Nyalandu atuma kikosi kazi kumaliza nyoka wa Koboko Urambo

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,364
2,000

SERIKALI imetuma kikosi maalum cha askari wa kupamba na ujangili Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora ili kukabiliana na nyoka aina ya Koboko ambao hadi sasa wamesababisha vifo vya watu wanne.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati akizungumza na waandishi wa habari bungeni mjini hapa.

"Jana (juzi), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, aliniambia nyoka aina ya koboko walivamia kijiji kimoja Urambo, na wale nyoka ni hatari sana huwezi kumpiga kwa risasi,"alisema

Alisema idadi ya nyoka katika eneo la Urambo imekuwa hatarishi kwa hiyo, ametuma kikosi maalum dhidi ya ujangili cha Tabora.

"Nimeagiza waende wakakae na hao wanakijiji waangalie jinsi ya kuwaua, tatizo huwezi kuwapiga hao nyoka kwa bunduki, hata ukiwa na bunduki atakurukia na kukuua, uwezo wake wa kukimbia ni mkubwa,"

"Kwa hiyo wananchi wanaoutaalam mkubwa kushinda wale wahifadhi kwa hiyo nimeagiza wakae na wananchi watafute njia za kuwamaliza,"alisema

Aliwataka wakazi wa Urambo kutoandamana kwenda katika ofisi za mbunge wao Sitta kwa kuwa serikali imeshachukua hatua za kuwauwa nyoka hao.

Chanzo:Tanzania daima
 
Asa'rile

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
439
195
labda taarifa kidogo kuhusu aina hii ya nyoka Koboko wakoje kwa picha na sumu yake inaathiri kwa kiwango gani, msaada tutani..:becky:
Ni nyoka warefu sana, from 10 - 13 ft, wana kichwa kama cha kuku-jogoo, hata wakati wa alfajr huwa wanawika kama jogoo!

Itabidi hao askari wavamie mapori ya kuanzia mbuga za Usisya, ushokola,Mabama, usoke, ichencha, Urambo zote, kaliua, hadi ng'ambo ya malagarasi kule nguruka.

wana sumu kali sana kupita ile ya Cobra (hata hao cobra pia ni wengi sana mkoani Tabora).
 
C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
4,934

wana sumu kali sana kupita ile ya Cobra (hata hao cobra pia ni wengi sana mkoani Tabora)
Mkuu acha fiksi
Koboko hana kichwa cha kuku wala jogoo
Koboko ni Spices fulani ya Cobra ukimuona koboko unaweza fikiri ni Cobra anainua kichwa kama Cobra ila tofauti ya koboko na Cobra ni kuwa Koboko wanapatikana huku nchi za tropic na Kobra anapatikana sana Asia

Yaani ni sawa sawa na Cheetah, Tiger na Leopard

Sema koboko ni aggressive, yuko sharp na faster
Hizo za ana kichwa cha kuku sijui bla bla gani ni uzushi mtupu

Nimeshakutana nao two times mara ya kwanza nilipokuwa na NGO moja hivi waliokuwa attached na animal planet ndio nikawajua vyema

Mara ya pili nilikutana nao kwenye msitu wa pemba mpazi story yake ni scary kidogo tulikuwa na wazungu tunatoka skonge tunaenda mbeya ndani ya gari alikuwa jamaa ambaye ndio mwenyeji wetu (Local) jamaa alikuwa ana dawa zake za kienyeji

Kufika pemba mpazi tukapata pancha na tukawa hatuna spare ikabidi tuagize spare skonge sasa ikabidi tukoke moto pale just imagine kati kati ya huo msitu yule jamaa akachukua dawa akazungushia territoty yetu kwamba hiyo territory sio simba, sio mbung'o wala sio nyoka wa aina yeyote atakayesogea na kweli baada ya muda akapita nyoka ambaye it looks like Cobra ila mweusi yule jamaa akatuambia huyo ndio mwenyewewe the One KOBOKO.. Baadae nitawawekea picha yake sema niko kwenye mishe mishe

So story za kuwika sijui kichwa cha kuku ni uongo
Ila ni kweli anaweza kuingia kwenye darasa la wanafunzi 45 na baada ya dakika 5 wanafunzi wote wakawa maiti

