Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Hayo hayanipi shida wanaomwita hilo jina hawaujui Uislaam. Mimi kumuita mtu baba asiyenizaa ni NO. Na nnauhakika ni wengi wengine walio kama mimi.
Huyu cha-ukorofi nadhani mngeishia nae hapa, kubishana nae kwa tafsiri yake ya baba ni sawa na kupigia mbuzi gita. Maana yeye ana tafsiri yake ambayo aipo universal bali ya imani yake tu bila ya kujali wengine awaoni hivyo si ki imani tu bali hata kialisia. Ni sawasa na kumwambia nyama ambayo ajachinja muislam ni kitoweo, unajuwa wazi faiza atakataa hilo na kuita kibudu tu hicho na sababu zake zitakuwa ndio hizi za ki-minority. Wakati realistically dunia karibu yote itaita kitoweo na watu wadini zote isipokuwa yake. Ni ushauri wa bure.

Lakini hili si kusema kwamba nakubaliana kiii hivyo na sifa ulizo mmwagia huyo JKN hapa na kutaka kutuaminisha amna kama yeye. Wakati kuna ushahidi wa kutosha kwamba jamaa kafeli vibaya sana kama kiongozi na alikuwa alipwaya sana huo ndio ukweli. Nitarudi kupengua vizuri hoja yako kuu baadae yenye vitu kibao ulivyotubambikia wasomaji kutaka kumpa Mwalimu sifa asizo stahili kabisa.
 
Hayo hayanipi shida wanaomwita hilo jina hawaujui Uislaam. Mimi kumuita mtu baba asiyenizaa ni NO. Na nnauhakika ni wengi wengine walio kama mimi.
Kumbe watu wanapoteza muda kukubishia wakati huo ni msimamo wako binafsi? FF wewe mwite utakavyo, kwa vile hakukuzaa waweza mwita Kaka wa Taifa, mjomba wa Taifa au hata sheikh (mzee kwa tafsiri yako) wa Taifa.
Ili mradi moyo wako upate burudani

 
Hizi salamu murua kwa wafitini, wazandiki na waongo kama FF. Ni zawadi safi kwa sikukuu ya Krimas na Mwaka mpya. Baada ya kufanya disucussin na FF NA ku-analyze majibu yaKE nachoweza kusema ni KUWA FF ni mweupe pe kichwani kwake na anatakiwa kufanyiwa matibabu ya kichwa, hayuko sawa, hayupo consistent, haelewa anacho-argue, ni kama kinyonga na kigeugeu. Kwa sababu ya tatizo la kiakili alilo lano anaona sawa kujaribu kuonyesha kuwa binadamu ni yule aliyekatika dini yako wengine siyo binadamu. Bahati mbaya sana akili yake haiendani na mazingira ya nchi yetu kwa vile watu wameingiliana sana wa dini tofauti na makabila tofauti na wanasaidiana bila kujali dini. Hata wanaoana bila kujali dini ilimradi wamependana watu wanaoana.
 
Riwaichii na Rais ni wapi na wapi?, sema hakuna neno lingine mbadala ndio mkalizuwa hilo kuwa ni Rais. Rais ni neno la Kiarabu "Ra'yes" sasa usitake kutuaminisha kuwa Kiswahili kina maneno ya Kiroma, lakini kuwa kina maneno Kiarabu sina haja hata ya kukupa darsa kwa hilo, hata neno Swahili lenyewe ni Kiarabu. Hilo Ruwaichii kikabila gani hicho kichina? ukweli ni kuwa sijawahi kulisikia leo ndio mara ya kwanza. Na usitake kulibadili kwani watu wa kanisa mmezowea kubadili majina.

Wala likiwepo halina tatizo kwani ma Rais ni wengii tu wapo hata makampuni, Lakini baba hilo ni kanisani tu na baba yangu mzazi. Maana kanisani kuna ma baba ambao hata kuzaa hawaruhusiwi.

Dada Faiza, naomba nikukumbushe jambo moja tu, katika lugha..hakuna lugha isiyokopa maneno ya lugha zingine. Kiingereza kimekopa maneno ya ki-Yunani karibia 15% Kiingereza kimekopa maneno ya Kijarumani karibia 12% Sasa Kisuahili hakiwezi kuona aibu kukopa maneno ya ki-Arab, ukizingatia kamba ndefu inayotuunganisha katika historia. Hilo si ajabu sana dada. Hata wa-Arab wenyewe wana maneno yanayoshabihiana na ki-Ebrania, wala hawawezi kudai hilo neno msilitumie kwenye shughuli za masinagogi yenu...

Dini na lugha, dini na historia, dini na uchumi? Hii ni Tanzania au Tanganyika yetu sote, au ?
 
Ji habari reeeefu halisomeki, wala sina muda wa kulisoma, kwa kifupi:

Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga

KWELI SASA NIMEAMINI fAIZAFOXY NI JK! MTANZANIA PEKEE ASIYEMPENDA WALA KUMUHESHIMU MWALIMU NYERERE!
 
  1. Kenya – Jommo Kenyatta – natumaini sote tupo pamoja katika hili;
Moi nakumbuka alijaribu hiyo ya kutaka kuwa baba wa Taifa...
 
Hivi kama patrice Lumbumba angechukua nchi na kuweka misingi ya kikomunisti nchini Zaire, kweli Lwambo na Lipua Lipua wangetamba barani africa?SI unajua wakomunistoi huondoa hati miliki za wanamuziki nakuwadhoofisha wanamuziki? Je zaire ingecheza world cup 1974 na kuchukua AFCON mwaka huo huo? Tazama nchi za kikomunisti zilivyo dolola kisoka mara baada ya kuuingiza ukomunisti nchini mwao. Ulaya mashariki yote, hamna hata nchi moja inayoweza kuifunga Ivory Cost, Ghana, Cameroon na Zambia.

Wazaire walijua kabisaa tokea zamani kuwa ukomunisti ni Unyama. Hivyo walimchinja Lumumba na kumtia mwili wake katika pipa la acid ayeyuke mpaka mifupa. halafu mpaka leo kaburi lake halijaonekana. Hapo waliwakomboa sana watu wenye vipaji vyao na kuajilika navyo kama vile kina Lwambo, DR Nico, Verkyis, Josky Kiambukuta, shaba kahamba na wengine wengi.

Nchi kama guine, ilikuwa taifa bora kwa soka hapa africa. Lakini mara baada ya kuingiza ukomunisti tuu, klabu yake ya Hafia iliyowahi kutwaa ubingwa wa africa mara nne iliporomoka vibaya sana. Soka la guine likafa na kukabakia makwaya na magwaride tuu.

Halafu lazima ukumbuke kuwa ukomunisti hapa africa, umeuwa watu wengi sana kuliko vita vya uhuru. Tazama walivyouana Angola, Msumbiji, Congo Brazavile na Ethiopia. ni ukweli kabisaa kuwa , shetani alitaka kuitawala dunia kwa kupitia sera za kinyama za kikomunisti. wazaire usiwalaumu kwa kumyonga Lumumba, hakuwa na tofauti na kina Boris Pugo-wa Urussi.

sasa hivi zaire ni taifa la tatu duniani , kwa kupeleka viaja wake kucheza soka la kulipwa ulaya mashariki na magharibi mpaka bara la america. Ya kwanza ni Brazil, na ya pili ni algentina.

Ukomunisti haujui kabisaa kulea vijana . Huwatumia viajan kuimba kwaya, kucheza gwaride na kuwapeleka mashambani kulima.

Haya ni maneno ya mtu aliyechanganyikiwa. Bila shaka siku zaenda mbio, na muda wako wa kuendelea kufaidi mali ndani ya uvivu wako unazidi kuyoyoma. Bado miaka minne........
 
bwana Mchambuzi wewe unasema mimi nakwepa hoja yako, mbona unakuwa msahaulifu mimi nasimamia ndani ya hoja yako ile ile, ulipotamka wazi tofauti kati ya heshima ya "baba wa Taifa " na "Raisi bora" ukasema wazi kwamba "Ubaba wa Taifa" ni jambo la kisheria, NIKAKUOMBA ULETE HIYO SHERIA ILI BASI TUPROVE KWAMBA MWALIMU NYERERE NI "BABA" WA TAIFA KWA MUJIBU WA SHERIA BADO HUJAILETA HAPA JAMVINI.

Sasa basi unaposema kwamba Bunge limeridhia Nyerere kuitwa baba wa Taifa kati ya mwaka 2003 na 2005, basi maana yake mwaka 2002 kurudi nyuma hakuwa baba wa Taifa, UNLESS OTHERWISE UBADIRISHE USEMI WAKO KWAMBA "UBABA" WA TAIFA NI HESHIMA YA KISHERIA.

NDIYO MAANA NI MUHIMU SANA UKATULETEA SHERIA INAYOMTAMBUA NYERERE KAMA BABA WA TAIFA, LA SIVYO HILI LITAENDELEA KUWA NI MAONI YA MTU MMOJA MMOJA.

sasa wewe unataka kujua maoni yangu kuhusu "Ubaba wa Taifa", maoni yangu ni haya yaafuatayo.
(1) WAASISI WOTE WA TAIFA LETU WENYE MCHANGO MZITO , KAMA NI WA KIUME BASI NI MABABA WA TAIFA, NA WA KIKE NI MAMA WA TAIFA.
(2) UBABA WA TAIFA SIYO LAZIMA UWE RAISI WA KWANZA, KUWA RAISI NI MGAWANYO WA KAZI TU, LAKINI MTU YEYOTE ALIYEFANYA JUHUDI KUBWA ZA KULINUFAISHA TAIFA ZIMA WAKATI ULE WA UASISI WA TAIFA LETU BASI NI BABA WA TAIFA, KWA MAANA HIYO MTU KAMA KAWAWA NA KARUME SENIOR NINAWAONA KAMA MABABA WA TAIFA.
(3) NYERERE NINAMUONA PIA KAMA BABA WA TAIFA
(4) MPAKA MIAKA TAKRIBAN 30 HIVI YA UCHANGA WA TAIFA, NACHUKULIA KAMA MWENDLEZO WA UASISI KWA HIYO MTU YEYOTE ATAKAYETUMIKIA TAIFA KWA UADILIFU MKUBWA NA KUWA KATIKA NAFASI YA MAAMUZI MAZITO YA UMMA NA KUFANYA VYEMA BASI NI BABA WA TAIFA, KWA MAANA HII NAMUONA SOKOINE KAMA BABA WA TAIFA, NAMUONA ALHAJI MWINYI KAMA BABA WA TAIFA.

KWA NINI NYERERE HAWEZI KUWA BABA WA TAIFA PEKE YAKE?
(1) TANZANIA IMEUNDWA NA NCHI MBILI HURU ZANZIBAR NA TANGANYIKA, NYERERE SI MUASISI PEKE YAKE, YUPO MZEE KARUME, KAMA HOJA NI UASISI WA TANZANIA BASI NDO AWE BABA WA TAIFA BASI NA MZEE KARUME ANASTAHILI AWE BABA WA TAIFA

(2) KAMA NI SUALA LA UTENDAJI KAZI KIPINDI CHA UTAWALA WAKE BASI TUMEONA KASORO NYINGI SANA ZA UTENDAJI WAKE WA KAZI SITAKI KUZIRUDIA( KUNA MADA MAALUM KABISA YA HILO HAPA JF).

(3) KAMA TUKIKUBALI KWAMBA ZANZIBAR WANA MTU WAO WANAYESTAHILI KUMUITA BABA WA TAIFA, BASI NYERERE HAWEZI KUWA BABA WA TAIFA PEKE YAKE MAANA TAYARI UPANDE MMOJA WA MUUNGANO TAYARI UNA MTU AMBAYE ASHAPEWA HESHIMA HIYO.

Kwa haraka haraka, kwani sina mud asana, nadhani sasa nimekuelewa. Mbali ya wewe kusubiri nilete taarifa za bunge kuridhia heshima hii kwa Mwalimu, msimamo wako juu ya hii mada ni kama ifuatavyo:

a)Baba wa taifa sio lazima atokane na mchango wake kama kiongozi wa harakati za mapambano dhidi ya ukombozi au uhuru wa taifa husika; badala yake anaweza kuwa mtu mwingine yoyote ambae hata hakushiriki harakati hizo (mfano umemtaja Sokoine);

* Hili nilishalieleza kwenye my original post - kuhusu mchakato wa mtu kupitia before he's conferred with such a title; and this was based on the global view ambayo ni standard kwa nchi zote, na ndio maana kimataifa Mwalimu anatambulika hivyo; Kama hoja yako hapa ni kukataa kupangiwa views kama taifa (Tanzania) juu ya nani anastahili na nani hastahili na badala yake kila taifa liwe na vigezo vyake, huo ni mjadala mzuri, lakini hapa sio mahali pake; mjadala wa hapa ni je, wenzetu Afrika, Asia etc, wanatumai vigezo gani? Na nikaelezea kwamba kwa maana hiyo, hata sisi Nyerere ni Baba wa taifa; vinginevyo mjadala huu unaweza kwenda out of hand na tukaanza kuulizana kama Nyerere alikuwa na jeraha lolote la risasi Vis-a-Vis mwanaharakati mwenzake kupoteza mguu kabisa; the global view doesn't detail such; vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa JKN ndie baba wa taifa;

b) Mtazamo wako wa pili: Nyerere sio Baba wa Taifa la Tanzania hata tukiamua kuiweka Zanzibar pembeni kwa dakika moja (nasema hivi kwa sababu umemtaja Sokoine);

* Hoja yako ya msingi hapa ni kwamba wapo watu wengine wanaostahili kupewa heshima hiyo kutokana na mchango wao katika taifa hili; hili nimeshalisema hapo juu na pia katika my original post; Otherwise kwa hoja hii, you are challenging the current global consensus on what establishes mtu kuitwa baba wa taifa; Mtazamo kwamba Sokoine, which means basi hata majina kama Msekwa, Msuya, kwamba wanastahili, can be very stimulating intellectually; ningependa kwa wakati mwingine kuingia katika mjadala huu kwani najua nitajifunza mengi; pia inaweza kuleta mabadiliko ya kifikra na kimtazamo kuhusu dhana nzima ya baba wa taifa, iwapo utalipanga in a good research context, and convince mabadiliko hayo kitaifa au hata kimataifa; Vinginevyo mpaka hilo litokee, mawazo yako nitaendelea kuyaheshimu juu ya Sokoine kustahili, lakini huku nikiendelea kuamini kwamba Mwalimu bado ni baba wa Baba wa taifa, kutokana na qualifications which have been already established in a global sense, hence emulated hapa kwetu; vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa JKN ndie baba wa taifa;

c) Mtazamo wako wa tatu ni kwamba Nyerere sio baba wa taifa hata katika mazingira ya Muungano (kwani umetoa hoja juu ya umuhimu wa Karume);

* Hili nilishalijibu katika hoja yangu ya msingi, ni kiasi cha wewe tu kurejea sehemu nayozungumzia Ubaba wa taifa na Muungano ambapo nilitoa mifano ya George Washington kama Muasisi wa Muungano wa Marekani uliokuwa na mataifa 16 tu (sio 50 ya leo); baadae muungano ukavunjika kwa miaka mitano, na uliporudi ukarudi na mataifa mengine mengi zaidi na kuzaa USA tofauti kabisa leo hii (50 states), na kwamba ingawa yote haya yalitokea akiwa hayupo, bado akapewa heshima hiyo; pia nikaeleza jinsi gani muungano wetu unachukua sura ile ile, mfano nikataja Tume ya Mark Bomani vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa JKN ndie baba wa taifa;

d) Mtazamo wako wa Nne ni kwamba Baba wa taifa sio lazima awe Rais wa kwanza wa Jamhuri huru;
* Hili nililielezea katika my original post kwamba sio lazima, ingawa mara nyingi waliendelea na hatua ya kuwa Marais wa kwanza wa Jamhuri huru husika; na kwamba kikubwa kuhusu baba wa taifa ni uongozi wake katika mapambano ya ukombozi kwa taifa husika; vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa JKN ndie baba wa taifa;

e)Mtazamo wako wa tano ni kwamba hauna tatizo na neno BABA WA TAIFA kwa misingi ya dini;

* Hata kama ungekuwa na tatizo na hili, nilishalisemea kwamba naheshimu sana mtazamo huu kwani hakuna BABA katika Uislam. Nikashauri kwamba ni muhimu tufikie consensus on a term ambayo itakidhi mahitaji ya pande zote za jamii, as long as wana msimamo mmoja juu ya heshima hiyo kwa Nyerere; lakini kama hata katika hilo hakuna consensus, ofcurse kila mtu yupo huru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa JKN ndie baba wa taifa;

f) Mtazamo wako wa sita/mchango wako tuseme, hautoi hisia zozote kwamba Tanzania tunahitaji mapinduzi mapya ili kumpata baba wa taifa;

* Hii inatokana na hoja yako kwamba wapo tayari watu wanaostahili kuitwa baba wa taifa, lakini sio Nyerere. Mjadala huu nao ni very stimulating kwani pia una challenge the current consensus kwamba baba wa taifa is inherent na harakati za ukombozi/uhuru; hili tumeshaliongelea hapo juu; vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa JKN ndie baba wa taifa;

g) Mtazamo wako wa saba/mchango wako unatoa hisi kwamba Historia iliyopo ya taifa letu inatosha kutuzalia baba wa taifa mwingine kwa kutengua heshima wa baba wa taifa aliyepo, Nyerere ili apewe mtu mwingine ambae anastahili zaidi;

* Hii nayo ina challenge the current global consensus jinsi gani baba wa taifa anapatikana; ni hoja yenye mchanganyo sana, vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa JKN ndie baba wa taifa;

h) Mtazamo wako wa nane, Nyerere hastaili kuwa Baba wa taifa kutokana na mapungufu yake kiutendaji;

Hili nilishalizungumzia katika my original post nilipo ongelea mapungufu ya George Washington na wengine katika utawala wao; mfano, tofauti na Nyerere ambae angalau aliruhusu demokrasia ya chama kimoja, marekani haikuwa na chama chochote cha siasa chini ya baba wao wa taifa, George Washington; pia mchakato wa katiba mpya ya taifa la Marekani ulifanywa kwa njia zisizo za kidemokrasia kwani ilikuwa ni Washington na kikundi kidogo sana cha wanajeshi na wanasiasa; na katiba hiyo ilihusu mataifa 13 tu, na baadae wakati wa utawala wake, amendmentz zikafanywa kuruhusu mataifa mengine matatu; akafariki na katiba juu ya mataifa 16 (sio 50 ya leo) lakini bado akawa baba wa taifa; vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge vigezo vilivyopo kuhusu baba wataifa, san asana iwapo suala la utendaji liwe featured; na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa JKN ndie baba wa taifa;

h) Na mtazamo wako wa tisa, Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzani, mbali na kutamka kutakuwa na Rais wa TZ na wa Zanzibar, haitambua heshima ya baba wa taifa.

Mimi sikusema chochote juu ya katiba, hapo unajichanganya, nimesema heshima hii inatambulika na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuomba unipe muda nije na taarifa kamili;

Nipo safarini mkoa kidogo lakini nina access ya internet from time to time, ntajitahidi kujibu hoja zako as much as I can;
 
Nyerere alikabidhiwa hii nchi, watu wameshikana, kusini mpa kaskazini, mashariki mpaka magharibi, hakuna ugomvi wala vita. hakuna asiyemkaribisha mwenzake. Tulikuwa hata tukifuturu mwezi wa Ramadhani tunatandika nje na kila apitae, ahlan wa sahlan, hakuna anaebaguliwa. Lakni alipoingia yule mzee, hata hicho chakula kilikuwepo tena?

Hakuna aliloongozea Nyerere sanasana kaharibu tu. Na sasa mnataka kutubambikia cheo cha kikatoliki? simply NO.

Na Mwl. Nyerere ameondoka tukiwa tumeshikamana, haya yanayojitokeza sasa hivi ni umsikini uliokithiri kwa watanzania; mpaka Mwl. Nyerere anaondoka madarakani waislamu ilikuwa hatushundwi na futari, waislmu tulikuwa tunakula futari hadi 5 yote ile ilikuwa neema ndio sababu tulikuwa tunakaribishana; hivi maharage yamekuwa anasa utamkaribisha jirani? Waislamu Ramadhani iliyopita wamefunga kwa tabu sana; sijui unatumia tathmini gani Ramdhani za wakati wa Mwl. Nyerere nilikuwapo na wakati huu naziona siwezi kuzifananisha hata kidogo. Ikiwa Mwl. Nyerere aliharibu mbona hakuna linalotengamaa hadi sasa?

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Mi nashauri mkubaliane kutokukubaliana. Mwandishi ameelezea utofauti kati ya Baba na Rais bora wa Taifa,kila mtu ameelewa,labda kama mtu hakubali. Halafu ameonyesha kuwa asili ya ubaba wa taifa ama jina hilo haikutokea kanisa katoliki wala si Roma wanaotoa jina hilo kwa viongozi wa nchi hapa duniani,iwe za kiislamu au kikristo. Hata hatukuwahi kusikia aliyetoa jina hilo alikuwa kardinali Rugambwa au Pengo! Mi nadhani imechukuliwa kifamilia zaidi kwamba...kiongozi wa familia huwa ni mwanamume. Na kwa bahati ni kwamba wanaharakati wengi katika ukombozi na mapinduzi ya nchi zao,walikuwa wanaume... Kifamilia kuna mambo ambayo hayakamiliki hadi baba aje.. Heshima ya ubaba,ni kuonesha uongozi,msimamo,ujasiri,vision,na maamuzi ambayo hata kama yatapingwa na watoto au wake zake,ya baba yanakuwa ya mwisho.. Someone can correct me ila huo ndiyo ufahamu wangu.

Hii ikoje
 
kwa haraka haraka, kwani sina mud asana, nadhani sasa nimekuelewa. Mbali ya wewe kusubiri nilete taarifa za bunge kuridhia heshima hii kwa mwalimu, msimamo wako juu ya hii mada ni kama ifuatavyo:

a)baba wa taifa sio lazima atokane na mchango wake kama kiongozi wa harakati za mapambano dhidi ya ukombozi au uhuru wa taifa husika; badala yake anaweza kuwa mtu mwingine yoyote ambae hata hakushiriki harakati hizo (mfano umemtaja sokoine);

* hili nilishalieleza kwenye my original post - kuhusu mchakato wa mtu kupitia before he’s conferred with such a title; and this was based on the global view ambayo ni standard kwa nchi zote, na ndio maana kimataifa mwalimu anatambulika hivyo; kama hoja yako hapa ni kukataa kupangiwa views kama taifa (tanzania) juu ya nani anastahili na nani hastahili na badala yake kila taifa liwe na vigezo vyake, huo ni mjadala mzuri, lakini hapa sio mahali pake; mjadala wa hapa ni je, wenzetu afrika, asia etc, wanatumai vigezo gani? Na nikaelezea kwamba kwa maana hiyo, hata sisi nyerere ni baba wa taifa; vinginevyo mjadala huu unaweza kwenda out of hand na tukaanza kuulizana kama nyerere alikuwa na jeraha lolote la risasi vis-a-vis mwanaharakati mwenzake kupoteza mguu kabisa; the global view doesn’t detail such; vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa jkn ndie baba wa taifa;

b) mtazamo wako wa pili: Nyerere sio baba wa taifa la tanzania hata tukiamua kuiweka zanzibar pembeni kwa dakika moja (nasema hivi kwa sababu umemtaja sokoine);

* hoja yako ya msingi hapa ni kwamba wapo watu wengine wanaostahili kupewa heshima hiyo kutokana na mchango wao katika taifa hili; hili nimeshalisema hapo juu na pia katika my original post; otherwise kwa hoja hii, you are challenging the current global consensus on what establishes mtu kuitwa baba wa taifa; mtazamo kwamba sokoine, which means basi hata majina kama msekwa, msuya, kwamba wanastahili, can be very stimulating intellectually; ningependa kwa wakati mwingine kuingia katika mjadala huu kwani najua nitajifunza mengi; pia inaweza kuleta mabadiliko ya kifikra na kimtazamo kuhusu dhana nzima ya baba wa taifa, iwapo utalipanga in a good research context, and convince mabadiliko hayo kitaifa au hata kimataifa; vinginevyo mpaka hilo litokee, mawazo yako nitaendelea kuyaheshimu juu ya sokoine kustahili, lakini huku nikiendelea kuamini kwamba mwalimu bado ni baba wa baba wa taifa, kutokana na qualifications which have been already established in a global sense, hence emulated hapa kwetu; vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa jkn ndie baba wa taifa;

c) mtazamo wako wa tatu ni kwamba nyerere sio baba wa taifa hata katika mazingira ya muungano (kwani umetoa hoja juu ya umuhimu wa karume);

* hili nilishalijibu katika hoja yangu ya msingi, ni kiasi cha wewe tu kurejea sehemu nayozungumzia ubaba wa taifa na muungano ambapo nilitoa mifano ya george washington kama muasisi wa muungano wa marekani uliokuwa na mataifa 16 tu (sio 50 ya leo); baadae muungano ukavunjika kwa miaka mitano, na uliporudi ukarudi na mataifa mengine mengi zaidi na kuzaa usa tofauti kabisa leo hii (50 states), na kwamba ingawa yote haya yalitokea akiwa hayupo, bado akapewa heshima hiyo; pia nikaeleza jinsi gani muungano wetu unachukua sura ile ile, mfano nikataja tume ya mark bomani vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa jkn ndie baba wa taifa;

d) mtazamo wako wa nne ni kwamba baba wa taifa sio lazima awe rais wa kwanza wa jamhuri huru;
* hili nililielezea katika my original post kwamba sio lazima, ingawa mara nyingi waliendelea na hatua ya kuwa marais wa kwanza wa jamhuri huru husika; na kwamba kikubwa kuhusu baba wa taifa ni uongozi wake katika mapambano ya ukombozi kwa taifa husika; vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa jkn ndie baba wa taifa;

e)mtazamo wako wa tano ni kwamba hauna tatizo na neno baba wa taifa kwa misingi ya dini;

* hata kama ungekuwa na tatizo na hili, nilishalisemea kwamba naheshimu sana mtazamo huu kwani hakuna baba katika uislam. Nikashauri kwamba ni muhimu tufikie consensus on a term ambayo itakidhi mahitaji ya pande zote za jamii, as long as wana msimamo mmoja juu ya heshima hiyo kwa nyerere; lakini kama hata katika hilo hakuna consensus, ofcurse kila mtu yupo huru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa jkn ndie baba wa taifa;

f) mtazamo wako wa sita/mchango wako tuseme, hautoi hisia zozote kwamba tanzania tunahitaji mapinduzi mapya ili kumpata baba wa taifa;

* hii inatokana na hoja yako kwamba wapo tayari watu wanaostahili kuitwa baba wa taifa, lakini sio nyerere. Mjadala huu nao ni very stimulating kwani pia una challenge the current consensus kwamba baba wa taifa is inherent na harakati za ukombozi/uhuru; hili tumeshaliongelea hapo juu; vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa jkn ndie baba wa taifa;

g) mtazamo wako wa saba/mchango wako unatoa hisi kwamba historia iliyopo ya taifa letu inatosha kutuzalia baba wa taifa mwingine kwa kutengua heshima wa baba wa taifa aliyepo, nyerere ili apewe mtu mwingine ambae anastahili zaidi;

* hii nayo ina challenge the current global consensus jinsi gani baba wa taifa anapatikana; ni hoja yenye mchanganyo sana, vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa jkn ndie baba wa taifa;

h) mtazamo wako wa nane, nyerere hastaili kuwa baba wa taifa kutokana na mapungufu yake kiutendaji;

hili nilishalizungumzia katika my original post nilipo ongelea mapungufu ya george washington na wengine katika utawala wao; mfano, tofauti na nyerere ambae angalau aliruhusu demokrasia ya chama kimoja, marekani haikuwa na chama chochote cha siasa chini ya baba wao wa taifa, george washington; pia mchakato wa katiba mpya ya taifa la marekani ulifanywa kwa njia zisizo za kidemokrasia kwani ilikuwa ni washington na kikundi kidogo sana cha wanajeshi na wanasiasa; na katiba hiyo ilihusu mataifa 13 tu, na baadae wakati wa utawala wake, amendmentz zikafanywa kuruhusu mataifa mengine matatu; akafariki na katiba juu ya mataifa 16 (sio 50 ya leo) lakini bado akawa baba wa taifa; vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge vigezo vilivyopo kuhusu baba wataifa, san asana iwapo suala la utendaji liwe featured; na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa jkn ndie baba wa taifa;

h) na mtazamo wako wa tisa, katiba ya jamhuri wa muungano wa tanzani, mbali na kutamka kutakuwa na rais wa tz na wa zanzibar, haitambua heshima ya baba wa taifa.

mimi sikusema chochote juu ya katiba, hapo unajichanganya, nimesema heshima hii inatambulika na bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania na kuomba unipe muda nije na taarifa kamili;

nipo safarini mkoa kidogo lakini nina access ya internet from time to time, ntajitahidi kujibu hoja zako as much as i can;

bwana mchambuzi naona sasa unazidi kuhamisha mlingoti wa goli katika mada hii!, umekuja na views zako halafu unataka kutulazimisha eti global consensus ndiyo iko hivyo!. Je una criteria yoyote, au tamko lolote la kimataifa linalostandardize heshima ya ubaba wa taifa iweje?- ndo maana mimi ninasema bila data, research, dont do some conclusions

hebu angalia hapa chini ulichokiandika then compare na maandishi yangu niliyoandika tuone kama umeniquote sawa.

f) mtazamo wako wa sita/mchango wako tuseme, hautoi hisia zozote kwamba tanzania tunahitaji mapinduzi mapya ili kumpata baba wa taifa;

* hii inatokana na hoja yako kwamba wapo tayari watu wanaostahili kuitwa baba wa taifa, lakini sio nyerere. mjadala huu nao ni very stimulating kwani pia una challenge the current consensus kwamba baba wa taifa is inherent na harakati za ukombozi/uhuru; hili tumeshaliongelea hapo juu; vinginevyo ofcourse una uhuru wa kuendelea to challenge utaratibu uliopo, na mpaka mabadiliko yatokee, tukubali kwamba kwa maoni ya wengi, kwa sasa jkn ndie baba wa taifa;

hebu angalia mimi niliandikaje:

sasa wewe unataka kujua maoni yangu kuhusu "ubaba wa taifa", maoni yangu ni haya yaafuatayo.
(1) waasisi wote wa taifa letu wenye mchango mzito , kama ni wa kiume basi ni mababa wa taifa, na wa kike ni mama wa taifa.
(2) ubaba wa taifa siyo lazima uwe raisi wa kwanza, kuwa raisi ni mgawanyo wa kazi tu, lakini mtu yeyote aliyefanya juhudi kubwa za kulinufaisha taifa zima wakati ule wa uasisi wa taifa letu basi ni baba wa taifa, kwa maana hiyo mtu kama kawawa na karume senior ninawaona kama mababa wa taifa.
(3) nyerere ninamuona pia kama baba wa taifa
(4) mpaka miaka takriban 30 hivi ya uchanga wa taifa, nachukulia kama mwendlezo wa uasisi kwa hiyo mtu yeyote atakayetumikia taifa kwa uadilifu mkubwa na kuwa katika nafasi ya maamuzi mazito ya umma na kufanya vyema basi ni baba wa taifa, kwa maana hii namuona sokoine kama baba wa taifa, namuona alhaji mwinyi kama baba wa taifa.

sasa basi ni kwamba mchambuzi unaniwekea maneno mdomoni, mimi namuona nyerere kama baba wa taifa, lakini siyo peke yake, ghafla kwenye hoja yako niliyoinukuu unadai eti nawaona kuna watu wanastahili ubaba wa taifa lakini siyo nyerere, wapi nimesema hayo?. Au husomi vizuri mabandiko ya wengine?.

So far ninaendelea kusubiri hiyo sheria iliyotungwa kumpa nyerere heshima ya ubaba wa taifa, hapo ndipo tutakapojua "ubaba wa taifa" umeanza 1961, 1964, 1985 au 2003/2005, maana ni wewe uliyesema kwamba heshima ya ubaba wa taifa ni jambo la kisheria.

bwana Mchambuzi, hiyo hoja unayodai kwamba "Global Consensus" inafanana na mtizamo wako ni technique ya Generelization, kwa sababu huna evidence ya kuback up na hiyo claim pia.

Suala la Nyerere kuwa baba wa taifa "PEKE YAKE", AU Nyerere kuwa baba wa Taifa "NA WENZAKE", Litaendelea kuwa ni maoni ya mtu mmoja mmoja.
 
Baada ya kukusoma kwa kina nina masuala mawili tu

Mosi Kwani Nelson Mandela ni baba wa taifa la South Africa?

Pili, unaposema mnalinda misingi aliwaachia huyu mnaemwita baba wa Taifa lenu je ni kweli na una uhakika na hili? Kumbuka kuwa Nyerere alijenga misingi ya Ujamaa na kujitegemea. Je mpaka leo mnafuata siasa hizi?

Nyerere alibainisha wazi maadui zake wakuu ni watatu na alijitahidi kupambana nao. nao ni ujinga, maradhi na umasikini. Je sio tu mpaka anaondoka aliwashindwa, je vipi sana hususan huyu umasikini unapanda au kupungua?

Lakini pia kumbuka Nyerere hakupigania uhuru bali alipewa uhuru ofisini pasi na kumwaga damu. Na Tanganyika tokea historia na historia hakuna tarbia ya makabila kupigana vita hivyo inchi ilikuwa shwari tu tangu na hata bada ya uhuru.

naomba ufafanuzi wako.

 
bwana mchambuzi naona sasa unazidi kuhamisha mlingoti wa goli katika mada hii!, umekuja na views zako halafu unataka kutulazimisha eti global consensus ndiyo iko hivyo!. Je una criteria yoyote, au tamko lolote la kimataifa linalostandardize heshima ya ubaba wa taifa iweje?- ndo maana mimi ninasema bila data, research, dont do some conclusions

hebu angalia hapa chini ulichokiandika then compare na maandishi yangu niliyoandika tuone kama umeniquote sawa.



hebu angalia mimi niliandikaje:



sasa basi ni kwamba mchambuzi unaniwekea maneno mdomoni, mimi namuona nyerere kama baba wa taifa, lakini siyo peke yake, ghafla kwenye hoja yako niliyoinukuu unadai eti nawaona kuna watu wanastahili ubaba wa taifa lakini siyo nyerere, wapi nimesema hayo?. Au husomi vizuri mabandiko ya wengine?.

So far ninaendelea kusubiri hiyo sheria iliyotungwa kumpa nyerere heshima ya ubaba wa taifa, hapo ndipo tutakapojua "ubaba wa taifa" umeanza 1961, 1964, 1985 au 2003/2005, maana ni wewe uliyesema kwamba heshima ya ubaba wa taifa ni jambo la kisheria.

bwana Mchambuzi, hiyo hoja unayodai kwamba "Global Consensus" inafanana na mtizamo wako ni technique ya Generelization, kwa sababu huna evidence ya kuback up na hiyo claim pia.

Suala la Nyerere kuwa baba wa taifa "PEKE YAKE", AU Nyerere kuwa baba wa Taifa "NA WENZAKE", Litaendelea kuwa ni maoni ya mtu mmoja mmoja.

Nasizi kusisitiza Ni sheria gani na ya mwaka gani iliyopitishwa na Bunge kumpa Nyerere Ubaba wa Taifa?

 

Nyerere alibainisha wazi maadui zake wakuu ni watatu na alijitahidi kupambana nao. nao ni ujinga, maradhi na umasikini. Je sio tu mpaka anaondoka aliwashindwa, je vipi sana hususan huyu umasikini unapanda au kupungua?


Kwenye ujinga takwimu zipo. Kama unaona Nyerere alishindwa basi hakuna aliyewai kfanikiwa kama yeye iwe ni Tanzania au afrika kuondoa illiteracy . Ni vision na sera zake za muda mrefu na mfupi(UPE) zilifanikisha hilo.......

Baada ya yake ikawa ni bora liende . kuna watoto waningia darsa hadi la tatu hawajui kuandika, Mtihani imefutwa, etc

Unasemaje kuhusu hoja hiyo tuhamie kwenye vilivyobaki viwili.
 
Kwenye ujinga takwimu zipo. Kama unaona Nyerere alishindwa basi hakuna aliyewai kfanikiwa kama yeye iwe ni Tanzania au afrika kuondoa illiteracy . Ni vision na sera zake za muda mrefu na mfupi(UPE) zilifanikisha hilo.......

Baada ya yake ikawa ni bora liende . kuna watoto waningia darsa hadi la tatu hawajui kuandika, Mtihani imefutwa, etc

Unasemaje kuhusu hoja hiyo tuhamie kwenye vilivyobaki viwili.


Nisome vizuri. Suala langu limejikita kwenye umasikini.

Je umeangalia katika world rank ya umasikini wakati mnapata uhuru mlikuwa wapi na waki anaondoka mlikuwa wapi na leo hii mnashikilia namba ngapi?
 
Nisome vizuri. Suala langu limejikita kwenye umasikini.
Je umeangalia katika world rank ya umasikini wakati mnapata uhuru mlikuwa wapi na waki anaondoka mlikuwa wapi na leo hii mnashikilia namba ngapi?

Word rank ya umasikini kwa indicators/impactors gani. Unajua hata taifa la USA ni tajiri kuliko taifa a Norway kwa vigezo fulani vya IMF lakini ukichambua zaidi (katika level ya mwananchi) na kwa undani Taifa la Norway na sweeden ni tajiri zaidi kuliko marekani...........

Sasa ebu weka hizo indicators za umasikini unazotomia kabla ya nyerere uchukua nchi. then weka hizo indicicators baada ya nyerere kung'atuka. Alfu tungalie hadi leo hii hz economic inidcators na impactors mbali mbali zinamfavour nani

NB
huwezi kuondoa umasikini kukiwa na ujinga.Labda kama ni kuondoa umasikini kwa wachache. Je wakati IMF sasa inatusifia(Kuondoa umasikini) vipi illiteracy level yetu???? Ebu shusha data unazotumia labda tutaongea lugha moja......
 
Word rank ya umasikini kwa indicators/impactors gani. Unajua hata taifa la USA ni tajiri kuliko taifa a Norway kwa vigezo fulani vya IMF lakini ukichambua zaidi (katika level ya mwananchi) na kwa undani Taifa la Norway na sweeden ni tajiri zaidi kuliko marekani...........

Sasa ebu weka hizo indicators za umasikini unazotomia kabla ya nyerere uchukua nchi. then weka hizo indicicators baada ya nyerere kung'atuka. Alfu tungalie hadi leo hii hz economic inidcators na impactors mbali mbali zinamfavour nani

Ndugu yangu usitake kuzunguka saana,

Kumbuka waazungu wanasema in order to build something strong it helps to start with best and possible materials. Sasa msingi mbovu uliowekwa na Nyerere ndio unawamaliza sasa. Kumbuka kuwa alisema bayana ili Tz iendelee inahitaji vitu vinna yaani watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Nikuulize ni kipi Tz imekikosa mpaka wakti wa Nyerere aliweza kuasisi ulanguzi na uhujumu uchumi kitu ambacho kimekomaa na leo umekuwa ufisadi?

Lakin hata ,agazeti yenu usomi. Je hujui kama Tz ni nchi ya tatu toka chini kwa kutembeza kibakuli yaani ombaomba duniani? fuatilia income per capital.

 
Hukuwepo wakati wa Nyerere na kadi za reshen utamuachia nani? Unanchekesha.

Mama Faiza Foxy unanchekesha sana resheni ilikuwapo mpaka kwenye ndizi, muhogo, ndizi mzuzu, maharage, samaki na nyama? Usitake kuwadanganya vijana resheni ilikuwapo kwa bidha adimu ambayo sana sana ilikuwa sukari; hivi sasa vitu madukani je watanzania wanavimudu? Jaribu kuwa mkweli

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Mama Faiza Foxy unanchekesha sana resheni ilikuwapo mpaka kwenye ndizi, muhogo, ndizi mzuzu, maharage, samaki na nyama? Usitake kuwadanganya vijana resheni ilikuwapo kwa bidha adimu ambayo sana sana ilikuwa sukari; hivi sasa vitu madukani je watanzania wanavimudu? Jaribu kuwa mkweli

Chama
Gongo la Mboto DSM.

Maduka ya kaya yaliuza mpaka sabuni za kuogea na kufulia sio chakula pekee. Zote hizo zilipatikana kwa resheni
 
Back
Top Bottom