Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,741
- Thread starter
- #141
Nusu Siku Ndani ya Jeneza - 17-
"KABLA sijaendelea na somo langu la uhusiano wa nyota na maisha yenu binadamu, kuna jambo moja nataka niwaambie," alisema yule kiumbe huku akituangalia kwa zamu sote tuliokuwemo chumbani humo.
Alipofika kwangu , alinikazia sana macho na kuanza kunisogelea huku akinitazama kwa umakini kama aliyenifananisha.
"Unajua ninyi binadamu mnatushangaza sana, yaani mnasumbuliwa na vitu vidogovidogo sana wakati uwezo wenu ni mkubwa kuliko kiumbe yoyote huko duniani na hata huku kwetu!" aliendelea kufafanua huyo kiumbe baada ya kurudi kwenye eneo lake la awali na kutufanya tukae kimya sana na kuendelea kumsikiliza kwa umakini wa hali ya juu mno. Akaendelea
"Kitu kikubwa ambacho ni kidogo lakini kinawasumbua sana, ni kutokuwa na uamuzi wenye msimamo au kufanya mambo hata ambayo hayakuwa kwenye mipangilio maalumu."
Alipofikia hapo, akanyamaza kidogo na kuanza kutuangalia tena kama awali.
"Hamjawahi kumuona au kumsikia mtu akisema kuanzia leo sitaki kufanya jambo fulani lakini muda mfupi tu baadaye, unasikia au kuona akikifanya?" akatulia tena na kuendelea;
"Mfano unakuta mtu anasema, kuanzia leo sinywi tena pombe, nitatunza sana pesa zangu hadi nikamilishe lengo fulani.
"Lakini, saa chache mtu huyohuyo unamkuta baa akiwa na rafiki zake akizungusha raundi za bia hadi anaishiwa kabisa pesa, lakini akiamka asubuhi akiwa hana pesa anajuta sana, anajilaumu sana na kujiapiza kutorudia tena lakini atakapopata pesa tena anaendelea kufanya jambo lilelile la kunywa pombe na kupoteza pesa!"
Kila mmoja wetu alitingisha kichwa kuashiria kukubaliana na kiumbe huyo.
"Hapo inakuwa hivi, mtu huyo anakuwa na roho ya umasikini ambayo kila akipata pesa au kitu chochote cha thamani, inamuingia na kuanza kumpelekesha na baada ya kutimiza dhamira hiyo inamtoka na ndiyo hapo mtu anaanza kujilaumu ni kwa nini alifanya ufujaji wa namna hiyo.
"Au unakuta mtu amekaa mahali fulani, anapita mtu akiuza kitu ambacho hata hukuwaza kukinunua kabisa. Lakini anamaliza pesa yote na wakati mwingine kitu hicho hakina umuhimu hata kidogo.
"Hiyo yote ni kutokuwa na msimamo wa maamuzi hali ambayo hupandikizwa na roho hiyo niliyoitaja huko nyuma.
"Lakini watu wenye imani kubwa kabisa na mungu wenu, huwa hawakutani na mambo kama hayo. Ndiyo maana baadhi yenu wenye imani kubwa hata kama vipato vyao ni vya kawaida, maendeleo yao huwa yako juu sana kwa sababu hawana roho huyo mchafu, fuatilieni sana."
Kila mtu alikuwa kimya, tukimsikiliza kiumbe huyo. Ilikuwa ni elimu ambayo sikuwahi kuisikia mahali popote duniani!
"Ninyi binadamu mna uwezo mkubwa sana, ndiyo maana hata mungu wenu kabla hajawaumba, alisema aumbe watu wa kufanana naye! Kwa maneno mengine ninyi ni mfano wake! Si kwa sura bali kiuwezo japo si kwa asilimia zote.
"Sasa mbona mnayumbishwa na mambo madogo kama hayo? Ndiyo maana kutokana na imani yenu ndogo wengi wenu hukimbilia kwa waganga bila kujua kabisa kuwa hata hao waganga huongozwa na roho wachafu juu ya nyota zenu.
"Huko mbele nitafafanua zaidi kuhusu waganga wenu wa kienyeji na jinsi wanavyowaibia kwa kutumia nyota zenu, ila kwa sasa nilitaka niwagusie kidogo kuhusu imani kabla sijaendelea na somo hili la nyota.
"Angalia hata sisi, japo tuliasi, lakini tunawazidi mambo mengi sana kwa sababu tunakuwa na imani kwa mambo tuyatendayo.
"Mfano, kiumbe yoyote akiwa na imani pasipokuwa na shaka, anaweza kutembea hata juu ya maji! Lakini akiwa na mashaka kidogo tu, lazima azame.
"Ndiyo maana hata yule Petro, alipokuwa na yule nabii wenu alijawa na imani na akaweza kutembea juu ya maji lakini alipoanza kuwa na mashaka kidogo tu alianza kuzama!" alisema yule kiumbe na kutulia kidogo.
Alitoa mfano wa Petro kwa kutaja jina nabii wetu, akiwa na maana Yesu ila asingeweza kutaja jina Yesu kwani ni mwiko mkubwa sana kule kulitaja.
Je, nini kitafuata? Usikose Kufuatilia kesho wakati kama huu