dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,496
- 3,461
SERIKALI imetuma kikosi maalum cha askari wa kupamba na ujangili Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora ili kukabiliana na nyoka aina ya Koboko ambao hadi sasa wamesababisha vifo vya watu wanne.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati akizungumza na waandishi wa habari bungeni mjini hapa.
"Jana (juzi), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, aliniambia nyoka aina ya koboko walivamia kijiji kimoja Urambo, na wale nyoka ni hatari sana huwezi kumpiga kwa risasi,"alisema
Alisema idadi ya nyoka katika eneo la Urambo imekuwa hatarishi kwa hiyo, ametuma kikosi maalum dhidi ya ujangili cha Tabora.
"Nimeagiza waende wakakae na hao wanakijiji waangalie jinsi ya kuwaua, tatizo huwezi kuwapiga hao nyoka kwa bunduki, hata ukiwa na bunduki atakurukia na kukuua, uwezo wake wa kukimbia ni mkubwa,"
"Kwa hiyo wananchi wanaoutaalam mkubwa kushinda wale wahifadhi kwa hiyo nimeagiza wakae na wananchi watafute njia za kuwamaliza,"alisema
Aliwataka wakazi wa Urambo kutoandamana kwenda katika ofisi za mbunge wao Sitta kwa kuwa serikali imeshachukua hatua za kuwauwa nyoka hao.
Chanzo:Tanzania daima