NYARAKA: Madudu mengine ya William Mhando ndani ya TANESCO

NYARAKA: Madudu mengine ya William Mhando ndani ya TANESCO

Huu si wakati wa kulalamika ni wakuchukuwa hatua, haiwezekani kila kukicha bei ya umeme inapanda kumbe tunaneemesha matumbo ya watu tukichakachua umeme mnangaka ujinga huu.
 
Tuleteeni hapa ya kina RIDHIWAN haya ya kina Mhando mnawaonea tu tumeanza huko huko juu. Hakuna lolote hapa. Mnapakana matope nini wenyewe kwa wenyewe Makambale mnawaacha..
 
Shark,

Hapo unaongelea ya 2008 nadhani. Na 2011?

Kwani 2008 Mhando alikuwa Mkurugenzi wa Tanesco? au hii ya Mwakanyamale inahusiana vipi na nafasi ya Mhando kule Tanesco?. Labda fikra zangu, naona hii ya 2011 inambada kimaadili ila ya 2008 ipo too personal between him and the said MC Donald...wataalamu wanaweza kutujuza zaidi hayo mahusiano yaliingilia vipi Tanesco.
 
Shark,

Hapo unaongelea ya 2008 nadhani. Na 2011?

Kwani 2008 Mhando alikuwa Mkurugenzi wa Tanesco? au hii ya MC Donald Mwakamele inahusiana vipi na nafasi ya Mhando kule Tanesco?. Labda fikra zangu, naona hii ya 2011 inambada kimaadili ila ya 2008 ipo too personal between him and the said MC Donald...wataalamu wanaweza kutujuza zaidi hayo mahusiano yaliingilia vipi Tanesco.
 
Sawa mkuu, hii ndiyo Tanzania tunayoishi lakini hatujui kinachoendelea ila tumebakia kulalamika bila kufanya mabadiliko. Kwa kuwa wanasiasa wanajua vile Watanzania ni wasahaulifu, basi watafanya kila wawezalo kutunyonya hadi tone la mwisho
 
Halafu mtu ananyanyuka na povu na jasho kumtetea mtu kama huyu. Zitto amejishusha sana na haaminiki tena!! Huwezi kutetea mtu kama huyu unless nawe una maslahi huko. Pengine sasa tunamwelewa Zitto toka wakati ule alipolazimisha lile suala la majenereta TANESCO.

Huyu Mhando hakuwa wa kumfukuza tu bali kumfilisi na kumfunga hadi afie jela yaani kifungo cha maisha. Huwezi kupewa dhamana katika shirika la umma halafu unafanya biashara na mkeo tena ya wizi. Nadhani mlisikia taarifa ya wizi mwingine wa manunuzi ya vile 'vikombe' vya Tanesco inatolewa juzi kwenye TV live. Mzungumzaji alikuwa anawasifu waliotoa taarifa kuwa ni 'whistle blower'.

Kheri mzee mwenye hekima na misimamo kuliko kijana mnafiki na kigeugeu. Zitto agenda yako ya umri sasa tunaona haina mashiko kama haya ndiyo unataka kuyaendekeza. Kama unajifanya hukujua kinachoendelea siku zote huko TANESCO, haya mpaka sasa mbona uko kimya ebu toa comments juu ya nyaraka hizi tusikie! Nadhani sasa umebaki ni jina tu lakini moyo na ubongo si yule tuliyembeba wakati amefukuzwa Bungeni!!
 
