Nyalandu acha siasa katika misiba

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
17,034
7,590
Nimekuona na nimekushangaa ukiwa busy Arusha unazengea zengea kama nzi karibu na bucha, unatafuta nini Arusha? Hivi huu msiba ni wa Taifa ama kuna masrahi ya watu hapa?

Hata kama una mashirika yako lakini kufikia hatua ya kumwambia mkuu wa mkoa eti pesa itàkayochangwa ihusike kujenga hospitali, si jambo baya lakini mbona haya sikuyaona ukiyasema kule Kagera kwenye tetemeko? Lwakatare alisimama akaomba misaada ya kisaikolojia kwa baadhi ya wahanga ila sijawahi kuisikia hata sauti yako moja. Ama kwako Tz ni hapo Arusha tu? Achia mbali kuzungumza, sikuwahi kukushuudia ukizengea kule hata kwenda kusema pole tu ila leo uko busy Arusha. Watanzania ubaguzi wetu, chuki na roho za kwanini tusipoangalia vitatupeleka pabaya, ubaguzi ni mkubwa sana. Na hawa wanaojiita viongozi wa siasa ndo wako mstari wa mbele kushadadia.

Nyarandu, siku ikitokea kwingine kama ilivyoyokea Arusha usiache kwenda kutoa msaada kwani kusaidia eneo unalotoka tu ukawaacha wengine wasiokuwa na wa kuwasaidia si sawa, unaleta tafsiri mbaya sana
 
Kwanza hiyo kazi imefanywa na wale wazungu watatu na hilo shirika ndio limewasafirisha.

Nyalandu anatajwa kusaidia tu kuishawishi serikali kutoa passport lakini kazi kubwa imefanywa na wale wazungu watatu ambao ndio waliwatoa wale watoto kutoka kwenye lile gari lililopata ajali(wreckage) na kisha kuanza mipango ya kuwahamishia US kwa matibabu zaidi.

Sio maneno yangu haya na kwa ushahidi fungua hii link hapa chini:

Iowan missionaries help to save 3 kids in Tanzania bus crash

Yeye tunaweza kumshukuru kwa kuwa kiungo tu kati ya serikali na wasamaria hawa.
 
Nijuavyo mimi huyu Nyarandu anaishi Arusha. Sasa sioni kwa nini asishiriki kwenye msiba. Pia, si peke yake ambaye hakwenda kutoa pole kule Kagera, hata sizo alikuja kwenda wakati watani zake wameanza kusahau yakiyowakuta. Wacha wivu! Nyarandu abarikiwe kwa ila alilofanya katika kuwafariji wafiwa na kusaidia kwa namna yoyote aliyoweza.
 
Nijuavyo mimi huyu Nyarandu anaishi Arusha. Sasa sioni kwa nini asishiriki kwenye msiba. Pia, si peke yake ambaye hakwenda kutoa pole kule Kagera, hata sizo alikuja kwenda wakati watani zake wameanza kusahau yakiyowakuta. Wacha wivu! Nyarandu abarikiwe kwa ila alilofanya katika kuwafariji wafiwa na kusaidia kwa namna yoyote aliyoweza.

Kwani ndiyo Mbunge wa Arusha??
 
Watu hamna dogo, sasa wewe ndo unataka uongee? Kama kasaidia walau kuunganisha waathirika na Samaritans unataka akae kimya? Kakosea wapi alivyoongea ITV?
 
Hivi hii ndiyo siasa mlisema ilifanyika?? Nyalandu, tafuta tena na fedha kidogo uwaongezee wale wafiwa kwani nasikia zile zenyu za bunge zilipigwa panga. Usiishie tu kujenga hospitali kwanza bali ongeza kidogo rambi rambi ila upeleke kwa mkono wako mwenyewe.
 
You need to know Nyalandu ni mwenyekiti wa lile shirika hapa Tanzania na hata kabla ya wazungu wale kwenda ngorongoro wakakutana na ajal walkua wametoka Singida kukagua miradi wanayofadhili na walkua na Nyalandu kW wiki nzima sasa sjui shida yako we we mwenye post ni nin? Kuona Nyalandu akiratibu hiyo support au? Tuache ujinga wakati mwingine.Fanya na we we tuone ili tujifunze kwako
 
Back
Top Bottom