Nyaronyo Kicheere 'ahamia CCM'

Nyaronyo Kicheere 'ahamia CCM'

Ni vigumu sana kwa Lumumba BK7 na makada wa CCM kuweza kudadavua na kuilewa lugha ngumu kama aliyotumia Bw. Kicheere.
 
Yani hata wewe umeuweka ubongo wako rikizo? Umeshindwa kabisa kumuelewa Kicheere?

:shock::shock::shock::shock::shock:.....NIMEMWELEWA KULIKO WEYE VILE NAMFAHAMU FIKA.........MIMI NIMEONGEZEA KACHUMBARI TU.......WENGI HAWAKUIONA HIYO POST YAKE NYINGINE AMBAYO MODS WAMEIFUNGA BILA SABABU!!!!
 
Ha! Ha! Ha! Ha! Kumbe ccm tamu namna hiyo ! Au ndiyo maana wanalogana ?
 
Nimegundua kuna watu huwa wanasoma vichwa vya habari tu humu JF na kukimbilia ku-comment. Sasa kama mnashindwa kusoma haka ka-paragraph kamoja, je ikiwa habari ndefu si ndiyo mnaipotezea kabisa.
 
Mwandishi Mahiri wa Makala na Mwanasheria wa Jijini Dar es Salaam Nyaronyo Mwita Kicheere amehamia CCM, Chanzo gazeti la -----
Mkuu New Force, jameni hizi avatar nyingine!, muwe na huruma japo kidogo, wengine wenzenu tuu dhaifu, hivyo avatar kama hizi ni kutiana tuu majaribuni!, badala ya concenrate na suject matter unajikuta unaishia kukodolea macho avatar huku mawazo yakikupeleka kwengine!.

Hebu wewe jifikiriea avatar kama hii halafu msomaji post ni mtu wa Kanda ya Ziwa!.

image.tiff


Pasco.
 

Attachments

  • profilepic178729_1.gif.jpeg
    profilepic178729_1.gif.jpeg
    42.4 KB · Views: 87
Ccm inapendwa jamani, tuache utani

Inapendwa sana kwa kuwa inaficha maovu yote,ukiwa na biashara yoyote isiyofuata sheria wewe tundika bandera tuu ya kijani hakuna atakayekugusa
 
Mwandishi Mahiri wa Makala na Mwanasheria wa Jijini Dar es Salaam Nyaronyo Mwita Kicheere amehamia CCM, kati ya sababu kubwa zilizomhamisha CHADEMA, anasema Viongozi wake hawana sura ya Tabasamu, tofauti na viongozi wa CCM, Kikubwa zaidi anasema ameamua kuipenda CCM kwa kuwa Mwenyekiti wake Jakaya Kikwete ni mtu Rahimu, anayependa watu wake na kuwahurumia kutokana na magumu ya maisha, Juzi juzi ametangaza jinsi alivyopelekewa orodha ya majangili 40 wanaotikisa mbuga zetu lakini hakuwachukulia hatua yeyote kwa kuwa wanafanya ujasiriamali kujikimu na wanaweza kuwekeza. Nyaronyo amesema pia, anahamia CCM kwani kesho au keshokutwa akikamatwa na ngozi ya Chui, ya Mamba, au meno ya Tembo atapata msamaha kama wale 40 waliosamehewa na Kikwete.

Nyaronyo anasema, CHADEMA wangekuwa madarakani leo, ambao viongozi wao hawana tabasamu, akamtaja Mbowe Slaa, Lissu na Lwakatare nchi isingekalika, maana ni wazee wa visasi, maana Wezi wangekamatwa, watekaji wangesakwa, wauza dawa za kulevya wangekuwa wote gerezani.

Tena akaongeza kuwa hii si mara ya kwanza Kikwete kusamehe. Amesamehe Majangili 40, kama alivyosamehe wezi wa EPA, Nyaronyo anasema Tumshukuru Mungu kwa kuwa na Kikwete, Rais anayesamehe. = Chanzo gazeti la -----

🙂🙂....................you cant be serious aisee
 
Kimsingi makala ya Nyaronyo Mwita Kicheere yenye kichwa cha habari " Nimehamia CCM, CHADEMA hakunifai" ambayo ameitoa kwenye gazeti la ----- la leo 20/2/2014 ni makala ya kuwananga viongozi wa CCM na serikali yake. Mifano yote aliyotoa ni kwa lengo la kuonesha kimafumbo namna ambavyo viongozi wa CCM na serikali yake wanavyoshindwa kuchukua hatua kali kwa wafanyao maovu nchini.Kwa mfano tafakari anaposema "Kikwete anafahamu fika kwamba meno ya tembo na vipusa havifiki mjini bila lusafirishwa katika magari ya chama(CCM) na yale ya polisi ambayo hayakaguliwi kwenye vizuizi vya barabarani ndiyo maana kaamua kutoikuchukua hatua na pia kwa kujua wale walionufaika watawekeza nchini".
 
Back
Top Bottom