Nusu siku ndani ya jeneza

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,305
2,000
EMMANUEL Muhuge Magende, mkazi wa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam anasimulia kisa alichowahi kukumbana nacho miaka mitatu (2010) nyuma baada ya kugongwa na gari dogo akiwa

anavuka barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni, jirani na msikiti.
Anasema: Nakumbuka ilikuwa tarehe kumi na tisa, mwezi wa saba, nilipanda daladala pale sokoni

Kariakoo. Hili daladala lilikuwa likienda Mwenge kupitia Kinondoni kisha kupita Morocco na kuunga Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.


Nilikaa kwenye siti ya kwanza mlangoni. Wakati naingia, kwenye siti hiyo alikaa mzee mmoja kwa makadirio ya umri alikuwa kama ana miaka sabini hivi.
Huyu mzee mimi nilipoingia tu, akasimama na kuniambia nikae pale ambapo pembeni yake palikuwa na abiria. Nilimkatalia kwa sababu daladala lenyewe lilijaa, sasa mzee kama yeye akiniachia siti mimi ambaye wakati huo nilikuwa na miaka 45 nilihisi si sawa.
Cha ajabu huyu mzee alilazimisha sana akisema yeye anakwenda kukaa siti ya nyuma. Ilifika mahali nilimkubalia, nikakaa yeye akatoka kuelekea nyuma lakini sikumfuatilia hadi kukaa kwake.
Muda huohuo, daladala liliondoka, likapita njia yake hadi Faya ambapo halikusimama kwa sababu nafasi haikuwepo. Kufika Magomeni ya Hospitali, daladala lilisimama, abiria walishuka wengi tu hadi nafasi ya kukaa watu wengine ikabaki. Wakati abiria wakishuka nilikuwa namwangalia mmoja baada ya mwingine ili kama kuna yule mzee nimwambie namlipia nauli, lakini hakuwepo, nikajua bado yupo ndani.
Daladala lilipoondoka hapo halikusimama Kituo cha Morocco Hotel mpaka Mkwajuni ambapo mimi nilikuwa nashuka. Kwa kuwa nilikuwa jirani na kondakta nilimwambia shusha hapo Mkwajuni, akagonga daladala likasimama. Nilisimama huku nikimwangalia yule mzee ili nimwambie namlipia, lakini sikumwona!
Nilishuka, kufika chini nikasimama ili kuvuka barabara maana nilikuwa naishi upande wa pili wa kituo hicho.
Cha ajabu sana nikamwona yule mzee kwa ng’ambo akiwa anatembea kwenda uelekeo uleule ninaokwenda mimi.
Nilivuka barabara haraka ili nimuwahi, lakini nikiwa katikati ya barabara hiyo gari dogo, jekundu, lilitokea upande wa Kinondoni Studio na kunifuata kwa kasi. Nilifanya jitihada zote kulikwepa lakini ilishindikana, likanigonga! Sikujua kilichoendelea.
***
Mbele yangu kulikuwa na jumba kubwa la kifahari, sikujua kama wanaishi wanadamu au la! Nilitembea kuelekea kwenye ile nyumba. Ilijengwa si kwa matofali wala simenti, ilionekana kama vioo vya kujitazamia ndivyo vilitumika sana.
Nilikuwa katika hali ya kuogopa sana, hivyo kufika kwangu kwenye nyumba ile kulikuwa na maana ya kuomba msaada. Kuogopa kulisababishwa na mazingira, sikuona jua, sikuona mawingu wala sikuona ardhi, nilitembea juu ya vioo.
Ili uingie mlangoni kulikuwa na ngazi tatu. Nilikanyaga ya kwanza na ya pili, nilipotaka kukanyaga ya tatu, mlango ulifunguka wenyewe nikaingia kama kwa kulazimishwa.
Ndani niliwakuta watu wengi weupe, naweza kusema walikuwa Wazungu pia naweza kusema walikuwa Waarabu, lakini hakukuwa na mtu mweusi hata mmoja.
Watu wote waliniangalia nilipokuwa naingia, wakanishangilia sana huku wengine wakiwa wanapiga vigelegele. Lakini pamoja na vigelegele hakukuwa na mwanamke.
Walikuwa wanaume wenye midevu mingi, warefu mfano wa watu warefu wakiwa wawili kwa kwenda juu hivyo mimi nilikuwa nawaangalia kwa juu.
Mmoja alinifuata na kunishika mkono. Akatembea na mimi hadi kwa wenzake, mmoja akanipokea hapo akanipeleka mbele ya jumba hilo ambako pia kulikuwa na mlango mkubwa kama niliouingia.
“Unajua uko wapi hapa?” aliniuliza.
“Niko ugenini.”
“Ni ugenini ndiyo, ni wapi?”
“Mimi sijui.”
“Ngoja nikuoneshe ulikotoka,” alisema yule mtu na kunitoa nje, tulitoka na yeye, akanyoosha mkono kuangalia juu huku akisema:
“Unakuona kule?”
Niliinua macho na kuangalia juu, nikaona dude kubwa likiwaka kama mwanga wa taa za kisasa.
“Umeona kule?” yule mtu aliniuliza.
“Ndiyo,” nilimjibu.
“Ni nini?”
“Dude.”
“Siyo dude, wewe umetoka kule.”
“Ina maana ile ni dunia?”
“Ile ni dunia, na pembeni yake unachokiona kidogo ni mwezi.”
“Huku sasa ni wapi?”
“Huku sasa ndiko wanakokuja watu waliokufa wakisubiri kupewa adhabu.”
“Ina maana mimi nimekufa?” nilimuuliza, akacheka sana kuonesha kwamba mimi ni mjinga sana kama sijui kama nimekufa.
“Unataka kujua kama umekufa au la!”
“Ndiyo, nataka kujua.”
Alinirudisha ndani ambapo hakukuwa na mtu hata mmoja, tukatembea kuelekea upande wa mashariki mwa jumba hilo hadi kwenye mlango mwingine mkubwa sana, ukafunguka wenyewe. Tuliingia ndani ambako tulikuta watu mchanganyiko, wengine weusi kama mimi wengine weupe.
Walikuwa wamekaa wakiangalia skrini moja kubwa sana. Ndani ya skrini hiyo kulikuwa na watu wanafanya mambo mbalimbali. Wengine walikuwa wanafanya zinaa, wengine wanaiba, wengine wanapigana, wengine wanachinja binadamu wenzao.
Kifupi ni kwamba watu walikuwa wakifanya madhambi ndicho nilichokibaini mimi.
Watu wote walikuwa wamekodolea macho ile skrini, lakini tulipoingia sisi wakageuka kutuangalia. Mmoja akauliza:
“Huyo naye haamini kama amekufa?”
Yule niliyekuwa naye akajibu:
“Ndiyo.”
Nilikaribishwa kiti nikakaa halafu skrini ikazimwa. Baada ya muda ikaanza kuonesha picha yangu. Nilionekana napanda daladala Kariakoo. Picha hiyo ikanionesha nikiwa nazungumza na yule mzee akisema anipishe kwenye kiti chake.
Cha ajabu, huyo mzee awali alionekana kama nilivyomwona mimi lakini ghafla akageuka, akawa mweupe kama watu niliowakuta kwenye lile jumba.
Tukio zima lilionekana, daladala likipita Magomeni, likakata kona kwenda Hospitali na kupita Hoteli ya Morocco hadi Mkwajuni.
Nilimwona yule mzee akitoka kwenye daladala kwa kupitia kioo cha mbele cha dereva kisha akavuka barabara kabla hata daladala halijasimama.
Nilionekana nashuka, natembea kwenda kuvuka barabara. Lile gari jekundu lilizuka tu palepale jirani yangu na kunigonga.


