Nusu siku ndani ya jeneza

Nusu siku ndani ya jeneza

Kwa Mtu Mwenye nyota ya Ndoo Tabia yake ni Upepo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa (AQUARIUS - Does It in the Water (January 20 to February 18) na kisha tena umetoa maana ya herufi ya kwanza katika nyota jina langu linaanza na herufi ''z''
HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo. Herufi Z inawakilisha Nyota ya Ng’ombe.

MASWALI YANGU NI HAYA
1: m2 unaweza kuwa na nyota mbili maana hapo kwa maelezo yuako tiyali ni nanyota mbili
2:
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Ndoo Tabia yake ni Upepo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa (

AQUARIUS - Does It in the Water (January 20 to February 18)............

mkuu mm nimezaliwa katika ya hzo trh hapo juu NA linaanza na herufi Z vp tabia za watu wenye nyota hyo na wafanye kazi ya dizain gan au biashara ya dizain gani na pia pia wanatakiwa wawe na marafiki wa aina gani na vp mahusiano yao ya kimapenzi huwa wanakuweje
?
 
EMMANUEL Muhuge Magende, mkazi wa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam anasimulia kisa alichowahi kukumbana nacho miaka mitatu (2010) nyuma baada ya kugongwa na gari dogo akiwa

anavuka barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni, jirani na msikiti.

Anasema: Nakumbuka ilikuwa tarehe kumi na tisa, mwezi wa saba, nilipanda daladala pale sokoni

Kariakoo. Hili daladala lilikuwa likienda Mwenge kupitia Kinondoni kisha kupita Morocco na kuunga Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Nilikaa kwenye siti ya kwanza mlangoni. Wakati naingia, kwenye siti hiyo alikaa mzee mmoja kwa makadirio ya umri alikuwa kama ana miaka sabini hivi.

Huyu mzee mimi nilipoingia tu, akasimama na kuniambia nikae pale ambapo pembeni yake palikuwa na abiria. Nilimkatalia kwa sababu daladala lenyewe lilijaa, sasa mzee kama yeye akiniachia siti mimi ambaye wakati huo nilikuwa na miaka 45 nilihisi si sawa.
Cha ajabu huyu mzee alilazimisha sana akisema yeye anakwenda kukaa siti ya nyuma. Ilifika mahali nilimkubalia, nikakaa yeye akatoka kuelekea nyuma lakini sikumfuatilia hadi kukaa kwake.
Muda huohuo, daladala liliondoka, likapita njia yake hadi Faya ambapo halikusimama kwa sababu nafasi haikuwepo. Kufika Magomeni ya Hospitali, daladala lilisimama, abiria walishuka wengi tu hadi nafasi ya kukaa watu wengine ikabaki. Wakati abiria wakishuka nilikuwa namwangalia mmoja baada ya mwingine ili kama kuna yule mzee nimwambie namlipia nauli, lakini hakuwepo, nikajua bado yupo ndani.
Daladala lilipoondoka hapo halikusimama Kituo cha Morocco Hotel mpaka Mkwajuni ambapo mimi nilikuwa nashuka. Kwa kuwa nilikuwa jirani na kondakta nilimwambia shusha hapo Mkwajuni, akagonga daladala likasimama. Nilisimama huku nikimwangalia yule mzee ili nimwambie namlipia, lakini sikumwona!
Nilishuka, kufika chini nikasimama ili kuvuka barabara maana nilikuwa naishi upande wa pili wa kituo hicho.
Cha ajabu sana nikamwona yule mzee kwa ng’ambo akiwa anatembea kwenda uelekeo uleule ninaokwenda mimi.
Nilivuka barabara haraka ili nimuwahi, lakini nikiwa katikati ya barabara hiyo gari dogo, jekundu, lilitokea upande wa Kinondoni Studio na kunifuata kwa kasi. Nilifanya jitihada zote kulikwepa lakini ilishindikana, likanigonga! Sikujua kilichoendelea.
***
Mbele yangu kulikuwa na jumba kubwa la kifahari, sikujua kama wanaishi wanadamu au la! Nilitembea kuelekea kwenye ile nyumba. Ilijengwa si kwa matofali wala simenti, ilionekana kama vioo vya kujitazamia ndivyo vilitumika sana.
Nilikuwa katika hali ya kuogopa sana, hivyo kufika kwangu kwenye nyumba ile kulikuwa na maana ya kuomba msaada. Kuogopa kulisababishwa na mazingira, sikuona jua, sikuona mawingu wala sikuona ardhi, nilitembea juu ya vioo.
Ili uingie mlangoni kulikuwa na ngazi tatu. Nilikanyaga ya kwanza na ya pili, nilipotaka kukanyaga ya tatu, mlango ulifunguka wenyewe nikaingia kama kwa kulazimishwa.
Ndani niliwakuta watu wengi weupe, naweza kusema walikuwa Wazungu pia naweza kusema walikuwa Waarabu, lakini hakukuwa na mtu mweusi hata mmoja.
Watu wote waliniangalia nilipokuwa naingia, wakanishangilia sana huku wengine wakiwa wanapiga vigelegele. Lakini pamoja na vigelegele hakukuwa na mwanamke.
Walikuwa wanaume wenye midevu mingi, warefu mfano wa watu warefu wakiwa wawili kwa kwenda juu hivyo mimi nilikuwa nawaangalia kwa juu.
Mmoja alinifuata na kunishika mkono. Akatembea na mimi hadi kwa wenzake, mmoja akanipokea hapo akanipeleka mbele ya jumba hilo ambako pia kulikuwa na mlango mkubwa kama niliouingia.
“Unajua uko wapi hapa?” aliniuliza.
“Niko ugenini.”
“Ni ugenini ndiyo, ni wapi?”
“Mimi sijui.”
“Ngoja nikuoneshe ulikotoka,” alisema yule mtu na kunitoa nje, tulitoka na yeye, akanyoosha mkono kuangalia juu huku akisema:
“Unakuona kule?”
Niliinua macho na kuangalia juu, nikaona dude kubwa likiwaka kama mwanga wa taa za kisasa.
“Umeona kule?” yule mtu aliniuliza.
“Ndiyo,” nilimjibu.
“Ni nini?”
“Dude.”
“Siyo dude, wewe umetoka kule.”
“Ina maana ile ni dunia?”
“Ile ni dunia, na pembeni yake unachokiona kidogo ni mwezi.”
“Huku sasa ni wapi?”
“Huku sasa ndiko wanakokuja watu waliokufa wakisubiri kupewa adhabu.”
“Ina maana mimi nimekufa?” nilimuuliza, akacheka sana kuonesha kwamba mimi ni mjinga sana kama sijui kama nimekufa.
“Unataka kujua kama umekufa au la!”
“Ndiyo, nataka kujua.”
Alinirudisha ndani ambapo hakukuwa na mtu hata mmoja, tukatembea kuelekea upande wa mashariki mwa jumba hilo hadi kwenye mlango mwingine mkubwa sana, ukafunguka wenyewe. Tuliingia ndani ambako tulikuta watu mchanganyiko, wengine weusi kama mimi wengine weupe.
Walikuwa wamekaa wakiangalia skrini moja kubwa sana. Ndani ya skrini hiyo kulikuwa na watu wanafanya mambo mbalimbali. Wengine walikuwa wanafanya zinaa, wengine wanaiba, wengine wanapigana, wengine wanachinja binadamu wenzao.
Kifupi ni kwamba watu walikuwa wakifanya madhambi ndicho nilichokibaini mimi.
Watu wote walikuwa wamekodolea macho ile skrini, lakini tulipoingia sisi wakageuka kutuangalia. Mmoja akauliza:
“Huyo naye haamini kama amekufa?”
Yule niliyekuwa naye akajibu:
“Ndiyo.”
Nilikaribishwa kiti nikakaa halafu skrini ikazimwa. Baada ya muda ikaanza kuonesha picha yangu. Nilionekana napanda daladala Kariakoo. Picha hiyo ikanionesha nikiwa nazungumza na yule mzee akisema anipishe kwenye kiti chake.
Cha ajabu, huyo mzee awali alionekana kama nilivyomwona mimi lakini ghafla akageuka, akawa mweupe kama watu niliowakuta kwenye lile jumba.
Tukio zima lilionekana, daladala likipita Magomeni, likakata kona kwenda Hospitali na kupita Hoteli ya Morocco hadi Mkwajuni.
Nilimwona yule mzee akitoka kwenye daladala kwa kupitia kioo cha mbele cha dereva kisha akavuka barabara kabla hata daladala halijasimama.
Nilionekana nashuka, natembea kwenda kuvuka barabara. Lile gari jekundu lilizuka tu palepale jirani yangu na kunigonga.

Je, kiliendelea nini? Tuonane jioni ...
u
Duu noma sn
 
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Punda Tabia yake ni moto ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( ARIES - The Aggressive

(March 21 to April 19)

Kwa Mtu Mwenye nyota ya Ng'ombe Tabia yake ni Udongo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( TAURUS - The Tramp

(April 20 to May 20)

Kwa Mtu Mwenye nyota ya Mapacha Tabia yake ni upepo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( GEMINI - The Twin

(May 21 to June 20)

Kwa Mtu Mwenye nyota ya Kaa Tabia yake ni maji ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( CANCER - The Beauty (June 21 to July 22)

Kwa Mtu Mwenye nyota ya Simba Tabia yake ni Moto ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( LEO - The Lion (July 23 to August 22)

Kwa Mtu Mwenye nyota ya Mashuke Tabia yake ni udongo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( VIRGO - The One

that Waits (August 23 to September 22)

Kwa Mtu Mwenye nyota ya Mizani Tabia yake ni Upepo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa (LIBRA - The Lame One

(September 23 to October 22)

Kwa Mtu Mwenye nyota ya N'ge Tabia yake ni maji ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( SCORPIO - The Addict

(October 23 to November 21)

Kwa Mtu Mwenye nyota ya Mshale tabia yake ni moto ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( SAGITTARIUS - The

Promiscuous One (November 22 to December 21)

Kwa Mtu Mwenye nyota ya Mbuzi tabia yake ni udongo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( CAPRICORN - The

Passionate Lover (December 22 to January 19)

Kwa Mtu Mwenye nyota ya Ndoo Tabia yake ni Upepo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa (

AQUARIUS - Does It in the Water (January 20 to February 18)

Kwa Mtu Mwenye nyota ya Samaki Tabia yake ni Maji ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( PISCES - The Partner

for Life (February 19 to March 20)

Kaka mzizi mkavu,nilitaka kujua kuhusu nyota ya mapacha(gemin) na kama kuna hadith nyengine link tofauti na malkia wa gorl na hii ,za ukweli sana,mungu akupe maisha marefu,uzi zako zaukweli
 
vipi kwa watu wenye nyota ya N'gombe (TAURUS) ??

#MziziMkavu

NYOTA YA NG'OMBE
(TAURUS)

Hii ni nyota ya pili katika mlolongo wa nyota 12.

Wenye nyota hii ni wale ambao wamezaliwa kati ya tarehe 21 April na May 20 ya mwaka wowote.

  • Sayari yao ni Venus (Zuhura).
  • Siku yao ya bahati ni Ijumaa.
  • Namba yao ya bahati ni 6.
  • Rangi yao ya bahati ni kijani.
  • Asili ya nyota yao ni Udongo.

KIPAJI CHA NG'OMBE

(BODY-CENTERED)
Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa kilicho ndani ya mwili wao ambacho ni pamoja na kuelewa mambo kimbele, hesabu, kuponya kwa kutumia mikono na kwa kumwagia mtu maji.

TABIA YA NG'OMBE:

Wenye nyota hii ni watu wanaopenda kujishughulisha katika shughuli nyingi. Ni watu wakarimu na wanaopenda kusaidia watu, na wana tabia ya uvumilivu na subira katika jambo lolote wanalolifanya.
Ni watu wenye malengo na wenye msimamo thabiti, wasiopenda kupindishwa na wana tabia ya ubishi na ukaidi hasa katika jambo lao wanalolitaka.

TABIA YA NG'OMBE KATIKA MAPENZI:

Wenye nyota hii ni waaminifu sana katika mapenzi na wanaohitaji ulinzi katika mapenzi na njia au mwenendo unaoeleweka.
Pamoja na kwamba asili yao ni udongo, wanaweza kuwa ni wenye mahaba na mapenzi makubwa kwa wapenzi wao.
Uhakika wa mapenzi ndio jambo kubwa ambalo wenye nyota hii huangalia kwanza na baadae Penzi hilo liwe lenye hisia na mpangilio.
Pamoja na hisia kali walizonazo, wao ni watu imara na wasiobadilika hivyo kuwafanya watu wenye shauku kutovutiwa nao.
Uaminifu ni jambo la pili ambalo wenye nyota hii wanalo hivyo kuwafanya wao wawe watu wenye kuaminika na hiyo inasababisha wawe wenye wivu kupindukia.
Wanachotakiwa kufanya ni kujitahidi kuwapa nafasi wapenzi wao la sivyo watajikuta wako peke yao. Ndoa kwao ndio uamuzi mzuri kuliko kuishi na wapenzi. Tabia yao ni ya kudumisha jambo fulani wanaloliamini au walilolianzisha na hawapendi kubadilishwa.
{mospagebreak}

MATATIZO YA KIAFYA:

Nyota hii inatawala shingo, koo, koromeo, kidevu na sehemu ya chini ya taya.
Kwa asili wenye nyota hii ni watu wabishi na wenye kufanya mambo kwa upole na wagumu kubadilika.
Wanapenda sana vyakula vitamu na vyenye mafuta na huwezi kuwabadilisha katika hilo na wengi wao wanakuwa wanene kupita kiasi na inakuwa ni vigumu sana kuwashawishi kuamka na kufanya mazoezi ya mwili.
Tatizo lingine ni kufanya kazi kupita kiasi ambalo linawafanya wapate matatizo ya mvutano na misuli hasa katika sehemu zilizotajwa. wenye nyota hii wanatakiwa wajihadhari na mpangilio wao wa chakula na wafanye mazoezi kwa wingi.

KAZI ZA WENYE NYOTA YA NG'OMBE:

Wenye nyota hii wana falsafa ifuatayo kulingana na kazi; "panda mbegu iote, mti uote halafu ule matunda". Ni watu ambao wanafuata mpangilio wa kikazi na wanaopenda kujituma na kujishughulisha. Wengi wenye nyota hii ni wafanyakazi wazuri na wanapenda wapewe muda kujenga vipaji na utaalamu wao wa kazi.
Kazi zao zinakuwa kazi za muziki, kazi zinazohusiana na chakula, hoteli, migahawa, kazi za ujenzi, kazi za mashamba, kazi za uhasibu, na kazi za sanaa hasa uchoraji au uchongaji vinyago.

FAMILIA ZA NG'OMBE:

Wazazi wa familia za Ng'ombe ni watu wenye msimamo, wakutegemewa na wanaothamini familia zao, na wako tayari kugombana na mtu yeyote kwa ajili ya watoto wao.
Ni wazazi wanaopenda kufuata mambo ya kizamani au ya asili hasa katika masuala ya nidhamu. wanapenda sana kuheshimiwa na watoto wao na huwashawishi au kuwashauri wawe huru.
Ni wazazi wanaotegemea watoto wao wafuate nyayo zao hasa katika biashara au kazi wanazozifanya, hivyo watoto wa wazazi Ng'ombe wanakuwa na muda mdogo wa kufikiria mambo mapya.
Ni wazazi ambao hufanya kazi kwa bidii kuhakikisha watoto wao hawakosi wanachokitaka na wanapenda watoto wao wawe na elimu nzuri. Hata hivyo ni wazazi ambao wanategemea watoto wao wafuate wanavyotaka wao vinginevyo inakuwa matatizo.

MADINI YA NG'OMBE:

Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa ALMASI au EMARALD.
Mawe haya yanawafanya wenye nyota ya ng'ombe wawe katika hali yao ya kike kike (Feminine) vili vile thamani ya mawe haya ni uthibitisho wa nyota hii katika fedha.

UHUSIANO WA KIMAPENZI:

(NG'OMBE NA N'GE):
Tabia ya uaminifu na ukweli waliokuwa nao wenye nyota ya ng'ombe inakuwa ni faraja kubwa kwa nyota ya Nge ambao wana tabia ya wivu kupita kiasi na kudhania maovu, kutuhumu na kushuku.

VYAKULA VYA NG'OMBE:

Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndivyo vinavyotawaliwa na nyota yao; Tofaa (apple), (oysters), viazi mbatata (potatoes), na dover sole.

NCHI ZA NG'OMBE:

Ili kupata mafanikio ya kinyota, kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao; baadhi ya nchi hizo ni USSR (Urusi), Ireland, St louis,na Lucerne (Switzerland).

RANGI ZA NGOMBE:

Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi za kijani au rangi za pinki au rangi ya bluu ambayo haijakoza katika nyumba zao au sehemu zao ya biashara ili kuleta mvuto wa kinyota.

Ukitaka kujuwa Pete ya Bahati yako au Pete ya kinga yako dhidi ya maaduwi zako wasiliana na mimi kwa njia ya Email nitumie baruwa ya pepe Email yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com

Kaka mzizi mkavu,nilitaka kujua kuhusu nyota ya mapacha(gemin) na kama kuna hadith nyengine link tofauti na malkia wa gorl na hii ,za ukweli sana,mungu akupe maisha marefu,uzi zako zaukweli
Hadithi si za ukweli ni za kutunga tu mkuu.

NYOTA YA MAPACHA (GEMINI)

  • Hii ni nyota ya tatu katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21 Mei na 20 Juni ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni Mercury (Attarid).
  • Siku yao ya bahati ni Jumatano.
  • Namba yao ya bahati ni 5.
  • Rangi yao ya bahati ni njano na bluu isiyoiva.
  • Asili ya nyota yao ni upepo.

KIPAJI CHA MAPACHA: (TELEPATHIC):

Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa cha kuwasiliana na watu ambao wako mbali kwa kutumia akili zao au hisia walizokuwa nazo.

TABIA ZA MAPACHA:

Watu wenye nyota hii ni watu wenye hisia kali sana ambao wanakasirika upesi, ni watu wasiotulia na wenye uwezo mkubwa wa kujieleza na kuzungumza na wanaweza sana kushawishi watu.
Ni watu ambao wanapenda sana mabadiliko na tofauti na wanapenda sana kujua mambo, wanapenda watu na wanapenda kujumuika na watu lakini wakati mwingine hawaeleweki. Wanapenda kusafiri sana.

TABIA YA MAPACHA KATIKA MAPENZI:

Watu wenye nyota ya Mapacha wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika.
Pamoja na kwamba hawapendi kubanwa sana , ni watu wachamgamfu na wenye mahaba mazuri.
Ni watu wenye asili ya mawasiliano na ni vigumu sana kuwafanya wajinga hivyo basi wakishampenda mtu wanahakikisha kwamba hawamchoshi huyo mpenzi. Watatumia muda mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano unazidi kuwepo.
Katika mapenzi, wao wanapenda vitu tofauti tofauti na wanahisi wamechoshwa basi huwa wa kwanza kuondoka aidha kwa muda au moja kwa moja.
Uaminifu ni kitu kigumu kwa watu wenye nyota hii na wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.
Wengi wao wanafikia hatua ya kuishi maisha ya sehemu mbili; mke na bwana au bwana na mke.
{mospagebreak}

MATATIZO YA KIAFYA:

Nyota hii inatawala mabega, mikono, viganja na sehemu ya juu ya mbavu.
Tatizo la kutopumzika kwa sababu ya kutafuta mambo mapya ndio yanayosababisha maradhi kwa wenye nyota hii. Wanafikia mpaka hali ya kuisahau miili yao na mara nyingi wanapata matatizo ya neva kutokana na uchovu kwa mishughuliko mingi.
Matatizo yanayotokana na nyota hii ni mgonjwa kukosa pumzi (bronchitis), pumu (asthma), matatizo ya kifua, mafua, flu, ajali za mara kwa mara kwenye mikono na mabega.

KAZI ZA WENYE NYOTA YA MAPACHA:

Kwa vile wenye nyota hii asili yao ni upepo na wao ni wenye kuzaliwa kwenye mawasiliano na uhusiano, wanapenda sana uhuru na uwazi katika kazi zao.
Wanapenda sana kazi ambazo zinawashughulisha na kufanya akili zao zisipumzike lakini siyo jambo hilo hilo kwa muda mrefu. Kuwa na mawasiliano na watu wengi kwa wakati mmoja ndio jambo linalopendwa na wenye nyota hii. Kazi zao hasa ni zile zinazohusiana na mambo ya utangazaji wa radio na televisheni.
Kazi ambazo zinahusika na mambo ya vitabu au uchapishaji vitabu. Kazi za kufundisha na kazi za ushauri nasaha.
Vilevile wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi za ukalimani au kazi za biashara lakini zinazohusiana na safari za nje.

FAMILIA ZA MAPACHA:

Watu wa nyota ya Mapacha ni waliochangamka na wenye hiari na wazazi wa Mapacha huingia katika msisimko wa watoto wao kwa raha.
Ni wazazi wenye furaha muda wote katika kutekeleza shughuli zao za nyumbani pamoja na kupenda kucheza na watoto wao na wana mipango mizuri na wanajua wapi wakiwapeleka watoto watafurahi.
wenye nyota hii wanathamini sana elimu na hawawezi kuishi bila mawasiliano na habari, hivyo huwa wanapenda kuwanunulia watoto wao vitabu vingi.
Tatizo linalotokea iwapo mtoto ataonyesha kwamba hapendi kusoma na watajaribu kila njia kumuweka katika njia wanayoitaka wao. Wakishindwa wanaacha.
Wazazi wa Mapacha hawawezi kuelezea jambo na hawana uvumilivu wa kun'gan'gania kwa mtoto asiyeelewa mambo.

MADINI YA MAPACHA:

Wenye nyota ya Mapacha wanatakiwa wavae madini ya Agata au kito chochote chenye rangi ya njano. Kito hicho inasemekana kinamuwezesha mvaaji awe na uwezo wa mawasiliano na ufahamu.

UHUSIANO WA KIMAPENZI:

(MAPACHA NA MSHALE)

Tabia ya Mapacha ya kupenda kufahamu na kuelewa mambo hutulizwa na tabia ya Mshale ambao ni wasomi na wenye kuelewa mambo mengi.

VYAKULA VYA MAPACHA:

Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndio vinavyotawaliwa na nyota yao. Vyakula vyenyewe ni kuku, rasiberi, karoti na uduvi.

NCHI ZA MAPACHA:

Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota hii wanashauriwa watembelee au waishi katika nchi au miji ifuatayo inayotawaliwa na nyota yao. Nchi hizo ni Ubelgiji na Wales, na baadhi ya miji ni London (Uingereza) na San Fransisco (Marekani).

RANGI ZA MAPACHA:

Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi za njano au bluu isiyoiva ambayo inapendeza ikipakwa ndani ya nyumba.

Ukitaka kujuwa Pete ya Bahati yako au Pete ya kinga yako dhidi ya maaduwi zako wasiliana na mimi kwa njia ya Email nitumie baruwa ya pepe Email yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com
 
Nusu Siku Ndani ya Jeneza 22-

Baada ya kuangalia tunampa mawazo yule mwombaji. Kama alikuwa anaangalia picha za harusi, sisi tunampa mawazo ya kumwambia:
Ile picha siku ya harusi yako, ulipendeza sana. Itabidi siku moja uchukue picha moja ukaitengenezee fremu kubwa, unajua ule ni ukumbusho mzuri sana?

Au utakuta binadamu yupo kanisani, wakati wa kuomba yeye hafumbi macho. Tunachofanya tunampa mawazo, kama ni kwa mchungaji wake aliye mbele anaweza kujikuta akisikia sauti ikisema:
Lakini mchungaji wako huyu anajua sana mafundisho, si eti? Binadamu bila kujua anaweza kusema moyoni &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];ni kweli anajua'. Halafu tunaendelea kumpa mawazo mengine, tunamwambia:
Leo ukitoka hapa ukamjulie hali dada'ko, si uliambiwa jana anaumwa sana. Atakuona humjali usipokwenda. Binadamu huyu ndani ya moyo wake atasema:
&[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Ni kweli, nikitoka tu naenda.'
Hapa nataka kuwaambia jambo moja muhimu sana kwamba hali hiyo husababisha kuondoka kwa uwepo wa Mungu wenu katika maombi. Siku zote nguvu ya maombi ndiyo inayofanya kazi katika maisha yenu ya duniani.
Binadamu kama mngejua kwamba maombi yanaweza kuwafanya mkawa juu basi mngekesha usiku na mchana mkiomba, lakini kwa sababu hamjui ndiyo maana mnalia kila siku na mnakumbwa na matatizo kila kukicha.
Wapo binadamu ambao kuomba kwao ni kila siku asubuhi, usiku wakitaka kulala na wanapopatwa na matatizo lakini nataka kuwaambia nyie kwamba muda mzuri wa kuomba ambao huwa unatusumbua sisi hata katika utawala wetu ni usiku wa manane.
Muda huo anga huwa jeupe, sisi watumishi wetu wanakuwa wamerudi kujipanga kwa mambo mengine. Muda huo maombi ya binadamu kwa Mungu wao yanaweza kupita na kufika kwa mhusika bila kukumbana na kizuizi chochote kile.
Labda niwakumbushe kama mmesahau. Katika maandiko ya Mungu wenu kuna mahali palionekana mtu alikuwa akiomba (Daniel) lakini maombi yake yalizuiwa na mkuu wa anga ambaye ni wa huku kwetu, ikabidi mtumishi mmoja wa Mungu wenu (Malaika Mikaeli) ashuke na silaha (sime) ili kumpigania yule mtu maombi yake yapite.
Sisi tuna uwezo wa kuzuia maombi yenu yasiwafikie kama Mungu wenu atakuwa amewajibu. Ndiyo maana yule mtu aliambiwa na yule mtumishi kwamba maombi yake yalishafika kule juu kwa Mungu wenu na alijibiwa, lakini majibu yalizuiwa angani kwa siku kadhaa.
Sasa kama ni hivyo hapa tunajulishwa kwamba kumbe binadamu mnaweza kuomba na mkajibiwa lakini majibu hayo sisi wakuu wa anga tunaweza kuyazuia kwa siku kadhaa. Hapa kinachotakiwa kwa binadamu ni kuzidi kuomba kwa kupinga nguvu ya wakuu wa anga wanaozuia maombi.
Wapo binadamu wakiomba shida zao zinaendelea kuwepo mpaka wanasema Mungu hanisikilizi au amenitenga lakini kumbe sababu kubwa ni hiyo majibu yamezuiwa angani.
Leo nawafunulia siri hii nyie kwa sababu si wa kule tena na mkirudi mtafanya kazi chini ya sisi kwa kiapo kikuu, atakayekiuka atakuwa amejitabiria kifo kibaya mwenyewe.
Aliposema hivyo tu nikajikuta nakosa nguvu ya mwili, nilijisemea moyoni kwamba ina maana mimi nitakuwa nikifanya kazi za kishetani? Ina maana mimi si binadamu tena? Nikataka kumuuliza swali, lakini yeye akawahi kwa kusema:
Sasa tumalizie na nyota ya Samaki ambayo kwa jina lingine inaitwa Pisces. Hii nyota inawahusu watu wote waliozaliwa Januari 21 hadi Februari 20. Wenye nyota hii watakuwa wazuri sana kama watakuwa waigizaji, wanamuziki, kazi ya huduma ya matibabu, hasa unesi, ulinzi kama polisi wa majini na utumishi wa Mungu.
Wako waigizaji wengi maarufu duniani ambao walianzia kwa kuwa chini wakapanda kwa sababu tu ni wenye nyota hii ya Samaki.
Mtu mwenye nyota hii, siku moja akijaribu kazi ya sanaa atashangaa itakavyomtoa katika maisha yake yote.
Nyota zote nilizozitaja si rahisi mtu kujua zilivyo, lakini kama atafuatilia sana ataweza kubaini. Wale watu wasiopenda kwenda kwa wataalam wa kuangalia nyota, hao wanaweza kujua nyota zao kwa tabia ya kufanya jambo moja baada ya jingine.
Kama watauza duka halafu ndani ya miezi sita hawoani mafanikio ni bora kubadili. Wengi wanazijua nyota si kwa kugundua bali katika kuhangaikia maisha tu wanajikuta wamebahatika kufanya mambo yanayoendana na nyota zao.
Kuna kitu cha kujifunza mtakaporudi duniani kwa njia nyingine lakini si ile mliojia huku na kule mtatakiwa kutosema au kuanika lolote la huku, naamini hili nalizungumzia kama msisitizo kwani nimeshalisema awali.
Kama atatokea binadamu kati yenu akaanza kuanika siri alizoziona na kujifunza huku huyo atakuwa ametangaza hali ya hatari kati yake na yetu sisi wakuu wa anga ya juu.
Haya sasa inabidi kila mmoja apite mbele yangu na kukiri kwamba atakaporudi ulimwenguni atafanya kazi chini ya maelekezo yetu. Nataka kuwahakikishia kwamba kila mmoja wenu atakuwa akisikia maelekezo yetu pale ambapo patakuwa pagumu sana atasaidiwa kwani sisi hatushindwi na binadamu yeyote yule.
"Alipomaliza kusema hivyo, alituamuru kila mmoja apite mbele yake ili amuwekee mikono kama kiapo chake. Hali ilikuwa sivyo kwangu sikutaka kabisa kukubaliana na tukio lile.
"Sikuwa tayari kupita kwake na kuniwekea mkono au mikono kwani hilo nililiona kama ni kumsaliti Mungu wangu ambaye niliamini hata wao viumbe pia hawamuwezi.

