Nyalandu atuma kikosi kazi kumaliza nyoka wa Koboko Urambo

Nyoka wa kumuogopa zaidi nadhani ni kifutu na ndie hasa anayeongoza kwa kuua watu kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

kifutu mtembea upande upande, hatari sana huyo.

Nimeipenda sana hii thread. Kwa sisi ambao hatujaishi vijijini tunajifunza kitu.

Kifutu anaitwaje kwa Kizungu? Nataka nimsome naye habari zake. Nimemsoma huyu Black Mamba aisee ni Nyoka hatari sana na inadaiwa kwamba ndiye the world's most dangerous snake.
 
Eeh jamani eeeh. Mbona tunatishana mchana???

Kama kuna mwenye pic na video atupie kama mbwai mbwai tuu.

Mimi mwenyewe imenitisha sana, nilikuwa ninasoma maelezo ya wadau hapa na experiences zao na huyu Nyoka aisee inaonekana ni Nyoka hatari sana. Nimemsoma habari zake ndo nimezidi kuogopa zaidi.

Experts wenyewe wanadai huyu Black Mamba ndiye Nyoka hatari zaidi Duniani. Inawezekana na mdomo wake umekuwa mweusi namna ile kwasababu ya ukali wa sumu yake.
 
ahsante kwa kunifungua macho, sikua najua yote haya..

kwa kuongezea...mbinu gani zinaweza kusaidia kukabiliana nae.

Kaka Morphine hao wanaenda kula posho na matunda pori tu hasa yanayoitwa nhondwa maana ndo msimu wake huu. Huyo nyoka ni mtalaamu wa kusoma mazigira hakuna mfano. Usiku hutoa kichwa shimoni na kuanza kupiga kelele kama msuguano wa msumeno wa kukatia mbao usiotumia umeme. Nyoka hao huhama wenyewe kila pori linapokuwa linafyekwa (uharibifu wa mzigira unapofanywa hasa ukataji miti). Hakuna watakachofanikiwa labda wapige mabomu kama yale ya Syria au kuteketeza miti yote hasa aina ya "migobeko" ambayo ndio beach zake koboko. Mie nilicheka sana baada ya kumuona Nyalandu akiwahadaa wana Urambo. Njia nyingine ya kienyeji ni pamoja kumuuita Koboko kwa style ya mluzi ukiwa umetengeneza banda la miti ya kijani japo na imani za dawa za kienyeji hutumika. Wakati tukiwinda ndege kwa style ya mluzi koboko alikuwa anatuibukia mara kwa mara lakini ujasiri wa kupambana nae ulikuwa unatoweka na kila mtu kutelekeza ndege na koboko anajilia na kusepa zake. Ni kama hadithi lkn amini usiamini. Kwanza dawa kama hizo waliokuwa nazo washaaga dunia na mara nyingi zilikuwa zinapatikana kwa Wagoyangi (malenga wa ngoma za kucheza na nyoka)
 
Mkuu acha fiksi
Koboko hana kichwa cha kuku wala jogoo
Koboko ni Spices fulani ya Cobra ukimuona koboko unaweza fikiri ni Cobra anainua kichwa kama Cobra ila tofauti ya koboko na Cobra ni kuwa Koboko wanapatikana huku nchi za tropic na Kobra anapatikana sana Asia

Yaani ni sawa sawa na Cheetah, Tiger na Leopard

Sema koboko ni aggressive, yuko sharp na faster
Hizo za ana kichwa cha kuku sijui bla bla gani ni uzushi mtupu

Nimeshakutana nao two times mara ya kwanza nilipokuwa na NGO moja hivi waliokuwa attached na animal planet ndio nikawajua vyema

Mara ya pili nilikutana nao kwenye msitu wa pemba mpazi story yake ni scary kidogo tulikuwa na wazungu tunatoka skonge tunaenda mbeya ndani ya gari alikuwa jamaa ambaye ndio mwenyeji wetu (Local) jamaa alikuwa ana dawa zake za kienyeji

Kufika pemba mpazi tukapata pancha na tukawa hatuna spare ikabidi tuagize spare skonge sasa ikabidi tukoke moto pale just imagine kati kati ya huo msitu yule jamaa akachukua dawa akazungushia territoty yetu kwamba hiyo territory sio simba, sio mbung'o wala sio nyoka wa aina yeyote atakayesogea na kweli baada ya muda akapita nyoka ambaye it looks like Cobra ila mweusi yule jamaa akatuambia huyo ndio mwenyewewe the One KOBOKO.. Baadae nitawawekea picha yake sema niko kwenye mishe mishe

