Mkuu Zing,
Nitakujibu kwa mfano. Kwanini Uchagani hasa nilipofika mie Marangu, mwika, Kibosho na Rombo kwa ujumla wana maendeleo sana (wamesoma, wana maji, wana umeme, wana barabara, wana mashule, wana majumba mazuri ya kulala in totality) lakini hamna vijiji vya ujamaa?
Ninge fanya vijiji vya ujamaa kulingana na mazingira. Isingekua swala la NGUVU. Ningeweka huduma kama ilivyo Kilimanjaro.
Ni hilo tu. Na kumbuka sipingi the concept napinga utekelezwaji wake.
Chunguza sana
Mkuu FP,
Hilo la kilimanjaro kutokuwa na vijiji vya ujamaa kuna mdau ameligusia bila shaka utakuwa umemuelewa. Na kwakuwa mpango wa vijiji vya ujamaa haukutekelezwa huko basi ni dhahiri kwamba pale palipoonekana pako vizuri kimiundombinu ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa jamii, serikali iliwaacha waendelee kuishi vivyo hivyo.
Ukitaka kuwatendea haki watanzania wenzako unapozungumzia maendeleo katika maeneo yaoi, unazungumzia kilimanjaro kuwa mbele kielimu, miundombinu, maji, umeme na nyumba nzuri, usisahau historia ya Tanganyika enzi za ukoloni. Utakubaliana nami kwamba wamisionari wa kikristo waliingia maeneo hayo mapema sana na wakawekeza kwa kujenga mashule na miundombinu mbalimbali.
Watoto wa kichaga wakapata nafasi ya kusoma na hivyo wakapata nafasi ya kuajiriwa na serikali ya kikoloni na hatimaye Tanganyika huru. Na kwakuwa walikuwa wamesoma vizuri bila shaka wakapata nafasi za kulitumikia taifa hili katika nafasi za ajira za serikali na mashirika ya umma, tena wakiwa wengi ukilinganisha na makabila mengine.
Katika mazingira hayo utaona kwamba walifanikiwa kujiletea maendeleo makubwa ya miundombinu, kielimu, kiuchumi, maji na makazi.
Kwa ujumla wake mpango wa vijiji vya ujamaa uliwasaidia wale wa jamii zilizokuwa zimetawanyika sana na watu wako mbali na huduma za msingi kama shule na hospitali.
Kwa mfano kwa mkoa wa Mara tulifaidika sana na mpango huo wa vijiji kwakuwa jamii zetu wengi ni wafugaji, wakulima na wavuvi. Huduma za afya na elimu zilikuwa zinapatikana kwa watu kutembea umbali mrefu sana kuzitafuta. Wazee wangu walikuwa wakitembea takribani kilometa 50 kuifikia hospitali lakini sasa tunatembea kilometa 5. Wazee wangu walikuwa wakitembea takribani kilometa 35 kuifikia shule, sisi tumetembea kilometa 4 kuifikia shule.
Kiujumla vijiji vya ujamaa vimetusaidia sana. Kuna wale wanaosema watu waliliwa na simba kwa sababu ya kupelekwa porini. Je wanafuatilia kuona ni wananchi wangapi bado wanaliwa na simba hadi leo hii tukiwa na miji mikubwa iliyojaa watu na miundombinu bora?
Nenda Doma-Mikumi hapo uone shughuli yake, nenda rombo huko, nenda lindi huko ruangwa, na maeneo mengine mengi vilio havijakwisha, simba wanaendelea kula watu!