Nyaronyo Kicheere: Kikwete ananichukia bila sababu

Nyaronyo Kicheere: Kikwete ananichukia bila sababu

Status
Not open for further replies.
Hapa ndo tunaona watu wanaojua kusoma Nazi nzuri zinazoandikwa na with we ye skill kama Nyaronyo nawale wanao papukiaambo.Hongera Nyaronyo kwa kutufanya tufikiri critically.Hii no fasihi na hapa ndipo kwakwe.
 
Jamani haya yamepita, sidhani kama rais anaweza kuteua tena wapya tofauti na wale 201. Kaka mleta mada rais hakuona umuhimu wako ndio maana hakukuteua. Mtatiro huenda alipendekezwa na mapendekezo yake yakakubarika. Sasa jamani tuache kurumbana tuwatakie utekelezaji mwema walioteuliwa na bunge la katiba kwa ujumla. Tumuache rais apumue, nae ni binadamu. Unaposema fulani alikuwa na sifa hakuchaguliwa unakosea. Kwa sababu wenye sifa wapo wengi pia huenda alikuwa anabalance hata mambo ya ibada(imani) sasa hawezi kuchukua wote wa mlengo mmoja.
 
Mbona wewe ndiyo unakurupuka, KICHERERE ametumia nafsi yake kuwakilisha wengine ambao wameachwa na kwa maana hiyo hata majibu ya hoja yake lazima yabebe nafsi yake haizalishi anakusema wewe, mimi au yule. Pole wewe mkuu, taratibu tu utajifunza.

Mkuu hebu tulia na uache ushabiki usokuwa na maana. ngoja nikwambie: Hii ni katiba ya nchi si mambo ya mzaha wala kufadhiliana. Tafakali kwa umakini mkubwa utaona mapungufu kibao katika suala zima la uteuzi huu. Iwapo unasema makundi yanayofanana lazima ujue yanafanana katika mantiki ipi na unafanyanje katika kuhakikisha kuna usawa. Raisi wenu alikomalia sana yy ndo afanye uteuzi wa jina mojamoja na kwa kufanya hivyo aliona ana uwezo mkubwa wa kuchambua jina kwa jina, sema mwenyewe kafaulu au kafeli katika hilo? mfno mdogo: Julius Mtatiro ni jina kubwa katika medani za siasa katika nchi hii, leo unamwondoa katika sehemu ya siasa tena akiwa mtendaji mkuu wa chama cha siasa halafu unasema ni wa kundi la malengo yanayofanana na Kajubi-mwanahabari. wapi na wapi? Tatizo lako na wenziyo ni kwamba MMESHAFIKA MWISHO WA KUFIKIRI HIVO MMEBAKIZA UBISHI HATA KATIKA JAMBO LILILO WAZI, nafikiri eneo lenu sahihi ni kule chitchat
 
Mkuu, hoja ya Kicheere ni kuwa kuna watu wameteuliwa na wengine wameachwa, pia anataka kutuaminisha kuwa uteuzi wa Rais haukuzingatia vigezo hasa kwa vile kuna watu wanaonekana wana malengo tofauti ila wamewekwa kwenye malengo yanayofanana. Turudi kwenye Sheria iliyompa Rais mamlaka hayo, JE sheria inasemaje baada ya Rais kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba? Je inatoa fursa ya watu kuhoji na pengine kubatilisha uamuzi wake?

Kwa akili hizi akija nyumbani kwako akasema ni zamu yake kulala na mkeo utampigia makofi na kusema huruhusiwi kuhoji kwa sababu sheria inamruhusu! Chabruma na thatha nendeni shule, shule ni muhimu sana. hizo kofia na tshirts mnazopewa haziwezi kuwasitiri uchi wenu. THINK OUT OF THE BOX MAN!!!!!!
 
Wengine hamjamwelewa Kicheere. Hana maana kwanini yeye hajachaguliwa. Ana maana wapo wenye sifa nyingi wameachwa na wenye sifa kidogo wamechaguliwa. Wengine wamelazimishwa kuchaguliwa kwenye makundi ambayo wanaambiwa wana malengo yanayofanana ili mradi tu na wao wamechaguliwa. Uchaguzi wa baadhi ya wajumbe haukuwa balanced kwa mfano kuchagua watu wanaowakilisha wafugaji kutoka sehem chache za nchi badala ya kuchukua sehemu mbali mbali za nchi
 
Hii makala tusimwangalie mwandishi kama yeye binafsi,tuangalie mbele kidogo,ujumbe ulipo,tuwe wasomi kidogo wa fasihi,mimi binafsi nimeipenda sana kuna sehemu nimecheka,jamaa alikuwa mwalimu wa ukweli,kawakilisha ujumbe kwa staili ya kipekee sana..
 
Khaa!!! Laki saba kwa siku mchezo! Lazima roho imuume.
 
