Nyalandu acha siasa katika misiba

Nyalandu acha siasa katika misiba

View attachment 509507 Kwa mara nyingine jana nimeshuhudia maajabu mengine ya wanasiasa kutaka kupiga kiki za nguvu mahali pasipo takiwa. Kulikuwa na sababu gani kuandaa meza na hotuba wakati wa kuwaaga wagonjwa waliokuwa wanahitaji dharula kama mlivyo tuambia awali?
Hivi waliokuwa wanahutubiwa hapo ni hao watoto au waliokuwepo hapo au taifa kwa ujumla?
Hivi ilikuwa sahihi kuwalaza wagonjwa hapo hadhara ili mtoe hotuba zenu? Kwa nini wagonjwa hawakuingizwa kwanza kwenye ndege ili muendelee na hizo hotuba zenu,au mliogopa ndege itaondoka kabla hamjamaliza kukiki?
Najua mtakasilika lakini huu ndio ukweli najiuliza mengi lakini naachia hapo, ni hayo tu waheshimiwa!!!
Makamera, movies, MA pic pic sana tuu
 
Kuna watu kama ingekuwa tunaruhusiwa kutoa mapendekezo ,ningependekeza wawe wanyamapori at least tungepata hata kitu kwenye utalii

Halafu mzazi unakuta huyu ni mtoto wako,mbaya zaidi kijana Wa kiume,hawezi kuganga na kupigana mwenyewe kwa ajili ya tumbo na familia yake,kutwa kuwashadadia wanaume wenzake duu
 
Nimekuona na nimekushangaa ukiwa busy Arusha unazengea zengea kama nzi karibu na bucha, unatafuta nini Arusha? Hivi huu msiba ni wa Taifa ama kuna masrahi ya watu hapa?

Hata kama una mashirika yako lakini kufikia hatua ya kumwambia mkuu wa mkoa eti pesa itàkayochangwa ihusike kujenga hospitali, si jambo baya lakini mbona haya sikuyaona ukiyasema kule Kagera kwenye tetemeko? Lwakatare alisimama akaomba misaada ya kisaikolojia kwa baadhi ya wahanga ila sijawahi kuisikia hata sauti yako moja. Ama kwako Tz ni hapo Arusha tu? Achia mbali kuzungumza, sikuwahi kukushuudia ukizengea kule hata kwenda kusema pole tu ila leo uko busy Arusha. Watanzania ubaguzi wetu, chuki na roho za kwanini tusipoangalia vitatupeleka pabaya, ubaguzi ni mkubwa sana. Na hawa wanaojiita viongozi wa siasa ndo wako mstari wa mbele kushadadia.

Nyarandu, siku ikitokea kwingine kama ilivyoyokea Arusha usiache kwenda kutoa msaada kwani kusaidia eneo unalotoka tu ukawaacha wengine wasiokuwa na wa kuwasaidia si sawa, unaleta tafsiri mbaya sana

Kweli kabisa na mwambie na umkanye aache siasa katika suala la Kamanda wetu Lissu hapo Nairobi
 
Connection gani amefanya? Yeye hana tofauti na wapiga zumali anavizia wazungu wamesharekebisha kila kitu ye anaingia katikati
Hata Nairobi kwa Lissu aache kupiga zumali maana sisi makamanda tumesharekebisha
 
Mbona ameshindwa kuwasaidia watu wa Singida? wazungu wale waliona huruma wenyewe hakuna cha Nyalandu wala Lema.
Kabisa Nyalandu hafai kwa kweli. Lazima tumtimue pia hapa Nairobi kwa Kamanda Lissu. Mnafiki sana huyo jamaa.
 
Kagera hapakuwa na Wazungu,
Mzungu hata akienda India kwa wabaguzi wa Rangi namba moja duniani atapewa heshima tele na tena atakabidhiwa na mke kabisaaa..!
kwa hiyo usishangae ya nyalandu kujikomba kwa hao Wazungu.....

Na sasa hivi Nyalandu kaanza kujikomba kwetu makamanda eti afanye mipango ya kumtafutia matibabu Lissu. Hatutaukubali unafiki wake huo.
 
Mojawapo ya kazi ya kiongozi ni kufariji.
BIG UP Mh.Nyalandu.
 
Maafa yale ni mtaji wa kisiasa kwa wengine........sadly!
Na nidyo maana hatutaki huyo Nyalandu atumie matibabu ya Kamanda wetu Lissu kujijenga kisiasa. Sisi makamanda tutachangishana mpaka mwisho tukisaidiwa na jeshi la mtu mmoja la kukodi Mange.
 
29037dcea971d5a7b8a67954d0503125.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwacheni nyalandu MTU wa watu. Agombee urais 2020
 
Na maafa haya ni mtaji wa kisiasa kwa kina nani mkuu!?
Tujifunze kuweka akiba ya maneno waungwana.


Bado ni mtaji kwa waliyoyafanya japo sio kwa result waliyo itegemea. With TL out of the way who will call the shots against the mighty?

Una lingine?
 
Back
Top Bottom