So story za kuwika sijui kichwa cha kuku ni uongo
Ila ni kweli anaweza kuingia kwenye darasa la wanafunzi 45 na baada ya dakika 5 wanafunzi wote wakawa maiti

Na si kweli anaweza kukwepa risasi ila kutokana na movement zake za kwenda round and round huku anakuja kwako kwa kasi ni vigumu kupata clear shot so kumuua ni kazi

kuhusu kuwika hyo ni kweli.. Kwani mie ni mzaliwa wa kaliua pale ushokola nasema haya kwa kua nimejionea... Na karib kila siku utasikia watu wameua nyoka
 
Kaka Morphine hao wanaenda kula posho na matunda pori tu hasa yanayoitwa nhondwa maana ndo msimu wake huu. Huyo nyoka ni mtalaamu wa kusoma mazigira hakuna mfano. Usiku hutoa kichwa shimoni na kuanza kupiga kelele kama msuguano wa msumeno wa kukatia mbao usiotumia umeme. Nyoka hao huhama wenyewe kila pori linapokuwa linafyekwa (uharibifu wa mzigira unapofanywa hasa ukataji miti). Hakuna watakachofanikiwa labda wapige mabomu kama yale ya Syria au kuteketeza miti yote hasa aina ya "migobeko" ambayo ndio beach zake koboko. Mie nilicheka sana baada ya kumuona Nyalandu akiwahadaa wana Urambo. Njia nyingine ya kienyeji na dawa zingine za kienyeji ni kumuuita Koboko kwa style ya mluzi ukiwa umetengeneza banda la miti ya kijani,wakati tukiwinda ndege kwa style ya mluzi koboko alikuwa anatuibukia mara kwa mara lakini ujasiri wa kupambana nae ulikuwa unatoweka na kila mtu kutelekeza ndege na koboko anajilia na kusepa zake. Ni kama hadithi lkn amini usiamini. Kwanza dawa kama hizo waliokuwa nazo washaaga dunia na mara nyingi zilikuwa zinapatikana kwa Wagoyangi (malenga wa ngoma za kucheza na nyoka)

Wang'waa faza hapo kwenye red mimi mwenyewe nilimshangaa alikuwa anaongea utafikiri ni viumbe vyenye permanent address kuwa ukimfata kesho au keshokutwa utamkuta anakusubiri.
 
Mkuu acha fiksi
Koboko hana kichwa cha kuku wala jogoo
Koboko ni Spices fulani ya Cobra ukimuona koboko unaweza fikiri ni Cobra anainua kichwa kama Cobra ila tofauti ya koboko na Cobra ni kuwa Koboko wanapatikana huku nchi za tropic na Kobra anapatikana sana Asia

Yaani ni sawa sawa na Cheetah, Tiger na Leopard

Sema koboko ni aggressive, yuko sharp na faster
Hizo za ana kichwa cha kuku sijui bla bla gani ni uzushi mtupu

Nimeshakutana nao two times mara ya kwanza nilipokuwa na NGO moja hivi waliokuwa attached na animal planet ndio nikawajua vyema

Mara ya pili nilikutana nao kwenye msitu wa pemba mpazi story yake ni scary kidogo tulikuwa na wazungu tunatoka skonge tunaenda mbeya ndani ya gari alikuwa jamaa ambaye ndio mwenyeji wetu (Local) jamaa alikuwa ana dawa zake za kienyeji

Kufika pemba mpazi tukapata pancha na tukawa hatuna spare ikabidi tuagize spare skonge sasa ikabidi tukoke moto pale just imagine kati kati ya huo msitu yule jamaa akachukua dawa akazungushia territoty yetu kwamba hiyo territory sio simba, sio mbung'o wala sio nyoka wa aina yeyote atakayesogea na kweli baada ya muda akapita nyoka ambaye it looks like Cobra ila mweusi yule jamaa akatuambia huyo ndio mwenyewewe the One KOBOKO.. Baadae nitawawekea picha yake sema niko kwenye mishe mishe

So story za kuwika sijui kichwa cha kuku ni uongo
Ila ni kweli anaweza kuingia kwenye darasa la wanafunzi 45 na baada ya dakika 5 wanafunzi wote wakawa maiti

Na si kweli anaweza kukwepa risasi ila kutokana na movement zake za kwenda round and round huku anakuja kwako kwa kasi ni vigumu kupata clear shot so kumuua ni kazi

mkuu ulichoeleza ni kweli ila naomba nikusahihishe kidogo!