Wengi tunaingia kichwa kichwa kwenye hii makala kwa kuwa tumamtazama Nyaronyo kama Nyaronyo. Nilichokielewa mimi katika makala hii Nyaronyo anawawakilisha wale wote ambao hawakutendewa haki kwa kutochaguliwa kwa kuwa wana sifa pengine zaidi ya wengi walioteuliwa. Na pia anaonyesha kwa jinsi gani mteuzi hakuwa makini katika kuunda makundi mbalimbali na kuchagua wawakilishi wake. We have to read between the lines

Tunahitaji watu wenye uelewa kama wako ndugu
 
Mkuu wewe ni kilaza wa kufa mtu,na shaka sana na vyeti vyako.First class ya 4.1? Mimi nina 4.3 ya UDSM lakini ni Upper second!!!!Wenzio akina Mtatiro lazima washangae kundi la maajabu walilowekwa pamoja.
 
Hii makala ya Nyaronyo Kicheere kama mtu usipoisoma kwa makini, ukaamua kuikurupukia tu kama wengi wanavyofanya ni dhahiri kuwa hutaielewa kabisa.
Ametumia falsafa kubwa sana katika kuiwasilisha kwahiyo unahitaji kuwa na uhuru wa akili ili kumuelewa!
 
Mkuu wewe ni kilaza wa kufa mtu,na shaka sana na vyeti vyako.First class ya 4.1? Mimi nina 4.3 ya UDSM lakini ni Upper second!!!!Wenzio akina Mtatiro lazima washangae kundi la maajabu walilowekwa pamoja.

tikiti maji tu hilo, linasumbua watu humu!
 
kwani hao wote majina yao hayakupendekezwa regardless na makundi yepi. Nakumbuka wakati nachagua shule wakati namaliza darasa la saba, nilichagua shule kubwa kubwa tu kama Mzumbe, Ilboru, Kibaha Sekondari na zinazofanana na hizo. kwa kuwa wastani wangu haukutosha kwenda kwenye hizo shule, nilichaguliwa kujiunga na shule ya Sekondari Ruvuma. Sikulalamika na wala sikushtuka bali nilimshukuru Mungu kwa kuchaguliwa.

Hata nilipomaliza kidato ya Nne, nimechaguliwa kwenye combination ambayo haikuwa chaguo langu la kwanza, ila kwa vile nimechaguliwa sijulaumu na nilifurahia kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano tena kwa shule ambayo haikuwa kwenye akili yangu.

Pia nilipomaliza kidato cha Sita, nilipenda kuwa Mwanasheria. Ila kwa vile ushindani ulikuwa mkubwa na nafasi zilikuwa chache, nilichaguliwa kujiunga na shahada ya kwanza katika masomo ya Sayansi ya Siasa na Utawala. Tena Chuo nilichopata si kilichokuwa chaguo langu namba moja. Ila kwa vile nimepata chuo huku wenzangu wakikosa, nilimshukuru Mungu.

Baada ya kumaliza chuo, maajabu yalijitokeza tena. Kwa masomo yangu, nilitegemea kupata kazi za utawala, ila haikuwa hivyo, niliajiriwa kuwa jeshini. Nikiwa Jeshini, nilitegemea kuwa nitakuwa mtawala ndani ya jeshi, wapi bana, nilijikuta napelekwa kwenye kikosi cha maji pale Kigamboni. Utawala na kuogelea wapi na wapi. haya nikiwa pale niliotegemea nittakuwa afisa wa juu kutokana na sifa yangu ya elimu, tena First Class mwenye GPA ya 4.1, nilishangaa kupangwa kwenye Lindo kama kawaida huku nikishika mtutu usiku kucha. Sikushangaa sana kwa vile nina kazi, nilimshukuru Mungu. Kwa sasa Mambo yamekaa barabarani.

Hivyo Namshangaa Mtatiro, Kushangaa kuwekwa kwenye kundi moja na Mukajanga
Mkuu hakuna First Class ya 4.1 GPA.First Class ni 4.4-5.0.Tafiti kwanza kabla ya kuandika.Labda kama ilikuwa Stashahada au Astashahada
 
Huyu NANYORO atakuwa miongoni mwa wale 118 waliojipendekeza wenyewe.
Kama ulisoma walau hadi Kidato cha Nne, lazima utakuwa ulisoma kitu kinaitwa FASIHI. Kwa mtu asiyenyambulisha mambo, ni ngumu kuuelewa ujumbe kama anaoutoa Nyaronyo na mwisho wake utaishia kutumia akili nyepesi kuhukumu kuwa jamaa alijipendekeza mwenyewe sasa ametoswa. lakini ukitumia akili kufikiri kwa umakini, Nyaronyo anatoa ujumbe mkubwa sana hapa na ambao una mafunzo mengi ndani yake. Try to think big, otherwise 'Ficha Upumbavu wako' (Invisible)!
 
Kuchagua wajumbe 200 kutoka waombaji 3000 tena wengi walio na sifa zinazofanana ni kazi ngumu. Kwa waliochaguliwa wakati mwingine wajihesabu ni bahati zaidi kuliko hata sifa. Kama ni sifa hata Nyaronyo Kicheere anazo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom