North Mara: Kashfa ya maji ya sumu toka mgodini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

North Mara: Kashfa ya maji ya sumu toka mgodini!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 26, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Taarifa kwa vyombo vya habari: Kujibu taarifa zilizotolewa kwenye gazeti siku ya Jumapili, tarehe 21 Juni 2009

  Mara, Juni 23 2009 – Uongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unapenda kukanusha vikali shutuma zilizotolewa na gazeti la Mtanzania la Juni 21 2009, likidai kwamba watu 21 na zaidi ya ng’ombe 200 kutoka Kata ya Kibasuka, wilaya ya Tarime wamekufa kutokana na kunywa maji yenye Kiwango Kidogo cha Uasidi kwenye Maji ya Mto Tigithe. Taarifa hiyo iliyoandikwa na mwandishi wake Bw Christopher Gamaina ikimnukuu kwa kirefu Diwani wa Kata ya Kibasuka na kuvumisha kuwa vifo hivyo vimesababishwa na uvujaji wa maji kutoka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.

  Tunapenda kusema kwamba malalamko haya si ya kweli na ni batili. Taarifa hiyo haikufanyiwa uchunguzi, ina malengo mabaya, na siyo ya msingi kabisa; jambo ambalo limethibitishwa na mamlaka zinazohusika.

  Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo;


  • Mnamo Juni 15 2009 Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ilipokea nakala ya barua ya malalamiko kutoka kwa Diwani wa Kata ya Kibasuka iliyotumwa kwa ofisi ya Waziri Mkuu.


  • Barua hiyo ilidai kwamba watu 18 na zaidi ya ng’ombe 200 kutoka kata ya Kibasuka wilaya ya Tarime wamekufa kutokana na kunywa maji yenye kiwango kidogo cha uasidi ya mto Tigithe .


  • Mara baada ya kupata taarifa hizo mgodi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara uliwasiliana na mamlaka husika ili kuzihimiza kufanya uchunguzi.


  • Mnamo tarehe 21 Juni 2009, timu ya uchunguzi iliundwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime kuchunguza malalamiko hayo.


  • Timu hiyo iliyowajumuisha Afisa Afya Mkuu wa Wilaya, Afisa Maendeleo ya Kilimo na Mifugo wa Wilaya, Mkuu wa Polisi wa Wilaya pamoja na Afisa Afya wa Mkoa walitembelea vijiji vilivyotajwa kwenye barua hiyo ambavyo ni pamoja na kituo cha afya cha Nyarwana, ambacho kwa mujibu wa barua hiyo kilikuwa na taarifa muhimu za kuthibitisha shutuma hizo. Timu hiyo ya uchunguzi iliongea na mkuu wa kituo hicho na kuchunguza kumbukumbu za matibabu ambapo zote zilishindwa kuthibitisha shutuma hizo.


  • Zaidi ya hayo wakati Diwani wa Kata ya Kibasuka alipokutana na timu hiyo ya uchunguzi, alishindwa kuthibitisha vifo vya watu hao 21 aliowaripoti. Pia alishindwa kuandaa mkutano na wafugaji wa ng’ombe 200 aliodai wamekufa na vilevile alishindwa kuonyesha mizoga yao. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pia ilitoa taarifa kwamba Diwani huyo wa Kata baadae alidai kwamba vyombo hivyo vya habari vilimnukuu vibaya.

  Mgodi wa Dhahabu wa North Mara inakusudia kufungua rasmi malalamiko kwa Baraza la Habari Tanzania na kuchukua hatua zozote muhimu ili kuepusha shutuma zisizo na ukweli zinazokusudia kuchafua heshima yake na kusababisha msuguano na jamii inayouzunguka.

  Kuhusu Shirika la Dhahabu la Barrick
  Shirika la Dhahabu la Barrick ni kampuni ya uchimbaji madini inayoongoza ulimwenguni. Hisa za Barrick zimeorodheshwa katika soko la hisa la huko Toronto na New York.

  Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Tanzania inaendesha migodi minne nchini Tanzania. Ambayo ni Bulyanhulu, North Mara, Tulawaka na Buzwagi.

  Imetolewa na:
  Teweli Kyara Teweli
  Uhusiano na Mawasiliano
  Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Tanzania,
  Kitalu 1736, Br. Hamza Aziz,
  S.L.P 1081, Dar es Salaam
  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

  NB:

  Kwanini Barrick?

  Kwanini uchunguzi wa mambo ya namna hii usiwe na SOP yake inayofuatwa nchi nzima badala ya kila tukio kutafutiwa njia yake ya kuchunguza?

  Kwanini tume ya Haki za Binadamu isipewe jukumu la kuchunguza tuhuma za aina hii au kitengo fulani chini ya Jeshi la Polisi na taasisi za haki?


   
  Last edited by a moderator: Jun 30, 2009
 2. G

  Gashle Senior Member

  #2
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mzee MJJ,

  Inauma kwa kweli! Ndio hapo mimi ninaposema watu kama kina Teweli hawa sijui kama ni Watanzania wa kweli. Shame on you Teweli kwa upotoshaji wa makusudi. Kwa hiyo kwa mujibu wa Barrick wenyewe wanaona mambo yanakwenda sawa tu huko Tarime? Watu walioharibiwa na hizo kemikali wazushi sio?

  Ole wenu viongozi wa Tanzania, ole wenu wanafiki wakubwa na wasaliti kama Teweli! Sijui kama huyu bwana anayo nafsi ya kumsuta na kumhukumu. Again, shame on you Teweli Teweli na Barrick yako.

  By the way, sihitaji kujua profile ya Barrick,sihitaji kujua kuwa Barrick ni shirika la uchimbaji madini linaloongoza duniani. Sihitaji kujua kuwa wameorodheshwa katika soko la hisa la wapi! Hainisaidii chochote mimi Mtanzania na ndugu yangu anaendelea kuugua kwa mateso pale Tarime. Shame, shame!
   
 3. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Viumbe vimeathirika kwa kunywa maji yenye "kiwango kidogo cha uasidi."

  Ina maana kiwango cha uasidi kingekuwa kikubwa zaidi ndio bora, au?
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Maneno yenye rangi nyekundu yamenifurahisha!!!!!!!
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Jamaa kafanya direct translation ya "trace amounts of acids" (inawezekana hapa kwenye acids kunafichwa misumu).Halafu hata hatuambiwi ni acid gani, maana asidi nyingine zipo katika udongo tu na haziwezi kudhuru watu wala mifugo.

  Hapa naona kama kuna mercuric acids zinazotumiwa katika kusafisha gold zinafichwa kwa jina hili generic la "uasidi".Inawezekana kabisa tushalishwa mi mercuric nitrates inayotumika kusafisha dhahabu kiholela na ambayo nchi zilizoendelea kama US ziliishaipiga marufuku tangu 1940's huko.

  Asidi gani isiyotajika hiyo? Wanapunguza makali ya hoja hao.Na wamewakuta watu wa press kwetu wanawashindilia ujinga tu.
   
  Last edited: Jun 26, 2009
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,554
  Likes Received: 18,239
  Trophy Points: 280
  Hii issue is more serious than it looks, PM Pinda kaona ndio serikali imezinduka, sasa kazi ya uchunguzi rasmi itaanza.
  Pia msimlaumu ofisa wa Barrick kwa kutoa taarifa aliyoitoa, yeye anatimiza majukumu yake.
  Ukiwa PR wa kampuni yoyote, you may have to compromise patriotism with professionalism. Kwenye professionalism, ni be professionnal forget everything else.
  Nimeshuhudia madaktari wazembe wakipoteza maisha ya watu in the cover of professionalism. Watanzania tulalishwa sumu kila siku bila kujua in the name of investors.
  Hapa ndipo tunapohitaji the true patriotic lawyers watakaowapigania wananchi wasio na kitu, na nawahakikishia kama kina Tundu Lissu na LEAT yao wakinterverne seriously na legaly, Barrick statement would not be the same again. Tuendelee kusubiri, time will tell.
   
 7. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Nchi hii ingekuwa ni nchi inayofuata utawala bora baadhi ya viongozi wangeenda na maji kwa madhara hayo. Tatizo tunakumbatia wawekezaji mno hata kuwaweka rehani Watanzania.

  Baadhi ya viongozi wamesikika wakisema hakuna madhara yoyote yaliyokwishatokea kwa mujibu wa vyombo vya habari na licha ya wakili Tindu Lissu kupiga kelele naye anadai serikali imekuwa kimya kwa muda mrefu na halafu Waziri Mkuu Pinda anasema hawakuwa hawajui! Siamini kabisa!

  Ili haki itendeke kwa wananchi hao baadhi ya viongozi serikalini wawajibike kwa kung'atuka na halafu waxhukuliwe hatua na pia mgodi husika uwalipe wananchi hao fidia kwa kuhatarisha afya zao na mali zao na uhabibifu wa mazingira!
   
 8. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna mambo mengi, Ndugu yangu Mzee mwanakijiji, Mtafute Tindu Lissu akwambie mambo haya ni ajabu sana na pia inauma sana sana kama Watanzania wanakufa hivi kwasababu ya mambo ya ajabu kama haya, Mzee mwanakijiji mtafute Askofu Mokiwa akwambie tena
   
 9. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kwangu mimi maneno hayo yamenikera na yanaonesha jinsi gani hawa jamaa walivyo na kiburi,yaani mtuhumiwa aende akamhimize mwenye mamlaka ya kuchunguza amchunguze,afu yeye tena[huyu mtuhumiwa]atoe na taarifa????

  na pia diwani,ambaye kwa mujibu wa taarifa hiyo,ndie aliandika barua kwa PM na nakala kuwatumia hawa wenye mgodi anageuka anasema walimnukuu vibaya,wakati ni yeye aliyeandika barua???????? soma hapa Barua hiyo ilidai kwamba watu 18 na zaidi ya ng’ombe 200 kutoka kata ya Kibasuka wilaya ya Tarime wamekufa kutokana na kunywa maji yenye kiwango kidogo cha uasidi ya mto Tigithe .
  kuna nini kilitokea hadi huyu diwani akaikana barua aliyoandika???????
   
 10. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kiwango cha Usaidi ni (Cynide)wanayo sema.Hili Jambo limekaaa kisiasa zaidi ya ukweli wa kawaida....Ukiangalia hiyo report ni ya kijiji kilichomba mbali na mgodi wa dhahabu wa North Mara ambao ni nyamwanga.Yes the river falls zinakwaenda mpaka uko na wao huja kulishia ng'ombe pande hizo?Kwanini watu wa nyamongo 2Km from mine site and 3-4 Km kutoka maji yenye cynide yalipo wasiathirike all that long?

  Kuna kitu kinaitwa Rom pad 7km kutoka mgodi uliko lakini karibu na mashimo zinakichimbwa dhahabu ambako ndio maji hayo yapo....kila mgodi maji hayo yapo.Na yamehifadhiwa kwa ungalifu wa hali ya juu na kuwa monotored every day.Hatujasikia malalamiko haya...RESOLUTE NZEGA,BULYANHULU KAHAMA,GEITA MWANZA,TULAWAKA BIHARAMULO,WALA BUZWAGI KAHAMA.Ni Tarime tu!!!Hatujiulizi ni kwanini?Ina maana wa tarime tu barrick inaamua kuyamwaga kwa makusudi?Kwa mtizamo wa kawaida si kweli....

  Ukweli ni kwamba intruders(wez wa mawe ya dhahabu)baada ya shimo moja kusimama uchimbaji wakawa hawana cha kufanya kwa kuwa wanategemea production iwepo ili na wenyewe waweze kupata mawe yenye dhahabu..sasa baada ya kukosa..wakaamua kutafuta kitu mbadala cha kuiba wapate kipato...see sasa wameiba carpet hilo a linalo zuia maji yasiingie ardhini na kuwa contaminated na maji salama yanayo tumika kwa matumizi ya binadamu.

  Maji yakatiririka kwenda mtoni ng'ombe wakanywa.Binadamu kwa kweli sina uhakika....kwangu mie sijaona muathirika hata mmoja zaidi ya meneno ya mwenyekiti huyu....je hilo ni tatizo la nani?Wananchi ? au Barrick?Tungalie katika upanda wake hata hao walio iba....au kukata hilo carpet ni wananchi wa mbali na eneo la mgodi..hii naweza sema ni ukosefu wa uelewa..kwani wakijiji wa nyamongo wao hawajawahi fanya makosa hayo.Wanajua madhara.

  Wanaposema kiwango kidogo cha Usaidi(cynide)ni kweli kwa kuwa cynide nyingi inakuwa imesha tumika kwa kazi yake...hicho kinachopelekwa uko ni kwa sababu ya kuhifadhiwa na kuendelea kuwa treated mpaka itakapo fika 0.00%.Na hii hufanyika kwa kuongeza maji mengi.
   
 11. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Nchi hii ina matatizo sana, hakuna utaratibu wowote ule uliopo ambao una deal na mambo kama haya. NEMC wapo lakini hawa jishughulishi na lolote lile juu ya swala hili.

  Kutokana na mpact kubwa iliyotokea mimi nadhani kwanza Serikali ilitakiwa kusimamisha shughuli zote za uzalishaji za North Mara Mine ndio uchunguzi ufanywe na sio kulifanya swala la kisiasa zaidi.
   
 12. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Kwa mawazo yako kukaa kimya ni sawa na kutoathirika? Afadhali kuliko kusema kinachosemwa ni siasa (yaani kuwa watu na mifugo havijathirika) ni afadhali ungesema uchunguzi ufanyike kuona ni kwa kiasi gani hizo tuhuma ni kweli.

  Kuna mambo mengi yanfanyika hapa nchini na watu hawajui wafanye nini na kama wananchi hawana njia ya kufanya siamini kuwa hawana matatizo. Migodi yote hapa nchini inapigiwa kelele watu kunyanyasika lakini hawasikilizwi na wengine wamekata tamaa kabisa.

  Hata mimi naona hayo unayosema nayo yamejaa siasa kabisa!
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Buswelu,
  Mkuu inaopnyesha wewe huelewi kabisa uzito wa swala hili badala yake unatafuta vijisababu bila kuelewa impact inayotokana na hazardous waste toka migodi ya dhahabu..
  Unapohoji ukaribu wa kijiji hicho na mgodi una maana gani? yaani unaamini haiwezekani kwa sababu ati kijiji kiilicho karibu na mgodi ule hawajadhurika mkuu wangu kujenga hoja yako wakati sidhani kama unafahamu mifereji - Ephemeral drainage system wala dump area ya hizo waste za mgodi huo ziko wapi!.

  Kwa Mtanzania huhoji ukweli wa taarifa kama hioi wakati ushahidi upo, watu wamekufa, mifugo imekufa leo unataka watu tuamini kwamba hakuna sababu.. Ndicho Barricks walichofanya wamekana vifo hivyo kutokana na waste zao lakini pia wameshindwa kutuambia sababu zilizosababisha vifo vya watu na mifugo..meaning uchunguzi wao ulikuwa hauna utaalam kabisa.
  Huwezi kwenda fanya uchunguzi wa kisayansi kuhusiana na vifo, ukashindwa kupata sababu lakini uka rule out wastes zinazotokana na mgodi huo.. I doubt hao wachunguzi wetu ambao hawakusomea madini, wameweza ku identify AMD (Acid Mine Drainage) discharger na waste accumulations ziko sehemu gani kabla hawaja rule out hizo acidic mine waste kuwa ndio sababu.. kisha basi hiyo taarifa ya Barricks haikuzungumzia kabisa uchafu wa madini yao hupelekwa wapi ama hutupwa wapi..
  Na kikubwa nilichoelewa mimi, Objective ya uchunguzi huu ulikuwa kukana/kufuta/kupinga madai ya wananchi hivyo uchunguzi ulikuwa na malengo ya kuwasafisha Barricks, badala ya kuchunguza na kutoa map ya mineralogy mine affected areas kuonyesha kwamba isingewezekana vifo hivyo kutokana na waste zao..

