Nyerere kaondoka Duniani akiwa kaacha heshima kubwa mno kimataifa.
Wanasiasa wa Tanzania wamekuwa hawaachi kumtaja huyu Mzee kila mara kwenye kampeni au hotuba zao.
Alimshauri rafiki yake mkubwa hayati Nicolai Cesesscue enzi za uhai wake akiwa Rais wa Romania aachie ngazi ili kulinda heshima yake ,Nicolai hakusikia matokeo akaja kuuawa kikatili yeye na mkewe.
Alimshauri Kaunda wa Zambia naye hakusikia, "mzee mwenzangu waachie Vijana ulinde heshima yako ".
Kaunda akapuuza ushauri wa Nyerere matokeo yake akaja kuondoka Kwa aibu ya kushindwa uchaguzi, badala ya kustaafu, yaani Rais wa kwanza wa nchi unagombea tena, what a shame?
Heshima ya Nyerere Kwa Africa inazidiwa na Mandela tu, ukimtoa Mandela hakuna Rais tena wa kufananishwa na Nyerere ktk bara la Africa.
Kwanza alikuwa akiaanza kuongea unatamani uendelee kumsikiliza tu muda wote hata Kama ulikuwa na stress Ukisikiliza hotuba za Nyerere stress zinapungua.
Ukombozi wa mataifa ya kusini mwa Africa huwezi kuujadili bila kumjadili Nyerere ambaye ndo alikuwa key point ya Ukombozi Huo.
Ni katika Kipindi cha Urais wake Tanzania iliheshimiwa na hata kuogopwa na mataifa makubwa Duniani.
Pamoja na matatizo ya hapa na pale, lakini enzi zake uchumi wa Tanzania ulikuwa juu, pesa ilikuwa na thamani kubwa, noti ya mwisho Kwa thamani kubwa ilikuwa noti ya sh 100.
Elimu ilikuwa juu, siyo kama leo hii ambapo hata kiswahili tu kinawapa shida hata wahitimu wa vyuo vikuu, neno "hela " wanatamka "ela" neno "halafu "wanatamka "alafu " eti hao ni university graduates, kwenye English ndo unaweza hata kulia Kwa namna wanavyoboronga.
Enzi zake hata intelligence ya nchi ilitisha, TISS ya Nyerere haikuwa tofauti na CIA hutaki kuamini acha.
Wakati wa vita vya Kagera, TISS ilimzunguka Idd Amin Spain, alikuwa ameagiza makombora ya kisasa yenye nguvu lakini akajikuta anayakosa na yakaangukia mikononi mwa Tanzania.
Hatukuwa na silaha Kali Kama za Idd Amin, lakini tulikuwa na intelligence imara mno, hii ndo ilifanya tushinde vita bila msaada wa nchi yoyote, Idd Amin pamoja na kusaidiwa na Gaddafi bado tuliweza kumtwanga hadi akaikimbia Uganda.
Inahitaji Kitabu kuandika mambo mazito aliyofanya Nyerere.
Lakini alimkosea nini Mungu huyu mzee?
Mwandishi Munga Tehenani (RIP) aliandika Kitabu kiitwacho "Nyerere alikuwa mchawi ".
Kitabu hiki hakikukaa mitaani hata siku tatu kikawa kimepotea kimaajabu, ilikuwa ni kati ya mwaka 2001 au 2003.
Inadaiwa aliingia maagano na kuzimu na fimbo yake ndo ilikuwa muongozo wa mambo yake yote.
Maagano yoyote ya nguvu za giza humkasirisha Mungu na kukilaani kizazi cha mtu aliyeingia maagano hayo.
Mungu hulaani kuanzia watoto na hata vitukuu na vilembwe na hata kizazi cha nne.
Familia ya Rais Kennedy wa US aliyepigwa risasi mwaka 1963 imepukutika yote Kwa vifo vya ajali na kuuawa, hakuna alama yoyote ya Kennedy Marekani, yamebakia majina tu.
Nikiitazama Kwa jicho la tatu familia ya Nyerere haiko sawa, imefunikwa na giza nene, haing'ai, haionekani, it looks like Nyerere left no children to walk his ways,haya ni mambo ya Ulimwengu wa roho.
Hata ukuu wa wilaya tu imekuwa ishu? wanapata watu ambao wanaonea wivu wenzao wanaoinuliwa na Mungu, yaani mtu anataka ampangie hadi Mungu kwamba fulani anapaswa kuwa maarufu na mwingine hatakiwi.
Matendo yetu yawe mema au mabaya yana reflect maisha yetu ya baadaye.
Tuwe makini sana na tujae hofu ya Mungu .
cc:mshana jr
Makala ijayo
😀ini ni Ugonjwa wa akili
Sent using
Jamii Forums mobile app