Je, kiliendelea nini? Tuonane jioni ...
 

Munkari

JF-Expert Member
Feb 9, 2013
8,090
2,000
Ndiyo mana huwa nasubiri hadi mwisho nilifaidi sana ile ya malkia wa masokwe yan nilikuwa nachagua tu muda gani nisome hadi nikaimaliza! Aagh we Mzizi ikiisha niite aisee!
 
Last edited by a moderator:

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,305
2,000
Mkuu mzizimkavu si umalizie tu ... mambo gani sasa ya kuanza kepeana genye tena?
Da! ndo nn sasa
duh! Ndo mana sipendagi riwaya
Unasoma nini kama hupendi Riwaya? hukulazimishwa kusoma wewe.
Heri nisingeanza kuisoma.
Hata kuweka (Like) Munashindwa? halafu munataka niweke Hadithi yote Ahhhhh wachoyo nyinyi ............................
Mbona umeiweka kidogo sana?
Hata kuweka (Like) Munashindwa? halafu munataka niweke Hadithi yote Ahhhhh wachoyo nyinyi ............................
Ningejua nisingesoma
Ndiyo mana huwa nasubiri hadi mwisho nilifaidi sana ile ya malkia wa masokwe yan nilikuwa nachagua tu muda gani nisome hadi nikaimaliza! Aagh we Mzizi ikiisha niite aisee!
Miujiza ama nini??,
Hata kuweka (Like) Munashindwa? halafu munataka niweke Hadithi yote Ahhhhh wachoyo nyinyi ............................
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,305
2,000
NUSU SIKU NDANI YA JENEZA - 2-


ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Tukio zima lilionekana, daladala likipita Magomeni, likakata kona kwenda Hospitali na kupita Hoteli ya Morocco hadi Mkwajuni.
Nilimwona yule mzee akitoka kwenye daladala kwa kupitia kioo cha mbele cha dereva kisha akavuka barabara kabla hata daladala halijasimama.
Nilionekana nashuka, natembea kwenda kuvuka barabara. Lile gari jekundu lilizuka tu palepale jirani yangu na kunigonga.
SASA ENDELEA