Na si kweli anaweza kukwepa risasi ila kutokana na movement zake za kwenda round and round huku anakuja kwako kwa kasi ni vigumu kupata clear shot so kumuua ni kazi
koboko anaweza kabisa akawa ni huyu

na kobra wa kawaida ni huyu

na black mamba ni mwingine kabisa na yeye ni huyu
todauti kati ya black mamba na cobra na koboko ni kwamba black mamba hata hatuni sana kama kobra na koboko ila kobra na koboko ukiwaangalia kwa haraka haraka unaweza sema ni cobra na ndio maana hakuna official name ya koboko kwa sababu wote huwa wanawawaita ni kobra
 
lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,498
0
Ni nyoka warefu sana, from 10 - 13 ft, wana kichwa kama cha kuku-jogoo, hata wakati wa alfajr huwa wanawika kama jogoo!
Itabidi hao askari wavamie mapori ya kuanzia mbuga za Usisya, ushokola,Mabama, usoke, ichencha, Urambo zote, kaliua, hadi ng'ambo ya malagarasi kule nguruka.
wana sumu kali sana kupita ile ya Cobra (hata hao cobra pia ni wengi sana mkoani Tabora)
Aiseee ningekuwa mwenyeji wahuko naona ndugu wangenisahau kabisaaa kwa hiyo storia yao niliyoipata hawa ni viumbe hatari sana kuishi nao kijiji kimoja.
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
11,087
2,000
Inasikitisha kuwa bado karne hii tunafikiri kwenda kuwinda nyoka wakiwa katika mapori yao ya asili, haki yao ya kuishi iko wapi?, hata hivyo, inaonesha serikali hii huwa haifuatilii kilicho fanyika katika eneo moja ili kiweze kufanyika katika eneo lingine.

Kama nyarandu angekuwa na wasaidizi makini( na kama anawasikiliza ama kuwashirikisha) atakuwa amejulishwa kuwa eneo la mazimbu ilipojengwa kambi ya wakimbizi wa south africana sasa ni campus ya Sokoine university of agriculture kulikuwa na nyoka wengi tena wa aina mbalimbali,

ili kuwaondoa nyoka hao, WAFADHIRI (DANIDA) waliojenga yale majengo (kambi) walipandikiza wadudu jamii ya sisismizi ambao wenyeji huwaita majimoto, wadudfu hawa walifukuza nyoka wote katika eneo lile kwani nyoka yeyote akikatika katikati yao akifanikiwa kutoka basi anabahati ya CCM.

Namshauri waziri nyarandu na brother SIX watumie utaalam na si mabavu ya magobole ya ant poaching squad.
ESCROW uyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
nyamwenga

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
661
0
Ni nyoka warefu sana, from 10 - 13 ft, wana kichwa kama cha kuku-jogoo, hata wakati wa alfajr huwa wanawika kama jogoo!
Itabidi hao askari wavamie mapori ya kuanzia mbuga za Usisya, ushokola,Mabama, usoke, ichencha, Urambo zote, kaliua, hadi ng'ambo ya malagarasi kule nguruka.
wana sumu kali sana kupita ile ya Cobra (hata hao cobra pia ni wengi sana mkoani Tabora)
mkuu waende hadi nsogolo na msitu wa ugala. Ila huyu nyoja jeuri yake mchana tu ila usiku humtoi nje hata kwa fimbo anaogopa sana bundi.

Kuna poli moja lipo katikati ya kijiji cha usimba na igwisi kata ya kazaroho mule wamowengi sn nimewinda sn mule na nilikuwa navaa kofia za wahandisi coz hawa nyoka wanapenda sana kugonga kichwani.

Kiujumla urambo yote na vijiji vyake hadi mapoli ya ulyankulu kwenye kijiji cha wachawi huko hawa nyoka ni wengi kama mchanga! Koboko hauawi kirahisi lazima uwe mbunifu la sivyo anakutanguliza ahela.

Aheri ya swira japo nao ni wengi ila wanauawa kirahisi cha msingi tu uwe jasiri!! Hicho kikosi kazi sijui kina idadi gani ya watu na sijui watajigawaje maana mapoli ya urambo yenye koboko yalivyokaa nahisi uwezekano wa kuyafikia yote ni mdogo sn!
 
uyui kwetu

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
1,029
2,000
Mkuu acha fiksi
Koboko hana kichwa cha kuku wala jogoo
Koboko ni Spices fulani ya Cobra ukimuona koboko unaweza fikiri ni Cobra anainua kichwa kama Cobra ila tofauti ya koboko na Cobra ni kuwa Koboko wanapatikana huku nchi za tropic na Kobra anapatikana sana Asia

Yaani ni sawa sawa na Cheetah, Tiger na Leopard

Sema koboko ni aggressive, yuko sharp na faster
Hizo za ana kichwa cha kuku sijui bla bla gani ni uzushi mtupu

Nimeshakutana nao two times mara ya kwanza nilipokuwa na NGO moja hivi waliokuwa attached na animal planet ndio nikawajua vyema

Mara ya pili nilikutana nao kwenye msitu wa pemba mpazi story yake ni scary kidogo tulikuwa na wazungu tunatoka skonge tunaenda mbeya ndani ya gari alikuwa jamaa ambaye ndio mwenyeji wetu (Local) jamaa alikuwa ana dawa zake za kienyeji

Kufika pemba mpazi tukapata pancha na tukawa hatuna spare ikabidi tuagize spare skonge sasa ikabidi tukoke moto pale just imagine kati kati ya huo msitu yule jamaa akachukua dawa akazungushia territoty yetu kwamba hiyo territory sio simba, sio mbung'o wala sio nyoka wa aina yeyote atakayesogea na kweli baada ya muda akapita nyoka ambaye it looks like Cobra ila mweusi yule jamaa akatuambia huyo ndio mwenyewewe the One KOBOKO.. Baadae nitawawekea picha yake sema niko kwenye mishe mishe

So story za kuwika sijui kichwa cha kuku ni uongo
Ila ni kweli anaweza kuingia kwenye darasa la wanafunzi 45 na baada ya dakika 5 wanafunzi wote wakawa maiti

Na si kweli anaweza kukwepa risasi ila kutokana na movement zake za kwenda round and round huku anakuja kwako kwa kasi ni vigumu kupata clear shot so kumuua ni kazi
naongezea hapo anagonga Zaidi utosini anakimbia sana na pindi anapokufikia husimama na ni lazima akuzidi urefu ili azma yake yakukugonga utosini. kwetu tulimuua mmoja kwa mtu mmoja kubeba ndoo iliyojaa uji wa moto
 
Enoch Bonobo

Member
Nov 24, 2014
7
0
Koboko hauwawi kibabe na buduki wajomba bali kwa njia rahisi km kipande cha mti cha urefu wa two /three ft mponde nacho kikakamavu kwa kulenga lakin ukiwa umekilaza mara akikiona ataanza ujinga wake waku round round akiwa ameinua kichwa kwa kukuduata ndo atakpokutana nacho hapo ndo mwisho wa uhai wake ujue.
 
Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,509
2,000
Ni nyoka warefu sana, from 10 - 13 ft, wana kichwa kama cha kuku-jogoo, hata wakati wa alfajr huwa wanawika kama jogoo!

Itabidi hao askari wavamie mapori ya kuanzia mbuga za Usisya, ushokola,Mabama, usoke, ichencha, Urambo zote, kaliua, hadi ng'ambo ya malagarasi kule nguruka.

wana sumu kali sana kupita ile ya Cobra (hata hao cobra pia ni wengi sana mkoani Tabora).
Hao nyoka ni hatari! Usiombe ukutane nao
 
wakulichomeka

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
498
195
labda taarifa kidogo kuhusu aina hii ya nyoka Koboko wakoje kwa picha na sumu yake inaathiri kwa kiwango gani, msaada tutani..:becky:
Hao nyoka nihatali sana wanasum kali akikuuma humalizi dakika tano lazima ufa naanapo taka kuuma maranyingi hulenga utosini rangi zao ni nyeupe wanamictari kama yanjano shingoni wengine wakijivu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
wakulichomeka

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
498
195
Nilienda tabora kunanyoka wengi sana yani kukutana nanyoka nijambo la kawaida ila koboko ninoma hata hao walio enda wawe makini nyoka hatari sana hao

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom