Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Unajua huwa inanishangaza sana watu wanapomdhihaki mwalimu na swala la maendeleo wakati wao wenyewe ndio wameharibu maendeleo. Hivi pamoja na ujenzi wa shule na vitu vyote hivi kuna mtu anaweza kunambia University bora zaidi ya UDSM? kuna anaweza kunambia leo tuna Hospital gani bora kwa huduma kuliko Muhimbili, anaweza kunambia tuna hata Hotel gani bora kuliko alizoziacha mwalimu bila kuwepo na utata..Na hata viwanda vikubwa na bora zaidi ya vile alivyoaviacha mwalimu?...

Labda mimi siijui vizuri Tanzania lakini nachokiona ni kwamba vitu vile vile vinapopata msimamizi mzuri vimeweza kuboreshwa zaidi ktk huduma, hivyo vilikosa usimamizi mzuri na kwa bahati mbaya mwalimu hakuwa msimamizi bali sisi wenyewe tuloviua vingine leo tunamlaumu mwalimu..
 
Mara nyingi "maadui" wa hayati Mwl. Nyerere wanakuwa subjective na personal zaidi. Mimi sio mshabiki au muumini wa hayati Mwl. lakini nakubaliana sana na uliyoyasema, kwa vile yako kimantiki na kimtiririko.

Asante Mchambuzi
 
Mkuu Zing,

Nitakujibu kwa mfano. Kwanini Uchagani hasa nilipofika mie Marangu, mwika, Kibosho na Rombo kwa ujumla wana maendeleo sana (wamesoma, wana maji, wana umeme, wana barabara, wana mashule, wana majumba mazuri ya kulala in totality) lakini hamna vijiji vya ujamaa?

Ninge fanya vijiji vya ujamaa kulingana na mazingira. Isingekua swala la NGUVU. Ningeweka huduma kama ilivyo Kilimanjaro.

Ni hilo tu. Na kumbuka sipingi the concept napinga utekelezwaji wake.

Chunguza sana

@FairPlayer
Maendeleo ya uchagani yana historia yake. Sidhani kama yanahusiana na vijiji. Moja ya chachu kubwa katika kuleta maendeleo ya wachaga ni ujio wa wazungu. Kwa sababu ya hali ya hewa nzuri, wazungu walichagua kuishi maeneo ya uchagani. Kuishi kwao maeneo haya kuliwafaidisha wenyeji kwani vitu km shule, makanisa, mahospital vilijengwa na kuwaendeleza wenyeji. Ukienda uchagani majengo ya shule za zamani kabisa mpaka sasa bado yapo na yanatumika. Utakutana na majina ya shule (hayatumi sasa) kama ..... Upper school, .... extended school, ...... middle school nk. Jambo jingine lililowasaidia wachaga ni hali ya hewa nzuri na zao la kahawa. Zao la kahawa lili-play role kubwa kabisa katika kusomesha watoto wa wachaga. Na vilevile usisau kuwa wachaga wana utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii na kwa kuweka malengo....
 
Bi Faizafoxy,
Waarabu wanatumia neno Waalid Alamat kama wadhifa (title) - Father of the nation hilo usikatae ingawa kweli haina maana ndio Uislaam.. Neno hilo lipo ktk matumizi ya kiarabu na ukiandika maneno hayo utaandika kama alivyoandika Askari kanzu.. Na Ibn inatumika kwa mtu na ubini wake (nasaba) lakini sio title..
 
Kwenye historia ya JF sijawahi kukutana na thread ndefu kama hii halafu upupu mtupu..

Eti Nelson Mandela, baba wa taifa wa South Africa sijui umeipata wapi hii
 
@mchambuzi

Kwanza, hoja yako ni dhaifu na ndefu bila sababu najisikia vibaya kupoteza muda kusoma habari ndefu yenye mantiki ndogo sana, kubembeleza watu kumkubali nyerere ha!

Pili, Mimi baba yangu ni mume wa mama yangu period..nyerere ni rais wa kwanza wa Tanzania siyo baba yangu na wala hawezi kuwa baba wa mtoto wangu NEVER ukimpenda sana jazeni vitabu lakini mimi na ukoo wangu hiyo sifa hatutampa hadi kifo...

Tatu, Unajua kabisa hana sifa hizo ndio maana mnalazimisha watu na kutafuta popularity..kibaya mnajitmebeza sana poleni

Kwangu mimi ni Baba wqa kanisa kwa mujibu ya mafundisho yao ya dini na faida walizopata kanisa chini ya utawala wake.
 
Pili, Mimi baba yangu ni mume wa mama yangu period..nyerere ni rais wa kwanza wa Tanzania siyo baba yangu na wala hawezi kuwa baba wa mtoto wangu NEVER ukimpenda sana jazeni vitabu lakini mimi na ukoo wangu hiyo sifa hatutampa hadi kifo...

Na tunaomuona , tunamuita na wengine mpaka wameandika (mf Mohamed Said) kuwa A .sykes ni "baba" unatuambiaje?

Kwenye historia ya JF sijawahi kukutana na thread ndefu kama hii halafu upupu mtupu..

Inawezekana wewe jukwaa hili halikufai . labda wewe ni mtu wa Physics na hesabu. Tulia kawenye majukwa ya tenolojia na udaktari
Ukitaka kukutana na nyingine ndefu soma hii
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/177005-makala-za-mohamed-said-katika-mwananchi-miaka-50-ya-uhuru-wa-tanganyika.html.

Kuhusu upupu hapo nadhani ni mtazamo. Lakini ili upupu uwe upupu onyesha au nukuu kuwa hapa na pele ni upupu.
 
Shauri zenu lakini si mimi wala watoto wangu wala ukoo wangu NEVER!

IKo wazi asiyekuwa na utamaduni ni mtumwa.

Toka enzi na enzi mtoto ni wa jamii. Kwa wengine tumeualia na tumelelewa atika a sehemu ambapo baba ni baba na mama ni mama. Kiafrika wazazi wako wewe Topical natakiwa niwaheshimu kama wazazi wangu . Sadly siku hizi sio hivyo..............

Pole sana kama hujawai ku ex perince rich and undistored culture ya kiafrika au ya kitanzania.

Ndiyo haya tunaita maendeleo ya kuiga iga lakini ya matatizo yake tunayaona. Kama ulzaliwa na kukuia maghorofani hata likizo hukwenda kumsabahi bibi/babu shamba/kijijini mambo kama haya lazima yawe msamiati kwako. . Lazima yawe NEVER lakini ni dalili za kukosa utamaduni.
 
Huwezi kulazimisha rais wa kwanza nyerere kuwa baba..bana

kama wewe unataka na wote wajaze vitabu lakini si mimi na watu wangu..we are not proud for him for anything useful ..
 
Huwezi kulazimisha rais wa kwanza nyerere kuwa baba..bana

kama wewe unataka na wote wajaze vitabu lakini si mimi na watu wangu..we are not proud for him for anything useful ..

sijalazimisha mkuu nakueleza concept ya ubaba/ umama in aits origina african culture amabyo wewe kwanza unataka kupinga kwamba mipaka yake ni ya kibaiolojia tu.

Hapo uko wrong. Ndio maana nakuambia unless umekulia maghorofani au huna experince ya kukulia mazingira ya kiafrika/kItanzania. kama ni hivyo unakosa culture ya uafrika. Naweza kukuelewa . Lakini ni wazi asiyekuwa na utaduni ni mtumwa.

Moja ya utamaduni tulinao waafrika ndio huo unapoongelea neno "baba" na "mama" ni zaidi ya bailojia. Usishangae watu siku hizi wanalamika siku hizi utovu wa nidhanu wa vijana na hata mashuleni . Moja ya sababu ni watu wenye mawazo kama yako.
 
Nashukuru, sasa kama kawa Magamba,Mmeacha kujadili mada ya Mkuu hapo juu mnamjadili FF-muislam wa bongo ya Mwl.Nyerere Baba wa Taifa la JMT,ha ha haaaaaa.Hao ndio Waislam wa bongo,wanajiona bora kuliko waislam wa Iran,Saudia,Yemen,Bahrain,Kuwait yaaaaaaani ni mzuka laaaaana ati!!!!!!!!:hat:
 
sijalazimisha mkuu nakueleza concept ya ubaba/ umama in aits origina african culture amabyo wewe kwanza unataka kupinga kwamba mipaka yake ni ya kibaiolojia tu.

Hapo uko wrong. Ndio maana nakuambia unless umekulia maghorofani au huna experince ya kukulia mazingira ya kiafrika/kItanzania. kama ni hivyo unakosa culture ya uafrika. Naweza kukuelewa . Lakini ni wazi asiyekuwa na utaduni ni mtumwa.

Moja ya utamaduni tulinao waafrika ndio huo unapoongelea neno "baba" na "mama" ni zaidi ya bailojia. Usishangae watu siku hizi wanalamika siku hizi utovu wa nidhanu wa vijana na hata mashuleni . Moja ya sababu ni watu wenye mawazo kama yako.

Huo utamaduni unasema mtu anaweza kuwa baba (apart from baba mzazi) anatakiwa awe na sifa zipi?

Hopefull atakuwa mtu ambaye ameifanyia familia, anafahamika katika familia kama somebody with usefull contribution (thinking aloud), au jirani mwema, ndugu mwema, huwezi kumuita dhulmaji baba ...BIG NO..

Sasa nyerere ana contribution gani kwetu, (sitaki kusoma ujinga wenu mlioujaza kanisani) kwa familia yangu kwa jamii yangu; ..NONE

NEVER hawezi kuwa baba..lakini nyie mkitaka mpeni na muiteni chochote..not me, US..etc..kuna ubaya mkuu wewe si umefaidi sana na nyerere muite baba yako who cares, don't tell me or teach me who deserve to be called father etc..
 
Huo utamaduni unasema mtu anaweza kuwa baba (apart from baba mzazi) anatakiwa awe na sifa zipi?
Too late kuulizia sifa . elewa tu asitye uwa na utaduni ni mtumwa. Lakini kama wewe uizaiwa kukulia na kuleewa washinton DC au London siwezi kushangaa
Hopefull atakuwa mtu ambaye ameifanyia familia, anafahamika katika familia kama somebody with usefull contribution (thinking aloud), au jirani mwema, ndugu mwema, huwezi kumuita dhulmaji baba ...BIG NO..
Hapa sasa ndio unaleta utata. Kwanza umeshaseme Big No . Ebu turudi nyuma uone mtu asiyekuwa na principle anavyoyumba yumba

Topical said:
..Pili, Mimi baba yangu ni mume wa mama yangu period..nyerere ni rais wa kwanza wa Tanzania siyo baba yangu na wala hawezi kuwa baba wa mtoto wangu NEVER ukimpenda sana jazeni vitabu lakini mimi na ukoo wangu hiyo sifa hatutampa hadi kifo..

Nikakuuliza
fahari said:
...Na tunaomuona , tunamuita na wengine mpaka wameandika (mf Mohamed Said) kuwa A .sykes ni "baba" unatuambiaje?

Ukajibu
Topical said:
Shauri zenu lakini si mimi wala watoto wangu wala ukoo wangu NEVER!

Sasa ni ueleweke vipi kwako ni never au mpaka ni kwa baba mzazi tu au mpaka aiswe mwizi au mradi asiwe Nyerere ????????
.

Sasa nyerere ana contribution gani kwetu, (sitaki kusoma ujinga wenu mlioujaza kanisani) kwa familia yangu kwa jamii yangu; ..NONE

Nachoolewa msimamo wako toka kule juu ni Kuwa anayetakiwa kuitwa baba ni baba/mama ni wa kibaiolojia tu. Kwanza kubali kuwa kiafrika na hata kitanzania baba na mama ni zaidi ya baba mzazi na mama mzazi. Jisahihishe hapo ndio tuendelee. Bila hivyo itakuwa kutwangwa maji kwenye kinu. Ni sawa sawa sawa mchina kukosoa utamaduni wa mzungu.........

NEVER hawezi kuwa baba..lakini nyie mkitaka mpeni na muiteni chochote..not me, US..etc..kuna ubaya mkuu wewe si umefaidi sana na nyerere muite baba yako who cares, don't tell me or teach me who deserve to be called father etc..

Wewe kwako umeshathibitisha huna au hujakulia mazigira ya utamaduni wa kiafrika. Issue yao sio tu kwa nyerere. Nimekuwekea tu hapo mfano je ni kosa hata mzee wetu A. sykes kumuita "baba" kama anavyofanya na tulivoyokubaiana na Mohamed saidi juu ya wazee wetu . Umekimbia hoja tena kwa neno la herufi kubwa wewe kwako ni NEVER.
 
Kwanza futa kauli yako ya kuwa mimi ni mdogo kwako, kwa jinsi ulivyoandika nnauhakika umri wako ni mdogo sana, basi kama si umri, una mapungufu mengine ya kiufahamu...
Wewe dada mdogo FaizaFoxy acha jazba. Hata usemeje ukweli unabaki pale pale kwamba mimi ni kaka yako kiumri. Nasema hivi kwa sababu kuna mada flani umechangia kuhusu Azimio la Arusha (1967) na kusema wakati huo ulikuwa mdogo. Hapo imenifanya nijue kwamba wewe ni mdogo kwangu. Usifikirie wote humu jamvini tulizaliwa jana. Kasirika utakavyo lakini ukweli utabaki ulivyo!

Sitajibu hizo pumba nyingine ulizoziweka kwa sababu zimejaa uongo uliotukuka utokanao na ghadhabu ya kuumbuliwa. Na wewe kama kweli ni muislamu wa dhati basi tafadhali tafakari!
 
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.
Wewe ndio unajijaza ujinga. Ulitaka tumwite nani? Kwa ridhaa yetu sisi Watanzania na Ulimwengu kwa ujumla tuliamini tunaamini anastahili sifa hiyo. You can't take it too bad so sad!! Ukweli utabaki ni Mwalimu Nyerere ni mfano wa kuigwa duniani. Nchi za Magharibi zinamuheshimu na kumuheshimu itakuja kuwa wewe acha chuki zako za kidini hapa!! Nyerere ni Baba wa Taifa kwa dini zote makabila yote imani zote kwa WaTanzania. Upo hapo???
 
Haya endeleeni kuwafundisha watoto wenu hayo..

Sisi tutawafundisha watoto wetu tunayofikiri ni sahihi

kuna tatizo wakuu..ya nini kutujazia habari, kama vile hakubaliki vile ndio maana mnajazana kumbembeleza watu watambue hicho mnachotetea..aargh
 
- Vita vya Kagera ambavyo vimeirudisha taifa nyuma kiuchumi mpaka tukawa tunapanga foleni ya unga wa YANGA, wakati essence ni kumweka rafiki yake madarakani. Kutumia resources za taifa.

Mkuu FairPlayer,

Swala la vita vya Kagera limekuwa likipotoshwa na watu kwa muda mrefu. Nina hakika kwamba maamuzi ya Nyerere kumpiga Idd Amin, yangeweza kufanywa na Rais yeyote yule ambaye angekuwa madarakani wakati huo. Huwezi ukavamiwa halafu ukakaa kimya bila kujitetea au kulinda mipaka yako.

Ni ukweli ambao haupingiki kwamba mapinduzi ya Obote hayakumfurahisha Nyerere. Obote alikimbilia Tanzania na kuomba hifadhi lakini pia alikuwa bado anatamani kurudi madarakani. Kitendo cha Nyerere kukubali kumweka Obote Dar es Salaam kwa namna yoyote ilikuwa ni kujitakia matatizo kwa sababu Idd Amin lazima alijua kwamba Obote anaweza kuitumia Tanzania kuandaa mashambulizi ya kumrudisha madarakani, kwa hiyo kitendo cha Obote kukubaliwa kuishi Dar es Salaam kiliongeza kutoaminiana kati ya Uganda na Tanzania na given kwamba Nyerere hakuitambua serikali ya Idd Amin mara baada ya mapinduzi.

Hilo la Obote kutaka kurudi madarakani ni kweli lilifanyiwa majaribio mwaka 1972, lakini liliwahusisha akina Museven na wapinzani wengine ambao walikuwa ni vijana wa Obote. Obote alijua kwamba alikuwa na support kubwa within Uganda na kumbe he was wrong na ndio maana hawakufanikiwa. Kwa bahati mbaya kabisa zoezi hilo halikufanikiwa na matokeo yake ilikuwa ni kumfanya Amin arushe mabomu Mwanza na Bukoba. Kwa kuwa Nyerere alijua kosa lake, wala majeshi ya Tanzania na serikali yake hawakujibu kitu waliishia kimya kimya.

Tension iliendelea kwa muda mrefu, akina Museven walifungua kambi za mafunzo ya vijana wa kutoka Uganda ambao walikuwa wamekimbilia Tanzania. Lakini kwa kuwa kitengo cha usalama cha Amin kilikuwa makini sana, habari zilimfikia Amin kuwa Tabora (to be specific, Kigwa) kulikuwa na kambi za vijana wa Uganda chini ya Museveni. Kwenye makubaliano ya Mogadishu ya ku-difuse tension kati ya Tanzania na Uganda, Uganda ilitoa condition ya kufungwa hiyo kambi ya Kigwa na Nyerere alikubaliana nao na ilifungwa. Ndipo Museven alipohamia Nachingwea ambako ilikuwa ni ngumu sana kwa Amin kujua kinachoendelea kwani mikoa ya huko kusini ilikuwa na askari wengi sana na wengine walikuwa masalia ya askari wa marehemu Samora. Wakati haya yote yakitokea Nyerere alisha-give up plan yoyote ya kumsaidia Obote kurudi madarakani baada ya makubaliano ya Mogadishu.

Mimi nilikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakiamini kwamba Tanzania ndio ilimchokoza Idd Amin mwaka 1978, lakini ukweli ni kwamba Amin ndiye aliichokoza Tanzania. Tanzania haikuwa imejiandaa kwa vita ya aina yoyote ile na Uganda na ndio maana ilichukua karibu mwezi mzima kwa Tanzania kuanza vita rasmi tangu siku askari wa Amin walipobomoa daraja la mto Kagera na kupandisha bendera ya Uganda ndani ya mpaka wa Tanzania.

Kuthibitisha hili, askari waliokwenda frontline mwanzoni kabisa mwa vita walitoka Songea, vikosi vya kusini ndio pekee ambavyo vilikuwa tayari na ninadhani ni kwa sababu Nyerere alikuwa anahofia zaidi nchi za kusini kuliko nchi za kaskazini na magharibi mwa Tanzania. By then Banda alikuwa haeleweki na pia hali ya Msumbiji ilikuwa bado iko tete na Angola pia moto ulikuwa unawaka na Zimbabwe walikuwa bado hawajapata uhuru. So, vikosi vya kusini vyote vilikuwa viko ready masaa 24 kwamba lolote likitokea ni swala la kusogeza zana na kazi inaanza.

Hii clip angalia/sikiliza kuanzia 05:22 na kuendelea mbele kidogo ili umsikilize Amin kwa kauli yake mwenyewe akiwa anatamba na bendera ya CCM.

Vita vya Kagera (Kagera War) - Part 1 of 4 - YouTube

Sasa swali linakuja, je, baada ya huo uhuni alioufanya, ni Rais gani wa nchi angekaa kimya bila kujibu? Ndugu zangu wachagga hata ukiingia hatua moja ndani ya mpaka wa kihamba yake atakutokea na panga. Ndio ije kuwa umevuka mpaka, umevunja daraja na kuua wananchi wake halafu akuache tu?

Kuna wengi ambao wanasema kwamba tulitakiwa ku-reclaim ardhi ambayo ilikuwa imechukuliwa na then tuishie hapo. Lakini kuishi ujirani na mtu kama Amin ni kujitakia matatizo, maana huwezi jua next atakuja na nini. Nyerere alishafanya assessment ya na kujiridhisha kwamba Amini alikuwa anapigika tu na kwa msaada wa akina Museveni ambao walikuwa na contacts within Uganda. Kama Tanzania ingefanya kosa la kumwacha Idd Amin madarakani basi tungeendelea kuwa kwenye tension siku zote na kusubiri mpaka Mungu amchukue Amin na huwezi jua ni nani angefuata baada ya Amin.

Ni kweli Tanzania tulikumbwa na hali ngumu ya uchumi mwanzoni mwa miaka ya 80 na kuendelea, lakini it was a global crisis, hata US nao walikuwa recession miaka early 80s. Sema kwamba timing ya vita ilitokea kipindi kibaya ambacho kilikuwa pia ni cha recession worldwide. Je, Tanzania ingesubiri recession ipite ndipo ipigane vita au iende kukomboa ardhi yake iliyokuwa imechukuliwa na Amin?
 
Haya endeleeni kuwafundisha watoto wenu hayo..

Sisi tutawafundisha watoto wetu tunayofikiri ni sahihi

kuna tatizo wakuu..ya nini kutujazia habari, kama vile hakubaliki vile ndio maana mnajazana kumbembeleza watu watambue hicho mnachotetea..aargh
Topical, hakuna mtu anayekubembeleza aisee, hapo unakosea. Wewe kama hukubali asemayo mtoa mada huo ni muangalio wako na kwa upande wangu sina tatizo na hilo. Tunaishi kwenye zama za fikra huria, kwa hiyo unao uhuru wa kuwafundisha watoto wako kile unachokiona ni sahihi.

Kitu kimoja tukubaliane kama waTanzania, nacho ni kwamba mfarakano utokanao na tofauti za kidini hauna tija kwa taifa!
 
Back
Top Bottom