Nusu siku ndani ya jeneza

Nusu siku ndani ya jeneza

kuendelea kujibizana na wewe ni ujuha wewe ndio u watch out maana umedandia treni safari si yako aliestaili kujibu au kuuliza simuoni siku reply in ur comment mbona unapenda ligi mpendwa nime reply kwa mtu mwingine kabisa unavyojishaua kama umejibiwa wewe sipendi u gomvi fuatilia vzr maana nilikua nakujibu ili kuondoa haya malumbano hii reply ni ya mwisho sikujibu tena iam waitting for mzizi mkavu na hadithi yake not you mzizi mkavu naomba uje na hiyo hadithi au tuambie tuonane lini mpendwa maana naona uzi wako umeingiliwa kuna thread mpya inataka kuanzishwa hapa
 
MziziMkavu umenirudisha huku kwa ufundi wako wa stori zenye uhalisia ktk jamii.Mungu akubariki kaka
 
kuendelea kujibizana na wewe ni ujuha wewe ndio u watch out maana umedandia treni safari si yako aliestaili kujibu au kuuliza simuoni siku reply in ur comment mbona unapenda ligi mpendwa nime reply kwa mtu mwingine kabisa unavyojishaua kama umejibiwa wewe sipendi u gomvi fuatilia vzr maana nilikua nakujibu ili kuondoa haya malumbano hii reply ni ya mwisho sikujibu tena iam waitting for mzizi mkavu na hadithi yake not you mzizi mkavu naomba uje na hiyo hadithi au tuambie tuonane lini mpendwa maana naona uzi wako umeingiliwa kuna thread mpya inataka kuanzishwa hapa
ndugu punguza hasira mvumilie tu maana wote hatuko sawa maana tumetofautiana sana
 
Sasa Mzizi Mkavu leo ndio inapita kimya? tupia sehemu inayofuata tupunguze stress za Xmass gift maana hadi sasa bila bila
 
Nusu Siku Ndani ya Jeneza-14-


ILIPOISHIA JANA:
"Ile timu nyekundu ilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kushinda maana mtaalam wao alikuwa mzuri, lakini nilipofika
uwanjani niliwanyong'onyesha miguu ikawa mizito."
"Vurugu ulizituliza?"
"Ndiyo mkuu."


"Sasa hakikisha kila mwaka upinzani unakuwa mkali kwa timu hizi. Sitaki moja iwe juu ya mwenzake kwa sababu ikitokea hivyo mashabiki watapungua na sisi lengo letu mpira uendelee kuwa na mashabiki wengi kuliko wanaokwenda kanisani."
"Hilo halina shida mkuu."ENDELEA SASA


"PIA nafikiria kwamba ili ushindani uwe mkubwa wachezaji wa timu ya kijani waende kwenye timu ya rangi nyekundu na wa nyekundu waende ya kijani, kusiwepo madhara lakini."
"Sawa mkuu."
"Kaa chini, simama Shubiraa."


Niligeuka kuangalia nikamwona kiumbe mwingine kasimama, huyu hakuwa anatisha, unaweza kusema ni binadamu kama sisi. Aliposimama akainamisha kichwa, akakiinua mkuu akamuuliza:
"Makahaba wameongezeka kama nilivyoelekeza siku unakwenda?"
"Ndiyo mkuu."
"Umefanyaje?"


"Nilichofanya mkuu, nimehakikisha wanaume wenye kupenda kulala na makahaba wanaongezeka, pia wanawake wengi, hata wa maofisini, wanafunzi na wake za watu nimewatia kiu ya kupenda kuwa makahaba.

"Pia nilihakikisha nafanya juu chini ili warembo wengi nao watamani kazi hiyo. Ndiyo maana hata mavazi yao siku hizi ni ya kikahaba tu. Msichana anavaa kisketi kifupi sana."
"Sawa, lakini kuna jambo la kukuongezeahapo.


Nitafanya hivyo siku nyingine. Kwa leo kapange mikakati yako halafu utaniambia kwenye ufunguzi," alisema yule mkuu. Sikujua ni ufunguzi gani. Hakuishia hapo, akaangaza kulia na kushoto akaita:

"Wewe Balozeti, simama." Aliyesimama safari hii ambaye ni Balozeti alisimama mbele yangu. Nikamwangalia kwa umakini wa hali ya juu maana alikuwa mrefu sana, kama binadamu wawili mmoja apande na kusimama juu ya kichwa cha mwenzake. Halafu mweusi tii.
"Balozeti nilikupa mkakati gani?"