Nilijiona nilivyokuwa naweweseka kujitetea mpaka nagongwa na kunyooshanyoosha miguu kisha nikakata roho.
Lile gari jekundu baada ya kunigonga liligeuka palepale kurudi lilikotokea tena kwa kasi kisha likafutika. Nilishtuka sana, kumbe halikuwa gari halisi.
"Kwa hiyo ina maana kifo changu kilitengenezwa?" niliuliza katika hali ya kushtuka.
Wale watu wakacheka, lakini hawakunijibu chochote kuhusu swali langu ila mmoja akaniuliza:
"Unataka kujua msiba wako ulivyo nyumbani kwako?"
"Nionesheni nione."
Mmoja wao alisimama, akaenda pembeni, kuna sehemu kulikuwa na boksi jeupe sana, akaminya pembeni, ghafla pale kwenye skrini pakatokea watu wengi sana, wengine walikuwa wakilia kwa kuomboleza, wengine wakiwa wamelala chini.
Ilikuwa kama vile naangalia picha laivu, mpigapicha alitembeza kamera yake vizuri wakati mwingine aliwavuta waombolezaji mpaka karibu ambapo niliweza kuwatambua. Nilimtambua kaka yangu, anaitwa Sato, nilimwona mjomba wangu anaitwa Salehe, nilimwona mzee mmoja jirani yangu mkubwa anaitwa baba Naomi. Vijana mbalimbali wa mtaani pia niliwaona.
"Bado unataka tuendelee kukuonesha?" mmoja aliniuliza.
"Nionesheni mke wangu alivyo," nilisema huku macho yangu yakiwa bado kwenye skrini. Nikaona kamera ikitembea kutoka nje kwenda ndani, sebuleni kwangu! Mke wangu alikuwa akipepewa kwa sababu alipoteza fahamu kwa kulia.
Chini ya skrini hiyo wakati mke wangu akionekana paliandikwa maneno haya; mke wa marehemu Emmanuel Muhuge Magende akipepewa baada ya kupoteza fahamu kufuatia kifo cha mumewe.
Haya maneno yalikuwa yakitembea kutoka upande wa kulia kwenda kushoto, yaani ilikuwa kama natazama taarifa ya habari kwenye tivii.
"Ina maana wote wanaokufa huwa wanabahatika kuona misiba yao ilivyo kule duniani?" niliuliza kwa sauti.
"Ndiyo. Lakini ni wale wanaokufa wakiwa upande wetu tu."
"Sijawaelewa, upande wenu ni upi na mwingine ni upi?"
"Upande wetu ni kwa mkuu wetu, shetani mkuu, mwenye mamlaka kubwa katika dunia," alisema mmoja.
"Upande mwingine?" niliuliza nikiwaangalia kwa zamu.
Cha ajabu nilipouliza kuhusu upande mwingine, wote walinigeukia na kuniangalia kwa macho ya kutisha. Nikapeleka macho kwenye skrini, ilikuwa imezimwa.
Mtu mmoja akaja na kunishika mkono akanivuta, tukainuka na kuanza kutembea kuelekea kwenye mlango mmoja, hatua moja kabla ya kuufikia mlango huo ulifunguka wenyewe.
Tukaingia humo lakini tukakutana na mambo tofauti kabisa, hali ya humo ndani ilikuwa ya kutisha, kulikuwa kukiwaka moto kama wa vibatari au mwenge wa Uhuru iwe zaidi ya kumi.
Halafu mlikuwa na moshi mzito ulionifanya nikohoe kupita kiasi huku macho nayo yakianza kuwasha.
Tulikuwa tukitembea kuelekea sehemu nyingine, mimi sikujua ni wapi tunaelekea. Ghafla tukatokea kwenye uwanja mkubwa mlemle ndani, katikati ya uwanja kuna watu walikuwa wamekaa na kuuzunguka moto mkubwa sana ambao katika kuwaka kwake ulikuwa ukitoa mlio wa moto unavyofanya, ta! tata! ta!
Yule mtu alinipeleka kwa mwingine ambaye ni miongoni mwa waliokaa, lakini alionekana kama ni mkubwa au niseme ni bosi wao. Alinipokea na kunikaribisha niketi kwenye kiti kilichokuwa pembeni yake.
"Habari za jehanam bwana mdogo?" yule mtu alinisalimia, nikahamaki kwa kusema:
"Mi sijatoka jehanam, nimetoka duniani."
Alicheka kidogo, akasema kwani hujui kwamba dunia yote ni jehanam?"
"Siyo kweli."
Niliposema siyo kweli, akanyoosha kidole kwa pembeni kwenye ule uwanja, ikatokea skrini kubwa sana, ni kubwa kweli. Palepale nikaona jua linazama yaani kunakuchwa, halafu watu wanatoka majumbani, wengine wanakwenda kuiba, wengine wanakwenda kuingia nyumba za wageni kuzini.
Niliwaona watu wengine wanaingia baa kunywa pombe na kulewa sana hadi kupigana, kuuana. Niliwaona watu ambao kwa mavazi yao walionekana ni viongozi wa dini, walikuwa wakiingia nyumba za wageni na kufanya zinaa.
Huwezi amini, niliweza kuwaona askari polisi wakienda kuua mahali na kupora mali, nikawaona wake za watu, waume za watu nao wakisaliti ndoa waziwazi, nikawaona wachawi wakienda kuwaroga watu wema. Kifupi niliona kila aina ya uovu.
"Umeiona dunia yako?" yule mtu aliniuliza.
"Nimeiona ndiyo."
"Siyo jehanam pale?"
"Kusema kweli siyo jehanam, bali matendo ya binadamu ndiyo wanaiaharibu dunia kwa hiyo dunia si jehanam."
"Sisi huku ndiyo tunajua kwa sasa dunia ni jehanam. Unajua kwa nini sisi tumeamua dunia kuiita jehanam?"
"Si kwa sababu ya uovu wake."
"Si hilo tu, kuna lingine."
"Lingine kama lipi?"
Aliniangalia kwa muda kisha akasema:
"Mara nyingine tunatuma vijana wetu duniani kwenda kupeleka uovu mpya, lakini wanaporudi wanatuletea uovu mkubwa zaidi na mpya unaofanywa kwa ubunifu wa hali ya juu na akili za mwanadamu."
"Mfano kama nini?"
"Mifano ipo mingi tu. Sisi huku hatukuwahi kujua kama kuna dini itaruhusu waumini wake kuwa mashoga wakati vitabu wanavyovitumia kwenye nyumba zao za ibada tena wanavishika mikononi kila Jumapili vinakataza ushoga."
"Pia sisi hatukuwahi kutuma uovu duniani wa baba mzazi kumwingilia binti yake wa kumzaa mpaka kumjaza mimba na kujifungua mtoto."
"Sisi huku hatukuwahi kutuma uovu duniani wa mume kumchinja mkewe hadi kutenganisha kichwa chake."
Nilibaki namtumbulia macho kwani aliyokuwa akiyasema kama ni kweli ibilisi hausiki basi wanadamu wamekuwa watu wabaya zaidi kuliko ibilisi mwenyewe.
Yule mtu akaendelea kusema:
"Imefika hatua sisi huku mnaotuita mashetani tunakuja duniani kupata uovu mpya unaotungwa na vichwa vya binadamu, lakini siku zimekaribia sana, haya mambo yote yatawekwa wazi na kila mtu atajua nyinyi binadamu na sisi shetani nani muovu wa kweli."
Nilishangaa sana, nikamuuliza:
"Nyinyi si ndiyo mnauleta uovu wote duniani halafu wanadamu wanauchukua na kuanza kuufanyia kazi?"
Ili kujua zaidi usikose kusoma wiki ijayo kwenye gazeti hilihili.


