Nyama mabuchani zinapuliziwa Rungu!!! Take care... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyama mabuchani zinapuliziwa Rungu!!! Take care...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tuko, Jan 16, 2012.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Uchunguzi wa kuaminika uliofanyika katika maduka mengi Dar, Moro na miji kadhaa mingine umegundua kuwa wauza nyama wamekuwa wakifanya mchezo hatari wa kupulizia nyama sumu za kuua wadudu ili kuzuia inzi. Sumu zinazotumika sana sana ambazo watu wengi hutumia kuua mbu ni rungu, Hatari, expel, Baygon, Hit, doom na nyinginezo.
  Katika maduka mengi siku hizi ukienda utaona nyama imetundikwa sehemu ya wazi lakini hakuna inzi. Wafanyabiashara wa nyama wameona kuwa hiyo ndiyo mbinu ya kuvutia wateja ambao wengi hawapendi kununua nyama ambayo imekaliwa na inzi.
  Uchunguzi huo ulifanyika kwa kuwauliza wauza nyama ambao baadhi walikiri kufanya hivyo ili kuvutia biashara. Uchunguzi pia umebaini kuwa pamoja na kufanya zoezi hilo kwa usiri mkubwa, baadhi ya wanunuzi wamekuwa makini kwa kuinusa nyama wanayonunua, kwani kwa kufanya hivyo harufu ya 'sumu' huwa dhahiri.

  Napenda kuwatahadharisha tunapoenda kununua nyama tuwe makini, maana madawa haya japokuwa yanasemwa kuwa hayana madhara makubwa kwa binadamu, lakini mojawapo ya ingredient yake (piperonyl butoxide) iliyomo kwenye hizi sumu, inafahamika kuwa ina madhara makubwa kwenye kukua na kukomaa kwa ubongo hasa kwa watoto.

  Source; mimi mwenyewe ambaye nimeshiriki kwenye uchunguzi huu.
   
 2. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Wabheja sana....
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Khaaa!..
   
 4. m

  mhondo JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kwanını wasııweke kwenye makabatı ya vıoo?
   
 5. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ahsante sana.
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Naweza kukubaliana nawewe kwani ukienda buchani mida ya sa 8 mchana kuendelea utakuta nzi wengi sn wamekufa wametapakaa chini ukiuliza wanakwambia wameweka dawa, je ni dawa gani hy? Yaweza kuwa ni moja kati ya hz ulizotaja, NASHUKURU MUNGU KWANI NILISHASITISHA ZOEZI LA KULA NYAMA SIKU NYINGI SN KWA KUHOFIA MADHARA YAKE.
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Lol! Kwanini wasile keki?
   
 8. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #8
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Una heri sana wewe uliyeweza kusitisha kula nyama. Wengine nyama ndo chakula kwetu...

  Hata hivyo sijui unakula nini kisicho na madhara...
   
 9. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  You don't mean it... tell me it's a joke!
   
 10. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #10
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  ha ha ha ha... Umenikumbusha siku baba yangu alikuja kwenye harusi mjini akalishwa keki, baadae ananiuliza eti kwa nini walidanganya wanampa keki alafu wakampa kipande cha andazi? Yeye anajua kuwa keki ni ndafu...
   
 11. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #11
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  I am not joking and you can test it.. Nenda buchani, chukua nyama alafu inuse... utasikia. Huwa hata ikipikwa bila kuwekwa viungo vingi. you smell it. Na siku hizi imekuwa common sana...
   
 12. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #12
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  joto litaiharibu.
  Au waunganishe hayo makabati na AC?
   
 13. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #13
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  You still think it is a joke?!, mimi nimeshuhudia mwenyewe expel ikipulizwa kwenye nyama na nzi wakidondoka.
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Jan 16, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  nyama ya kuku wa kienyeje nafuga mwenyewe,maharage nalima mwenyewe na mbogamboga pia nalima mwenyewe,
   
 15. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #15
  Jan 16, 2012
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Inasemekana na samaki wanawahifadhi kwa dawa za kuhifadhia maiti, samaki wakavu wanwapak thiodane kidogo na mafuta ya samaki
   
 16. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #16
  Jan 16, 2012
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kabichi zinapuliziwa ngao ile dawa ya mbu ili wadudu wasiziharibu, JE tutafika?
   
 17. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #17
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  mimi na nyama za mabuchani basi tena,nitakuwa nawahi saa 11 pale machinjioni moro nachukua kabla ya mapolizio ta sumu

  la sivyo ufugaji wa kuku wa kienyeji utaendelea

  tuwe makini jamani
   
 18. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #18
  Jan 16, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,597
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Kitimoto wanalishwa Arv's ili wakue fasta, chips nazo twaambia kuna sehemu zakaangwa na mafuta ya transfoma, watz tunaenda mbona ubinadamu umeisha mioyoni mwetu.....Mungu tusaidie
   
 19. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #19
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,758
  Trophy Points: 280
  Jamani ill be the first
  to die! Nyama km vile
  nimechanjwiwa!
  Asubuhi nyama mchana
  hiyohiyo
  saiv nakula ugal wa
  muhogo na nyama ya kima! Ngoja ntafte
  seremala antengezee cascade kabisaaa!
   
 20. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  kama ni kweli basi kuna haja ya kuwapima akili zao inawezekana zimeloose
   
Loading...