dolphien dominic
Member
- Dec 11, 2013
- 15
- 5
daaaah aiseee mkuu mzizi mkavu umenigusa kila kona leo
Daah,haya mambo hua sipendagi,sasa mpka kesho tena saa kama hiyo..kumi na besenga ila kila baada ya dk 20 nachek ka umebadil mawazo
Duuh,.... Ha ha ha, si udhamini show hilo mkuu?
Nusu Siku Ndani ya Jeneza-20-
ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Kazi zao zenye kuwapa mafanikio ni uhusiano kataika jamii, ushauri wa masuala ya ndoa. Wengi
waliotaka kupeana talaka waliposuluhishwa na wenye nyota hii walirudiana na ndoa kudumu.
Pia ni wafanyabishara wakubwa sana hasa ya mambo ya sanaa, mambo ya sheria au uhakimu. Mtu
mwenye nyota hii akiwa wakili anashinda sana kesi na wateja kwake hawapungui. Kama atakuwa
hakimu atakuwa anatoa huku ya haki kwenye kesi ngumu.
SASA ENDELEA
Kwa wale wanaoamua kufanya biashara ya sanaa hufanikiwa sana, mfano ni kama wanamuziki akina Lil Wayne, Bella Thorne, Eminem, Kim Kardashian, Will Smith, Ushar Raymond na Snoop Dogg.
Wapo marais wenye nyota hii na waliongoza mataifa makaubwa, mfano ni Jimmy Carter wa Marekani. Marais wengi wenye nyota hii hufanya kazi zao kwa busara sana na utulivu, hawakurupuki, si wapenda vita wala udikteta.
Wanapoachia madaraka wengi huishi maisha ya heshima sana na jamii huwatambua miaka na miaka.
Wacheza mpira wenye nyota hii pia hungara sana ulimwenguni, kama akina George Opong Weah, Muset Ozil, Ibrahimovic, Vidoc, Defoe na wengine kibao ambao nyota zao ni Libra na wakafanya vizuri kwenye mpira wa miguu.
Ipo nyota inaitwa Nge, lugha ya kigeni inaitwa Scorpio. Hii ni nyota ya nane kati ya kumi na mbili za duniani. Hiii ni nyota yenye majukumu mengi sana, dunia imeendelea kupitia watu wenye nyota hii. Kama wanadamu wangejua wangefanya juu chini kuzaa kipindi cha nyota hii ya Scorpio.
Mtu mwenye nyota hii ili afinikiwe anatakuwa kufanya kazi za madawa, upelelezi na uchunguzi. Hata wavumbuzi wengi wa mambo ya kihistoria wapo kwenye kundi la nyota hii.
Watu waliogundua vitu vingi vya kisayansi, kama ndege, meli nakadhalika wanatoka kwenye nyota hii.
Lakini kuna binadamu wanasumbuliwa sana na mambo ya mapenzi, washauri wao wakubwa wanatakiwa watu wenye nyota hii.
Kuna nyota inaitwa Sagittarius au Mshale. Hii nyota inawafaa sana watu ambao watafanya kazi za kusafiri, kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupeleka bidhaa au kuchukua, lakini wanasheria wazuri sana wanatokea kwenye nyota ya Mshale. Wakiwa waandishi wa habari wanakuwa mahiri zaidi na huvuma muda wote.
Ili wawe na mafanikio makubwa, wenye nyota hii wanatakuwa pia kufanya kazi ya ualimu, wachungaji wa makanisa wanaweza kujikuta wanavuta waumini wengi sana kama wana nyota ya Mshale. Wachungaji wenye nyota hii, wanakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kutenda miujiza mingi ya kuwashangaza wengi.
Pia wenye nyota hii wana uwezo mkubwa wa akili, kufikiri na kukwamuka kutoka katika matatizo. Mwanamke yeyote, hata kama ana nyota ya Simba, akiolewa na mwenye nyota ya Mshale atakuwa chini yake tu.
Nizungumzie nyota ya Capricorn au Mbuzi kwa jina la kujulikana kule duniani mnakotokea nyinyi. Hii nyota huwa ya utajiri mkubwa kama wahusika watafanya shughuli zifuatazo:
Uinjinia, uchoraji wa ramani za majengo, watafiti wa ardhi, kuajiriwa serikalini. Mara nyingi mwenye nyota hii akiajiriwa serikalini hupanda cheo kwa kasi sana, anaweza kuanzia chini akapanda hadi kuwa waziri na watu wakamshangaa.
