Nyaronyo Kicheere: Kikwete ananichukia bila sababu

Nyaronyo Kicheere: Kikwete ananichukia bila sababu

Status
Not open for further replies.
Hiyo ni fasihi wakuu, msianze kumshambulia nyaronyo bure!
 
Hiyo ni fasihi wakuu, msianze kumshambulia nyaronyo bure!
...na hapa ndipo 'home of great thinkers', jiulize nchi hii ina safari ndefu kiasi gani hata kuanza kulielewa tatizo!

 
Mleta mada ana hoja ipi ya msingi? kutoteuliwa? Kati ya watanzania wote walioachwa yeye ndiyo anafaa?

Kama nimumuelewa mwanahabari, ametumia lugha ya picha kuzungumzia kundi la watu walioachwa kuteuliwa kwenye Bunge la Katiba, na kundi la waliochaguliwa ambao ana mashaka na uteuzi wao. Amaezungumza kwa kuwakilisha wengi kuanzia wafugaji, walemavu sahihi lakini pia kauliza jinsi gani mwandishi wa habari anakua na malengo sawa na mwanasiasa tena mwanasiasa??? Ndio mana kasema labda malengo yao ya pamoja mwandishi na mwanasiasa ni kumchafua E.L.

Najaribu kumsoma mwandishi katika 3D
 
Tungekuwa wote ni Pro-Utaifa tungeweza kuijadili kwa manufaa ya Taifa kuliko Vyama vyetu.Kwani vyama vyaweza kufa na Nchi kuwepo daima.
 
Hapa tu ndipo nawainulia Watanzania mikono!! Kwanza hawajui kusoma juu ya mistari mwisho wanakurupuka kama yule Chaburuma eti Nyaronyo kachanganyikiwa! Hv ww unamfahamu vizuri Nyaronyo na aina ya uandishi wake? Basi kwa kukusaidia anza kununua gazeti la ----- kila siku ndipo utaanini kuwa katika waandishi bora ambao Tanzania ilipata kuwa nao basi Nyaronyo ni mmoja wao. Hivi kwa mawazo yako unafikiri kweli mwandishi analalamika kwa kuachwa ktk Bunge la Katiba lililojazwa wana CCM magamba? Hapana. Sisi tunaomjua Nyaronyo tumeshia kucheka hadi kuvunjika mbavu kwani hapo ndipo utajua nani mwandishi na nani kanjanja katika fani ya uandishi. Big up sana bwana Nyaronyo Mungu akupe afya njema uendelee kutuburudisha na aina hii ya uandishi.

Ukiona elimu ni gharama basi ujaribu ujinga- Mwl. Julius K. Nyerere.
 
kwani hao wote majina yao hayakupendekezwa regardless na makundi yepi. Nakumbuka wakati nachagua shule wakati namaliza darasa la saba, nilichagua shule kubwa kubwa tu kama Mzumbe, Ilboru, Kibaha Sekondari na zinazofanana na hizo. kwa kuwa wastani wangu haukutosha kwenda kwenye hizo shule, nilichaguliwa kujiunga na shule ya Sekondari Ruvuma. Sikulalamika na wala sikushtuka bali nilimshukuru Mungu kwa kuchaguliwa.

Hata nilipomaliza kidato ya Nne, nimechaguliwa kwenye combination ambayo haikuwa chaguo langu la kwanza, ila kwa vile nimechaguliwa sijulaumu na nilifurahia kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano tena kwa shule ambayo haikuwa kwenye akili yangu.

Pia nilipomaliza kidato cha Sita, nilipenda kuwa Mwanasheria. Ila kwa vile ushindani ulikuwa mkubwa na nafasi zilikuwa chache, nilichaguliwa kujiunga na shahada ya kwanza katika masomo ya Sayansi ya Siasa na Utawala. Tena Chuo nilichopata si kilichokuwa chaguo langu namba moja. Ila kwa vile nimepata chuo huku wenzangu wakikosa, nilimshukuru Mungu.

Baada ya kumaliza chuo, maajabu yalijitokeza tena. Kwa masomo yangu, nilitegemea kupata kazi za utawala, ila haikuwa hivyo, niliajiriwa kuwa jeshini. Nikiwa Jeshini, nilitegemea kuwa nitakuwa mtawala ndani ya jeshi, wapi bana, nilijikuta napelekwa kwenye kikosi cha maji pale Kigamboni. Utawala na kuogelea wapi na wapi. haya nikiwa pale niliotegemea nittakuwa afisa wa juu kutokana na sifa yangu ya elimu, tena First Class mwenye GPA ya 4.1, nilishangaa kupangwa kwenye Lindo kama kawaida huku nikishika mtutu usiku kucha. Sikushangaa sana kwa vile nina kazi, nilimshukuru Mungu. Kwa sasa Mambo yamekaa barabarani.

Hivyo Namshangaa Mtatiro, Kushangaa kuwekwa kwenye kundi moja na Mukajanga

mkuu chabruma mbona ka una elimu kubwa inayopingana na vitu unavyochangiaga humu ndan au ndo nguvu ya noti imekuziba mdomo........!!
 
Ukiwa na njaa kali kama ya nyaronyo kicheere lazima uandike makala kama hii

Sijui nikuambieje? kuna vitu vingine lazima uwe na roho mtakatifu ili aweze kukutafasiria. wewe umesoma kama ilivyo, jitahidi tena kufikiria kiundani, hakumaanisha kuwa yeye binafsi
 
Nashukuru sana kaka KYORASANGI kwa kudadavua wasifu wa SOPHIA MCHAFU
KIUKWELI KUNA kasoro kubwa sana kwenye uteuzi huu wa wajumbe wa bunge la katiba ndicho kitu Nyahoro kachere alicho taka kutufikirisha sisi wasomaji wa fasihi yake
 
Wadau, ujumbe wengi hawakuulewa kabisa, Kiswahili ni Lugha yetu kwa wale wasiolewa ujumbe mzima wajaribu kurudia tena kusoma mada iliyowekwa jamvini.

Jamaa ana ujumbe mzito sana na wenye hisia ndani yake na si yeye binafsi anataka nafasi hiyo bali anawasemea jamii nyingine kabisa.

Wanajamii tuendele Kujifunza na kusoma Lugha ya Kiswahili.
 
Maandiko mengine yanahitaji umakini kusoma,c kukurupuka mwishowe uonekane kanjanja-copy and paste!
 
nyaronyo kicheere,jina lako baya ndo maana kakupiga bench, alifikiri ni kicheche akaogopa kuingiza wanyama bungeni.
 
Nimeamini tulio wengi hatujui mafumbo(misemo) Hongera sana Nyaronyo Kcheere kuna kitu nimeng`amua kwenye makala yako.
 
wenye upeo mfupi utawaelewa kwa haraka
mwandihsi katumia lugha nzuri katika tasnia yake
hapa hajizungumzii yeye,anazungumzia watu wenye sifa walioachwa badala yake tukaona watu wasistahili kuwamo,kazungumzia makundi yalioachwa nk.
Chabruma kiswahili form 4 ulipata ngapi?????????????? kama hata alichoandika umeshindwa kumwelewa...kazi tunayo

Hakika Nyaronyo Kicheere amechanganyikiwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom