Nyaronyo Kicheere: Kikwete ananichukia bila sababu

Nyaronyo Kicheere: Kikwete ananichukia bila sababu

Status
Not open for further replies.

sawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
2,752
Reaction score
932
Katika gazeti la MAWlO la leo, 13 Februari, mwandishi Nyaronyo Kicheere, ametoa mpya. Ameandika makala moja nzuri sana kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba. Anasema, pamoja na kuwa na sifa, lakini Rais Jakaya Kikwete hakumteua.

Anasema, "Sikushangaa kuachwa na Rais Kikwete kwa sababu namfahamu ------ huyu ananichukia sana tena sana. Tatizo langu kubwa ni kwamba sielewi sababu ya Rais wa nchi kunichukia kiasi hiki!"

Baadhi ya maneno yaliyomo kwenye makala hiyo ni haya yafuatayo:


Kwenye orodha ya wateule Bunge la Katiba yamo majina ya watu waliokubuhu katika kumtukana Waziri Mkuu aliyestaafu kwa kashfa, Edward Ngoyai Lowasa, kama Paulo Makonda, mbona na mimi wakati ule naandikia ----------- tulimsakama sana Lowasa hadi gazeti letu likafungiwa hadi leo? Mbona sijateuliwa mimi niliyekuwa mhariri wake katika bunge hilo?

Mie mwalimu wa zamani, mwalimu mkuu mstaafu, mwanahabari na mhariri mahiri wa ----- hivi sasa, pia sasa ni mwanasheria wa Kujitegemea, kweli sifai kuteuliwa mbunge wa Bunge la Katiba? Hapana! Ninafaa sana ila Rais Kikwete ana chuki binafsi dhidi yangu.

Pamoja na kwamba vigezo vyote vya kuteuliwa mjumbe wa Bunge la Katiba ninavyo bado sikuteuliwa. Kwa mfano, mimi ni mtoto wa mfugaji, nami mwenyewe nafuga mbwa mmoja, paka mmoja, kuku na shwaini kadhaa, kwa nini sikuteuliwa angalau kuwawakilisha wafugaji?

Mheshimiwa rais eti kawateua Hawa Mchafu, Rebeca Masato, Tomas Minyaro, Tedy Malulu na Omary Husein kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba kuwawakilisha wavuvi! Hawa walipendekezwa na nani, wapi na lini?

Mbona sisi wafugaji wa samaki tuliochimba mabwawa na madimbwi makubwa hatukuarifiwa nasi tuteue au tupendekeze wenzetu tunaofuga nao samaki au hao wavuvi walionekana bora zaidi kuliko sisi tunaofuga samaki na kutunza mazingira?

Halafu wewe angalia majina ya watu walioteuliwa kuwakilisha vyama vya wafugaji, eti ni William Ole Nashi, Mabada Matagu, Dorin Maro, Hamis Mlondwa, Esta Chuma, Said Abdala Bakari na Zuberi Khan! Hakuna Marwa, Chacha wala Mwita Maranya! Kwa nini? Kwani wafugaji hapa Tanzania ni akina nani?

Nasema hapa ndipo nilipostahili kuteuliwa kuwawakilisha wafugaji kutoka Mara akina Nyamburi, Nyangombe, Nyamhanga, Nyamrasa, Nyamtembera na hata hao akina Chacha, Mwita na Marwa. Hapa Kikwete hakuniteua pia kwa sababu ananichukia na hapa kanionea.

Eti kwa busara ya rais wetu, wajumbe wa Bunge la Katiba wenye Malengo yanayofanana ni: Dk. Xtina Mzava, Paul Makonda, Jesca Mtavasavangu, Julius Mtatiro, Abdalla Bulembo, Hemed Panzi, Dk. Zainab Gama, Paulinus Mtenda, Almas Maige, Pamela Masae, Kajubi Mukajanga, Kadari Singo, Yusuph Omar Chunda, Fatma Musa, Profesa Abdul Sherif na Rehema Said Shamte.

Kajubi Mukajanga wa Baraza la Habari Tanzania ana malengo gani yanayofanana na Julius Mtatiro wa Chama cha Wananchi (CUF)?

Tunaomba tuambiwe Abdallah Bulembo wa Wazazi wa CCM ana malengo gani yanayofanana na Yusufu Omar Chunda yule mwandishi wa habari kutoka nchi jirani ya Zazibar?

Au sisi ambao majogoo yetu hayawiki siyo vilema vilevile? Mbona hatukuulizwa ili tuandikishwe na kuteuliwa mmoja wetu kuwakilisha kundi lenye ulemavu wa majogoo?

Ina maana nani atatusemea huku hajui adha ya kuwa na jogoo lemavu lisilowika wala kuhudumia matembe? Tafadhali Kikwete acha chuki fanya uteuzi kwa umakini bila kubagua.

Makala kamili inapatikana katika ukurasa wa nne wa gazeti hilo
 
kajubi Mukajanga anamalengo gani yanayofanana na Julius Mtatiro?juzi mtatiro akihojiwa na star tv yeye mwenyewe ameshangaa
 
na hao wavuvi wa zanzibar hawatambui waliochaguliwa na JK
 
Huyu NANYORO atakuwa miongoni mwa wale 118 waliojipendekeza wenyewe.
 
Hakika Nyaronyo Kicheere amechanganyikiwa.


When you read between the lines, kuna ka-ujumbe kamo humo! Ila tu, the whole thing is now time barred! Pole ndugu yangu Nyaroonyo. Kuhusu majogoo yanayoshindwa kuhudumia matembe; nimecheka hadi basi!
 
Hakika Nyaronyo Kicheere amechanganyikiwa.

Tatizo ni yale mapengo yake...nimemuelewa sehemu moja tu ya kundi la watu wenye malengo yanayo fanana..hakika nilijiuliza Kajubi Mukajanga ana malengo gani yanayo fanana na huyu Abdallah Bulembo ambaye alijifanya kutumia jina la rafiki yake mpenzi Abdallah Majura ili apate cheap popularity..sijaelewa!
 
Mleta mada ana hoja ipi ya msingi? kutoteuliwa? Kati ya watanzania wote walioachwa yeye ndiyo anafaa?
 
jf bado wana uchungu na m.a.w.io na m.w.a.naHa.l.isi,najua mleta mada aliandika majina ya hayo magazeti lakini mods wameweka dash dash.
 
Mada kama hizi zinatuchosha sana. Naibu Katibu Mkuu kiongozi alitolea ufafanuzi kuwa wajumbe waliojipendekeza wenyewe kisheria hawaruhusiwi, sasa huyu KICHERE hata kama anaongea kwa niaba ya wenzake ambao walifanya hivyo atambue kuwa sheria haiwaruhusu.
 
kajubi Mukajanga anamalengo gani yanayofanana na Julius Mtatiro?juzi mtatiro akihojiwa na star tv yeye mwenyewe ameshangaa

kwani hao wote majina yao hayakupendekezwa regardless na makundi yepi. Nakumbuka wakati nachagua shule wakati namaliza darasa la saba, nilichagua shule kubwa kubwa tu kama Mzumbe, Ilboru, Kibaha Sekondari na zinazofanana na hizo. kwa kuwa wastani wangu haukutosha kwenda kwenye hizo shule, nilichaguliwa kujiunga na shule ya Sekondari Ruvuma. Sikulalamika na wala sikushtuka bali nilimshukuru Mungu kwa kuchaguliwa.

Hata nilipomaliza kidato ya Nne, nimechaguliwa kwenye combination ambayo haikuwa chaguo langu la kwanza, ila kwa vile nimechaguliwa sijulaumu na nilifurahia kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano tena kwa shule ambayo haikuwa kwenye akili yangu.

Pia nilipomaliza kidato cha Sita, nilipenda kuwa Mwanasheria. Ila kwa vile ushindani ulikuwa mkubwa na nafasi zilikuwa chache, nilichaguliwa kujiunga na shahada ya kwanza katika masomo ya Sayansi ya Siasa na Utawala. Tena Chuo nilichopata si kilichokuwa chaguo langu namba moja. Ila kwa vile nimepata chuo huku wenzangu wakikosa, nilimshukuru Mungu.

Baada ya kumaliza chuo, maajabu yalijitokeza tena. Kwa masomo yangu, nilitegemea kupata kazi za utawala, ila haikuwa hivyo, niliajiriwa kuwa jeshini. Nikiwa Jeshini, nilitegemea kuwa nitakuwa mtawala ndani ya jeshi, wapi bana, nilijikuta napelekwa kwenye kikosi cha maji pale Kigamboni. Utawala na kuogelea wapi na wapi. haya nikiwa pale niliotegemea nittakuwa afisa wa juu kutokana na sifa yangu ya elimu, tena First Class mwenye GPA ya 4.1, nilishangaa kupangwa kwenye Lindo kama kawaida huku nikishika mtutu usiku kucha. Sikushangaa sana kwa vile nina kazi, nilimshukuru Mungu. Kwa sasa Mambo yamekaa barabarani.

Hivyo Namshangaa Mtatiro, Kushangaa kuwekwa kwenye kundi moja na Mukajanga
 
jf bado wana uchungu na m.a.w.io na m.w.a.naHa.l.isi,najua mleta mada aliandika majina ya hayo magazeti lakini mods wameweka dash dash.

sawa tu sasa mke wako ameomba talaka kuja haja gani ya kujipitisha pitisha tena nyumbani kwako?
 
Tunaomba tuambiwe Abdallah Bulembo wa Wazazi wa CCM ana malengo gani yanayofanana na Yusufu Omar Chunda yule mwandishi wa habari kutoka nchi jirani ya Zazibar?
tumekupata
 
Ukiwa na njaa kali kama ya nyaronyo kicheere lazima uandike makala kama hii
 
Kicheere njaa inemuma pole wewe ushazoea kula kimteremko hahaha waswahili bhana ingelikuwa kujitolea ungesema anakuchukia?acha kutuchanganya kijana na rudia tena hizo ni njaaaaa!!!!
 
Wengi tunaingia kichwa kichwa kwenye hii makala kwa kuwa tumamtazama Nyaronyo kama Nyaronyo. Nilichokielewa mimi katika makala hii Nyaronyo anawawakilisha wale wote ambao hawakutendewa haki kwa kutochaguliwa kwa kuwa wana sifa pengine zaidi ya wengi walioteuliwa. Na pia anaonyesha kwa jinsi gani mteuzi hakuwa makini katika kuunda makundi mbalimbali na kuchagua wawakilishi wake. We have to read between the lines
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom