Of course Mathematics is not a science is an art of dealing with numbers, science use Mathematics but Mathematics does not use science.Kwa tafsiri ya mahesabu haya, Hesabati inaelekea kuwa ni sanaa zaidi kuliko sayansi.
Tatizo la Tanzania ni kuwa sheria hazifuatwi. Tumegeuka kama katika hadithi ya George Owell ya Shamba la Wanyama, kila mmoja anabadilisha sheria, ikiwemo katiba, kwa maslahi yake. Tukumbuke masuala ya Muungano yalikuwa 11 tu, ghafla bin vu tunaona yamekuwa mara mbili. Kwa misingi hiyo ya kufuata maslahi, kutofuata sheria na hakuna wa kusema lolote kwani akisema itabidi na yeye aulizwe, Tanzania Bara walimwaga mboga, Tanzania Visiwani wamemwaga ugali.kitendo cha zanzibar kufanya marekebisho ya katiba yao yanayokwenda kinyume na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa kweli hata mimi nashangaa ndio maana wanatarajia kusherehekea siku ya uhuru wa TanzaniaHivi, Zanzibar iliungana na Tanganyika zikatengeneza Tanzania. Tanganyika ilipotelea wapi?
Juma Duni Haji alikuwa analijibu swali hilo kupitia ITV usiku huu.
Alimtaja Nyerere kuwa ndiye aliyeifuta Tanganyika na waraka alikuwa nao mkononi anausoma, siukumbuki ni upi.
awa jamaa walifanya mlinganyo huu;
t[SUB]1[/SUB]+ z = t
where t[SUB]1[/SUB]= tanganyika
z= zanzibar
t= tanzania
but t[SUB]1[/SUB] ~ t
then the equation becomes t + z = t
hapo ndipo TANGANYIKA yangu ilipo fia duh !!!!!H
I wish ... Tungepata kwa KINA makubaliano Rasmi Kati ya Rais na CDM yaliyofikiwa kutokana na nyaraka hizi!!
Nadhani ukiutazama huo waraka wa magwanda wanashindwa kuelewa kuwa Zanzibar ni nchi, ina Rais wake, ina Katiba yake, ina Bendera yake, ina Wimbo wake wa Taifa. Na hapa ni nchi zimeungana tu, na hata huo waraka uliwekwa wa 1964 ni amendment tu, jee waraka orijino kabla haujawa amended uko wapi?
Mimi nadhani tufike mahala tuwe wakweli tu katika nafsi zetu. MIUNGANO yote duniani sasa hivi ime/inasambaratika. Huu wa kwetu upo kwa nguvu ya dola tu tangu siku nyingi.
Nitatoa mifano michache:
-USSR haipo tangu mwanzoni mwa miaka ya 90.
-Chekoslovakia haipo.
-Yugoslavia haipo.
-Sudan imezaa Sudan ya Kusini na Darfur inakuja.
-Ethiopia imezaa Eritrea na Ogaden inakuja.
- Somalia sasa hivi kuna Somaliland na Puntland.
-Ubelgiji hata kuunda serikali moja ni taabu.
Kosa lilifanyika tangu mwanzo kwenye Muungano wetu huu. Nimewahi kumsikia Mwalimu akisema alichoambiwa na Karume mwaka 1964. Karume alitaka iwe NCHI moja. Mwalimu akamkatalia. Hili likawa doa la kwanza kabisa la Muungano huu. Haliwezi kurekebishika.
Zanzibar sasa ni NCHI kamili ingawa tunajidanganya kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku Maalim Seif akipata nafasi hata ya kukaimu ataitangaza Zanzibar kuwa Jamhuri.
Tatizo limekuwa kubwa zaidi baada ya JK kushindwa kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT. Mabadiliko ya hivi karibuni kwenye katiba ya Zanzibar yalipaswa kutangazwa kuwa ni batili. Rais wetu amekaa kimya.
Acheni ujinga wenu hata kama Muungano Zanzibar waende kivyao na sisi tubaki na Tanzania yetu,mimi sitaki kusikia upuuuzi unaoitwa Tanganyika
Waungwana nina maswali machache baada ya haya maongezi:
1. Kwa hiyo rais atasaini mswaada uwe sheria?
2. Je akishaisaini kama ilivyo bila kuingiza mapendekezo ya chadema, kutakuwa na nafasi tena ya kuingiza vitu vipya ndani ya sheria ambavyo kwenye mswaada havikuwepo?
3. Je kuna uwezekano (au kisheria inaruhusiwa) kwa rais kubadilisha mswaada na kuingiza mambo ambayo hayakupitishwa na bunge kabla ya kusaini mswaada uwe sheria?