Siamini serikali inakusanya kodi ipasavyo. Kanzidata ya wapiga kura 2015 na zingine zitumike kuwatambua walipakodi nchi nzima

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,876
20,284
Kuna mambo ambayo nakubaliana na hayati Magufuli khasa katika utekelezaji wa sera za CCM hususani dira ya maendeleo ya 2015-2025.

Hayati Magufuli alitaka kila mradi khasa ile miradi mikubwa ikamilike kabla ya 2020.

Moja ya miradi ambayo hata hivyo alitaka ikamilike mwaka huu ni ujenzi wa mji mkuu wa Dodoma na uwanja wa ndege wa Msalato.

Hiyo ni kwasababu tayari mabalozi wengi walipewa viwanja bure wajenge ofisi za ubalozi Dodoma na uwanja wa ndege utumike kitaifa na kimataifa.

Kuna mambo kama serikali kugharamia uchaguzi mkuu wa 2020 jambo ambalo liliwaudhi sana nchi rafiki na watoaji wakubwa wa misaada kwa Tanzania ambao walizoea kutoa fedha zao kwa ajili hiyo.

Lakini jambo moja ambalo mimi binfasi naona lilimpa shida hayati Magufuli ni namna ya kukusanya kodi ipasayo na kupanga matumizi ya fedha hizo.

Mbinu mojawapo alotumia ni kuwabana wafanya biashara kwa kuangalia mapato na aina ya biashara zao na kisha kuwapa uwanja mpana wa majadaliano ambapo walokubaliana kuwa kuna eneo walikwepa kulipa kodi.

Kwa mfano mfanyabiashara A alikwepa kodi kwa miaka zaidi ya ishirini na ili aweze kuendelea na biashara zake bila kuathirika kuna uwezekano mkubwa alikubaliana na serikali na TRA alipe fedha hizo labla bilioni 2 kugharamia kitu fulani.

Hivyo wananchi kufuraia kuona ndege zanunuliwa, madaraja kujengwa na midadi mingine mikubwa pengine ilikuwa ni fedha zilizotoka katika fungu la wakwepa kodi.

Mfano mwingine ni mfanyabiashara B ambae baada ya kupigiwa simu na kuambiwa ana kiasi fulani benki na atoe maelezo amezipataje fedha hizo kulinganisha na aina ya biashara yake njioa nzuri ya kukaa salama ilikuwa ni kuhakikisha anawasilisha hazina kupitia BOT kiasi cha fedha ambazo hakulipa kodi.

Mfano mwingine ni wauza madawa, maduka ya fedha za kigeni, biashara za utalii, mahoteli ya kugeni na wawindaji haramu hawa wote ilibidi waathirike na mtindo huu wa serikali ilopita ambayo raisi wa sasa Samia Suluhu Hassan alifahamu na bado akumbuka uzuri.

Ndo maana Sulemani Manji hakuweza kuendelea kuishi Tanzania na kufanya biashara zake kwa kuwa bado wale wahafidhina wa hayati Magufuli bado wapo na hawatoweza kumruhusu Manji akae na kuendeleza biashara zake kihalali.

Sasa tukirudi kwenye aina ya ukusanyaji katika mtindo wa huo pia ulichanganywa na mtindo wa kukusanya mapato yote hazina na kumfanya Magufuli aweze kuona kitu ndani ya boksi na kuweza kuamuru fedha zitumike vipi.

Lakini bado watu waliweza kuiba fedha hizo za makusanyo ya kodi katika halmashauri na wizi uliendelea kuwepio katika maeneo mengine kama MSD, na mahospitalini kwenye ugavi madawa na sehemu zingine nyingi tu.

Hata ulipoanzishwa mtindo wa kutoa namba maalum yaani Control namba, bado hakukuwa na mfumi thabiti ulohakikisha malipo yanaenda kwa huduma inayohusika.

Kwa mfano mtu akilipia Pasi ya kusafiria utakuta waandikiwa barua pepe inayokuambia kwamba malipo yako ya kitambulisho cha taifa yamekamilika badala ya pasi ya kusafiria.

Sasa tangu hayati Magufuli afariki miezi mitano ilopita kumekuja tozo tofauti zikiwemo tozo ya majengo na tozo ya miamala na leo hii tumeambiwa tozo ya majengo imetengeneza shilingi bilioni 48!

Hizi bilioni 48 ni fedha ndogo sana ukilinganisha na idadi ya majengo yote yaliyopo nchi nzima je, tuna majengo mangapi?

Au tozo za miamala zimeitengenezea serikali kiasi gani na je kiasi hicho cha mapato kitaendelea kupanda kulingana na mikakati ipi ilowekwa?

Si ni miezi zaidi ya sita au saba tuliambiwa majengo yote yalitakiwa kuwa yamesajiliwa na serikali za mitaa? Je taarifa zilizopo katika kanzidata ya wizara ya ardhi yalingana na kanzidata iliyopo tume ya uchaguzi, au iliyopo NIDA au vizazi na vifo?

Napendekeza serikali itumie Kanzidata ilotengenezwa mwaka 2015 ambayo iliorodhesha wapiga kura wote nchi nzima.

Kisha kanzidata hiyo ilinganishwe na kanzidata ya NIDA ambayo ina alama za vidole na picha za mhusika, kisha iunganishwe na kanzidata iliyopo wizara ya ardhi na mwisho kuoanishwa idara ya uhamiaji.

Kufanya hivi kwahitaji teknolojia ambayo kwa kuanzia naamini tunayo, na wataalam wa kutengeneza kanzidata tunao na wapo na wengine hawana kazi.

Hivyo serikali iunde timu maalum kwa ajili ya kazi hii ya kuhakikisha watanzania wote wamo kwenye "system".

hata mzee Slim ana vijana wenye utaalam wa hali ya juu kwenye hili tuombe msaada na nina imani hatosita kusaidia.

Hivyo TRA wanakuwa na kanzidata yao yenye mlipa kodi na TIN number kisha kufahamu aina ya kipato cha mlipa kodi kabla ya kuanza kumtoza.

Kila halmashauri itambue walipa kodi wake, majengo yote yaliyomo kwenye halmashauri iwe ya makazi au biashara, na nyumba zote taarifa zake ziwemo kwenye kanzidata ili kodi ya majengo ilipwe.

Hivyo hivyo kwa wilaya zote na hadi mikoani kila aina ya kodi ilingane na chanzo chake iwe jengo, kaduka, nyumba za makazi.

Biashara za aina zote migahawa, mahoteli, kumbi za starehe, machinjio, maegesho ya magari (wahindi wameshika hii kitu mijini), masoko na zingine zinazofahamika ni lazima zitambuliwe kwenye kila halmashauri, wilayani, mikoani na nchi nzima.

Suala la kodi si lelemama lahitaji mipango, welevu na umakini kulitatua.

Kwanza miezi mitano imepita hatujasikia makampuni kama ile ya Airtel na mashirika au mabenki yamegawana kiasi gani cha mapato na serikali

Nimalizie tu kwa kusema kukusanya bilioni 48 za tozo ya majengo ni fedha ndogo sana.

Tuketi chini na tuangalie na tuone tuna kanzidata zifuatazo, kanzidata ya tume ya uchaguzi -NEC, kanzidata ya NIDA, kanzidata ya TRA, kanzidata ya Ardhi, kanzidata ya Leseni ya udereva, kanzidata ya UHAMIAJI, kanzidata ya RITA na zingine kama zipo.

Tunashindwa kitu gani kutengeneza mfumo wa kodi wa nchi nzima kila mtanzania anaepaswa kulipa kodi akalipa kodi inavyostahiki?

Kanzidata ya 2015 itumike kuwatambua wapiga kura wote nchi nzima. Pia TRA na serikali itambue raia nchini wote wenye umri wa kulipa kodi, ikibidi sensa mpya inokuja iunganiswe na mpango huo.

Twataka kuona Tanzania ikirudi kwenye uchumi wa kati kama ilvyokuwa miezi mitano ilopita, ikijitegemea kwa baadhi ya masuala muhimu.

Au la, tujitafakari kama taifa.
 
Baada ya kuwafukarisha kwa viwango hivyo bado mnandoto ya kuendelea kujipatia kipato kutoka kwao, embu jitafakari kwa mara nyingine kabla ya kuja na upupu humu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom