Nusu siku ndani ya jeneza

Nusu siku ndani ya jeneza

funika kombe mwana haramu apite
Heri nusu shari kuliko shari kamili

Jamani Habari zenu?

Samahanini sana kama nitawakwaza kwa njia 1 ama nyengine.

Sisi binaadamu tunapoelekezwa njia nyepesi ya kuishi huwa tunakimbilia huko bila kujua au kujiuliza, je hiyo njia iko sahihi?

Lengine kuna baadhi wanajua kuwa hiyo njia sio sahihi Lakini kuna kitu anafatilia au kupenda(hadithi) kwahiyo kukemea kusema sio sahihi, anaogopa kumkasirisha muandishi, huo upungufu wa Imani.

Chengine, ibada ya nyota ina utapeli mwingi au uchawi labda niseme hivyo, maana utalazimishwa kuvaa Vito tofauti tofauti, pete, rangi na vitu vingi.

Jiulize utakapo fuata nyota hiyo unayoambiwa kweli utamuabudu mola wako kweli? Wakati nguvu ya nyota inakuwezesha kila kitu. Kwahiyo utaanza kuabudu nyota.

Ukisema unafuata nyota tu na huiabudu, wewe utakuwa hujui maana ya kuabudu!

Chengine nyota ni ibada ya majini wabaya/ mashetani au BINAADAMU wabaya. Kwanza kwa kufuata hadithi hii hii angalia hizo chapter za mwisho mwisho, nani anatoka ELIMU YA NYOTA? Jiulize upate jibu.

Kwanini afundishe Elimu ya NYOTE? Kwani anaogopa kumtaja YESU wakati anaweza kukufundisha Elimu ya nyota? (mimi muislamu).

Ndugu zanguni dini zipo nyingi sana, soma vitabu itafute elimu. Uijue dini iliyosahihi, na uifute kikamilifu. Kama uislamu, ukristo, ubaniani, upagani, unyota.n.k

Ni ukumbusho tu. No fight just peace!
 
Jamani Habari zenu?

Samahanini sana kama nitawakwaza kwa njia 1 ama nyengine.

Sisi binaadamu tunapoelekezwa njia nyepesi ya kuishi huwa tunakimbilia huko bila kujua au kujiuliza, je hiyo njia iko sahihi?

Lengine kuna baadhi wanajua kuwa hiyo njia sio sahihi Lakini kuna kitu anafatilia au kupenda(hadithi) kwahiyo kukemea kusema sio sahihi, anaogopa kumkasirisha muandishi, huo upungufu wa Imani.

Chengine, ibada ya nyota ina utapeli mwingi au uchawi labda niseme hivyo, maana utalazimishwa kuvaa Vito tofauti tofauti, pete, rangi na vitu vingi.

Jiulize utakapo fuata nyota hiyo unayoambiwa kweli utamuabudu mola wako kweli? Wakati nguvu ya nyota inakuwezesha kila kitu. Kwahiyo utaanza kuabudu nyota.

Ukisema unafuata nyota tu na huiabudu, wewe utakuwa hujui maana ya kuabudu!

Chengine nyota ni ibada ya majini wabaya/ mashetani au BINAADAMU wabaya. Kwanza kwa kufuata hadithi hii hii angalia hizo chapter za mwisho mwisho, nani anatoka ELIMU YA NYOTA? Jiulize upate jibu.

Kwanini afundishe Elimu ya NYOTE? Kwani anaogopa kumtaja YESU wakati anaweza kukufundisha Elimu ya nyota? (mimi muislamu).

Ndugu zanguni dini zipo nyingi sana, soma vitabu itafute elimu. Uijue dini iliyosahihi, na uifute kikamilifu. Kama uislamu, ukristo, ubaniani, upagani, unyota.n.k

Ni ukumbusho tu. No fight just peace!

comment yako ni fupi lkn inaujumbe mzito inshort inajitosheleza,nimekuelewa vyema,
kula big like.
 
Nusu Siku Ndani ya Jeneza-23-

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
“Alipomaliza kusema hayo, alituamuru kila mmoja apite mbele yake ili amuwekee mikono kama kiapo chake.
Hali ilikuwa sivyo kwangu sikutaka kabisa kukubaliana na tukio lile.
“Sikuwa tayari kupita kwake na kuniwekea mikono kwani hilo nililiona kama ni kumsaliti Mungu wangu ambaye niliamini hata wao viumbe pia hawamuwezi.
ENDELEA SASA…


NIKAANZA kuangaza huku na kule, moyo ukawa unaenda kwa kasi ya ajabu sana. Moyoni nikajawa na wasiwasi mkubwa ambao sikujua ulitoka wapi.
Nataka kila mmoja akae kwenye mstari kwa ajili ya kupita kwangu, ni kitendo cha haraka sana.
Akazidi kutuamuru yule kiumbe, lakini safari hii alikuwa makini na siriaz sana, kwani alikunja sura kwa kumaanisha alichokizungumza.
Wenzangu wote walijipanga mstari kwa ishara ya kukubaliana na amri ile, mimi na wenzangu wawili tulikuwa bado tukijikokota.
Basi, yule kiumbe akaamka na kuja hadi mahali tulipokuwa tumekaa.
Akatutaka sote tujipange mstarini kama alivyokuwa akielekeza.
Kwa shingo upande, tukajipanga kwenye mstari na kuanza kumsogelea yule kiumbe ili tukiri kuwa tutafuatisha maagizo yake.
“Sasa baada ya zoezi hili, kuna nguvu kubwa na ya ajabu mno itakayoingia ndani yenu, na mtakuwa viumbe wapya kabisa na kuyafurahia maisha haya kwani mtakuwa mkifanya mambo yenu kwa uhuru mkubwa bila kipingamizi chochote kutoka kwa viumbe dhaifu kama bibadamu,” alisema.
Akawa anasisitiza, lakini safari hii sauti yake ilitoka kwa juu sana huku ikiwa na kitetemeshi ndani yake, hali iliyomshitua kila mmoja wetu na kuanza kuingiwa na hofu kubwa ndani yetu.
“Zoezi likaendelea hadi ilipofika zamu yangu. Hakika sikuwa tayari kabisa kukiri mbele ya huyo kiumbe kuwa nitafuata amri zake. Nilijiona kuwa na hatia kubwa mno kufanya jambo hilo kwani lilidhihirisha kuwa Mungu wangu wa Mbinguni alikuwa ameshindwa mbele ya viumbe wale.
Wewe, sogea hapa muda umekwisha nataka tupangiane majukumu.
“Aliniamuru yule kiumbe baada ya kuona nasitasita kusogea karibu yake.
“Hapa naomba niseme jambo moja. Hakuna kitu ambacho viumbe wa aina hiyo huwakasirisha kama kuona binadamu wa kawaida anaonesha kiburi mbele yao.
“Basi, akawa ananiita nami niliendelea kusimama bila hata kujisogeza. Nikageuka kuwaangalia wenzangu ambao walikuwa wamekwisha tawazwa, nikakuta wakinishangaa. Lakini walikuwa tofauti kidogo. Macho yao yalikuwa makubwa na maangavu sana. Hata maumbo yao yalikuwa yamebadilika na kuwa makubwa kuliko yale ya awali”.
“Nikiwa naendelea kujiuliza, ghafla nikaanza kuona giza nene mbele yangu, kizunguzungu kikali kikanizingira na kuishiwa nguvu kabisa.”
“Kwa jina la Yesu Kristo aliye hai, kwa jina la Yesu, shetani tokaaa.
“Nilijikuta nikikemea kwa nguvu kubwa sana, sikuelewa ni wapi nilipata ujasiri huo, lakini nikazidi kukemea tena na tena.”
“Nilipokemea kwa mara ya mwisho, nilijikuta niko ndani ya jeneza!
“Jeneza lililokuwa limefunguliwa upande wa kichwa. Watu wengi walikuwa wakizunguka na wengine wakilia huku walikitaja jina langu, hali ilitisha.”
“Wakati naangaza huku na kule, nilishangaa kuona watu wote wakikimbia huku wakipiga mayowe na kusema marehemu amefufuka. Watu wote walikimbia na kuniacha peke yangu pamoja na mzee ambaye kwa kumuangalia kwa haraka, alikuwa ni mchungaji kutokana na aina ya mavazi aliyokuwa amevalia.”
“Mkononi alikuwa ameshika biblia. Akanitazama usoni na kukutanisha macho.
“Bila hata kumsalimia nikamuuliza mahali nilipokuwa.”
“Hapa ni kijijini kwenu Kilosa, tumekuja kukuzika,” alisema yule mzee huku akinisogelea kwa ujasiri mkubwa sana.
“Akapiga magoti na kujiegemeza kwenye jeneza na kuuunyosha ule mkono uliokuwa na biblia kwa upande wangu.
“Kunizika.”
“Ndiyo,” akanijibu yule mzee huku akianza kukemea kwa sauti ya chini mno.
“Sasa hivi ni saa ngapi,” nilimuuliza.
“Ni saa kumi na mbili jioni, tulikusafirisha kutoka huko ulikokuwa ukiishi tangu saa moja asubuhi, sasa kutokana na ubovu wa barabara, tumefika huku saa kumi na moja, kutokana na shughuli za kuweka mwili wako hapa na kukuaga, hatimaye imetimu saa kumi na mbili,” akazidi kunifafanulia yule mzee.
“Tulikuwa tumeamua kukuzika jioni hii kutokana na maamuzi ya kifamilia yaliyofikiwa na baadhi ya ndugu zako.”
“Nilikufa lini?”
“Ulikufa alifajiri, ilipotimu saa moja tukakuweka kwenye jeneza tayari kwa kukusafirisha,” akanijibu yule mzee ambaye alijawa na ujasiri wa ajabu mno.
Hapa naomba niseme kitu kimoja. Watu wa Mungu huwa na ujasiri wa hali ya juu mno, hata kama watakumbana na maajabu kama yangu ya kufufuka.
“Ina maana nimekaa nusu siku ndani ya jeneza?,” nikamhoji kwa huku nikiwa nimemkazia macho yule mzee.
“Ndiyo kijana wangu, umekaa nusu siku ndani ya jeneza, hebu nieleze ulikuwa wapi?,” aliniuliza yule mzee na kunifanya nishtuke kwani sikutegemea kama angeniuliza swali kama lile.

Itaendelea wiki ijayo... siku ya Jumamosi.......
 
ashukuriwe mungu ashukuliwe mungu aliye juuuuuuuu juujjuuuu..zaidi ya wote...tutashinda hila za adui kwa jina la yesuuuuuuuu
 
ILIPOISHIA WIKI
ILIYOPITA:
“Alipomaliza kusema hayo,
alituamuru kila mmoja
apite mbele yake ili
amuwekee mikono kama
kiapo chake.
Hali ilikuwa sivyo kwangu
sikutaka kabisa
kukubaliana na tukio lile.
“Sikuwa tayari kupita
kwake na kuniwekea
mikono kwani hilo nililiona
kama ni kumsaliti Mungu
wangu ambaye niliamini
hata wao viumbe pia
hawamuwezi.
ENDELEA SASA…
NIKAANZA kuangaza huku na
kule, moyo ukawa unaenda
kwa kasi ya ajabu sana.
Moyoni nikajawa na
wasiwasi mkubwa ambao
sikujua ulitoka wapi.
Nataka kila mmoja akae
kwenye mstari kwa ajili ya
kupita kwangu, ni kitendo
cha haraka sana.
Akazidi kutuamuru yule
kiumbe, lakini safari hii
alikuwa makini na siriaz
sana, kwani alikunja sura
kwa kumaanisha
alichokizungumza.
Wenzangu wote walijipanga
mstari kwa ishara ya
kukubaliana na amri ile,
mimi na wenzangu wawili
tulikuwa bado tukijikokota.
Basi, yule kiumbe akaamka
na kuja hadi mahali
tulipokuwa tumekaa.
Akatutaka sote tujipange
mstarini kama alivyokuwa
akielekeza.
Kwa shingo upande,
tukajipanga kwenye mstari
na kuanza kumsogelea yule
kiumbe ili tukiri kuwa
tutafuatisha maagizo yake.
“Sasa baada ya zoezi hili,
kuna nguvu kubwa na ya
ajabu mno itakayoingia
ndani yenu, na mtakuwa
viumbe wapya kabisa na
kuyafurahia maisha haya
kwani mtakuwa mkifanya
mambo yenu kwa uhuru
mkubwa bila kipingamizi
chochote kutoka kwa viumbe
dhaifu kama bibadamu,”
alisema.
Akawa anasisitiza, lakini
safari hii sauti yake ilitoka
kwa juu sana huku ikiwa na
kitetemeshi ndani yake, hali
iliyomshitua kila mmoja
wetu na kuanza kuingiwa na
hofu kubwa ndani yetu.
“Zoezi likaendelea hadi
ilipofika zamu yangu. Hakika
sikuwa tayari kabisa kukiri
mbele ya huyo kiumbe kuwa
nitafuata amri zake.
Nilijiona kuwa na hatia
kubwa mno kufanya jambo
hilo kwani lilidhihirisha
kuwa Mungu wangu wa
Mbinguni alikuwa
ameshindwa mbele ya
viumbe wale.
Wewe, sogea hapa muda
umekwisha nataka
tupangiane majukumu.
“Aliniamuru yule kiumbe
baada ya kuona nasitasita
kusogea karibu yake.
“Hapa naomba niseme
jambo moja. Hakuna kitu
ambacho viumbe wa aina
hiyo huwakasirisha kama
kuona binadamu wa kawaida
anaonesha kiburi mbele yao.
“Basi, akawa ananiita nami
niliendelea kusimama bila
hata kujisogeza. Nikageuka
kuwaangalia wenzangu
ambao walikuwa
wamekwisha tawazwa,
nikakuta wakinishangaa.
Lakini walikuwa tofauti
kidogo. Macho yao yalikuwa
makubwa na maangavu
sana. Hata maumbo yao
yalikuwa yamebadilika na
kuwa makubwa kuliko yale
ya awali”.
“Nikiwa naendelea kujiuliza,
ghafla nikaanza kuona giza
nene mbele yangu,
kizunguzungu kikali
kikanizingira na kuishiwa
nguvu kabisa.”
“Kwa jina la Yesu Kristo aliye
hai, kwa jina la Yesu,
shetani tokaaa.
“Nilijikuta nikikemea kwa
nguvu kubwa sana,
sikuelewa ni wapi nilipata
ujasiri huo, lakini nikazidi
kukemea tena na tena.”
“Nilipokemea kwa mara ya
mwisho, nilijikuta niko
ndani ya jeneza!
“Jeneza lililokuwa
limefunguliwa upande wa
kichwa. Watu wengi
walikuwa wakizunguka na
wengine wakilia huku
walikitaja jina langu, hali
ilitisha.”
“Wakati naangaza huku na
kule, nilishangaa kuona
watu wote wakikimbia huku
wakipiga mayowe na kusema
marehemu amefufuka. Watu
wote walikimbia na kuniacha
peke yangu pamoja na mzee
ambaye kwa kumuangalia
kwa haraka, alikuwa ni
mchungaji kutokana na aina
ya mavazi aliyokuwa
amevalia.”
“Mkononi alikuwa ameshika
biblia. Akanitazama usoni na
kukutanisha macho.
“Bila hata kumsalimia
nikamuuliza mahali
nilipokuwa.”
“Hapa ni kijijini kwenu
Kilosa, tumekuja kukuzika,”
alisema yule mzee huku
akinisogelea kwa ujasiri
mkubwa sana.
“Akapiga magoti na
kujiegemeza kwenye jeneza
na kuuunyosha ule mkono
uliokuwa na biblia kwa
upande wangu.
“Kunizika.”
“Ndiyo,” akanijibu yule mzee
huku akianza kukemea kwa
sauti ya chini mno.
“Sasa hivi ni saa ngapi,”
nilimuuliza.
“Ni saa kumi na mbili jioni,
tulikusafirisha kutoka huko
ulikokuwa ukiishi tangu saa
moja asubuhi, sasa kutokana
na ubovu wa barabara,
tumefika huku saa kumi na
moja, kutokana na shughuli
za kuweka mwili wako hapa
na kukuaga, hatimaye
imetimu saa kumi na mbili,”
akazidi kunifafanulia yule
mzee.
“Tulikuwa tumeamua
kukuzika jioni hii kutokana
na maamuzi ya kifamilia
yaliyofikiwa na baadhi ya
ndugu zako.”
“Nilikufa lini?”
“Ulikufa alifajiri, ilipotimu
saa moja tukakuweka kwenye
jeneza tayari kwa
kukusafirisha,” akanijibu
yule mzee ambaye alijawa
na ujasiri wa ajabu mno.
Hapa naomba niseme kitu
kimoja. Watu wa Mungu
huwa na ujasiri wa hali ya
juu mno, hata kama
watakumbana na maajabu
kama yangu ya kufufuka.
“Ina maana nimekaa nusu
siku ndani ya jeneza?,”
nikamhoji kwa huku nikiwa
nimemkazia macho yule
mzee.
“Ndiyo kijana wangu,
umekaa nusu siku ndani ya
jeneza, hebu nieleze ulikuwa
wapi?,” aliniuliza yule mzee
na kunifanya nishtuke kwani
sikutegemea kama
angeniuliza swali kama lile.
Itaendelea wiki ijayo...
 
Back
Top Bottom