Kuhusu kuwika hawa nyoka ni kweli wanawika kama jogoo anaejifunza kuwika na maranyingi huwa wanawika nyakati za usiku sana na wanapowika huwa wanakuwa ndani ya shimo huku wametoa vichwa nje

km nilivyoeleza awali hawa nyoka usiku ni waoga sn kwasababu ni kitoweo cha ndege aina ya bundi na kwa sababu bundi nae mchana huwa anauoni hafifu basi huu ndio muda ambao koboko anautumia kufanya mambo yake. Na ukifika usiku kwa bundi ndio kumekucha basi muda huo koboko anatulia kwenye mapango kwa kuhofia kuwa kitoweo!!

Koboko huwezi kumkimbia na ukigundua amekuona ni heri usimame wima kuliko kukimbia japo kusimama maisha yako yatakuwa 50/50 maana uhai wako utakuwa mikononi mwa koboko. Njia ya kujiepusha nae ni aheri ukalala chini nakuhakikishi kamwe koboko hakugongi ukiwa umelala.

Huyu nyoka anatisha sn yataka ujasiri sn kukabiliana nae coz ukimkorofi ugomvi wake huwa hauishi na anaweza akafunga barabara yaani no body in no body out!!

Anasumu kali sn akikugonga lazima tuimbe palapanda!
 
Lakini mbona wanadai siyo mkorofi? Wanadai ni hadi umkorofishe, la sivyo akishaona kuna mzozo yeye Koboko anakimbia. Au ni stories tu za Wazungu wanatuzingua?
 
Black mamba wameenea maeneo mengi ya urambo ukikutana nae soma dua za mwisho, nilimuona akiwa kwenye mti kapumzika mkia ukiwa unaning'inia nikadhani nyani jamaa akasema kama umewahi sikia koboko ndio huyo lakini usijali
 
Wang'waa faza hapo kwenye red mimi mwenyewe nilimshangaa alikuwa anaongea utafikiri ni viumbe vyenye permanent address kuwa ukimfata kesho au keshokutwa utamkuta anakusubiri.

Nakwambia tuna mawaziri wa ajabu sana mmoja wapo ni huyu Nyalandu. Binafsi nilifahamu ameamua kujitoa lawama kwamba hakushughulikia taarifa ya hao nyoka. Nyoka anakimbia mithili ya upepo hasa kwenye nyasi na matawi halafu upeleke askari waliozoea kusindikiza watalii namagobore kupambana na koboko!!
 
Huyu ndio koboko
 
Attachments

  • untitled.png
    untitled.png
    14.4 KB · Views: 588
  • 10426810_639536366133912_2484027650184607508_n.jpg
    10426810_639536366133912_2484027650184607508_n.jpg
    57 KB · Views: 702
  • BALCK MAMBA.jpg
    BALCK MAMBA.jpg
    9.8 KB · Views: 658
  • BLACK MAMBA.jpg
    BLACK MAMBA.jpg
    6.8 KB · Views: 644
  • BLACK MAMBA.png
    BLACK MAMBA.png
    23.9 KB · Views: 653
Ni black mamba hao, wana uwezo wa kugonga ng'ombe 15 kwa dkk moja. Ni hatari sana. Wana uwezo wa kunyanyuka juu mpaka nusu ya urefu wake, na wana kasi sana. Hawapendi kelele na ndo mana wanagonga sana ng'omne. Kaa mbali na koboko, ni agressive.

Kifutu a.k.a puff adder ni wafupi, wametuna, wapole, wana pembe, hukaa kimya chini ya majani makavu wanafanana nayo kwa rangi. Huwa hawashambulii mpaka wakanyagwe. Akikuuma inakula kwako ndani ya nusu saa, ukipona kiungo alichokuuma kitakatwa kwa kuoza. Ni noma.
Lkn nyoka hatari kuliko wote ni coral snake. Hawa wako maji chumvi wana rangi nyeusi na nyekundu kama bangili.. Akikuuma inakula kwako fasta Escrow hadithi...
 
Back
Top Bottom