Nusu siku ndani ya jeneza

Nusu siku ndani ya jeneza

MziziMkavu , swali moja kwako. Je, ni kwanini hayo "mapepo" yaliyomsababishia "mauti fake" bwana EMMANUEL Muhuge Magende, yanaonekana kuogopa sana Kanisa ni siyo nyumba nyingine za ibada?

Swali zuri sana bwana Domhome, embu MziziMkavu tujuze, mbona hawa viunbe huogopa makanisa tuh? Hizi dini zingine kwao wana zionaje?
 
mm nadhani wanaogopa sehemu linapo hubiriwa neno la kweli juu ya mungu tofauti na kanisa au jumba la ibada kumbuka maana ya kanisa ni wakusanyikapo watu either wawe wachache au wengi himladi wawe wanaabudu na kutangaza neno la mungu hilo ni kanisa tosha hivyo hivyo si lazima jengo kubwa lenywe waumini wengi ianweza kuwa ni sehemu watu wakafunga hema na wakawa wachache wakaanza kuabudu katika roho na kweli na shetani akahogopa sehemu hiyo
 
Mh! Unaweza ukawa upo sahihi,ila viumbe hivi mikakati yao ni kuumaliza ukristu ambao ni threat kubwa sana kwao. Na tangia hapo mwanzo hivi viumbe huogopa kutaja jina la Yesu Kristu ila la Mungu wanalitaja kama kawaida. Je hizi dini zingine na viongozi wao si vitisho kwao? Na kwa nini?
 
kiukweli waliosema raha ya chakula ukile cha moto hawajakosea mzizi mkavu hii hadithi inapungua ladha unavyoileta kila baada ya siku tatu nne ilikua hot bcz unaendelea hapo hapo basi hamu pia ya kuisoma inakua kubwa now unasahau hata iliishiaje kurudia kusoma huwezi yale ya nyuma ushasahau kama yalikua yanakupa wasiwasi wakutaka kujua itakuaje sasa hivi unaisoma tuu bcz ulishainza hata ukiikosa unaona sawa think about it ni vyema uilete full ili uanze nyingine mpya inanoga sana
 
Ni kweli kabisa. Maana hata mimi nimeanza kuichoka sasa. Delay nyingi kama Isidingo na hii siiangalii tena.
 
Mh! Unaweza ukawa upo sahihi,ila viumbe hivi mikakati yao ni kuumaliza ukristu ambao ni threat kubwa sana kwao. Na tangia hapo mwanzo hivi viumbe huogopa kutaja jina la Yesu Kristu ila la Mungu wanalitaja kama kawaida. Je hizi dini zingine na viongozi wao si vitisho kwao? Na kwa nini?
1: kuhusu mikakati yao ya kuumiza ukristo.............ndugu ningependa ujue swala sio kuumiza au kuumaliza kabisa ukristo hapana hapo swala ni kumaliza imani ya watu katika kumuabudu mungu either uwe mkristo au muuislamu bado shetani atakuwinda tu aktika kila njia hivyo atatumia kila njia mfano mzuri ameonesha upenzi wa mpira juu ya mashabiki badala ya upenzi wa watu kwenda kanisani au sehemu ya kuabudu sasa usiichukulie story kama ilivyo labda walilengwa sana wakristo hapana mfano mzuri mechi ingechezwa ijumaa inamaana wangevuna watu wengi wanaoenda kwenye mechi badala ya msikitini na hata ingekuwa jumamoc au j2 haliingekuwa ni hiyo hiyo.
2: kuogopa kutaja jina la yesu kristo: kwanza ili upate kuelewa inabidi utambue na kuamini mungu katika nafsi tatu yaani mungu baba ,mungu mwana na mungu roho mtakatifu zote zikiwa katika mungu mmoja ......sasa kulizungumzia jina la yesu ni kuzungumzia kuhusu nafsi ya pili ya mungu ambayo ni mungu mwana na ambayo ndiyo iliyokuwa tiyari kujishusha na kuja duniani kwa ajili ya ukombozi hivyo mungu mwana hakuwa na chochote cha kupewa za idi ya kupewa jina ambalo litakuwa na nguvu kuliko majina yote......hivyo naomba uelewe kuwa jina la yesu lina nguvu kuliko majina yote ndo maana watu wanakemea kwa kutumia jina la yesu......hivyo jua kwamba jina la yesu linanguvu kuliko jina la mungu maana ni zaadi aliyoitoa yy mwenyewe mungu...japo mungu huyohuyo ni mkubwa kuliko yesu
 
Nimekuelewa mkuu Sina cha kupinga hapo
 
MziziMkavu , swali moja kwako. Je, ni kwanini hayo "mapepo" yaliyomsababishia "mauti fake" bwana EMMANUEL Muhuge Magende, yanaonekana kuogopa sana Kanisa ni siyo nyumba nyingine za ibada?
Hii Hadithi ya kutunga sio ya ukweli hakuna Mapepo yanayoogopa Kanisa. Kungelikuwa kuna Mapepop yanaogopa Kanisa basi hata hao Wagonjwa wanaotolewa Mapepo kanisani wasingelikuwepo mkuu tumia akili zako za kuzaliwa. Hii ni Hadithi ya kutunga hakuna ukweli ndani yake.
 
Nusu Siku Ndani ya Jeneza-15-

ILIPOISHIA JANA:
Lakini kuna wachungaji waliosimama katika kuomba kila siku usiku na mchana wamekuwa wagumu kuwangilia na kuwapandikizia roho chafu.”
Nilimwona yule mkuu wao akikunja sura na kukasirika.
“Balozeti una maanisha sisi tunashindwa?”
“Mkuu ukweli hatuwezi kushindwa lakini ni kweli kwamba kuna wachungaji wamesimama kwenye neno. Kila tukiwafuata tunawakuta wanaomba au wametoka kuomba kwa hiyo bado wanakuwa na moto wa kutuunguza.”
SASA ENDELEA…

“
Siwezi kukubali kusikia hivyo unavyoongea wewe. Unataka twende na mimi kwa hao wachungaji nikaone huo moto wao kama utamudu kuniunguza?”
“Mkuu itakuwa vyema, lakini sipendi uende kwa sababu tunatafuta udhaifu wao ndiyo tuwaingie.”
Yule mkuu alimwangalia Balozeti kwa macho yaliyojaa hasira huku midomo ikimtetemeka. Nilitamani kumwambia Balozeti amruhusu mkuu wao aende ili na yeye akakumbane na huo moto maana alikuwa haamini kama upo kwa wachungaji wenye kuomba sana.
“Ni muda gani mnakwenda?”
“Usiku sana.”
“Lakini lile zoezi nililowaagiza kwamba hakikisheni waumini wa makanisa wanaingiwa na uvivu wa kuamka na kumwomba Mungu wao linafanyika?”
“Mkuu linafanyika tena kwa kasi nzuri.”
“Halio ikoje?”
“Yaani hali iko hivi, katika kila waumini kumi, ni mmoja au wawili ndiyo wanaoweza kupata muda wa kuushinda uvivu na kuamka kusali.”
“Wengine?”
“Hao wengine tisa au nane wao ukifika muda wa kuamka kusali wanasikia uvivu. Lakini wana uwezo wa kuamka na kufanya mambo mengine yasiyo ya kumpendeza Mungu. Wapo akina mama wanaamka saa kumi kuwahi kununua samaki, wapo wanaume wanaamka saa kumi kufanya shughuli nyingine.”
“Safi sana. Hilo ndilo tatizo la wanadamu, hawajui kama maombi ya usiku mwingi yana nguvu sana kuliko muda mwingine wowote ule.”
“Haya, ondoka sana. Wewe simama,” yule mkuu aliniambia mimi nisimame. Nikasimama wima kama askari.
“Wewe nataka kukupa mmoja wa viumbe wangu uende naye duniani kufanya kazi nitakayowaagiza, uwe uko tayari au hauko tayari si swala la kujieleza. Sumumu, upo?”
Sumumu alisimama na kusema yupo kwa sauti nzito sana.
“Wewe ulikwenda kufanya nini duniani? Maana sijakuona siku nyingi sana huku.”
“Mkuu ulinipa kazi ya kuhakikisha mitandao ya kijamii inaenea kwa kasi sana na binadamu kupoteza muda humo.”
“Umeifanya?”
“Kwa asilimia mia moja mkuu.”
“Nakumbuka nilisema wanafaunzi mashuleni wajue matumizi ya teknolojia mapema ili akili zao zizoee hivyo na kila jambo walifanya kwa kutumia teknolojia, wao watajua wameendelea kumbe akili zao zinadumaa. Ni sawa?”
“Ndivyo ilivyo mkuu.”
“Sasa toka na huyu, nataka mkahakikishe uchawi unatawala, wazee wanauawa sana kwa tuhuma za uchawi. Mzee akiwa na macho mekundu tu watu wajue ni mchawi, wamuue.”
Aliposema hivyo akamwangalia kiumbe mwingine kama aliyeachana na sisi, yaani mimi na Sumumu. Mimi nikanyoosha mkono, akaniuliza:
“Unasemaje? Zingatia kabla hujasema lolote kwamba nilishakuelekeza hoja zangu si za kukataa ni utekelezaji tu.”
“Sawa mkuu. Lakini mimi siwezi kwenda.”
“Haa!” viumbe wengine wote walishtuka na kusema hivyo.
“Unasemaje?” mkuu aliniuliza.
“Nasema siwezi kwenda.”
“Unanijua mimi ni nani?”
“Nakujua.”
“Ni nani?”
“Mkuu wa hawa.”
“Haa!” wale viumbe wengine walishtuka tena.
“Wewe unataka kucheza na moto?”
Nilijiuliza nitachezaje na moto wakati tayari niko kwenye eneo la moto.
“Mimi sichezi na moto.”
“Bali?”
“Bali nipo kwenye moto tayari.”
“Kingereza,” aliita.
“Naam mkuu.”
“Chukua huyu, mtumbukize kwenye wakorofi wenzake, akapate ile dawa yao kisha mlete hapa.”
Kingereza alinibeba juu kwa juu hadi kwenye ukumbi mmoja ambao kwa nje ulionekana moja kwa moja kwamba ndani kuna giza nene.
“Ingia,” Kingereza alinisukuma kwa mikono yake yenye nywele kama za kichwani.
Nilizama kwenye chumba hicho, nikawa sijui nitembee au nikae maana nilikuwa sioni mbele, kulia wala kushoto. Ghafla mwanga ulioonekana unatoka kwenye taa ya kibatali uliwaka ukiwa hafifu sana.
Niliwona wanadamu kama mimi wamesimama mstari mbele yangu, mtu wa kwanza kabisa mbele alikuwa anaingia kwenye mlango mwingine.
Baada ya kuingia ghafla kikasikika kilio huku akisema:
“Basi sirudii, sirudii jamani

Itaendela kesho usiku wakati kama huu.....
 
Swali zuri sana bwana Domhome, embu MziziMkavu tujuze, mbona hawa viunbe huogopa makanisa tuh? Hizi dini zingine kwao wana zionaje?
Hii Hadithi ya kutunga sio ya ukweli hakuna Mapepo yanayoogopa Kanisa. Kungelikuwa kuna Mapepop yanaogopa Kanisa basi hata hao Wagonjwa wanaotolewa Mapepo kanisani wasingelikuwepo mkuu tumia akili zako za kuzaliwa. Hii ni Hadithi ya kutunga hakuna ukweli ndani yake.
 
Hii Hadithi ya kutunga sio ya ukweli hakuna Mapepo yanayoogopa Kanisa. Kungelikuwa kuna Mapepop yanaogopa Kanisa basi hata hao Wagonjwa wanaotolewa Mapepo kanisani wasingelikuwepo mkuu tumia akili zako za kuzaliwa. Hii ni Hadithi ya kutunga hakuna ukweli ndani yake.

Poa, nimekuelewa MziziMkavu
 
Hii Hadithi ya kutunga sio ya ukweli hakuna Mapepo yanayoogopa Kanisa. Kungelikuwa kuna Mapepop yanaogopa Kanisa basi hata hao Wagonjwa wanaotolewa Mapepo kanisani wasingelikuwepo mkuu tumia akili zako za kuzaliwa. Hii ni Hadithi ya kutunga hakuna ukweli ndani yake.

Pamoja na kuwa ni hadithi ya kutunga lakini kwa kiasi kikubwa mambo mengi kama si yote yanaukweli kabisa. Hao wenye mapepo ndo maana yanaenda tolewa Kanisani na Watumishi/Waumini "waliosimama" sawasawa...
 
1: kuhusu mikakati yao ya kuumiza ukristo.............ndugu ningependa ujue swala sio kuumiza au kuumaliza kabisa ukristo hapana hapo swala ni kumaliza imani ya watu katika kumuabudu mungu either uwe mkristo au muuislamu bado shetani atakuwinda tu aktika kila njia hivyo atatumia kila njia mfano mzuri ameonesha upenzi wa mpira juu ya mashabiki badala ya upenzi wa watu kwenda kanisani au sehemu ya kuabudu sasa usiichukulie story kama ilivyo labda walilengwa sana wakristo hapana mfano mzuri mechi ingechezwa ijumaa inamaana wangevuna watu wengi wanaoenda kwenye mechi badala ya msikitini na hata ingekuwa jumamoc au j2 haliingekuwa ni hiyo hiyo.
2: kuogopa kutaja jina la yesu kristo: kwanza ili upate kuelewa inabidi utambue na kuamini mungu katika nafsi tatu yaani mungu baba ,mungu mwana na mungu roho mtakatifu zote zikiwa katika mungu mmoja ......sasa kulizungumzia jina la yesu ni kuzungumzia kuhusu nafsi ya pili ya mungu ambayo ni mungu mwana na ambayo ndiyo iliyokuwa tiyari kujishusha na kuja duniani kwa ajili ya ukombozi hivyo mungu mwana hakuwa na chochote cha kupewa za idi ya kupewa jina ambalo litakuwa na nguvu kuliko majina yote......hivyo naomba uelewe kuwa jina la yesu lina nguvu kuliko majina yote ndo maana watu wanakemea kwa kutumia jina la yesu......hivyo jua kwamba jina la yesu linanguvu kuliko jina la mungu maana ni zaadi aliyoitoa yy mwenyewe mungu...japo mungu huyohuyo ni mkubwa kuliko yesu

labda kwa ufafanuzi zaidi ni hivi kwann jina La Yesu lina nguvu kuliko jina la Mungu ? Mungu ni cheo kama ilivyo meneja,mkurugenz nk kwani kila mtu ana mkurugenz/meneja wake also hata kwa Mungu kuna watu wana Miungu yao na wanaiita Mungu etii. Mf;- kuna watu wanaamin Ng'ombe, masanamu,mibuyu,majin,wanaabudu hirizi zao viunoni, na wachina n'k nk
kwahyo hata ktk simuliz hii utaona kuna sehemu kwenye maswali na majbu utaona hao mashetan kutaja Mungu sio shida coz hata wao wana Mungu wao pia kumbuka kuna sehemu wanapata shida kutaja Mungu muumba mbingu na dunia hapo wanapata moto sana sababu yeye Ni Alpha na Omega na ndio Mungu pekee anayeweza kuua Mwili na Nafsi! Na ndio maana kwenye majibizano furani yule kiumbe alimwambia taja jina tu yaani Mungu na si vinginevyo(kuna sehemu mhusika alisema 'Mungu muumba Mbingu na Nchi').
Sasa kama nimeeleza kiasi fulani kwa jina la Mungu nadhan ktk Jina la Yesu kutakua hakuna maelezo mengi
Kwani Yesu lile ni jina lake sio cheo na ndio maana huwez kusikia kuna watu wanaabudu yesu wao -mf Mungu--miungu
na Yesu wakasema Miyesu, Noo kwa wangu upande sjawah kusikia
na ndio maana ukitumia jina Yesu hali si
shwali kabisa upande wao
lkn ukitaka kutumia jina Mungu taja ktk imani timilifu ktk Mungu wa kweli
kwa utukufu wake kuwa ndiye aliyeziumba Mbingu na Nchi, mfalme wa Mbingu na Dunia
hakuna mumgu wa mtu aliyeumba mbingu, hata hayo mahirizi hayauwi nafsi bali ni mwili tu ambao hauna kazi, hapo hapo hata kuumba mkono hayo ma miungu hayajaumba kabisa
nasema HAKUNA!!
Sijui kama nimeeleweka?
 
Hii Hadithi ya kutunga sio ya ukweli hakuna Mapepo yanayoogopa Kanisa. Kungelikuwa kuna Mapepop yanaogopa Kanisa basi hata hao Wagonjwa wanaotolewa Mapepo kanisani wasingelikuwepo mkuu tumia akili zako za kuzaliwa. Hii ni Hadithi ya kutunga hakuna ukweli ndani yake.

xmas hamna hadithi?
 
Nusu Siku Ndani ya Jeneza-16-
ILIPOISHIA JANA:
"Pia ukasema kwamba unataka kuhakikisha kuwa wanawake kwa kudai hali ya usawa wanaivunja tena kwa mara ya pili ile mari ya Mungu wao kwamba wao wameumbwa kuwa wasaidizi.
"Jingine kubwa ulisema kwa kudai huko haki lazima ndoa zitavunjika kwa sababu ya usawa kwani wanaume nao hawatakubali kutawaliwa na wanawake ambao watakuwa wanataka kuwatala."
SASA ENDELEA

"Sawasawa Humuli. Je, kuna dalili ya mafanikio kwa kiwango kikubwa?"
"Sana mkuu. Nchi kubwa na tajiri zote zinatetea wanawake, taasisi mbalimbali zimeanzishwa kwa ajili ya kuwatetea wanawake, baadhi ya nchi kwa sasa duniani zinatawaliwa na wanawake, yapo makanisa ambayo wanawake ndiyo viongozi, lakini pia tumehakikisha kwamba kila serikali inaweka wizara ya kutetea wanawake."
"Je, mmefanyaje ili serikali zisishtuke kwamba ni mkakati wetu?"
"Tumehakikisha tunaongeza, mfano wizara ikiwa ya wanawake tunaongeza na watoto au jinsia au walemavu."
"Je, mkakati mpya mnaokwenda nao mkiwa na huyo binadamu ni upi?"
"Huyu tutamtumia katika maeneo ambayo akifika yeye wanadamu watalainika kuliko sisi tukijifanya wanadamu."
"Sawa. Lakini huyu bado sijakubaliana naye kurudi huko, napenda sana akakae kwenye chumba cha tabia za wanadamu na sifa za nyota ili ajifunze, nataka akiondoka ame amejifunza kazi hiyo akawasaidie wenzake kule."
Aliposema hivyo, kiumbe mmoja alinishika mkono tukaondoka eneo hilo. Tulitembea umbali wa kama nusu saa tena kwa miguu lakini sikutokwa na jasho wala kuhusu joto maana kama nilivyosema, kule kuna mwanga mkubwa lakini hautokani na jua.
"Tunakwenda wapi?" nilimuuliza yule kiumbe, akanijibu kwa mkato:
"Chumba cha tabia na sifa za nyota."
"Ndiyo nini?"
"Utakwenda kuona."
Nilifunga mdomo, tukatembea mpaka kwenye jumba kubwa sana kama godauni, tukaingia ndani yake. Mle ndani nilikuta wanadamu wenzangu wamekaa kwenye madawati halafu kuna kiumbe kama anawafundisha bila kutumia ubao.
Nilipoingia tu, yule kiumbe aliyenipeleka akageuza na kurudi alikotoka. Yule kiumbe aliyekuwa akifundisha aliponiona alisimama kufundisha akanionesha sehemu ya kukaa.
"Una bahati somo letu ndiyo kwanza linaanza."
Nilikaa mkao wa kusikiliza.
"Karibu sana bwana, hiki ni chumba cha tabia za wanadamu na sifa za nyota zao. Eee, mara zote binadamu anakuwa na tabia ya kubadilika kutokana na siku aliyozaliwa. Binadamu aliyezaliwa mwezi wa Januari hawezi kuwa na tabia moja na yule aliyezaliwa mwezi wa Novemba.
Kila mwezi unatawaliwa na nyota yake. Ndiyo maana katika kuishi au kufanya kazi zenu mnatakiwa sana kuhakikisha zinalingana na nyota.
"Ziko nyota kumi na mbili na zote hizi zinatawaliwa na mkuu wa huku mliko. Sisi tunazijua nyota hizi kwa majina ya huku ambayo nyie hamuwezi kuyajua, ila kwenu mnaita hivi: Nyota ya kwanza, Punda au Aries kwa lugha ya kigeni.
"Hii nyota kama wewe unajijua unayo au unajua mwanao anayo ni nzuri kumkuza au kumuandaa kwa kazi kama za jeshini, uokoaji wa majanga mbalimbali, michezo, mfanyabiashara, ualimu na mambo yote yanayohusu usimamizi wa fedha kwa ujumla.
"Binadamu mwenye nyota hii akifanya moja ya kazi hizo atatajirika, atang'ara na atavuma sana. Kama ni mpira ndiyo binadamu wenzake husema f'lani ana kipaji. Huwezi kumkuta mhasibu mwenye nyota ya Punda anapata shoti kazini au anafungwa kwa wizi wa fedha.
"Mfanyabiashara mwenye nyota ya Punda mafanikio yake ni makubwa mno. Anaweza kutajirika mpaka watu wakasema ameroga au anafanya biashara na misukule. Lakini si kweli bali ameongozwa kwenye kazi ambayo ina nyota yake.
"Huwezi kumkuta mfanyabishara ana nyota ya Punda halafu anafilisika. Ile nyota peke yake inalinda fedha zake za kazi. Kwa wanajeshi, wengi wao hufikia kiwango cha kuwa mkuu wa majeshi, mkuu wa polisi, mkuu wa magereza na mambo mengine yenye mazingira hayo.
"Hata hivyo, wanajeshi wenye nyota hii ni rahisi kupindua nchi kwa mafanikio makubwa endapo hakutakuwa na uhusiano mzuri kati yake na serikali iliyopo madarakani.
"Pia wengi wenye nyota ya Punda hupenda kimiliki silaha lakini matumizi yao hayaendi kinyume na sheria ya nchi kama wengine. Ila akilenga mahali lazima apige. Wana shabaha sana.

Itaendelea Kesho wakati kama huu
 
labda kwa ufafanuzi zaidi ni hivi kwann jina La Yesu lina nguvu kuliko jina la Mungu ? Mungu ni cheo kama ilivyo meneja,mkurugenz nk kwani kila mtu ana mkurugenz/meneja wake also hata kwa Mungu kuna watu wana Miungu yao na wanaiita Mungu etii. Mf;- kuna watu wanaamin Ng'ombe, masanamu,mibuyu,majin,wanaabudu hirizi zao viunoni, na wachina n'k nk
kwahyo hata ktk simuliz hii utaona kuna sehemu kwenye maswali na majbu utaona hao mashetan kutaja Mungu sio shida coz hata wao wana Mungu wao pia kumbuka kuna sehemu wanapata shida kutaja Mungu muumba mbingu na dunia hapo wanapata moto sana sababu yeye Ni Alpha na Omega na ndio Mungu pekee anayeweza kuua Mwili na Nafsi! Na ndio maana kwenye majibizano furani yule kiumbe alimwambia taja jina tu yaani Mungu na si vinginevyo(kuna sehemu mhusika alisema 'Mungu muumba Mbingu na Nchi').
Sasa kama nimeeleza kiasi fulani kwa jina la Mungu nadhan ktk Jina la Yesu kutakua hakuna maelezo mengi
Kwani Yesu lile ni jina lake sio cheo na ndio maana huwez kusikia kuna watu wanaabudu yesu wao -mf Mungu--miungu
na Yesu wakasema Miyesu, Noo kwa wangu upande sjawah kusikia
na ndio maana ukitumia jina Yesu hali si
shwali kabisa upande wao
lkn ukitaka kutumia jina Mungu taja ktk imani timilifu ktk Mungu wa kweli
kwa utukufu wake kuwa ndiye aliyeziumba Mbingu na Nchi, mfalme wa Mbingu na Dunia
hakuna mumgu wa mtu aliyeumba mbingu, hata hayo mahirizi hayauwi nafsi bali ni mwili tu ambao hauna kazi, hapo hapo hata kuumba mkono hayo ma miungu hayajaumba kabisa
nasema HAKUNA!!
Sijui kama nimeeleweka?

mm nakubaliana na ww ndugu Gody ni kweli ayaesu ndiye jina lake ila nadhani utakubaliana na mm kwamba ile ni zaweadi tosha maana huyo huyo yesu alikuwa na majina zaidi ya moja ona hapa Emanuel likiwa na maana Mungu yupamoja nasi na lingine aliitwa Masia likiwa na maana ya mkombozi na jingine ambalo limekuwa maarufu zaidi ni hilo ya Yesu ambalo ndilo jina kubwa zaidi kuliko majina yote na jina hilo alipewa kama zawadi mfano ukitaka kuangalia huwezi kukemea mapepo kwa kutumia jina la Emanuel au masia na pepo likakutii ila ukitumia jina la Yesu pepo linakutii na kuondoka
 
Back
Top Bottom