bwana mchambuzi, kwanza naomba nikupongeze kwa kuwa muungwana, kwa kukiri pale ulipokosea, hivi ndivyo kijiwe chetu cha jf kinavyotakiwa kiwe!. Ni vyema next time ukaja na facts badala ya passion na emotion, wengi tunamkubali mwalimu lakini tunataka ifahamike wazi kwamba historia ya tanzania nyuma yake wapo watu wengi na wala siyo one man show.
Hata hivyo, kutamkwa kwa jina "baba" wa taifa ndani ya bunge bila kipingamizi haimaanishi nguvu ya kisheria ya jina hilo, au jambo hilo!. Bungeni kuna taratibu mbalimbali za kufuata ili kulipa jambo nguvu za kikanuni/kisheria.
Kwa mantiki hiyo basi, nasema kwamba tanzania tuna "mababa"/ mama wa taifa wengi, mwalimu akiwa mmojawapo, wengine miongoni mwao ni kama mzee karume, kawawa, wale 17 aliowataja jk, na wale waadilifu waliofanya kazi ya kusimika misingi ya taifa letu kama sokoine etc.
Hawa ndiyo founding fathers/ fathers of the nation.