Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Umeishia Darasa la ngapi chalii? Mbona unaji-contradict mwenyewe hapo kwenye red panakuhusu.

Ni bora yeye aliiga,bahati mbaya akafeli (in very minute percentage that can,t be defined).Mwinyi aliwaleta kutusaidia au Aliwauzia kabisa kila kitu-Loliondo gate ya Mwarabu toka UAE.Jakaya Kikwete Kapewa Suti katepeta anashindwa hata kuwakemea amebaki ndiyo mzee.IPTL,Richmond(alijua kila kitu kadiri ya Lowassa) hivyo aliwaleta watusaidie amethubutu,ameweza amesongeshwa mbele kuibomoa nchi.Muasisi wa Udini,matabaka,ubinafsi chako ni chako yaani laana mzuka!!!M

uislam Pekee na mbaye anamtambua Mwalimu kwa sababu Elimu na Taaluma yake sio-ya-kuchakachua ni Dr.wa ukeli Dr.Salim Ahmed Salim ambaye Mzee ruksa ali-trick akamzunguka aupate ukuu wa nchi,lakini hakuwa,asingekuwa na hatakuwa chaguo la watz kama JK,na ndio maana JK hataki mkumwita Baba wa Taifa Mwalimu. Na asipotubu dhambi alizomsingizia Dr.Salim nchi lazima impakate tu!!!!
Mkuu wangu,

Mie kijakazi wako nimeishia darasa la nne la zamani.
Samahani kama nimekukwaza kwa kujadiliana na wewe mwenye upeo mkubwa. Ila naomba usichoke kunisaidia kunifundisha mkuu wangu.

Nikisema China na Urusi nina maana nchi za kikomunisti au kwa lugha iliyozoeleka nchi ya kijamaa. Stalin alikuwa kiongozi wa Urusi (iliyoungana)

Nikisema angeleta wageni nina maana angeleta wageni kutoka magharibi (kwenye ubepari) maana mabepari ndio wanaweza kuendesha biashara yenye kuleta faida.

Mambo ya SAS na JK mie hayanihusu maana sio mada iliyopo mezani.

Nawasilisha mkuu wangu.

Ndimi,
 
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.
Hayo niliyategemea kutoka kwako na sivinginevyo, pole bi mkubwa!
 
Ukichunguza sana na kwa makini,wanaombeza na kusambaza chuki kwa Hayati baba wa Taifa hapa JF ni wale wapenzi wakubwa na watetezi wa CCM na utawala wa Awamu ya nne. Tujiulize kwa nini ni hivyo?
Lazima iko namna au ni mkakati maalum ambao haukuanzia JF ila una baraka toka juu.

Na kimsingi kuna dhana ambayo imesemwa sana na mie nimeishuhudia mara kadhaa..JK ni mzito kutamka Mwl kama baba wa Taifa,uwa anaishia kusema...mzee wetu,mwl,muasisi wa taifa hili nk...nadhani realy there is something wrong to this generation of JK and his government...na hawa akina Faizafoxy ni kama mbwa maana mfuga mbwa mwenyewe ndio chanzo cha tatizo....
 
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.

mzazi wako wa kiume huwa anaitwaje?
A. Baba B. Babu c. Sykes D. Mungu
Nadhani huwezi kosea maana hata yule mjukuu wako wa vidudu aweza jibu kwa usahihi!
 
Hivi kama patrice Lumbumba angechukua nchi na kuweka misingi ya kikomunisti nchini Zaire, kweli Lwambo na Lipua Lipua wangetamba barani africa?SI unajua wakomunistoi huondoa hati miliki za wanamuziki nakuwadhoofisha wanamuziki? Je zaire ingecheza world cup 1974 na kuchukua AFCON mwaka huo huo? Tazama nchi za kikomunisti zilivyo dolola kisoka mara baada ya kuuingiza ukomunisti nchini mwao. Ulaya mashariki yote, hamna hata nchi moja inayoweza kuifunga Ivory Cost, Ghana, Cameroon na Zambia.

Wazaire walijua kabisaa tokea zamani kuwa ukomunisti ni Unyama. Hivyo walimchinja Lumumba na kumtia mwili wake katika pipa la acid ayeyuke mpaka mifupa. halafu mpaka leo kaburi lake halijaonekana. Hapo waliwakomboa sana watu wenye vipaji vyao na kuajilika navyo kama vile kina Lwambo, DR Nico, Verkyis, Josky Kiambukuta, shaba kahamba na wengine wengi.

Nchi kama guine, ilikuwa taifa bora kwa soka hapa africa. Lakini mara baada ya kuingiza ukomunisti tuu, klabu yake ya Hafia iliyowahi kutwaa ubingwa wa africa mara nne iliporomoka vibaya sana. Soka la guine likafa na kukabakia makwaya na magwaride tuu.

Halafu lazima ukumbuke kuwa ukomunisti hapa africa, umeuwa watu wengi sana kuliko vita vya uhuru. Tazama walivyouana Angola, Msumbiji, Congo Brazavile na Ethiopia. ni ukweli kabisaa kuwa , shetani alitaka kuitawala dunia kwa kupitia sera za kinyama za kikomunisti. wazaire usiwalaumu kwa kumyonga Lumumba, hakuwa na tofauti na kina Boris Pugo-wa Urussi.

sasa hivi zaire ni taifa la tatu duniani , kwa kupeleka viaja wake kucheza soka la kulipwa ulaya mashariki na magharibi mpaka bara la america. Ya kwanza ni Brazil, na ya pili ni algentina.

Ukomunisti haujui kabisaa kulea vijana . Huwatumia viajan kuimba kwaya, kucheza gwaride na kuwapeleka mashambani kulima.

Hii haihusiani na thread iliyopo mbele yetu otherwise anzisha ya kwako inayojitegemea kama unataka coments. Naona umekurupuka ukastukia umeingia choo cha kile.
 
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.
So wewe mzazi wako wa kiume mwenzetu unamuita nani? Make huwezi kumuita baba kufanya hivo utakuwa unatukuza ukatoliki. Leo nimeona faida nyingine ya jamvi hili ni ; Yaani wenye akili na wajinga wanajileta wenyewe. Pole pole twaweza kujua taifa lina mbumbu wangapi. Long live JF
 
Hii imekaa vizuri sana na ni darasa zuri sana. Mbali na kuwa ni Rais wa kwanza wa Tanzania, mazuri ya Nyerere ukiamua kuyatafuta utayapata mengi sana, ukiamua kuyaandika utaandika na hata ukitaka kufundishia utapata mambo mengi sana ambayo yanaweza kutoa msingi mzuri kwa nchi yetu na Africa kwa Ujumla. Sidhani kama kuna kiongozi yeyote Africa aliyefanikiwa kwa kiasi cha Nyerere kuweza kuishi na kusimamia kile alichoamini ni bora kwa mwafrika. Ukitaka kuandika historia ya viongozi wengi utajikuja unaaandika historia binafsi, lakini historia ya Nyerere ni ya nchi, na Africa kwa ujumla.

Kulinganisha hili na mpira wa kulipwa au eti angechukua wakoloni tuliowaondoa ili waje kutuendeshea nchi ndio inaonyesha wanaokejeli ni wavivu wa kusoma hata yale uliyoandika hapo juu, ukiachilia mbali vyanzo vingine vya habari.
 
Ji habari reeeefu halisomeki, wala sina muda wa kulisoma, kwa kifupi:

Kama huu ungekuwa mkataba baina ya Tanzania na Mwekezaji, na wewe ukawa kiongozi wa nchi anayepaswa kuusani kwa niaba ya Watanzania, leo tungeanza kuibiwa, maana ungeusaini bila kusoma kwa sababu ni reeeeeeeeeefu. Afadhali Chief Mangungo alikuwa hajui kusoma aliposaini na Carl Peters. Leo watanzania wanajua kusoma, lakini wavivu wa kusoma mikataba yenye kurasa 50.
 
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.
Dada Mdogo FaizaFoxy (nasema hivyo kwa sababu nina uhakika mimi ni kaka yako mkubwa kiumri):-

1.Ni hivi karibuni nilikuwa Pakistan. Unapotua uwanja wa ndege Islamabad unakaribishwa na bango lisemalo "Welcome to the Islamic Republic of Pakistan". Lakini licha ya nchi hiyo kuwa ni ya mfumo wa kiislamu bado wanamuita kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo, Muhammad Ali Jinah, Baba wa Taifa "Baba-e-Qaum (بابائے قو&#1605😉".

2. Na sio Pakistan peke yake kati ya nchi za kiislamu ambako viongozi wamepewa wadhifa wa Baba wa Taifa. Kwa mfano Uturuki, Mustafa Kemal Atatürk (Atatürk = Great Father of the Turks). Sheikh Zayed bin Sultan Al Nahyan wa United Arab Emirates (والد الأمة = Waalid Alamat) na pia Ibn Saud of Saudi Arabia ( والد الأمة = Waalid Alam)

Kwa hiyo nadhani sio kila mada ni lazima uchangie kwa mtizamo wa kidini. Waswahili husema ujanja mwingi mbele giza!
 
Mkuu wangu,

Mie kijakazi wako nimeishia darasa la nne la zamani.
Samahani kama nimekukwaza kwa kujadiliana na wewe mwenye upeo mkubwa. Ila naomba usichoke kunisaidia kunifundisha mkuu wangu.

Nikisema China na Urusi nina maana nchi za kikomunisti au kwa lugha iliyozoeleka nchi ya kijamaa. Stalin alikuwa kiongozi wa Urusi (iliyoungana)

Nikisema angeleta wageni nina maana angeleta wageni kutoka magharibi (kwenye ubepari) maana mabepari ndio wanaweza kuendesha biashara yenye kuleta faida.

Mambo ya SAS na JK mie hayanihusu maana sio mada iliyopo mezani.

Nawasilisha mkuu wangu.

Ndimi

unaijua CHINA au unaisikia? ziulize hizo nchi za magharibi kuhusu China! ukipata jibu ndipo utaelewa kama tungewaiga mpaka leo hii tungekuwa wapi!!
 
Dada Mdogo FaizaFoxy (nasema hivyo kwa sababu nina uhakika mimi ni kaka yako mkubwa kiumri):-

1.Ni hivi karibuni nilikuwa Pakistan. Unapotua uwanja wa ndege Islamabad unakaribishwa na bango lisemalo "Welcome to the Islamic Republic of Pakistan". Lakini licha ya nchi hiyo kuwa ni ya mfumo wa kiislamu bado wanamuita kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo, Muhammad Ali Jinah, Baba wa Taifa "Baba-e-Qaum (بابائے قو&#1605😉".

2. Na sio Pakistan peke yake kati ya nchi za kiislamu ambako viongozi wamepewa wadhifa wa Baba wa Taifa. Kwa mfano Uturuki, Mustafa Kemal Atatürk (Atatürk = Great Father of the Turks). Sheikh Zayed bin Sultan Al Nahyan wa United Arab Emirates (والد الأمة = Waalid Alamat) na pia Ibn Saud of Saudi Arabia ( والد الأمة = Waalid Alam)

Kwa hiyo nadhani sio kila mada ni lazima uchangie kwa mtizamo wa kidini. Waswahili husema ujanja mwingi mbele giza!

well said!
 
Hadi sasa, wachangiaji wengi, zaidi ya asilimia 90 wanakubaliana na hoja kwamba heshima ya Baba wa taifa haina mwingine zaidi ya Mwalimu Nyerere; Kinachoendelea sana sana katika mjadala ni juu ya Ubora wa Sera zake, akifananishwa na marais waliomfuata. Katika mjadala wa namna hii, tusisahau kwamba Nyerere ni Rais pekee aliyeendesha uchumi kwa sera zilizoandaliwa na watanzania wa ajili ya Maendeleo ya watanzania. Sera ya Ujamaa na Kujitemea zilikuwa home grown, hazikuwa za kushinikizwa na mataifa au taasisi za nje.

Kuanzia mwaka 1985 alipochukua nchi Mwinyi, Marais wote wamekuwa wanatekeleza Sera na Maamuzi ya WorldBank, WTO, IMF, kama mashatri ya kupata misaada; Wakubwa wa OECD countries wamewapa hawa mapacha watatu dhamana ya kusimamia interest zao, that's how ukoloni mamboleo is working at present. Kwahiyo hawa mapacha watatu wakati wote, kwa kupitia misaada na mikopo yao, wanashinikiza kwa nchi maskini, sera ambazo zitawanufaisha OECD countries, sana sana kwenye sekta za madini, mafuta na mazao ya kilimo (sio ya chakula). Pia misaada yote na fedha zote wanazotoa wanataka ziende kwenye sekta ambazo zinafanya uchumi wetu uwe efficient for exports, mfano miradi ya barabara, lengo sio ili kijiji A na B viweze kufanya commerce kirahisi zaidi au kuwa na mawasiliano bora zaidi, bali kuongeza efficiency in terms of movement of cash crops na madini, from mikoani, kuja bandarini DSM for exports. Nia ya wakubwa hawa is to make sure that Sub Saharan Africa remains the rural back yard for Europe and North America. Bajeti zetu miaka yote zinapitiwa na kuhakikiwa na wakubwa hawa, wao ndio wanaamua nini iwe priority kwa mwaka ujao wa fedha. Huwa wanaamua iwe elimu, Kilimo, Miundombinu, etc ka jinsi wanavyotaka. Ushahidi huu upo hate kwenye tafit mbali mbali - google ‘Aid conditionality' to poor countries.

Kwa miaka kadhaa sasa, wakubwa hawa wamerudisha mambo mengi ya Mwalimu baada ya kuwa criticized sana juu ya sera zao ambzo zimemfanya mtanzania kuwa maskini zaidi. Mfano wanajitahidi sana kurudishia serikali maamuzi juu ya kuwekeza kwenye elimu – e.g; shule za kata sio ubunifu wetu, sisi ni watekelezaji.

Kwahiyo tumpime Nyerere kama Rais mwelekezaji dhidi ya Rais Mwinyi, Mkapa, na Kikwete kama marais watekelezaji. Hata kama mwaka 1985 asingekuwa Mwinyi Rais bali Amina, Peter, Rashidi, au veronica, Rais huyu angeitwa jina lile lile Mzee "RUKSA" kama angekuwa Peter au Rashidi; au Mama "RUKSA" kama angekuwa Amina au Veronika.
 
unaijua CHINA au unaisikia? ziulize hizo nchi za magharibi kuhusu China! ukipata jibu ndipo utaelewa kama tungewaiga mpaka leo hii tungekuwa wapi!!

Tungewaiga kivipi na tungekuwa wapi kivipi? maamuzi ya nchi gani iwe tajiri, ipi ibakia maskini sio ya taifa kujiamulia kienyeji - China wamelazimisha kwa sababu ya kuwa na mabomu ya Nuclear kwahiyo wanayatumia as a deterrent na wana bahati sana katika kipindi chote hicho waliwekeza katika sayansi na teknolojia kwa watu wake, sio kama North Korea;

Nchi kama South Korea, Malaysia, Singapore, wanasiasa wetu wanapotosha sana watanzania kwa kusema kwamba tulikuwa sawa, wao wameendelea; Pia mataifa makubwa yanapenda kutumia uongo huu ili na sisi tuone kwamba tukifuata maelekezo yao tutafika kule; Ni kweli hizi nchi zilikuwa sawa kimaendeleo kama Tanzania lakini kilichofanya ziendelee ni guided capitalism ya US, UK, France...wakati wa cold war; walimwagiwa fedha nyingi kupita kiasi ili kuwafanya waone Soviet sio lolote bali marekani kimaendeleo; Marekani aliogopa sana nchi hizi kuangukia upande wa Soviet; Mafanikio ya Hizi nchi yalitokana na serikali na bureucrats kujiingiza katika state entreprenuership; ila na wao walikuwa na akili ya kuwekeza kwenye elimu, sayansi na teknolojia kwa kutumia mabilioni yale ya fedha; Katika Africa, hatukuwa na bahati hiyo ya kuwa protected away from the Soviet; kazi hiyo kwa kiasi fulani aliachiwa kaburu; ila kuna nchi moja ambayo ingeamua ingekuwa mbali sana leo - ZAIRE - hawa walipewa kila kitu na west kwa mtindo ule ule wa South Korea, Zaire ilikua the main playground ya Ubepari VS ukomunisti, lakini Mobutu hakutumia nafasi ile;
 
Hii imekaa vizuri sana na ni darasa zuri sana. Mbali na kuwa ni Rais wa kwanza wa Tanzania, mazuri ya Nyerere ukiamua kuyatafuta utayapata mengi sana, ukiamua kuyaandika utaandika na hata ukitaka kufundishia utapata mambo mengi sana ambayo yanaweza kutoa msingi mzuri kwa nchi yetu na Africa kwa Ujumla. Sidhani kama kuna kiongozi yeyote Africa aliyefanikiwa kwa kiasi cha Nyerere kuweza kuishi na kusimamia kile alichoamini ni bora kwa mwafrika. Ukitaka kuandika historia ya viongozi wengi utajikuja unaaandika historia binafsi, lakini historia ya Nyerere ni ya nchi, na Africa kwa ujumla.

Kulinganisha hili na mpira wa kulipwa au eti angechukua wakoloni tuliowaondoa ili waje kutuendeshea nchi ndio inaonyesha wanaokejeli ni wavivu wa kusoma hata yale uliyoandika hapo juu, ukiachilia mbali vyanzo vingine vya habari.

Brilliant point.
 
..........................
Heshima ya Baba wa taifa inatambulika na bunge la nchi husika kwa mujibu wa Sheria, kwa kuzingatia kwamba bunge ndio chombo cha kuwakilisha maoni ya wengi. Heshima ya Baba wa taifa haina mahusiano yoyote na kitabu chochote kitakatifu (Quran au Biblia) hasa ukizingatia kwamba serikali nyingi, kikatiba, hazina dini. Ni muhimu tutambue kwamba, katika historia ya dunia, haijawahi kutokea hali ya kwa taifa lolote huru kuingia katika mzozo juu ya nani anastahili heshima ya kuwa Baba wa Taifa, kwa sababu, kama tulivyokwisha ona asili ya heshima hii ni hali ya mwananchi mmoja kujitoa mhanga kuongoza wengi katika harakati za ukombozi. Vilevile, hakujawahi kutokea mjadala unahusu Baba wa Taifa, katika taifa lolote huru duniani, unaligawa taifa kwa misingi ya kidini, kikabila, au itikadi ya siasa, pia kwa sababu, kama tulivyoona, ubaguzi wa aina yoyote ndicho kiini cha mapambano ya uhuru au ukombozi. Mjadala wa namna hii umejitokeza Tanzania, ambapo hata wenzetu wa Kenya ambao, kihistoria wamegawanyika sana kama taifa kikabila, bado hawatofautiani juu ya Baba wao wa Taifa Mzee Kenyatta. .......
Tuingie kwenye hoja ya pili inayohoji uhalali wa Mwalimu Nyerere kuwa Baba wa Taifa katika Muungano:

- JE WENYE HOJA ZA KUMKEJELI BABA WA TAIFA WANAJIFUNZA NINI?

- USHAURI KWA WAFITINI WA BABA WA TAIFA

· Ubaba wa taifa sio Mapenzi ya mtu mmoja mmoja aidha kwa kutumwa au kwa juhudi binafsi bali ni heshima kwa mujibu wa sheria kama tulivyokwisha ona. ....

..........................................

Mungu amrehemu Baba Wetu wa Taifa, Mwalimu Julius Kambaraga Nyerere.

Mungu Ibariki Tanzania.

Mkuu ungepenyezea Mkuu wa Kaya habari hii wakati wa sherehe za uhuru wa Tanzania Bara/Tanganyika juzi 9/12/2011. Ingependeza kweli.

Vinginevyo, naunga mkono hoja.
 
hakika wewe ni great thinker!
sasa ngoja tusubiri mitazamo ya kina FF,RITZ,MS,REJAO ili tujue nao wana maoni gani
Nilikuwa najiuliza ni nini chimbuko la hii tabia iliyoanzan siku hizi za karibuni ya kumchafua Mwl. J.K. Nyerere. Sasa nimeanza kuelewa kidogo na itakuwa vizuri kufuatilia na kujua hao wanaofanya hivyo wanafanya kwa sababu gani na kwa faida ya nani hapo baadae. Hii campaign itagonga mwamba tu kwa sababu huwezi kujisafisha mwenyewe wakati wewe u mchafu kwa kutaka kumpaka mwingine matope.
 
Mchambuzi,
Sasa kama mpo mnaoelewa kinachoendelea kwa kiwango kikubwa namna hii, kwa nini mko kimya? Hayo unayosema ni maelekezo toka nje watawala wetu wanayaorodhesha kama mafanikio kila uchao na wanataka tuamini hivo. Ingieni angalau Bungeni mpaze sauti huko zenye kuleta tija na mabadiliko ya maana.
Badala yake wasomi kama akina Zitto wanajielekeza kwenye mambo ya kuwapa umaarufu wa haraka kama posho. Bunge lijalo la January nadhani watajadili ndoa za jinsia moja!
 
Mchambuzi, nimekuvulia kofia. Kuna swali ningeomba yeyote mwenye kujua anisaidie: Kuna kazi fulani tulikuwa tunafanya wiki chache zilizopita, kuna point tulilazimika kupata kanda za taarifa za habari na magazeti ya miaka ya '70 na 80. Baada ya kumaliza navyo, nilitaka kupitia karibu kila kitu katika magazeti na taarifa hizo, pamoja na mengine mara kwa mara unasikia/soma kitu kama hiki...'Rais wa JMT amemstaafisha kwa manufaa ya umma aliyekuwa meneja/mkurugenzi wa .....' Je hii ina uhusiano wowote na hiyo inayosemwa kuwa walioharibu hawakuchukuliwa hatua?! Mzee mmoja ameniambia kuwa huko kustaafishwa kwa manufaa ya umma kuliwakumba wengi.
 
Wakuu WildCard na Mchambuzi,

Baba wa Taifa alikuwa HAAMBILIKI. Vijiji vingi ya Singida na Dodoma unavyoongelea ni vya UJAMAA na ndivyo vimekufa. Kwenda vijiji vya ujamaa kulifanywa bila tahmini na research ya kutosha. Mwalimu aliiga kila kitu Urusi na China bila ku LOCALIZE.

.
FP
Ukitazama mantik nzima ya vijiji vya ujamaa iikuwa nzuri na inasimama mpaka leo. Lakini kuna baadhi ya maeneo kulingana na utaratibu wao maisha.( eg ufugaji 100%) hawakuwa na utamaduni wa settle. So hilo iuwa ni tatizo moja Lakini failure ya vijiji vya ujamaa sehemu chache haiwezi kufunika sucess ya vijiji vya ujamaaa sehemu kubwa ya Tanzania

Unapokuwa na uhaba wa resoruces (wich is always the case) lazima kuna kitu kifanyike (organisation) Sasa kama unalaumu vijiji vya ujamaa ebu fafanu ungefanya nini wakati cha tofauti japo kuweka shule mbili za primary kwenye jamii zilizotawanyika.
 
Back
Top Bottom