Pasco hapa ndipo unapoweza kumaliza hasira za Boss wako, hakuna kulala mwambie Lowasa akupe details zote anazozifahamu lete mwaga hapa na from there indio utakuwa mwisho wa matumizi ya neno kujivuwa gamba.
Kuna storm kubwa inakuja ambayo cha kusikitisha mpaka sasa Watanzania wameshindwa kusoma alama za nyakati kwamba Mungu ameamuwa kujidhihirisha upande wa Wananchi lakini cha kushangaza taasisi za kiraia na kidini ziko kimya juu ya swala hili.
Kwa hakika huu ndio wakati muhafaka wa kuing'oa serikali ya Kikwete madarakani, hatuna sababu ya kusubili mpaka 2015 maana hata JK akisema avunje baraza lake leo atapata Mawaziri kutoka miongoni mwa Wabunge wepi? Lusinde!!??....
Yuko wapi kiongozi mkuu wa kisasa hapa nchini ambao wengi wa wanaoingia hii mikataba ama kawateua kwa kuwafahamu au kaletewa majina.
Na anachukuliaje hali kama hii wakati hao wateule wake wanaendelea kutafuna mbegu wakati mvua zaendelea kunyesha shamba liko tayari ila hakuna upandaji wowote? Tutavuna nini? majani? Tutapata wapi chakula kwa watoto na wajukuu zetu kama mbegu zote zitakuwa zimetafunwa na mwenye maamuzi ya kuwakataza wale yupo anawachekea?
Kumbe CCCC ni ya RA jamaa anatisha sana
"Politicians are often accused by their opponents of claiming to be honest and seek the truth while using spin tactics to manipulate public opinion"..... RA hapa munamleta kujenga chuki. Kwa taarifa yenu RA katulia sana sasa.... labda ataibukia Kagoda, makaburi yatakapofukuliwa soon. Hapa jibuni HOJA
Unajua kuna kitu ambacho mpaka sasa najiuliza kama nimesoma nikaelewa, au macho yangu yananichezea; MOU inasema kampuni ya China ina "build, own and operate, na ku-hand over baada ya miaka 45". Wakati huo huo mkopo toka Exim unachukuliwa na Tanzania, na pia kulipwa na Tanzania kwa interest ya asilimia 2%.
Hivi ni macho yangu au hizo ndio facts za huu mradi?
Mimi nadhani hapa shida sio kudownload hilo file, hapa shida lugha iliyotumika ndo tatizo.Acheni uvivu wakuu,kama mnatumia simu sawa, ila hapo kuna file Invisible ameattach mautamu yote yapo humo, kabla ya kucomment angalie kwanza maana amesema hapo inabidi u download hataki kumwaga mtama kwenye kuku wengi....
Haya ndiyo yalikuwa yanasemwa bungeni.
Hapa Invisible una maana gani kuwa Nundu ni msafi?
Nini kosa la Nundu hapo? Nundu amezuia kampuni moja isipewe huu mradi kwani wao ndio wapange bei, wafanye utafiti, wapewe kazi nayo ni CCCC na hayo ni kabla Nundu hajawa Waziri. Kwa hiyo afukuzwe kwa kuzuia ubadhirifu?
Mnaelewa mnachokisoma na kukisema?
kwanza huo mradi wake wa kuiweka nchi rehani kwa miaka 45 sio uhaini huo? si inatakiwa kupita katika baraza la mawaziri? au ndio ticts nyingine inaingia, kwa uwezo wa waziri sifikiri kama ni busara kusaini mkataba wa zaidi ya miaka 5, la sivyo aombe kibali cha baraza la mawaziri, kwa baraza lote kuuchambua huo mradi na kuona faida na hasara zake.Tanzania ni balaa, sasa huo mradi alioukata yeye wa wazili mwenzake wa $542,000,000 ambao wawekezaji hao wataendesha bandari kwa miaka 15, kisha unarudi serikalini-TPA, yeye wakwake wa bei nafuu ni $300,000,000, wawekezaji wataendesha mradi kwa miaka 45...... yupi nafuu kati yao?