Mkuu pole sana kwa kwikwi,Naona ulikuwana unatafuta upenyo wa kutoa chuki,hasira na kikohozi dhidi ya zitto
Umefunguja,japo sioni unazungumzia nini.
HIVI umeambiwa ZITTO ndiye Auditor wa mapato ya TANESCO,Hivi unadhani Zitto ndiye CAG wa Tanzania?
Utetezi wa zitto dhidi ya huyo Mhando ulikuwa katika kipengele kipi?Au unatabia ya Ku-generalize mambo kama under 18?
Zitto na kilichoandikwa hapo kwenye DOCUMENTS kunauhusiano gani?
Labda yawezekana hujasoma document hiyo imeandikwa nini,ila tu kiu cha kutapika majungu kilikufika ghafla ukaamua kuelekea kwenye kukoment bila kusoma.Rudi tena kasome inahusu nini,Sio kukimbilia kumtaja Zitto kwenye madudu yako​
 
System ya Tanzania imeoza! Ona sasa inazalisha hata watu wanaojidai ni wapinzani na watetezi wa wanyonge kumbe hawana lolote! Sasa kama ZZK katika hili sakata la Tanesco alilipigia debe naye ni kiongozi wa upinzani anayetaka kuwa raisi wa nchi itakuwaje? Huyu anaaminisha umma kuwa bila rushwa huwezi kuwa kiongazi hapa Tanzania? Hii inavunja moyo mno tutafanyaje sasa nchi yetu inakwenda na maji sababu ya wanafiki na wabinafsi?

One thing, our gratitude to the few brave ones who truly love our nation and bold enough to unleash some of the evils such as the Tanesco scandal and others to the open. This gives hope that one day our nation will be liberated from the claws of the wicked.
 
Sio kuwaacha kabisa ila nimejaribu kuangalia katika jicho la kuyatatua haya matatizo kwanza alafu from there tujenge utamaduni wa kuwajibika once mtu anapokosea, nikalinganisha na hiyo ya South Africa though maudhui yanatofautiana ila nimeangalia kwa nchi yetu kuna issue ya watu wanaingia katika uongozi kwa makundi hivyo inakuwa ngumu kumchulia hatua mwana mtandao mwenzao anapofanya kosa (that's why nikasema kuna haja ya kukaa chini na kuelezana ukweli ili huu utamaduni ukome maana mtu anafanya kosa alafu analindwa na kama atalipuliwa anajenga chuki, najua ni ngumu ila nikafananisha na SA kama kuna uwezekano tuje na utaratibu mpya wa kwamba makundi ni kwa ajili ya kuoigiana kampeni lakini isiwe ndio sababu ya ufanye utakacho na kulindwa kisa ulikuwa bega kwa gega katika kuhakikisha mgombea wenu anaingia katika uongozi).......

Naelewa J K nia yako njema ya kuweka mambo sawa pia naikubali tunapopishana ni jinsi kushughulikia madudu yaliyopo na hasa hili donda ndugu la kulindana na kugawana rasilimali zetu. inabidi hili litufikirishe.
 
Huyo ni Mhando na ni TANESCO tu. Bado hujaenda mashirika mengine mengi ya umma yanayobebwa na Serikali kwa gharama za walipa kodi wa nchi. Tanzania hatuwezi kubadilika bila kuiondoa ccm madarakani, full stop!
 
Huyu Mhando ndiye anaitwa engineer? Jamani hawa watu walisoma wapi kama wana akili ndogo na ujuzi mdogo hivi? Sijui ingekuwa Jakaya ingekuwaje?
 
Kwani 2008 Mhando alikuwa Mkurugenzi wa Tanesco? au hii ya MC Donald Mwakamele inahusiana vipi na nafasi ya Mhando kule Tanesco?. Labda fikra zangu, naona hii ya 2011 inambada kimaadili ila ya 2008 ipo too personal between him and the said MC Donald...wataalamu wanaweza kutujuza zaidi hayo mahusiano yaliingilia vipi Tanesco......

For all I know he must have been holding a managerial post in 2008. So what would be your defence?
 
Kweli uso wa Binadamu hauna haya.....Duuh!:glasses-nerdy:
 
hahahaha!! hao akina Kawawa; Sumaye; e.t.c kujazana BOT haifanani na huo mkataba wa Mhando?
anaandamwa kwa sababu kawazidi kete!!
wote ni wezi tu!!
 
Kuna watu wakishaona jina la Zitto au yeyote wasiyempenda basi huwa hawaangalii context isipokuwa wanachukua kineno wanachohisi kinatimiza haja zao na kuishia hapo. Kama alihitaji uchunguzi ufanyike tatizo liko wapi? Kama leo atakuja na utetezi baada ya ushahidi kuzidi kuonekana hapo ndo kuna issue!!!

Watu wa aina hiyo wanatanguliza chuki zao kuliko maslahi ya taifa.
 
Kwa kweli nchi yetu imeoza sana hii ishu ya Mhando yenye conflict of interest kwa kiwango hiki walipokuwa wanampa cheo cha Mkurugenzi hawakuona madudu haya?nchi imejaa uoza na rushwa kama kuomba maji ya kunywa. aibu sana.Kilichonisikitisha zaidi ni kuwa Mc Donald Liveline Technology inamilikiwa na huyo jamaa Mc Donald ni yule aliyeingizwa mjini na Johari (Blandina Chagula) katika kampuni ya filamu ambayo hata sasa ipo inaitwa RJ Company ikimilikiwa na Ray (Vincent Kigosi ) na Johari.

Wabunge waliotaka kukwamisha bajeti ni akina Munde Tambwe(viti maalum) Tabora,na wenzake.
 
Mkuu pole sana kwa kwikwi,Naona ulikuwana unatafuta upenyo wa kutoa chuki,hasira na kikohozi dhidi ya zitto
Umefunguja,japo sioni unazungumzia nini.
HIVI umeambiwa ZITTO ndiye Auditor wa mapato ya TANESCO,Hivi unadhani Zitto ndiye CAG wa Tanzania?
Utetezi wa zitto dhidi ya huyo Mhando ulikuwa katika kipengele kipi?Au unatabia ya Ku-generalize mambo kama under 18?
Zitto na kilichoandikwa hapo kwenye DOCUMENTS kunauhusiano gani?

Labda yawezekana hujasoma document hiyo imeandikwa nini,ila tu kiu cha kutapika majungu kilikufika ghafla ukaamua kuelekea kwenye kukoment bila kusoma.Rudi tena kasome inahusu nini,Sio kukimbilia kumtaja Zitto kwenye madudu yako​

Kuna ushahidi Mwingine hapa wa Zitto kumtetea Mhando...

..........Kuna kila dalili kuwa imeibuka vita ya wazi kati ya Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), huku Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco aliyesimamishwa kazi, William Mhando, akipigiwa debe la wazi na wabunge.

Taarifa zilizopatikana kwenye ofisi za Bunge zinasema kuwa Kamati ya Nishati na Madini inajipanga kukwamisha bajeti ya wizara hiyo kama Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco aliyesimamishwa kazi, Injinia Mhando, hatarejeshwa kazini huku wizara ikisisitiza kuwa amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wala hajafukuzwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, naye ana msimamo kuwa Mhando ameonewa na wizara inaweza kujiokoa kwa kumrejesha ofisini kisha ufanywe uchunguzi maalumu utakaoendeshwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG)............

CHANZO>>
Vita kubwa TANESCO
 
Naelewa J K nia yako njema ya kuweka mambo sawa pia naikubali tunapopishana ni jinsi kushughulikia madudu yaliyopo na hasa hili donda ndugu la kulindana na kugawana rasilimali zetu. inabidi hili litufikirishe.

Haya mambo ni complicated mdau ila yataisha ipo siku maana hakuna kitu kibaya kama watu ambao wapo kimya muda mrefu alafu ikatokea siku wakasema TUMEONEWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMENYANYASWA KIASI CHA KUTOSHA NA TUMEPUUZWA KIASI CHA KUTOSHA, UNYONGE WETU NDIO UMETUFANYA TUONEWE, TUNYANYASWE NA KUPUUZWA NA SASA TUNATAKA MAPINDUZI, ipo siku watu wataamua kwa pamoja kwani wanaolindana na kugawana rasilimali zetu ni wachache
 
Back
Top Bottom