  Sasa ebu tuambie ikiwa hawa watu hawakuona AMD wala kufahamu wastes ziko wapi utawezaje kujibu hoja hii ikiwa kila mgodi ni lazima uwe na dump area ya hizi wastes..
  Yaani mifugo na watu wale wamekufa ghafla tu on natural causes sio!..Kisha basi wala sii swala la kwanza kwa Barricks.. Hivi sasa wana kesi kubwa sana huko South Amerika inayohusiana na maswala kama haya haya leo sisi tunajaribu kuficha ukweli kama tulivyozoea kuficha..
  Ndio maana hata swala la Mapanki, tulikataa katakata kuwa hakuna kitu kama hicho wakati hali ilikuwa mbaya sana mkoani Mwanza..
  Kwa akili zetu, hadi mzungu atokee na kutusema ndipo tunaweza kukubaliana.. damn!
   
 14. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unawatetea Barrick halafu unakubali kwamba kuna viumbe vimekunywa maji yaliyoathirika kutoka mgodini. Sasa sijui kati ya tamko la Barrick na lako ni lipi la mwongo!

  Wapi imesemwa habari ya "kiwango cha Usaidi"? Umepata wapi hicho kitu "usaidi"?
   
 15. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkandara thanks kwa kuangalia hili kwa mapana...lakini naweza sema kuwa Ephemeral drainage system unayo zungumzia iko wazi kabisa kwa swala la mgodi wa Nyamongo au (North Mara)Unaweza pata hata ramani yake kama itabidi kufanya hivyo.Ili ku justify hoja hii.

  Hii itakupa mwangaza kwanini nasema kwanini kijiji cha tatu diwani wa chadema na tundu lisu wa waite waandishi wa habari mwanza kabla ya kuwa na vidhibitisho...mie ni mtu huru katika swala hili sina upande wowote.Ila kwa aliye uko anajua ni nini kinataka kufanyika siku hizi za mwisho...lazima kupata kula mwakani kwanza sema unaweza funga mgodi wa nyamongo wananchi wachimbe wenyewe....je unafanyaje hivyo?
  Mwanzoni habari hii ilipotiwa na gazeti moja kuwa ni ng'ombe 21 wamekufa....msemaji akiwa huyo huyo diwani....

  Kadri siku zinavyo kwenda ng'ombe wanaendelea kufa kwa maji yale ambayo mto unatembea(I hope unanisoma)....ambapo hata hicho kipande kilicho ibiwa na wenyeji wa kijiji hicho kimeshakuwa replaced.Na kwa taarifa yako acidi hiyo kadri inavyo zidi kuwa diluted kwenye maji ndivyo sumu inavyozidi kupungua...ntakuwekea statistic ni kiwango gani huwa kinasukumwa kwenda kwenye bwawa hilo...kama hutanisoma na hapa.

  Nafikiri tusilalamike kwa kuwa company imefanya hivyo...angalia nje ya box why tarime?Hao watu wanasemakana kufa au kuwa transfer bugando..je hospital mbona haina vielelezo?Ng'ombe 200 wamekufa kwa wiki moja basi hata mizoga ipo wapi?wamekula?wamezika?wametupa?

  Au hatutakiwi kujua sisi kujuwa barrick wameua watu na masumu yao?
  Sikujua kama na wewe unaweza kuongozwa na uchungu bila kuwa na mawazo yako...ohh...angalia upande wa pili wa swala hili.
   
 16. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Siko hapa kujustify kilicho tokea...naeleza kama mtu huru kabisa.So jibu hoja kwa mtizamo huo.
  Ambaye i have been to that area na mining zingine najua infrastructure ya mgodi na system ya maji ilivyo na maji ya sumu yanavyo kuwa treated.

  Lugha ni kwa ajiri ya mawasiliano kama umepata ujumbe hilo ndio lengo.
  Mambo mengine ni ya kwako.Rekebisha kama umeona kuna utofauti.
   
 17. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Mkuu... tupo pamoja.... labda nilisahau kuweka quotation marks kwenye yamenifurahisha = "yamenifurahisha"
   
 18. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hivi kwanini katika suala hili inaongelewa tindikali (acid) tu? Katika uchimbaji wa dhahabu kuna sumu nyingi zinazotumika mfano cyanide. Cyanide ni sumu inayoua upesi sana. Sasa endapo uchunguzi unaangalia tindikali peke yake ni makosa.

  Sijui machimbo ya Tz yapoje but i am sure watakuwa na tailing dams (mabwawa ya kutupa vumbi au tope zilizotoka kwenye mitambo ya kusafisha dhahabu. Sasa, kama hizo dams zinalinkage au zinaruhusu vumbi kusambaa hewani kuna uwezekano mkubwa wa cyanide kusambaa na kusababisha vifo.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Buswelu,
  Mkuu haya mazungumzo unayafanya ya kisomi sana wakati ni rahisi kabisa ktk fikra..
  Huwezi kunambia kwamba Cyanide na mercury, ambazo ni highly toxic substances zinaweza kuwa diluted na maji ya mto kirahisi kama unavyofikiria wewe. Hizi ni sawa na kuweka mafuta ndani ya maji ukasema yataweza kuwa diluted kutokana na wingi wa maji..
  Hii elimu yenu mnasoma wapi jamani...samahani lakini..wewe umeona meli zikimwaga mafuta baharini na leaching process yake huchukua miezi leo unanambia kuwa contamination ya cyanide au mercury inaweza kuwa desolved kirahisi mkuu wangu..

  Halafu kitu kingine unasema naweza kupata ramani ya AMD kwa mgodi huo wa Nyamongo meaning zipo deposits za Acid na hazardous terains kisha unakataa vifo vya wanyama hawa kwa kusema mbona wakazi wa Nyamongo hawajadhurika!..Hivi kweli unafahamu madhara ya kitu tunachozungumzia mmkuu wangu.. traces za hazardous zipo ktk ramani kisha unasema haiwezekani kudhuru watu kwa sababu hiyo ramani ina justify kitu fulani ni kitu gani hicho kwamba.. kwamba deposits za acid ni kidogo sana kiasi kwamba haziwezi kumdhuru mtu?..Ni vipimo gani mlivyotumia kuhakikisha madai haya! maanake majuzi tu daktari Muhimbili kamtoa mtu mguu wakati akiumwa kichwa..
  Kuna rafiki yangu alipata ajali akavunjika mikono yake wakamweka mavyuma kisha ati wakam refer akafanyiwe MRI...Huoni kama haya ni maajabu ya Mussa mkuu wangu lini mtu aliyewekwa vyuma mwilini ikapendekezwa na daktari mkuu afanyiwe MRI,chumba chenye sumaku za kuvuta vyuma...kwanza huruhusiwi kuingia mle na chuma cha aina yoyote mwilini.
  Haya wewe twambie hao ng'ombe na watu wale wamekufa kwa maradhi gani?..maana uchunguzi mmeufanya..

  Nziku,
  Mkuu wangu hawakufanya uchunguzi wowote zaidi ya kuissafisha barricks.. tumeyaona haya wakati wa Mapanki! hawana mpya siku zote miiko ya Mdanganyika ni pamoja na kutokubali makosa na kuomba radhi!
   
  Last edited: Jun 27, 2009
 20. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #20
  Jun 27, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  mbaya sana, tunajali wawekezaji kuliko raia na mazingira yetu. Hivi hawa jamaa wa LEAT (wanasheria wa mazingira) mbona siku hizi wapo kimya sana? Kama bossi wao bado ni Tundu Lissu, ni bora wamweke mtu mwingine kwani mpiganaji yupo busy sana.
   
Loading...