Itaendelea kesho
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,305
2,000
NUSU SIKU NDANI YA JENEZA - 3-

ILIPOISHIA JANA:
Nilibaki namtumbulia macho kwani aliyokuwa akiyasema kama ni kweli ibilisi hausiki basi wanadamu wamekuwa watu wabaya zaidi kuliko ibilisi mwenyewe.
Yule shetani akaendelea kusema:
"Imefika hatua sisi huku mnaotuita mashetani tunakuja duniani kupata uovu mpya unaotungwa na vichwa vya binadamu, lakini siku zimekaribia sana, haya mambo yote yatawekwa wazi na kila mtu atajua nyinyi binadamu na sisi shetani nani muovu wa kweli."
Nilishangaa sana, nikamuuliza:
"Nyinyi si ndiyo mnauleta uovu wote duniani halafu wanadamu wanauchukua na kuanza kuufanyia kazi?"

NENDA NAYO MWENYEWE

"Uovu wa baba mzazi kumlawiti mwanaye wa kumzaa?"
Alipoona nimesimama kimya kwa muda mrefu, akasema:
"Sasa tuondoke, tumekuonesha kwa sehemu tu, huruma ya wakubwa wa huku umekubaliwa kuendelea kuoneshwa sehemu nyingine."
Safari hii nilipelekwa kwenye uwanja ambao ulionekana vizuri kwani ilikuwa ni mchana, nikamuuliza yule shetani.
"Mbona kule tulikotoka ni usiku hapa ni mchana halafu ni karibu sana, inakuwaje?"
Akanijibu kwamba, umbali tulioutumia kutoka tulipokuwa hadi pale ni kama siku nzima.
"Siku nzima kivipi wakati tumetembea dakika tano tu?"
Alicheka, akasema:
"Huku dakika kumi ni kama siku mbili."
Kwenye uwanja huo tulikuta wanadamu wakiteketea kwa moto mkali huku wakilia na kuomboleza, wengi walikuwa wakisema wamekoma hawatarudia tena.
Mimi na yule shetani tulisimama kwa mbali, lakini joto kali la ule moto lilitupata ikabidi tujikinge uso kwa viganja.
Wale watu wanaoungua walipotuona walinyoosha mikono kuashiria kwamba wanataka kusaidiwa haraka, walikuwa wakituita.
"Pale ni motoni?" nilimuuliza.
"Motoni bado, pale ni sehemu wanayochukua mazoezi kabla ya kufika siku ya kuingia motoni."
Niliogopa sana, moyoni nilisema kama motoni kwenyewe bado, watu wanalalamika vile, sijui hiyo siku itakuwaje?
"Una swali au maswali?" aliniuliza, nikatingisha kichwa kumkubalia kwamba nina swali.
"Huku ni makao makuu ya shetani?"
"Ndiyo."
"Shetani mwenyewe mkuu anaishi wapi?"
"Kwake."
"Kwake ni wapi?"
"Makao makuu."
"Naweza kupata bahati ya kuonana naye?"
"Mimi mwenyewe sijawahi kumwona."
"Sasa mnafanyaje kazi?"
"Tunapata maelekezo kutoka kwa wasaidizi wake wa karibu, wao ndiyo huwa tunaweka vikao nao."
"Oke, kule nilikotoka," nilianza kusema akadakia kwa kusema:
"Duniani."
"Ee duniani. Wengi tunaamini nyiye," akadakia kwa kusema:
"Mashetani."
"Ee mashetani. Mna sura mbaya, mna mapembe, mna nundu, ngozi zenu si kama zetu, miguu yenu ni kwato za ng'ombe, macho mekundu, meno marefu kama kijiko, mna kucha ndefu sana, wakatili, wauaji na wazua balaa siku zote, sasa mbona sijaona shetani wa aina hiyo?"
"Shangaa wewe, binadamu wote wanaamini hivyo kwa sababu ya kusikia. Mmekuwa mkituchora vibaya sana kwenye makaratasi ili tuonekane wabaya hata kwa maumbile.
"Kwanza nikwambie kitu, hakuna binadamu aliyebahatika kutuona sisi mashetani tukiwa duniani tunatenda kazi yetu."
Nilishtuka kusikia hivyo, kwani mara nyingi nimewahi kusikia watu wanatokewa na majini, nikamuuliza:
"Na wale wanaotokewa na majini si wanadamu?"
Alicheka sana, akasema:
"Hapo ndipo penye utata mkubwa, wanadamu wote mnaamini majini ndiyo sisi. Hilo ni kosa, sisi siyo majini, ila wote wanaowatengeneza majini uwezo wanapata kwetu.
"Lakini sisi siyo majini. Sisi ni malaika tulioasi, tukaja kuishi huku."
"Huku kunaitwaje?"
"Nikuulize wewe, kule duniani huku mnakuitaje?"
"Ujinini."
Akacheka sana, akasema:
"Nimeshasema, sisi si majini, sisi ni malaika tulioasi, kule duniani mnatuita mashetani, makazi ya majini ni baharini, katikati huko, sisi hapa ni sehemu yetu."
"Inaitwaje?"
"Hilo ni fumbo zito kwenu wanadamu, wengi mnaamini sisi tunaishi jehanam, lakini jehanam ni mahali ambapo hakuna viumbe wanaoishi, ila pako tayari kwa ajili ya waovu siku ya kiama."
"Hata watu?"
"Hata binadamu."
"Kuna tofauti ya binadamu na mtu?"
"Kubwa sana."
"Ni ipi hiyo?"
"Binadamu ni yule mwenye tabia za kidunia, hamwogopi Mungu, anaweza kuua, anaweza kufanya lolote baya kwa mwenzake."
"Mtu?"
"Anakuwa na matendo mema. Maana Mungu alipoumba alisema anaumba mtu kwa mfano wake, ubinadamu umetokana na baba yenu Adamu, ndiyo maana watu wote wanaitwa binadamu, yaani Bin Adamu.
"Kwani neno bin si linatumika kwa wanaume tu, sasa mbona hata wanawake wanaitwa binadamu?"
"Tangu kale wakati wa Adam, mwanamke hakuwa na hesabu katika jamii.
Ndiyo maana watoto wa Adam, Kaini na Abel walioa dada zao na hawakuwa kwenye hesabu ya watoto wa Adam.
"Wewe umeishi duniani siku zote, umewahi kusikia watoto wengine wa Adam zaidi ya Kaini na Abel?"
"Sijawahi."
"Jiulize walioa wapi? Walioa dada zao kwa sababu walikuwa hawaingizwi kwenye hesabu. Unajua sisi mashetani tunajua mengi kuliko nyiye."
"Mh! Mi siamini kama Adam alikuwa na watoto wengine."
"Alikuwa nao. Si Adamu tu, kuna mtu alikuwa anaitwa Yakobo, unamkumbuka?"
"Ndiyo."
"Alikuwa na watoto wangapi?"
"Kumi na mbili."
"Si kweli, alikuwa na watoto kumi na tatu, mmoja wa kike aliitwa Dina, alizaliwa kwa mkewe Leah, ila kwa sababu alikuwa mwanamke hakuingia kwenye hesabu."
Nilitingisha kichwa kuelewa, ghafla ule moto uliokuwa unawachoma wale watu waliokuwa wanateketea ukazimika, wakawa wanaonekana kwenye majivu mengi wakiwa wamebadilika rangi ya ngozi zao.
Nilisikia nikiitwa kwa jina:
"Emmanuel Muhuge Magende."
Nilishtuka sana, nikakaza macho kuangalia kule, sauti ilionekana naifahamu, ila sikukumbuka mwenye nayo.
"Ni mimi James Mashaka mtoto wa mzee Mashaka Bwari pale kwenye kona ya kwenda nyumbani kwenu.
"Siku ile nakufa ulipita na teksi umebeba kitanda juu mbele kuna gari liliwazuia kwa sababu lilikuwa kubwa la kubeba maji machafu ikabidi msubiri."


Ili kujua zaidi usikose kusoma jioni...
 

SURUMA

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,901
1,250
[h=1]NUSU SIKU NDANI YA JENEZA - 3-[/h]
ILIPOISHIA JANA:
Nilibaki namtumbulia macho kwani aliyokuwa akiyasema kama ni kweli ibilisi hausiki basi wanadamu wamekuwa watu wabaya zaidi kuliko ibilisi mwenyewe.
Yule shetani akaendelea kusema:

“Imefika hatua sisi huku mnaotuita mashetani tunakuja duniani kupata uovu mpya unaotungwa na vichwa vya binadamu, lakini siku zimekaribia sana, haya mambo yote yatawekwa wazi na kila mtu atajua nyinyi binadamu na sisi shetani nani muovu wa kweli.”
Nilishangaa sana, nikamuuliza:
“Nyinyi si ndiyo mnauleta uovu wote duniani halafu wanadamu wanauchukua na kuanza kuufanyia kazi?”
NENDA NAYO MWENYEWE…


