Mkuu Chabruma, sijakupata vizuri unaposema kila ulichopenda hukupata ukapewa kingine kwako ni sawa? Je unatoa somo gani kwa vijana wetu, Kama ni mtaalamu wa Uhandisi wa MILOLONGO TIJA basi ikija FASIHI akubali tu? Binafsi kwa jinsi Nyaronyo alivyowasilisha ujumbe alilenga watu halisi katika kundi halisi na si kuwa yeye mwenyewe! Mfano huo mdogo wa Mtatiro kuwa na lengo moja na mwnahabari.
Ukisoma ujumbe ana maana kubwa sana!
Ukisoma ujumbe ana maana kubwa sana!
kwani hao wote majina yao hayakupendekezwa regardless na makundi yepi. Nakumbuka wakati nachagua shule wakati namaliza darasa la saba, nilichagua shule kubwa kubwa tu kama Mzumbe, Ilboru, Kibaha Sekondari na zinazofanana na hizo. kwa kuwa wastani wangu haukutosha kwenda kwenye hizo shule, nilichaguliwa kujiunga na shule ya Sekondari Ruvuma. Sikulalamika na wala sikushtuka bali nilimshukuru Mungu kwa kuchaguliwa.
Hata nilipomaliza kidato ya Nne, nimechaguliwa kwenye combination ambayo haikuwa chaguo langu la kwanza, ila kwa vile nimechaguliwa sijulaumu na nilifurahia kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano tena kwa shule ambayo haikuwa kwenye akili yangu.
Pia nilipomaliza kidato cha Sita, nilipenda kuwa Mwanasheria. Ila kwa vile ushindani ulikuwa mkubwa na nafasi zilikuwa chache, nilichaguliwa kujiunga na shahada ya kwanza katika masomo ya Sayansi ya Siasa na Utawala. Tena Chuo nilichopata si kilichokuwa chaguo langu namba moja. Ila kwa vile nimepata chuo huku wenzangu wakikosa, nilimshukuru Mungu.
Baada ya kumaliza chuo, maajabu yalijitokeza tena. Kwa masomo yangu, nilitegemea kupata kazi za utawala, ila haikuwa hivyo, niliajiriwa kuwa jeshini. Nikiwa Jeshini, nilitegemea kuwa nitakuwa mtawala ndani ya jeshi, wapi bana, nilijikuta napelekwa kwenye kikosi cha maji pale Kigamboni. Utawala na kuogelea wapi na wapi. haya nikiwa pale niliotegemea nittakuwa afisa wa juu kutokana na sifa yangu ya elimu, tena First Class mwenye GPA ya 4.1, nilishangaa kupangwa kwenye Lindo kama kawaida huku nikishika mtutu usiku kucha. Sikushangaa sana kwa vile nina kazi, nilimshukuru Mungu. Kwa sasa Mambo yamekaa barabarani.
Hivyo Namshangaa Mtatiro, Kushangaa kuwekwa kwenye kundi moja na Mukajanga