NSSF na MANJI

Semilong

JF-Expert Member
Mar 5, 2009
1,712
219
katika sakasaka yangu viwanja siku za karibuni mitaa ya kigamboni nimekuta mfanyabiashara Yusuf Manji ana eneo kubwa sana la ardhi ambalo ajaliendeleza au unaweza kusema land banking.
kuna vibao tu vya onyo usiingie kwenye eneo hili.
Leo kwenye gazeti la guardian NSSF wametangaza tenda na kutaka watu wenye heka zaidi ya 100 kwenye maeneo ya kigamboni wawauzie.

maswali mengi nimejiuliza nimekosa majibu.....
 
Kama unataka kupata jibu....kuanzia leo weka kautaratibu ka kununua Sema Usikike au This Day. Hata mwezi haufiki utapata jibu.
 
Mahusiano ya Manji na NSSF ni kama ya chatu na mbwa - mbwa akimwona chatu nguvu humwishia na pamoja na kujua atageuzwa kitoweo, hujipeleka mwenyewe aliwe. Na ukimwona Manji na NSSF wanaanza kuchangamkiana, ujue mafisadi CCM tayari wameshanawa na kukaa mkao wa kula. Masikini Watanzania ni kama vile tuko msituni tumezungukwa na wanyama wakali, sasa tukimbilie wapi ? Mbele Rostamu, kushoto Manji, kulia Patel na nyuma CCM. Kaazi kweli kweli !!
 
manji ataondoka na mabilioni yake kadhaa hapo!.....u just have to love Tanzania
 
Manji hauzi plots, yeye ni property developer!. Alikopa bilioni 10 mifuko ya pensheni, PPF, NSSF na PSPF. Akazitumia hizo bilioni 10 kununua plot pale Quality Park, akadevelop, akawauzia hao hao PPF, NSSF na PSPF kwa bilioni 50, alipolipwa, akawalipa lile deni lao la bilioni 10!.
 
Hizo ndio deal za mjini kaka,na ukisikia watoto wa mjini ndio hao,sio kwenda kushinda leaders jumapili kwenye ulevi au club sunciro ukapiga kelele zisizo maana ukasema wewe mjanja.
 
Hizo ndio deal za mjini kaka,na ukisikia watoto wa mjini ndio hao,sio kwenda kushinda leaders jumapili kwenye ulevi au club sunciro ukapiga kelele zisizo maana ukasema wewe mjanja.

Nenda wewe na ngozi nyeusi kwa Dr Dau kama atakupa hilo deal.....ati wanasema mhindi ukimpa dili analipa mswahili anaingia mitini
 
Na hapa ndipo tunapohitaji maoni ya "wakereketwa wa uzalendo wa nchi" ambao kwenye sakata nyingine walikuwa mstari wa mbele kuipigania Tanzania. Conveniently, watu kama GT wako kimyaaa kama vile hii thread haiwahusu au hawajaiona. Hizi double standards za JF ambazo mimi zinaniacha hoi sana. Kwa muda mrefu kumekuwa na madudu kwenye mifuko hii ya pensheni na hasa NSSF lakini coverage yake imekuwa very scanty. Mimi nina hakika hiyo deal tayari imefanyika na watu wanasubiri kununuliwa nyumba London.
 
Manji , Manji , na haya mashirika ya jamii ni pacha, wanafanya biashara halamu kitambo sasa.
ila kule mbele ya Geza Ulole kuna eneo lina zaidi ya Hekta 300 hivi limezungushhiwa uzio na vibao vinavyosema mali ya NSSF.
NA ENEO LA MANJI YUSUPH linaanzia hapa jirani na mikadi beach linaendelea hadi kule kwa Mwingira, ni zaidi ya hekta mia, na anaeneo lingine kule jirani na mji mwema kama unaelekea Kongowe....sasa hili eneo la hapa mikadi nasikia ni sehemu ya ule mradi usioeleweka , ila umepewa jina la mradi wa George Bush....
ila upo ushirika wa kinyonyaji kati ya wakuu wa mifuko ya jamii na Manji Yusuph fisadi namba mbili baada ya RA.
 
Dau anawatafutia hela CCM na makada wake kupitia manunuzi kama haya. Mmeimulika sana BOT lazima zitafutwe njia mbadala. CCM hawashindwi bwana!
 
katika sakasaka yangu viwanja siku za karibuni mitaa ya kigamboni nimekuta mfanyabiashara Yusuf Manji ana eneo kubwa sana la ardhi ambalo ajaliendeleza au unaweza kusema land banking.
kuna vibao tu vya onyo usiingie kwenye eneo hili.
Leo kwenye gazeti la guardian NSSF wametangaza tenda na kutaka watu wenye heka zaidi ya 100 kwenye maeneo ya kigamboni wawauzie.

maswali mengi nimejiuliza nimekosa majibu.....

Lazima ukose majibu kwa sababu ulishakuwa na assumptions zako.....

Pasco ameeleza vizuri sana. Manji ni Real Estate Developer the same as NSSF. Ila wewe unataka ku leta issues zako mwenyewe kwamalengo yako bila shaka. Ushauri wangu tusiandike na mate.. tungojee deadline ya tangazo lakuuza hivyo viwanja na tuone kama huyo Manji ataiuzia NSSF au la? badala ya kutumia muda mwingi kwenye tetesi.
 
Mahusiano ya Manji na NSSF ni kama ya chatu na mbwa - mbwa akimwona chatu nguvu humwishia na pamoja na kujua atageuzwa kitoweo, hujipeleka mwenyewe aliwe. Na ukimwona Manji na NSSF wanaanza kuchangamkiana, ujue mafisadi CCM tayari wameshanawa na kukaa mkao wa kula. Masikini Watanzania ni kama vile tuko msituni tumezungukwa na wanyama wakali, sasa tukimbilie wapi ? Mbele Rostamu, kushoto Manji, kulia Patel na nyuma CCM. Kaazi kweli kweli !!

tukimbilie CCJ
 
Back
Top Bottom