Itaendelea wiki ijayo ijumaa kama ya leo....
 
Heshima kwako. MziziMkavu kwa kweli unazidi kutupevusha akili zetu,ubarikiwe kwa kujitolea kufanya hivyo.
Tungefurahi na sisi wa nyota ya Mizani(libra) kama ungetujuza kuhusu Tabia,biashara,kazi,Uhusiano wa mapenzi,maradhi,madini,namba ya bahati na vingne vingi kama ulivyodadavulia wenye nyota ya Mapacha na Ng'ombe.

Yani kufundishwa ushirikina ndio kupevushwa akili?
 
Last edited by a moderator:
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Ndoo Tabia yake ni Upepo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa (AQUARIUS - Does It in the Water (January 20 to February 18) na kisha tena umetoa maana ya herufi ya kwanza katika nyota jina langu linaanza na herufi ''z''
HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo. Herufi Z inawakilisha Nyota ya Ng'ombe.

MASWALI YANGU NI HAYA
1: m2 unaweza kuwa na nyota mbili maana hapo kwa maelezo yuako tiyali ni nanyota mbili
2:
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Ndoo Tabia yake ni Upepo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa (

AQUARIUS - Does It in the Water (January 20 to February 18)............

mkuu mm nimezaliwa katika ya hzo trh hapo juu NA linaanza na herufi Z vp tabia za watu wenye nyota hyo na wafanye kazi ya dizain gan au biashara ya dizain gani na pia pia wanatakiwa wawe na marafiki wa aina gani na vp mahusiano yao ya kimapenzi huwa wanakuweje
?
Huwezi kuwa na nyota mbili ukiwa unajuwa Tarehe yako ya kuzaliwa huna haja ya kuangalia herufi . Ukiwa hujuwi tarehe yako ya kuzaliwa ndio waweza kuangalia herufi sasa wewe chaguwa moja usinichanganye akili yangu wewe unajuwa tarehe ya kuzaliwa kwanini unaangalia herufi?
 
Heshima kwako. MziziMkavu kwa kweli unazidi kutupevusha akili zetu,ubarikiwe kwa kujitolea kufanya hivyo.
Tungefurahi na sisi wa nyota ya Mizani(libra) kama ungetujuza kuhusu Tabia,biashara,kazi,Uhusiano wa mapenzi,maradhi,madini,namba ya bahati na vingne vingi kama ulivyodadavulia wenye nyota ya Mapacha na Ng'ombe.

NYOTA YA MIZANI (LIBRA)

  • Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 September na 22 Oktoba ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni VENUS (ZUHURA).
  • Siku yao ya Bahati ni Ijumaa.
  • Namba ya Bahati ni 6.
  • Rangi ya Bahati ni Kijani isiyoiva.
  • Asili ya nyota hii ni Hewa.

KIPAJI CHA MIZANI

(Extra Sensory Perception)
Wenye nyota hii wana kipaji cha kufumbua mafumbo na kujua siri za watu bila kuambiwa.

TABIA ZA MIZANI:

Wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kupenda usuluhishi, amani na upatanishi. Ni watu wasikivu, watiifu, na wepesi kuongozwa. Ni wenye maumbo ya kupendeza hasa wanawake. Kwa ujumla ni watu wenye roho nzuri na wanajua kupenda na wenye mahaba mengi.

Ni watu wastraabu, wenye adabu heshima na ni wakarimu kwa mtu yeyote na wanajipenda sana. Katika maisha yao wajipenda sana.

TABIA YA MIZANI KATIKA MAPENZI

Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye nyota hii ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye nyota hii wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.
Watu wa mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.
Kwa sababu hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina matatizo na zisizo na raha kwa sababu ya kuoa mapema bila kuangalia. Wenye nyota hii wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.
Katika suala la mahaba (Romance) na ngono (Sex) wao ni mabingwa. Wanajua sana kumpendeza mwanamke kwa maneno matamu yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.
Kwa ujumla wenye nyota ya Mizani wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao waishi katika hali nzuri.

TABIA YA MIZANI KATIKA FEDHA

Watu wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kutokuwa na maamuzi katika masuala ya fedha. Lakini hiyo siyo sababu ya wewe kufikiri kwamba wao ni wajinga.
Wanapofanya hivyo huwa wanapima au kufikiria kuona uwezekano wa fedha kutumika vizuri.
Ni watu wenye mipango mizuri na mara nyingi kwa kutumia uzoefu na kipaji chao kidiplomasia na upole, huwa wanapata mafanikio katika biashara zao.
Wana kipaji cha kuelewa watu wengine wanahitaji nini na wanatumia maneno matamu kuwashawishi wawape wanachokitaka na wanafanikiwa.
Wanapenda sana vitu vizuri na vyenye thamani na wako tayari kutumia fedha yeyote kutekeleza malengo yao.
Kwa ujumla ni watumiaji wazuri na wenye ubinafsi mkubwa.
{mospagebreak}

MAVAZI YA MIZANI

Wenye nyota ya Mizani wanatakiwa wavae nguo yenye kupendeza zenye mapambo na zenye kuashira mahaba.
Nguo ziwe za rangi ya Pinki au rangi ya udongo.
Kitambaa kiwe cha kotoni chepesi na chenye picha picha, kisiwe kile ambacho hakikuchorwa kitu.
Wavae sana mikanda na wapende kuvaa nakshi za maua pamoja na skafu au mitandio iliyoingia. Wanapendelea mavazi ya ushanga na mikufu.

MATATIZO YA KIAFYA

Nyota hii inatawala figo, sehemu ya utumbo mkubwa, kiuno, mpaka sehemu ya juu ya ------.
Sababu kubwa ya maradhi yao ni kwamba wanapenda sana kutafuta amani na suluhu hata wakiudhiwa au kukasirishwa. Matokeo yake wanavunjika moyo na kujinyima yale wanayoyapenda. Sana na hiyo inawafanya waudhike na wajisikie vibaya na inawasababishia maradhi.
Magonjwa yao makubwa ni figo, kibofu cha mkojo, ugonjwa usioambukiza wa ngozi unaowasha na unapojikuna huvimba (Eczema),maradhi ya misuli ya kiuno na matoki.
Tatizo lingine kubwa ni unene.Watu wa mizani wanapenda sana kula na hiyo inatokea sana wanapokuwa wameudhiwa. Wao wanaona ni bora zaidi kuondoa hasira zao kwa kula chakula.

KAZI ZA WENYE NYOTA YA MIZANI

Wenye nyota hii wanapenda sana kutumia uwezo wao wa kuzaliwa na inawawia vigumu wakati mwingine kutafuta kazi wanazozipenda.
Wanapenda kufanya kazi katika mazingira ya amani na yasiyo na usumbufu.
Kazi zao hasa zinakuwa za uhusiano wa jamii ushauri wa ndoa, biashara ya sanaa, ushauri wa mambo ya urembo au mwanasheria.

FAMILIA ZA MIZANI

Wazazi wenye nyota ya mizani wanapenda sana unadhifu na wanapenda watoto wao wawe nadhifu na wenye mavazi mazuri.
Wanapenda kutumia muda mwingi na fedha nyingi kuwafunza watoto wao tabia nzuri. Kwao ni muhimu sana mtoto akikubalika na kila mtu.
Wanapenda amani katika nyumba zao na wana tabia ya kuwapangia watoto wao namna ya kuishi na kufanya vitu ambavyo wao wnyewe wameshindwa kuvifanya.

MADINI YA MIZANI

Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa LAPIS LAZULI. Mawe kama nye rangi ya Bluu iliyokoza, wamisri wanayaita mawe ya peponi. Yakiwekwa kama kito kwenye pete ya dhahabu yanaleta mizani kwa wenye nyota hii.

UHUSIANO WA KIMAPENZI

(Punda na Mizani)
Tabia ya Punda ya haraka haraka. Vishindo na kutumia nguvu bila kufikiria, hulainishwa au kuzimwa na diplomasia, uerevu na ujanja wa mizani. Punda vile vile hupendezwa na uwezo au kipaji cha mahaba walichonacho wenye nyota ya mizani.

VYAKULA VYA MIZANI:

Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula au Matunda yafuatayo ambayo ndio yanayotawaliwa na nyota yao,Tufaha (Apple), viazi Mviringo (Potatoes), Chaza (Oyster) na Nyama ya Njiwa.

NCHI ZA KUISHI ZA MIZANI:

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii ya Mizani.
Miji hiyo ni Copenhagen (Denmark) na Vienna (Austria) na nchi ni Canada na Japan.

RANGI ZA MIZANI

Wenye nyota hii wanapenda rangi zilizopakwa juu juu na laini hivyo wanashauriwa watumie rangi ya aina yeyote lakini iwe hafifu katika nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara.

Ukitaka kujuwa Pete ya Bahati yako au Pete ya kinga yako dhidi ya maaduwi zako wasiliana na mimi kwa njia ya Email nitumie baruwa ya pepe Email yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Mzizi, nashukuru sana kwa ufafanuzi wa nyota ya Punda... Hii ndo nyota yangu kwa mujibu wa maelezo yako, na nilivyofuatilia tabia za nyota hii na kulinganisha na tabia zangu, zinafanana kwa asilimia 98%, pengine asilimia 2% zilizobaki sijajichunguza. Ila nimefurahi sana tena sana... Mkuu una uwezo mkubwa sana ambao awali sikuufikiria kuwa ungekuwa nao.. Wakati napitia maelezo yako juu ya nyota ya punda nilikuwa nashituka mara kadhaa nikidhani unaniona au unanijua vema. Mungu akuzidishie... Nina SWALI: mimi natakiwa kuoa mwanamke wa nyota gani? Je mwanamke mwenye jina linaloanzia G au A au W anaweza kuwa mke wangu? BIG LIKE 👍
 
Mzizi, nashukuru sana kwa ufafanuzi wa nyota ya Punda... Hii ndo nyota yangu kwa mujibu wa maelezo yako, na nilivyofuatilia tabia za nyota hii na kulinganisha na tabia zangu, zinafanana kwa asilimia 98%, pengine asilimia 2% zilizobaki sijajichunguza. Ila nimefurahi sana tena sana... Mkuu una uwezo mkubwa sana ambao awali sikuufikiria kuwa ungekuwa nao.. Wakati napitia maelezo yako juu ya nyota ya punda nilikuwa nashituka mara kadhaa nikidhani unaniona au unanijua vema. Mungu akuzidishie... Nina SWALI: mimi natakiwa kuoa mwanamke wa nyota gani? Je mwanamke mwenye jina linaloanzia G au A au W anaweza kuwa mke wangu? BIG LIKE 
Niambie jina lako la kwanza linaanzia na herufi gani? na pia niambie umezaliwa tarehe gani? kwanza ndio ninaweza kukujibu swali lako asante.
 
Hadithi si za ukweli ni za kutunga tu mkuu.

NYOTA YA MAPACHA (GEMINI)

  • Hii ni nyota ya tatu katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21 Mei na 20 Juni ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni Mercury (Attarid).
  • Siku yao ya bahati ni Jumatano.
  • Namba yao ya bahati ni 5.
  • Rangi yao ya bahati ni njano na bluu isiyoiva.
  • Asili ya nyota yao ni upepo.

KIPAJI CHA MAPACHA: (TELEPATHIC):

Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa cha kuwasiliana na watu ambao wako mbali kwa kutumia akili zao au hisia walizokuwa nazo.

TABIA ZA MAPACHA:

Watu wenye nyota hii ni watu wenye hisia kali sana ambao wanakasirika upesi, ni watu wasiotulia na wenye uwezo mkubwa wa kujieleza na kuzungumza na wanaweza sana kushawishi watu.
Ni watu ambao wanapenda sana mabadiliko na tofauti na wanapenda sana kujua mambo, wanapenda watu na wanapenda kujumuika na watu lakini wakati mwingine hawaeleweki. Wanapenda kusafiri sana.

TABIA YA MAPACHA KATIKA MAPENZI:

Watu wenye nyota ya Mapacha wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika.
Pamoja na kwamba hawapendi kubanwa sana , ni watu wachamgamfu na wenye mahaba mazuri.
Ni watu wenye asili ya mawasiliano na ni vigumu sana kuwafanya wajinga hivyo basi wakishampenda mtu wanahakikisha kwamba hawamchoshi huyo mpenzi. Watatumia muda mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano unazidi kuwepo.
Katika mapenzi, wao wanapenda vitu tofauti tofauti na wanahisi wamechoshwa basi huwa wa kwanza kuondoka aidha kwa muda au moja kwa moja.
Uaminifu ni kitu kigumu kwa watu wenye nyota hii na wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.
Wengi wao wanafikia hatua ya kuishi maisha ya sehemu mbili; mke na bwana au bwana na mke.
{mospagebreak}

MATATIZO YA KIAFYA:

Nyota hii inatawala mabega, mikono, viganja na sehemu ya juu ya mbavu.
Tatizo la kutopumzika kwa sababu ya kutafuta mambo mapya ndio yanayosababisha maradhi kwa wenye nyota hii. Wanafikia mpaka hali ya kuisahau miili yao na mara nyingi wanapata matatizo ya neva kutokana na uchovu kwa mishughuliko mingi.
Matatizo yanayotokana na nyota hii ni mgonjwa kukosa pumzi (bronchitis), pumu (asthma), matatizo ya kifua, mafua, flu, ajali za mara kwa mara kwenye mikono na mabega.

KAZI ZA WENYE NYOTA YA MAPACHA:

Kwa vile wenye nyota hii asili yao ni upepo na wao ni wenye kuzaliwa kwenye mawasiliano na uhusiano, wanapenda sana uhuru na uwazi katika kazi zao.
Wanapenda sana kazi ambazo zinawashughulisha na kufanya akili zao zisipumzike lakini siyo jambo hilo hilo kwa muda mrefu. Kuwa na mawasiliano na watu wengi kwa wakati mmoja ndio jambo linalopendwa na wenye nyota hii. Kazi zao hasa ni zile zinazohusiana na mambo ya utangazaji wa radio na televisheni.
Kazi ambazo zinahusika na mambo ya vitabu au uchapishaji vitabu. Kazi za kufundisha na kazi za ushauri nasaha.
Vilevile wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi za ukalimani au kazi za biashara lakini zinazohusiana na safari za nje.

FAMILIA ZA MAPACHA:

Watu wa nyota ya Mapacha ni waliochangamka na wenye hiari na wazazi wa Mapacha huingia katika msisimko wa watoto wao kwa raha.
Ni wazazi wenye furaha muda wote katika kutekeleza shughuli zao za nyumbani pamoja na kupenda kucheza na watoto wao na wana mipango mizuri na wanajua wapi wakiwapeleka watoto watafurahi.
wenye nyota hii wanathamini sana elimu na hawawezi kuishi bila mawasiliano na habari, hivyo huwa wanapenda kuwanunulia watoto wao vitabu vingi.
Tatizo linalotokea iwapo mtoto ataonyesha kwamba hapendi kusoma na watajaribu kila njia kumuweka katika njia wanayoitaka wao. Wakishindwa wanaacha.
Wazazi wa Mapacha hawawezi kuelezea jambo na hawana uvumilivu wa kun'gan'gania kwa mtoto asiyeelewa mambo.

MADINI YA MAPACHA:

Wenye nyota ya Mapacha wanatakiwa wavae madini ya Agata au kito chochote chenye rangi ya njano. Kito hicho inasemekana kinamuwezesha mvaaji awe na uwezo wa mawasiliano na ufahamu.

UHUSIANO WA KIMAPENZI:

(MAPACHA NA MSHALE)

Tabia ya Mapacha ya kupenda kufahamu na kuelewa mambo hutulizwa na tabia ya Mshale ambao ni wasomi na wenye kuelewa mambo mengi.

VYAKULA VYA MAPACHA:

Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndio vinavyotawaliwa na nyota yao. Vyakula vyenyewe ni kuku, rasiberi, karoti na uduvi.

NCHI ZA MAPACHA:

Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota hii wanashauriwa watembelee au waishi katika nchi au miji ifuatayo inayotawaliwa na nyota yao. Nchi hizo ni Ubelgiji na Wales, na baadhi ya miji ni London (Uingereza) na San Fransisco (Marekani).

RANGI ZA MAPACHA:

Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi za njano au bluu isiyoiva ambayo inapendeza ikipakwa ndani ya nyumba.

Ukitaka kujuwa Pete ya Bahati yako au Pete ya kinga yako dhidi ya maaduwi zako wasiliana na mimi kwa njia ya Email nitumie baruwa ya pepe Email yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com

Asante sana kaka
 
Back
Top Bottom