“Uovu wa baba mzazi kumlawiti mwanaye wa kumzaa?”
Alipoona nimesimama kimya kwa muda mrefu, akasema:
“Sasa tuondoke, tumekuonesha kwa sehemu tu, huruma ya wakubwa wa huku umekubaliwa kuendelea kuoneshwa sehemu nyingine.”
Safari hii nilipelekwa kwenye uwanja ambao ulionekana vizuri kwani ilikuwa ni mchana, nikamuuliza yule shetani.
“Mbona kule tulikotoka ni usiku hapa ni mchana halafu ni karibu sana, inakuwaje?”
Akanijibu kwamba, umbali tulioutumia kutoka tulipokuwa hadi pale ni kama siku nzima.
“Siku nzima kivipi wakati tumetembea dakika tano tu?”
Alicheka, akasema:
“Huku dakika kumi ni kama siku mbili.”
Kwenye uwanja huo tulikuta wanadamu wakiteketea kwa moto mkali huku wakilia na kuomboleza, wengi walikuwa wakisema wamekoma hawatarudia tena.
Mimi na yule shetani tulisimama kwa mbali, lakini joto kali la ule moto lilitupata ikabidi tujikinge uso kwa viganja.
Wale watu wanaoungua walipotuona walinyoosha mikono kuashiria kwamba wanataka kusaidiwa haraka, walikuwa wakituita.
“Pale ni motoni?” nilimuuliza.
“Motoni bado, pale ni sehemu wanayochukua mazoezi kabla ya kufika siku ya kuingia motoni.”
Niliogopa sana, moyoni nilisema kama motoni kwenyewe bado, watu wanalalamika vile, sijui hiyo siku itakuwaje?
“Una swali au maswali?” aliniuliza, nikatingisha kichwa kumkubalia kwamba nina swali.
“Huku ni makao makuu ya shetani?”
“Ndiyo.”
“Shetani mwenyewe mkuu anaishi wapi?”
“Kwake.”
“Kwake ni wapi?”
“Makao makuu.”
“Naweza kupata bahati ya kuonana naye?”
“Mimi mwenyewe sijawahi kumwona.”
“Sasa mnafanyaje kazi?”
“Tunapata maelekezo kutoka kwa wasaidizi wake wa karibu, wao ndiyo huwa tunaweka vikao nao.”
“Oke, kule nilikotoka,” nilianza kusema akadakia kwa kusema:
“Duniani.”
“Ee duniani. Wengi tunaamini nyiye,” akadakia kwa kusema:
“Mashetani.”
“Ee mashetani. Mna sura mbaya, mna mapembe, mna nundu, ngozi zenu si kama zetu, miguu yenu ni kwato za ng’ombe, macho mekundu, meno marefu kama kijiko, mna kucha ndefu sana, wakatili, wauaji na wazua balaa siku zote, sasa mbona sijaona shetani wa aina hiyo?”
“Shangaa wewe, binadamu wote wanaamini hivyo kwa sababu ya kusikia. Mmekuwa mkituchora vibaya sana kwenye makaratasi ili tuonekane wabaya hata kwa maumbile.
“Kwanza nikwambie kitu, hakuna binadamu aliyebahatika kutuona sisi mashetani tukiwa duniani tunatenda kazi yetu.”
Nilishtuka kusikia hivyo, kwani mara nyingi nimewahi kusikia watu wanatokewa na majini, nikamuuliza:
“Na wale wanaotokewa na majini si wanadamu?”
Alicheka sana, akasema:
“Hapo ndipo penye utata mkubwa, wanadamu wote mnaamini majini ndiyo sisi. Hilo ni kosa, sisi siyo majini, ila wote wanaowatengeneza majini uwezo wanapata kwetu.
“Lakini sisi siyo majini. Sisi ni malaika tulioasi, tukaja kuishi huku.”
“Huku kunaitwaje?”
“Nikuulize wewe, kule duniani huku mnakuitaje?”
“Ujinini.”
Akacheka sana, akasema:
“Nimeshasema, sisi si majini, sisi ni malaika tulioasi, kule duniani mnatuita mashetani, makazi ya majini ni baharini, katikati huko, sisi hapa ni sehemu yetu.”
“Inaitwaje?”
“Hilo ni fumbo zito kwenu wanadamu, wengi mnaamini sisi tunaishi jehanam, lakini jehanam ni mahali ambapo hakuna viumbe wanaoishi, ila pako tayari kwa ajili ya waovu siku ya kiama.”
“Hata watu?”
“Hata binadamu.”
“Kuna tofauti ya binadamu na mtu?”
“Kubwa sana.”
“Ni ipi hiyo?”
“Binadamu ni yule mwenye tabia za kidunia, hamwogopi Mungu, anaweza kuua, anaweza kufanya lolote baya kwa mwenzake.”
“Mtu?”
“Anakuwa na matendo mema. Maana Mungu alipoumba alisema anaumba mtu kwa mfano wake, ubinadamu umetokana na baba yenu Adamu, ndiyo maana watu wote wanaitwa binadamu, yaani Bin Adamu.
“Kwani neno bin si linatumika kwa wanaume tu, sasa mbona hata wanawake wanaitwa binadamu?”
“Tangu kale wakati wa Adam, mwanamke hakuwa na hesabu katika jamii.
Ndiyo maana watoto wa Adam, Kaini na Abel walioa dada zao na hawakuwa kwenye hesabu ya watoto wa Adam.
“Wewe umeishi duniani siku zote, umewahi kusikia watoto wengine wa Adam zaidi ya Kaini na Abel?”
“Sijawahi.”
“Jiulize walioa wapi? Walioa dada zao kwa sababu walikuwa hawaingizwi kwenye hesabu. Unajua sisi mashetani tunajua mengi kuliko nyiye.”
“Mh! Mi siamini kama Adam alikuwa na watoto wengine.”
“Alikuwa nao. Si Adamu tu, kuna mtu alikuwa anaitwa Yakobo, unamkumbuka?”
“Ndiyo.”
“Alikuwa na watoto wangapi?”
“Kumi na mbili.”
“Si kweli, alikuwa na watoto kumi na tatu, mmoja wa kike aliitwa Dina, alizaliwa kwa mkewe Leah, ila kwa sababu alikuwa mwanamke hakuingia kwenye hesabu.”
Nilitingisha kichwa kuelewa, ghafla ule moto uliokuwa unawachoma wale watu waliokuwa wanateketea ukazimika, wakawa wanaonekana kwenye majivu mengi wakiwa wamebadilika rangi ya ngozi zao.
Nilisikia nikiitwa kwa jina:
“Emmanuel Muhuge Magende.”
Nilishtuka sana, nikakaza macho kuangalia kule, sauti ilionekana naifahamu, ila sikukumbuka mwenye nayo.
“Ni mimi James Mashaka mtoto wa mzee Mashaka Bwari pale kwenye kona ya kwenda nyumbani kwenu.
“Siku ile nakufa ulipita na teksi umebeba kitanda juu mbele kuna gari liliwazuia kwa sababu lilikuwa kubwa la kubeba maji machafu ikabidi msubiri.”