"Nakumbuka mkuu. Ulisema nihakikishe watu wanapenda mikusanyiko isiyokuwa na maana kuliko kupenda kwenda kanisani."
"Sasa mbona makanisa yanajaza sana siku hizi?"
"Mkuu nilitumia mbinu moja kubwa na nzuri."


"Hebu nisimulie hiyo mbinu Balozeti maana nakuaminia sana wewe."
"Mkuu niliamua kuwapotosha baadhi ya wachungaji wapenda pesa kwa kuweka kipaumbele kwenye fedha badala ya kuhubiri neno la Mungu wao."
"Hali ikawaje au ikoje?"
"Kwa sasa wachungaji wengi wakisimama hawalizungumzi sana neno la
Mungu wao, wanatanguliza shida za mwili za binadamu."
"Mfano?"
"Mfano, tumewafanya wachungaji watoe matangazo redioni wakiuliza watu kama wanasumbuliwa na magonjwa sugu kama kansa, ukimwi, presha na mengine mengi.


"Lakini pia tumewafanya wachungaji haohao wakitoa matangazo yao waulize watu kama hawana kazi, wanatafuta watoto lakini hawapati, wanawake wanatafuta wanaume wa kuwaoa lakini hawapo.

"Matangazo haya yanasaidia kuwafanya watu wamiminike kwenye makanisa yao ambako neno linakuwa adimu. Kwa sababu hiyo siku hizi baadhi ya makanisa ya kilokole yana waumini wenye tabia kama za waumini wa makanisa ya kimwili."

"Sijapenda unaposema baadhi ya makanisa, mimi nataka makanisa yote yawe hivyo. Niahidi hapahapa Balozeti."

"Mkuu kwa heshima kubwa na nzito kwako na kwa kuzingatia hivi vita na kwa kuwa siku zimekwisha, ulimwengu umefikia ukingoni tayari na kwa kuwa mkakati wetu ni kuvuna wengi zaidi ili lile neno lao waingiao upotevuni
ni wengi nakuahidi kwamba makanisa yote yatakuwa hivyo."


"Kwamba?"
"Kwamba watasimama zaidi kwenye kuwapa waumini wao mambo ya kimwili na kusahau ya kiroho."
"Sawa. Mwaka elfu moja mia tisa na sitini tuliweka mkakati wa kuhakikisha makanisa yanakuwa mengi sana, wachungaji wanyang'anyane waumini lakini makanisa yote yakose nguvu, ilifanyika?"


"Ndiyo mkuu. Makanisa kwa sasa ulimwenguni kote ni mengi sana.
Tumejitahidi kuhakikisha baadhi ya maeneo kunakuwa na makanisa hata kwa umbali wa mita hamsini."


"Una maanisha nini?"
"Namaanisha kuna maeneo ambayo ukitembea umbali wa mita hamsini unakutana na kanisa. Wengine wanasali kama familia tu."


"Sawa. Vipi ule mpango wa kuwaingizia wachungaji roho za uzinzi, wizi, masengenyo, ubakaji, ulawiti na kupenda fedha kuliko kumpenda

Mungu?"
"Mkuu hilo lipo vizuri kwani kama utaangalia kwenye kumbukumbu zako za mwaka huu, wachungaji wengi siku hizi wanakumbwa na skendo hizo ulizozitaja licha ya kwamba waumini nao wameonekana hawapotezi imani kwa wachungaji hao licha ya vitendo viovu.


"Kwa hiyo?"

"Tunaendelea mkuu. Lakini kuna wachungaji waliosimama katika kuomba kila siku usiku na mchana wamekuwa wagumu kuwaingilia.

Ili kujua zaidi usikose kusoma baadae.......
 
MziziMkavu , swali moja kwako. Je, ni kwanini hayo "mapepo" yaliyomsababishia "mauti fake" bwana EMMANUEL Muhuge Magende, yanaonekana kuogopa sana Kanisa ni siyo nyumba nyingine za ibada?
 
Back
Top Bottom