Ni kwa afya yako, zingatia sana.

Ni kwa afya yako, zingatia sana.

maneka

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
835
Reaction score
1,194
Wadau hongereni kwa mapambano ya kimaisha. Naomba niwaeleze mtazamo wangu juu ya ukweli wa kimazingira, juu ya vyakula hasa NYAMA MABUCHANI NA SAMAKI MASOKONI NA BUCHANI.

Baada ya tarifa kwenye vyombo vya habari kutokea Mwanza ilivyosemekana kuwa inasemekana baadhi ya wafanya biashara wasio waaminifu kutia dawa au maji ya kuoshea maiti kwenye vyakula hivyo ili kuhifadhi visiharibike, nimefanya kuchunguza kwa macho kwa kigezo chepesi kabisa.

Nimejionea vyakula hivi masokoni INZI kwa maana ya wadudu hawasogelei kabisa kwenye nyama na samaki waliowengi masokini.

Sasa swali ni kwa nini Inzi wasisogee kwenye nyama na samaki hao? Hii si hali ya kawaida. Inasemekana magonjwa mengi yasiyoambukiza kama vile Kansa, sababu yake ni kemikali zinazo tiwa kwenye vyakula hivi ili visioze au kufukuzia inzi ili wateja waone kuna usafi na hivyo wavutike kununua. Ila usalama wake ni mdogo kwa afya ya walaji.

Ombi langu ni kwamba viongozi wetu wenye mamlaka walitazame na hili ili kulinda afya na ustawi wa Watanzania kabla ya madhara kujitokeza zaidi.

Unapo nunua Nyama au Samaki ni vizuri kuwa makeni na kipimo cha uwepo wa inzi ni ishara ya usalama wa chakula. Japo ukiona inzi buchani wapo ila hawagusi nyama yaani wanaishia kwenye kuta bila kusogelea nyama kuwa makini zaidi.

Nimechunguza baada ya kupokea taarifa siku chache juu ya lisemwalo kwenye taarifa ya hivi kaeibuni.

Ukiona inakufaa chukua hatua ukiona ni porojo na uvumi usio na maana potezea. Nimeona nikujuze tu kama tahadhari.
 
Sasa swali ni kwa nini Inzi wasisogee kwenye nyama na samaki hao? Hii si hali ya kawaida. Inasemekana magonjwa mengi yasiyoambukiza kama vile Kansa, sababu yake ni kemikali zinazo tiwa kwenye vyakula hivi ili visioze au kufukuzia inzi ili wateja waone kuna usafi na hivyo wavutike kununua. Ila usalama wake ni mdogo kwa afya ya walaji.

Ombi langu ni kwamba viongozi wetu wenye mamlaka walitazame na hili ili kulinda afya na ustawi wa Watanzania kabla ya madhara kujitokeza zaidi.
Kuna watu wanautwa bwana na bibi afya hao ni hatari sana, ndiyo wanaozembea kufanya kazi ya ukaguzi wa vyakula
 
Kuna watu wanautwa bwana na bibi afya hao ni hatari sana, ndiyo wanaozembea kufanya kazi ya ukaguzi wa vyakula
Yawapasa kutilia mkazo wa hali ya juu sana. Hii ni afya ya watu. Bila hivo hata TOZO haitapatikana kwa mgonjwa
 
Ila jamani wapo wafanyabiashara wanaozingatia usafi kiasi kwamba inzi hawawezi kuwa wengi. Nashauri tusihamasishe uchafu kwa kisingizio cha uwepo wa nzi kama kiashiria cha ubora wa chakula
 
Ila jamani wapo wafanyabiashara wanaozingatia usafi kiasi kwamba inzi hawawezi kuwa wengi. Nashauri tusihamasishe uchafu kwa kisingizio cha uwepo wa nzi kama kiashiria cha ubora wa chakula
Naungana nawe, ila kahakiki na jiulize kuna nini nyama iko mahala pa wazi halafu hakuna inzi anagusa. Leo hii mimi kwa macho yangu nimeona haya. Ndugu nawe chukua muda wa kulifanyia kazi, sokoni unaingia bure haulipii, nenda fanya kautafiti!!!!
 
Back
Top Bottom