Ili kujua zaidi usikose kusoma jioni...

Mhh....
 

Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,788
2,000
MziziMkavu, Kaka uko juu na kwakweli umenifanya niwe "mtumwa" kwa kuifuatilia hadithi hii hadi "Lyamba". Binafsi kwangu huna tofauti na ChaiChungu , ambaye naye aliwateka member humu kwa hadithi yake ya: Mjeda na demu wa Kinyiramba toka Shelui. Lakini pia aliyenibamba kabisa ni Majigo na stori yake: Nitakufa Mara ya Pili, hapa namkumbuka sana Mzee Manoni.
Much appreciated MziziMkavu!!
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,305
2,000
NUSU SIKU NDANI YA JENEZA - 4-

ILIPOISHIA :
"Emmanuel Muhuge Magende."
Nilishtuka sana, nikakaza macho kuangalia kule, sauti ilionekana naifahamu, ila sikukumbuka mwenye nayo.
"Ni mimi James Mashaka mtoto wa mzee Mashaka Bwari pale kwenye kona ya kwenda nyumbani kwenu. Siku ile nakufa ulipita na teksi umebeba kitanda juu mbele kuna gari liliwazuia kwa sababu lilikuwa kubwa la kubeba maji machafu ikabidi msubiri."
ENDELEA


MwilI mzima ulitetemeka, damu zilinisisimka kiasi kwamba nilihisi nataka kuanguka. Kijana huyo nilimkumbuka vizuri sana, ni kweli alikuwa jirani yangu wa Kinondoni Mkwajuni.
Nilijishika kifua, nikajizuia nisilie kwa sababu wakati wa msiba wake baba yake mzazi alilia sana, tena sana. Huyu kijana aliumwa tumbo tu, ghafla na baadaye kabla hajapelekwa Hospitali ya Mwananyamala aliaga dunia.
Wengi walisema hakufa bali alichukuliwa msukule sasa nijuavyo mimi binadamu wa kawaida tunaona wamekufa lakini katika hali ya uhalisia wanakuwa hai, sasa yule kijana kumwona kule ina maana alikufa kweli.
"Umenikumbuka sasa Emmanuel?" aliniuliza huku akiniangalia kwa macho yenye mategemeo fulani. Nadhani alijua mimi nitamuokoa kutoka alipo.
"Nimekukumbuka ndugu yangu, lakini sina cha kusema," nilimjibu kwa sauti ya juu huku nikitembeza shingo kumwangalia yeye na wakati huohuo kumwangalia yule kiumbe niliyekuwa naye.
"Basi, ukifika mwambie mzee nipo tabuni. Hali ya huku ni mbaya sana, hakuna maji ya kunywa, kuoga, chakula. Moto unaunguza sana, aniombee."
"Nitamwambia."
"Nitashukuru sana kaka ukifanya hivyo. Lakini waambie wote ndugu zangu na ndugu zako, waishi maisha ya toba kila siku, ili siku ikifika wasije huku, waende kule mbele," alisema huku akinyoosha kidole kuelekea sehemu nyingine ambapo niligeuza shingo kuangalia, lakini sikuona kitu.
Nikamuuliza yule kiumbe:
"Kumbe kuna sehemu nyingine zaidi ya pale?"
"Ipo lakini wewe huwezi kupaona."
"Kwa nini?"
"Huna uwezo."
Nilibaki kimya kwa muda nikiwa natafakari, mara yule kiumbe akaniambia:
"Sasa nataka kukupeleka kwenye eneo ambalo utakaowaona huko ndiyo mnaowasema duniani kwamba wapo."
Alinishika mkono na kuanza kuondoka kuelekea huko. Lakini hatua kama mbili mbele wakati tunaondoka, yule kijana alisema:
"Bro naona ndiyo unaondoka siyo? Kwaheri bwana, sisi huku tumeambiwa haya ndiyo makazi yetu milele na milele na si maisha."
Sikumjibu, lakini nilijiuliza maana ya ile kauli ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];haya ndiyo makazi yetu milele na milele na si maisha.'
Yule kiumbe akaniuliza:
"Nahisi kuna kitu ameongea yule kijana kimekutatiza, ni kweli?"
"Ni kweli kabisa."
"Ni kitu gani?"
"Yule amesema ameambiwa pale ndiyo makazi yake milele na milele na si maisha. Kwani kuna tofauti yoyote ya maisha na milele? Kule nilikotoka watu wakigombana unaweza kumsikia mmoja akisema &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];tusiongee milele au tusiongee maisha'.
Yule kiumbe alicheka, akaniangalia na kusema:
"Kule duniani mnajua mengi ya mwili lakini ya kiroho hamyajui, hilo ni tatizo kubwa sana."
"Kwa hiyo kuna tofauti?" aliniuliza.
"Kubwa tu."
"Kama ipi?"
"Maisha ni uhai wenu wa duniani. Mtu anatakiwa kusema tusiongee maisha lakini hatakiwi kusema tusiongee milele. Milele haina mwisho, lakini maisha yana mwisho.
"Kwa mfano wale pale kwenye moto wanaweza kusema watakuwa pale milele kwa sababu hakuna atakayekufa tena milele na milele."
"Kama maisha kwa mwanadamu ni uhai wake wa duniani, kama miaka kumi, arobaini, sitini, mia je milele ina urefu gani?" niliuliza.
Yule kiumbe aliniangalia kwa jicho kali kidogo, nahisi kama lilikuwa na mwanga wa taa ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];tyubu laiti' kwa ndani kisha akasema:
"Wewe kwa pale Kinondoni Mkwajuni ukisema unakwenda kwenu ni wapi?"
"Mara."
"Mara unakwenda kwa usafiri gani?"
"Basi."
"Unachukua muda gani?"
"Kama halitasimama njiani, tukitoka Dar asubuhi saa tatu usiku tunaweza kufika Mara."
"Oke, unamfahamu jongoo?"
"Namjua sana."
"Mwendo wake unaujua?"
"Naujua ndiyo."
"Sasa milele iko hivi, jongoo yule, atoke pale Mkwajuni kwa miguu yake ile kwenda Mara na kurudi Dar kisha kwenda tena Mara na kurudi Dar mara milioni mia moja, lakini pia haikaribii hata robo ya milele. Unapata picha ye milele?"
"Kumbe milele haina mwisho maana jongo kufika Mara kwa miguu yake ile ni miaka mingi sana bado kurudi na kwenda tena na kurudi."
"Haina mwisho, ni uhai wote."
Ghafla tulitokea kwenye eneo lenye giza nene, lakini tulipofika sisi kukawa na mwanga hafifu lakini wenye kuwezesha kumtambua aliye mbele yako.
Tulisimama kwa dakika moja, mara mwanga mkubwa ukawepo, lakini si wa jua. Vitu vya ajabu niliviona mbele yangu.
Viumbe wa ajabu kuliko yule niliyekwenda naye pale. Walikuwa kama binadamu lakini hakuna aliyekuwa amekamilika. Kila mmoja sehemu ya viungo alikuwa na walakini.
Mfano, mwenye macho, yalikuwa yametoka nje, pua kuinamia mbele kama inataka kudondoka, meno kama umma, kucha ndefu mfano wa kalamu, masikio yao yalipita kichwa na yalikuwa mapana kama ya tembo au ungo.
Muda mwingi walionekana kutoa ute vinywani mwao, mbaya zaidi au kilichonitisha sana ni jinsi walivyokuwa. Kama haraka ungeweza kusema mazezeta, angalia yao ni kama wanaumwa vile.
Nilibahatika kuwaangalia sehemu ya miguuni na kugundua kuwa, karibu wote walikuwa wana miguu inayofanana na ya ng'ombe kwa maana ya miguu yenyewe hadi kwato za kukanyagia.
Nilipenda kuuliza maswali kadhaa lakini nilishindwa kutokana na jinsi nilivyokuwa naendelea kuwashangaa. Wapo waliokuwa na mapembe mawili kwenye pande mbili za kichwa pia kuna wengine walikuwa na pembe moja tu juu ya paji la uso hivyo kuonekana kama yule mnyama aitwaye kifaru.
Kusema ule ukweli walitisha sana, kama mmoja wao ningebahatika kukutana naye barabarani tena tukiwa wawili lazima hali ya hewa ingebadilika, kama si mimi kuanguka na kufa basi ningekimbia huku nikipiga kelele sana.
"Una swali?" yule kiumbe wangu aliniuliza.
"Mengi sana."

"Uliza sasa."

Ili kujua zaidi usikose kusoma leo Jioni Itaendelea....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom