Nyama mabuchani zinapuliziwa Rungu!!! Take care...

Kabichi zinapuliziwa ngao ile dawa ya mbu ili wadudu wasiziharibu, JE tutafika?
MBOGAMBOGA ZINAZOONGOZA KWA KUPULIZIWA DAWA NI CHINESE NA CABAGE nyanya nazo zinawekwa dawa, ndo mana nikaamua kujilimia vimboga vyangu mwenyewe
 
Hii habari imewafikia wizara ya afya? Je na nyie mliogundua hivyo mmechukua hatua gani?
 
Hii habari imewafikia wizara ya afya? Je na nyie mliogundua hivyo mmechukua hatua gani?

Ni hatar kupublish habari kama hii mkuu. Tulishampoteza mwenzetu aliyekomalia hatchery moja kule Moshi. We have to b careful tunapocompromise maslahi ya watu.
 
Kwa siku kadhaa tuligundua watu wanashindwa kutengeneza mtindi kwa maziwa yanayonunuliwa mtaani. Tulitest samples chache tukagundua maziwa mengi yana kiwango kikubwa sana cha antibiotics. yan mtu anatibu ng,ombe, na kumkamua kabla dawa haijaisha mwilini.
 
ni hatar kupublish habari kama hii mkuu. Tulishampoteza mwenzetu aliyekomalia hatchery moja kule moshi. We have to b careful tunapocompromise maslahi ya watu.

maslah ya watu wachache inayomiza halaiki,mulika wooote
pambav
 
Naomba tule na tuishi kwa imani, mbona hata ajali zinaua sana??unadhani tutaishi milele??kila kitu kina madhara, sasa tule nini?sio kila mtu anaweza kulima au kufuga jamani....dah...Tatizo binadamu anataka kuishi milele wakati sisi wote ni wasafiri..tengenezeeni njia zenu
 
Kwa wale hambao hawana taarifa hii:

Uchunguzi wa kuaminika uliofanyika katika maduka mengi Dar, Moro na miji kadhaa mingine umegundua kuwa wauza nyama wamekuwa wakifanya mchezo hatari wa kupulizia nyama sumu za kuua wadudu ili kuzuia inzi. Sumu zinazotumika sana sana ambazo watu wengi hutumia kuua mbu ni rungu, Hatari, expel, Baygon, Hit, doom na nyinginezo.

Katika maduka mengi siku hizi ukienda utaona nyama imetundikwa sehemu ya wazi lakini hakuna inzi. Wafanyabiashara wa nyama wameona kuwa hiyo ndiyo mbinu ya kuvutia wateja ambao wengi hawapendi kununua nyama ambayo imekaliwa na inzi.

Uchunguzi huo ulifanyika kwa kuwauliza wauza nyama ambao baadhi walikiri kufanya hivyo ili kuvutia biashara. Uchunguzi pia umebaini kuwa pamoja na kufanya zoezi hilo kwa usiri mkubwa, baadhi ya wanunuzi wamekuwa makini kwa kuinusa nyama wanayonunua, kwani kwa kufanya hivyo harufu ya 'sumu' huwa dhahiri.

Napenda kuwatahadharisha tunapoenda kununua nyama tuwe makini, maana madawa haya japokuwa yanasemwa kuwa hayana madhara makubwa kwa binadamu, lakini mojawapo ya ingredient yake (piperonyl butoxide) iliyomo
kwenye hizi sumu, inafahamika kuwa ina madhara makubwa kwenye kukua na kukomaa kwa ubongo hasa kwa watoto.
 
Una heri sana wewe uliyeweza kusitisha kula nyama. Wengine nyama ndo chakula kwetu...

Hata hivyo sijui unakula nini kisicho na madhara...

Kuna hawa kuku wa mtumba hawa wenye mahips kama binadamu. Kuku hawana hata uwezo wa kukimbia, mi nilishaacha kuwala siku nyingi nikawa nakula nyama ya buchani. Kumbe huku nako wanaipiga rungu. Aisee!
 
Back
Top Bottom