haina "Baba" as singular bali ina plural "Fathers" Marekani kuna Founding Fathers. Naomba urekebishe hiyo ili uweze kuweka hiyo point unayojaribu kuweka.

Kulingana na hoja za "Mohamed Said" na Wanafikina wenzake, the phrase "Baba wa Taifa" has as its primary source the roughly equivalent English translation of the Kiswahili phrase "Baba wa Kanisa".

Sasa swali ni jee, nchi kama Pakistan, Uturuki, Turkemistan, Taiwan, India, etc zenye "Founding Father" (otherwise known as "Father of the Nation") A B C D, zote zilikuwa na historia ya "Mababa wa Kanisa"?
 
Ilijiingiza kwenye siasa za ndani ya CCM ikidhani kuna watu wanaiheshimu na kuisikiliza. Ikadhoofishwa kiaina tangu enzi za Mkapa. SAS alipojitokeza kupambana na WANAMTANDAO wakaimalizia kabisa.

This strongly suggests kwamba Nyerere Foundation imejiweka kisiasa zaidi; pengine nadhani inapata wakati mgumu sana wa kujipanga jinsi gani inaweza kuvaa viatu vya Mwalimu nyerere (ambavyo ni vikubwa sana ) in the political-social-economic spheres in today's context; Leo hii wameishia kuhojiwa tu kwenye TV kuzungumzia suala moja tu 'uadilifu', kwa mtindo wa kuelezea umma “enzi za Mwalimu…”; hii pekee haitoshi;

Mbali na kuwa na maonyesho kadhaa ya Mwalimu na kuuza vitabu vyake; Nadhani wangeenda mbali zaidi na kuja na kitu kama Jarida la kila mwezi lenye wachangiaji mbalimbali kutokana ndani, nchi za kusini mwa Africa, na wa nje ya Africa ambao ni wengi sana kama watapewa a platform; Jarida hili kwa mfano linaweza kuchagua likae kwenye mrengo upi in the liberal – conservative spectrum, e.g center left etc, kikubwa ni kujaribu balance hekima na malengo ya mwalimu kwa Tanzania na Afrika na uhalisia wa dunia ya sasa in the political, social and economic contexts; kuna waandishi na wasomi wengi sana vyuo vya ndani na nje ambao wameandika mambo mengi sana ya mwalimu lakini kwa sasa wanaona hakuna tena mwamko (both kijamii na kiuongozi) na hivyo kuacha shughuli hiyo;

NF pia wangeweza hata kuwa na weekly programs on TV and Radio ambazo ni provocative kidogo zenye nia ya kuelimisha vizazi vya sasa tumetoka wapi kama nchi, tupo wapi na tunaenda wapi, in a non-partisan way,huku wakiruhusu watu kupiga simu na kuuliza maswali mbalimbali, na wakiwa wabunifu, content ni nyingi sana, kipindi kinaweza kuwa stable for many years;

Muhimu zaidi, ni lazima wazee wa NF waachane na dhana kwamba wao ndio wamiliki, badala yake waonyeshe kwamba UMMA ndio wamiliki; pia wasiwe partisan, mfano Mzee Butiku wakati wote anazungumza kama Mwana CCM bila kufahamu kwamba aliyekuwa na usafi wa namna hiyo ndani ya CCM chafu lakini jamii kumsikiliza alikuwa ni Mwalimu pekee; by being non-partisan, huku wakionyesha UMMA kwamba wao ndio wamiliki kwa pamoja kama Taifa, inaweza saidia pelekea hata UMMA kuwachangia fedha kwa kadri ya uwezo wao;

NF ijijenge zaidi kama organization yenye a certain vision and school of thought – institute of Nyerere’s studies sort of thing (not chuo cha kumbukumbu ya Nyerere), vinginevyo haiwezi endelea kwa kutegemea personality ya Nyerere pekee, kwani organizations kama APPLE etc zingekufa with Steve Jobbs departure;

Cha muhimu pia waachane na ndoto za Urais, badala sasa yake waielimishe jamii kwa njia kama hizo hapo juu, na kujijengea heshima kama a think – tank, bila ya kuegemea chama chochote cha siasa ambayo itakuwa ina endorse any political party from time to time. The Foundation pawe nyumbani kwa CHADEMA, CCM, CUF, etc; itakuwa ngumu kufanya viongozi na wazee wa ndani ya CCM ya sasa kushirikiana nayo, lakini hakika haitakuwa vigumu kuwa karibu na vijana siku za mbeleni kama wakijipanga vizuri; pia itakuwa ngumu kwa upinzani kushirikiana nayo kwa sasa kwa kuhofia kutekwa kisiasa, something which is a legitimate threat, lakini nina uhakika hofu hii ikiondolewa, the foundation itakuwa kitu muhimu sana nyakati za shida na changamoto mbalimbali;
 
Kulingana na hoja za "Mohamed Said" na Wanafikina wenzake, the phrase "Baba wa Taifa" has as its primary source the roughly equivalent English translation of the Kiswahili phrase "Baba wa Kanisa".

Sasa swali ni jee, nchi kama Pakistan, Uturuki, Turkemistan, Taiwan, India, etc zenye "Founding Father" (otherwise known as "Father of the Nation") A B C D, zote zilikuwa na historia ya "Mababa wa Kanisa"?


Nimemuomba mwandishi wa hii article arekebishe kwanza. Marekani haina "Baba" as singular, pale kuna Plural "Fathers" as Founding Fathers.

Also, unashindwa kuelewa kwamba hayo mataifa uliyoyataja yaliwahi kutawaliwa na hao Wazungu (Wakristo) kabla ya kupewa Uhuru wao. Sas ni nini hoja yako.
 
Kwanza umekosea, Marekani haina "Baba" as singular bali ina plural "Fathers" Marekani kuna Founding Fathers. Naomba urekebishe hiyo ili uweze kuweka hiyo point unayojaribu kuweka.

Naomba mwandishi usahihishe please.
 
Hivi kama patrice Lumbumba angechukua nchi na kuweka misingi ya kikomunisti nchini Zaire, kweli Lwambo na Lipua Lipua wangetamba barani africa?SI unajua wakomunistoi huondoa hati miliki za wanamuziki nakuwadhoofisha wanamuziki? Je zaire ingecheza world cup 1974 na kuchukua AFCON mwaka huo huo? Tazama nchi za kikomunisti zilivyo dolola kisoka mara baada ya kuuingiza ukomunisti nchini mwao. Ulaya mashariki yote, hamna hata nchi moja inayoweza kuifunga Ivory Cost, Ghana, Cameroon na Zambia.

Wazaire walijua kabisaa tokea zamani kuwa ukomunisti ni Unyama. Hivyo walimchinja Lumumba na kumtia mwili wake katika pipa la acid ayeyuke mpaka mifupa. halafu mpaka leo kaburi lake halijaonekana. Hapo waliwakomboa sana watu wenye vipaji vyao na kuajilika navyo kama vile kina Lwambo, DR Nico, Verkyis, Josky Kiambukuta, shaba kahamba na wengine wengi.

Nchi kama guine, ilikuwa taifa bora kwa soka hapa africa. Lakini mara baada ya kuingiza ukomunisti tuu, klabu yake ya Hafia iliyowahi kutwaa ubingwa wa africa mara nne iliporomoka vibaya sana. Soka la guine likafa na kukabakia makwaya na magwaride tuu.

Halafu lazima ukumbuke kuwa ukomunisti hapa africa, umeuwa watu wengi sana kuliko vita vya uhuru. Tazama walivyouana Angola, Msumbiji, Congo Brazavile na Ethiopia. ni ukweli kabisaa kuwa , shetani alitaka kuitawala dunia kwa kupitia sera za kinyama za kikomunisti. wazaire usiwalaumu kwa kumyonga Lumumba, hakuwa na tofauti na kina Boris Pugo-wa Urussi.

sasa hivi zaire ni taifa la tatu duniani , kwa kupeleka viaja wake kucheza soka la kulipwa ulaya mashariki na magharibi mpaka bara la america. Ya kwanza ni Brazil, na ya pili ni algentina.

Ukomunisti haujui kabisaa kulea vijana . Huwatumia viajan kuimba kwaya, kucheza gwaride na kuwapeleka mashambani kulima.

inabidi ujifunze historia vizuri. Nani alikwambia kwamba Lumumba alitaka kuleta Ukomunisti Congo? Je, unajua "alikaa" madarakani siku ngapi? Je, waliompindua na kumuua ni akina nani? Ama kweli, hivi wewe nchi kama Congo unategemeal imeweza hata kufikia asilimia 0.00000000000000000000001 ya uwezo wake? Wewe ni kama wale wanaoridhika kupewa pipi huku wakinyang'anywa nyumba. Tafadhali uwe na uhakika na mifano unayotoa kabla ya kuitumia kujenga hoja.
 
Nimemuomba mwandishi wa hii article arekebishe kwanza. Marekani haina "Baba" as singular, pale kuna Plural "Fathers" as Founding Fathers.

Also, unashindwa kuelewa kwamba hayo mataifa uliyoyataja yaliwahi kutawaliwa na hao Wazungu (Wakristo) kabla ya kupewa Uhuru wao. Sas ni nini hoja yako.

Kwa hiyo una maana kwamba sababu za Kihistoria zinazoelezea kwa nini Mataifa yenye asilimia 90 hadi 99 ambayo raia wake wana imani tofauti kabisa na Ukristo kutumia msemo "Baba wa Taifa" unatokana na historia ya mataifa hayo "kutawaliwa na Wazungu (Wakristo)", si ndiyo?

Basi ni vyema (au kwa lugha nyingine, isingekuwa vibaya) kama ungewataja hao "Mababa wa Kanisa" kwenye nchi husika ambao, kwa tafsiri yako, ndiyo vyanzo vya jadi ya msemo wa "Baba wa Taifa" kwenye nchi husika.
 
atakaye vunja muungano atakuwa shujaa wa Taifa


Unaposema Hero una maana gani? You might have a point, but since haujatoa ufafanuzi, your statement sends zillions of meanings and interpretations, so inakuwa vigumu kwa baadhi yetu kukujibu kwa hoja. Neno HERO has the following synonyms:
Atakaevunja muungano atakuwa – Opportunist wa taifa?
Atakaevunja muungano atakuwa – Mercenary wa taifa?
Atakaevunja muungano atakuwa – Speculator wa taifa?
Atakaevunja muungano atakuwa - Wanderer wa taifa?
Atakaevunja muungano atakuwa – Fighter wa taifa?
Atakaevunja muungano atakuwa – Champion wa taifa?
Atakaevunja muungano atakuwa – Fortune hunter wa taifa?
Atakaevunja muungano atakuwa – Dare Devil wa taifa?
Atakaevunja muungano atakuwa – Explorer/adventurer wa taifa?
Atakaevunja muungano atakuwa – Pioneer or Groundbreaker wa taifa?
Atakaevunja muungano atakuwa – Brainish wa taifa?
Atakaevunja muungano atakuwa – Charlatan wa taifa?
Atakaevunja muungano atakuwa – Gambler wa taifa?

Natumaini unapoyazungumza haya haupo kwenye moja ya unions zenye mafaniko makubwa sana duniani - UNITED KINGDOM na UNITED STATES OF AMERICA, au haufikirii kukimbilia huko badala ya China, SAUDI ARABIA, JAPAN, AUSTRALIA, kila mara mawazo yenu yanapoletaga machafuko katika muungano wetu. Ni kawaida kwa watu wa namna yenu kupendelea kuishi UNITED KINGDOM au UNITED STATES, na kuukana kabisa uraia wenu kwa kujenga hoja na mawakili huko kwamba nyinyi ni wakimbizi of some sort kutoka Jamhuri ya MUUNGANO wa Tanzania, hivyo kuomba hifadhi na uraia kuishi katika MUUNGANO WA UK an MUUNGANO WA USA, na kuachana na maisha ya MUUNGANO WA TANZANIA, ambapo ni tabia zenu za kuukana ndizo zimepelekea machafuko ya kuwakimbiza.
 
Kwanza futa kauli yako ya kuwa mimi ni mdogo kwako, kwa jinsi ulivyoandika nnauhakika umri wako ni mdogo sana, basi kama si umri, una mapungufu mengine ya kiufahamu.

1. Pakistan ndio nani? mimi naongelea Uislaam, wewe unaongelea nchi? inawezekana kabisa kuwa kuna Waislaam lakini hawafati Uislaam. Ndio maana nikakuambia unaonesha una umri mdogo sana au una mapungufu ya kiufahamu.

2. Uturuki jibu lake ni kama namba 1. Hapo juu, hivi hujaona night clubs hapo Uturuki? na hizo nazao Uislaam unaruhusu? Fikiri.
Kuhusu yote uliyoandika si kweli kabisa, kwani umeyatunga, nimeishi, UAE, nimeishi Saudi Arabia na hakuna kitu kama hicho wala hawana kabisa hiyo kitu, tena umejaribu kuingia kwenye translation sites, uwadanganye wasiojuwa kiarabu. Hayo maneno ulivyoyaandika kiarabu ni grammatically incorrect, ingekuwa sahihi ingeandikwa "أبو الأمة", kwa grammar ya kiarabu huwezi kuandika neno والد halafu ukaandika الأمة haiji kabisa. Wadanganye wasiojuwa kiarabu.

Uislaam hauniruhusu kumuita yeyote asiye baba yangu aliyenizaa baba, Si Nyerere si yeyote uliyemtaja. Kunitajia hao ndio ina maana hao ndio wanaujuwa sana Uislaam? kijana, Unanchekesha.

Sasa unasema nisichangie kidini na kumuita Nyerere "baba" si udini huo? Unanshangaza! mababa wako kanisani tena hata kuzaa hawaruhusiwi na huitwa mababa. Mimi dini yangu hakuna kitu kama hicho, baba ni alienizaa tu. Full Stop. Hata ingekuwa mama yangu kaolewa na mume mwingine baada ya baba yangu, basi sithubutu kumuita baba. Si Uislaam.

Hivi hii ina uhusiano wowote na utofauti wa salaam za heshima kwa wakubwa zenu (BABA na MAMA) mnaposema Chei Chei badala ya Shikamoo?
 
Back
Top Bottom