Lakini wanasiasa wengi mahiri mkiwachunguza kwa karibu wana nyota hii ya Mbuzi. Tena wengi wanapopanda majukwaani hupigiwa makofi sana, hushangiliwa. Wana uwezo wa kuwashawishi watu kufanya jambo fulani, mfano kupigiwa kura.
Mtu akiwa na nyota ya Mbuzi na akataka kugombea nafasi ya siasa huwashinda wenzake kwa kura nyingi sana, ni mahiri wa kujibu maswali ya watu kama ataulizwa.
Kabla sijaendelea napenda kuwaambia kuwa maskini wengi au fukara wengi ni wale wanaofanya shughuli ambazo nyota zao zinakataa. Mtu nyota yake anatakiwa kuwa mwalimu, anaamua kuwa mfugaji, huyu lazima atalia. Kama atakopa mkopo kwa ajili ya kununua ngombe ili afuge atajikuta ngombe wote wanakufa kwa sababu nyota yake inakataa.
Pia kuna jambo moja ambalo binadamu wengi linawaingiza katika umaskini bila wenyewe kujua. Mfano, ni vibaya sana mtu kuishi kwenye nyumba ambayo, ukienda kazini, jua linakupiga usoni, ukirudi nyumbani jioni pia jua linakupiga usoni.
Hapa sidhani kama kuna sababu ya kufafanua sana, ni uelewa mdogo tu. Ni vizuri mtu anapoishi iwe sehemu ambayo akienda kazini anapigwa na jua kisogoni, akirudi jioni hivyohivyo.
Yule kiumbe aliposema hivyo tu mimi nikawaza kwamba, mfano mtu anaishi Kimara, kazi anafanyia Kariakoo, kwa hiyo asubuhi anapokwenda kazini jua linamuwakia usoni, jioni pia kwa sababu jua linakwenda kwenye kutua sasa.
Nikamwelewa kuwa, ana faida sana mfano, mtu anayeishi Magomeni halafu kazi anafanyia Ubungo, akienda kazini jua linampiga kisogoni, akirudi jioni jua linakuwa limeshageuka, pia litampiga kisogoni.
Akaendelea kusema:
Pia watu waogope sana kulala kwenye vyumba ambavyo madirisha yake yanatazama upande unaotokea jua au mlango unaoingilia chumbani unatazamana na karo la maji au sehemu ya kuoshea vyombo.
Vyombo vya kupikia, wengi wanasema wamekula vyakula vibaya wameendesha, lakini ukweli ni kwamba kupika chakula halafu ukatoka jikoni huku umechukizwa na jambo fulani husababisha anayekula matumbo kuendesha.
Wapo binadamu wanakula sana lakini hawanenepeshwi na chakula hicho, sababu kubwa ni tabia ya kula chakula huku mtu anayekula shingo yake imepindia upande mmoja, uwe wa kulia au kushoto na si nyuma wala mbele.
Je, nini kiliendelea? Tuonane ujumamosi ijayo.................
Samahani mzee ningependa kujua kila nyota na mwezi wake kama yawezekana. Mfn nyota ya simba ni mwezi wa ngap,mshale ni mwezi wangap n.k
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Punda Tabia yake ni moto ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( ARIES - The Aggressive
(March 21 to April 19)
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Ng'ombe Tabia yake ni Udongo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( TAURUS - The Tramp
(April 20 to May 20)
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Mapacha Tabia yake ni upepo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( GEMINI - The Twin
(May 21 to June 20)
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Kaa Tabia yake ni maji ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( CANCER - The Beauty (June 21 to July 22)
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Simba Tabia yake ni Moto ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( LEO - The Lion (July 23 to August 22)
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Mashuke Tabia yake ni udongo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( VIRGO - The One
that Waits (August 23 to September 22)
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Mizani Tabia yake ni Upepo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa (LIBRA - The Lame One
(September 23 to October 22)
Kwa Mtu Mwenye nyota ya N'ge Tabia yake ni maji ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( SCORPIO - The Addict
(October 23 to November 21)
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Mshale tabia yake ni moto ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( SAGITTARIUS - The
Promiscuous One (November 22 to December 21)
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Mbuzi tabia yake ni udongo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( CAPRICORN - The
Passionate Lover (December 22 to January 19)
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Ndoo Tabia yake ni Upepo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa (
AQUARIUS - Does It in the Water (January 20 to February 18)
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Samaki Tabia yake ni Maji ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa ( PISCES - The Partner
for Life (February 19 to March 20)
vp kwamtu aliezaliwa march 12 nyota yake ni ipi na huwa anatabia gani? PLEASE NAOMBA MSAADA WAKO.
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Samaki Tabia yake ni Maji ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa (PISCES - The Partner
for Life (February 19 to March 20)
NYOTA YA SAMAKI (PISCES)
- Hii ni nyota ya 12 katika mlolongo wa nyota 12
- Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 19 February na tarehe 20 Machi.
- Sayari yao ni JUPITER (MUSHTARA)
- Siku yao ya Bahati ni Alhamisi.
- Namba yao ya Bahati ni 8.
- Rangi yao ya Bahati ni Zambarau au Kahawia iliyochangamka.
- Asili ya nyota yao ni Maji.
VIPAJI VYA SAMAKI (VISIONARY)
Wenye nyota hii wana kipaji cha kufikiria jambo na kuliunda na likawa vile walivyotaka wao.
TABIA ZA SAMAKI
Watu wenye nyota ya Samaki ni wenye huruma, wapole na wenye moyo mzuri na hawawezi kukubali kumuona binaadamu mwingine akipata taabu au uchungu. Kwa hakika ni watu ambao wana hisia kati kwa
wengine ni watu ambao hawajipendelei na wako tayari wakati wowote kujitoa mhanga ili watu wanufaike, mapenzi yao au huruma kwa binadamu wengine hayana masharti yeyote.
Nafsi zao zimegawanyika katika nafsi ndogo ndogo kama vile muathiriwa mwenye kujitoa mhanga, mwokozi, na mkombozi.
Hayo yote yaliyotajwa wanaweza kuyatekeleza inapohitajiwa na ikiwa mwenye nyota hii akishatumbukia katika moja ya mambo hayo huwezi kumtoa.
Kwa ujumla nafsi za wenye nyota ya Samaki siyo za kidunia, ni watu wabunifu na wenye ndoto za kufikiri mambo ya baadaye na katika maisha yao wanaona raha sana kuwa na mawazo ambayo yatawaepusha na ugumu wa maisha.
Ikiwa wamekwama katika jambo lolote basi wataitafuta faraja au watajituliza kwa ulimwengu wao wa mawazo.
TABIA YA SAMAKI KATIKA FEDHA
Ni vigumu sana kukadiria tabia za wenye nyota hii katika fedha kwa sababau wote waliozaliwa katika nyota huwa wanachanganyikiwa kwa sababu huwa wanashindwa kutafautisha kati ya matumizi na thamani ya fedha.
Hii ni kwa sababu wanashindwa au hawakubali vikwazo kati ya muda na nafasi au za kwako na zangu, kwao kila kitu ni sawa sawa.
Pamoja na kwamba wana uroho wa pesa, uwezo na matamanio lakini wanajichukulia mambo kadri yanavyokuja. Kwao wakiwa na fedha sawa wakiwa hawana sawa vile vile kwao uwezo wa kubuni au kutunga taswira ni muhimu kuliko fedha.
Mara nyingi huwa wanajishughulisha na masuala ya kutatua matatizo ya watu wengine kuliko masuala ya kifedha. Wakati wote wako tayari kupoteza fedha kuliko kuibiwa ndoto zao.
TABIA YA SAMAKI KATIKA MAPENZI
Wenye nyota ya Samaki ni wenye kukamilika na Mahaba mengi na wanapenda sana kujitumbukiza na kuzama kwenye dimbwi la mapenzi.
Kuwa katika mapenzi ni kitu wanachokipenda na kukifurahia sana. Ni waangalifu wazuri kwa wapenzi wao wana huruma nyingi.
Ni watu wenye hisia kali za kimapenzi na ni wepesi kuathirika.
Mara nyingi huwa waoga wa vitu vya kimapenzi kwa sababu ya kuogopa kuvurugika kwa mipango yao ya baadaye.
Ni watu wenye kuyachukulia mapenzi kama ua la waridi na wanawaona wapenzi wao kama binaadamu wasio wa kawaida.
Tatizo lao kubwa la kimapenzi ni kwamba wanawaamini sana wapenzi wao na wanakuwa na mawazo au firika za kimapenzi ambazohazipo katika dunia hii.
Kwa ujumla wenye nyota hii wanapokuwa katika mapenzi wanakuwa wamejawa na shauku na mifano ya kuvutia na wanapenda wapwnzi wao waishi kiroho. Mategemeo yao yanakuwa makubwa na yaispotimia huwa wanavunjika moyo.
{mospagebreak}
MAVAZI YA SAMAKI
Wenye nyota ya Samaki wanatakiwa wavae nguo za michezo kama vile fulana au za kiasili na zilizoongezwa madoido na vimbwanga vingi.
Nguo zao ziwe za rangi ya Zambarau au Kahawia iliyochangamka na rangi ya bluu.
Kitambaa kiwe cha sufu (tweed)
Wanawake wapendelee sana kuvaa sketi, ikiambatana na mikanda na viatu vyao viwe vya bati.
MATATIZO YA KIAFYA
Nyota hii inatawala nyayo na vidole vya miguu.
Matatizo yao ya kiafya yanakuja pale wanaposhindwa kutekeleza ndoto zao au mipangilio yao kimaisha au wanapokorofishana na wapenzi wao.
Wanapoathirika na hayo yaliyotajwa hukimbilia kwenye ulevi na utumiaji vidonge uliokithiri.
Tatizo lingine ni maradhi ya nyayo za miguu, uvimbe unaotokana na baridi kali hasa katika vidole vya miguu.
KAZI ZA SAMAKI
Kugunuda muelekeo wa kimaisha kwa wenye nyota hii wakati mwingine huwa ni matatizo.
Tabia yao ya kushughulikia sana binaadamu wengine huwafanya wasiwe na muelekeo.
Wenye nyota hii wanatakiwa wasifanye ubaguzi katika kazi.
Wanatakiwa wafanye kazi ambazo zinazohusiana na kusaidia watu. Kipaji cha kutafsiri mambo huwasaidia vile vile kufanya kazi za sanaa kama vile kupiga picha na kazi za muziki au maigizo.
Kazi zingine zinazowafaa ni za kuhudumia wagonjwa, kucheza shoo, uaskari wa majini (Navy) kazi za dini au kazi za kutoa ushauri nasaha (Counselling).
FAMILIA ZA SAMAKI
Wenye nyota hii ni wazazi wenye hisia, wanaopenda watoto wao na wanahuruma hasa watoto wanapowasikiliza.
Pamoja na hayo wazazi wa Samaki wana matatizo ya kukubali kwamba watoto wanaweza kuwa tofauti na wao, hata mwishowe wanapokubaliana na hilo huwa wanawachukulia watoto wao kama wageni kuliko ndugu.
Mtoto akiwa anapenda kusoma na mwenye kujituma au akiwa na tabia ya kutumia sana akili kuliko moyo huwa hapendwi na mzazi wa Samaki.
Wazazi wenye nyota hii wana mipangilio mibovu ya nidhamu na muelekeo, hivyo watoto wakorofi huwa wanatumia mwanya huo kufanya mambo yao.
Hiyo ina maana kwamba watoto wa wazazi wa Samaki wanaweza kuharibika au kutumiwa kutokana na udhaifu wa wazazi wao.
{mospagebreak}
(MADINI YA SAMAKI)
Wenye nyota hii wanashauriwa wavae madini yanayoitwa.
Madini haya yanasaidia kupunguza hisia na kumuepusha mvaaji na ulevi.
UHUSIANO WA KIMAPENZI
(SAMAKI NA MASHUKE)
Tabia ya Samaki ya kuwa na mbinu na mawazo ya mambo ya baadaye huenda sambamba na tabia ya Mashuke ya utekelezaji na kujishughulisha bila kuchoka.
VYAKULA VYA SAMAKI
Wenye nyota ya Samaki wanashauriwa wapenda kula matunda au vyakula vifuatavyo.
Matunda ya Kunazi, Nyama mwitu kama Swala,nyati na kadhalika.
Vile vile wapendelee kula maboga.
NCHI ZA SAMAKI
Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao.
Nchi hizo ni Tonga na Tanzania na miji ni Alexandria (Misri) na Seville (Ufaransa).
RANGI ZA SAMAKI
Wenye nyota ya Samaki wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi ambayo haijakoza ya Bluu au Kijani au Urujuani (violet).
..................
Kwa Mtu Mwenye nyota ya Ndoo Tabia yake ni Upepo ni yule aliyezaliwa Tarehe hizi hapa (
AQUARIUS - Does It in the Water (January 20 to February 18)............
mkuu mm nimezaliwa katika ya hzo trh hapo juu vp tabia za watu wenye nyota hyo na wafanye kazi ya dizain gan au biashara ya dizain gani na pia pia wanatakiwa wawe na marafiki wa aina gani na vp mahusiano yao ya kimapenzi huwa wanakuweje
Kama mimi sijui tarehe yangu ya kuzaliwa, na majina yangu yanaanza na herufi M, M, N N hayo ni majina manne je siku yangu ya kuzaliwa ni ipi na nyota yangu ni nini?