Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kambarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani? Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono? Tujadili.
Misingi iliwekwa dada
FaizaFoxy. Kwa kifupi.....viongozi kuweka maslahi ya taifa mbele kuliko ubinafsi, viwanda (wewe dada wakumbuka kwenye hili, viatu vya bora, nguo kwa watoto, wakubwa na hasa kina mama), elimu, afya, miundombinu (kwa raia tulionawo), kutii sheria bila shuruti, siasa za kutofungamana na upande wowote, ustawi wa jamii na mengine kedekede..
Yaliendelea vizuri tu, ofcourse nayo yalihitaji kiongozi mwenye upeo kuyaendeleza yaliyowekwa na kuongezea mengine toka kwa aliyechukuwa udereva (KWA MASLAHI YA TAIFA).
Kilichotekea mwanzoni ilikuwa kama unafuu wa maisha kwa wananchi (Liberalisation of our Economy), ghafla mitumba ya kila aina ilimwagwa mtaani, kuanzia nguo za ndani mpaka magari! Ndiyo tujiulize
FaizaFoxy, je kwa hili tuliendeleza viwanda vyetu? ule unafuu je ulitusaidia kwa muda mfupi au ndiyo ulituharibu kabisa?!
Haya yakaja mambo ya "kila kitu ruksa", ikawa balaa, haya ya Almasi, Dhahabu na madini mengine kupitishwa kama njugu Airport ilikuwa kawaida! Ikafika mpaka wanyama hai kusafirishwa Airpot kama sio watu kuwinda na SMG au AK47! Kupeana vitalu vya kuwinda hovyo hovyo tu, kwenye madini ndiyo usiombe!
Haya yote yaliyokuja kutokea kweli bado tumlaumu Mwl. Nyerere?!
Tukatoka hapo yakaanza ya viongozi kuwa na "Conflict of Interests" kwenye makampuni binafsi, safari na posho kusafiri kwenda nje bila mtu yoyote kuhoji, ni madili juu ya madili! Bado tumlaumu Baba wa Taifa?!
Mpaka pale tulipofikia wenye chama tawala wakaona "this is too much"..Maana ikafika watu wakiiba kwenye taasisi za umma walikuwa wakionekana ni mashujaa na "role models"! Na mtoto asipoiba ili afanikiwe hata wazazi walikuwa wakimtukana, mfano....huyu bwege yupo TRA miaka 5 hana nyumba wala gari! Madawa ya kulevya yalijaa mitaani mpaka tukawa na mini versions of "El Chapo" kama sio "Escobar"!
It was terrible, the "Cycle" had to end and we needed to reverse, by going back to basics..Tatizo wale waliofaidika ambao ni wachache hawataki kurudi kule, tumeanza the "the blaming game", kwamba maisha ni magumu sababu ya huyu, hela hakuna mifukoni sababu ya huyu, hakuna safari wala wizi wa kijinga sababu ya huyu mkatili, kila kitu tunamlaumu yeye huku tukisahau DINI zote zakemea yote yaliyofanywa huko nyuma hata kama hatutaka kufanya yale tulioachiwa na Mwl. Nyerere..