North Mara: Kashfa ya maji ya sumu toka mgodini!

Kuna rafiki yangu alipata ajali akavunjika mikono yake wakamweka mavyuma kisha ati wakam refer akafanyiwe MRI...Huoni kama haya ni maajabu ya Mussa mkuu wangu lini mtu aliyewekwa vyuma mwilini ikapendekezwa na daktari mkuu afanyiwe MRI,chumba chenye sumaku za kuvuta vyuma...kwanza huruhusiwi kuingia mle na chuma cha aina yoyote mwilini.
Kama unamagnetic implant MRI no. Sio kila chuma ni magnetic. MRI ina various settings hivyo inawezekana kabisa mtu mwenye vyuma mwilini akafanyiwa MRI.

Hii ya Barric kali, there is more to it than what we hear and see. Kabla mradi haujapitishwa EIA ilifanyika na ikawa ok. Kila kinachotokea eti ni ajali!.
 
Buswelu,
Mkuu haya mazungumzo unayafanya ya kisomi sana wakati ni rahisi kabisa ktk fikra..
Huwezi kunambia kwamba Cyanide na mercury, ambazo ni highly toxic substances zinaweza kuwa diluted na maji ya mto kirahisi kama unavyofikiria wewe. Hizi ni sawa na kuweka mafuta ndani ya maji ukasema yataweza kuwa diluted kutokana na wingi wa maji..
Hii elimu yenu mnasoma wapi jamani...samahani lakini..wewe umeona meli zikimwaga mafuta baharini na leaching process yake huchukua miezi leo unanambia kuwa contamination ya cyanide au mercury inaweza kuwa desolved kirahisi mkuu wangu..

Halafu kitu kingine unasema naweza kupata ramani ya AMD kwa mgodi huo wa Nyamongo meaning zipo deposits za Acid na hazardous terains kisha unakataa vifo vya wanyama hawa kwa kusema mbona wakazi wa Nyamongo hawajadhurika!..Hivi kweli unafahamu madhara ya kitu tunachozungumzia mmkuu wangu.. traces za hazardous zipo ktk ramani kisha unasema haiwezekani kudhuru watu kwa sababu hiyo ramani ina justify kitu fulani ni kitu gani hicho kwamba.. kwamba deposits za acid ni kidogo sana kiasi kwamba haziwezi kumdhuru mtu?..Ni vipimo gani mlivyotumia kuhakikisha madai haya! maanake majuzi tu daktari Muhimbili kamtoa mtu mguu wakati akiumwa kichwa..
Kuna rafiki yangu alipata ajali akavunjika mikono yake wakamweka mavyuma kisha ati wakam refer akafanyiwe MRI...Huoni kama haya ni maajabu ya Mussa mkuu wangu lini mtu aliyewekwa vyuma mwilini ikapendekezwa na daktari mkuu afanyiwe MRI,chumba chenye sumaku za kuvuta vyuma...kwanza huruhusiwi kuingia mle na chuma cha aina yoyote mwilini.
Haya wewe twambie hao ng'ombe na watu wale wamekufa kwa maradhi gani?..maana uchunguzi mmeufanya..

Nziku,
Mkuu wangu hawakufanya uchunguzi wowote zaidi ya kuissafisha barricks.. tumeyaona haya wakati wa Mapanki! hawana mpya siku zote miiko ya Mdanganyika ni pamoja na kutokubali makosa na kuomba radhi!

Buswelu anahoja ya siri. Ninachofahamu mimi ni kwamba hiyo mercury haidissolve kwenye maji kirahisi na ndiyo maana kama maji hayo yatatiririka hadi ziwa victoria basi hata samaki wakipimwa wataonekana kuwa na mercury na hiyo itakuwa mwisho wa biashara ya minofu ya samaki.
Pili, jana tumemsikia naibu waziri wa mambo ya ndani Mr. Kagasheki aliyetembelea eneo hilo. Anakiri kuwa alitembezwa sehemu tofauti na kuona kuwa hakuna tataizo lolote wala madhara yaliyotokea, lakini mwananchi mmoja alimtonya kuwa mzee unapigwa changa la macho, akamwambia mahali halisi panapozungumzwa na alipoenda huko amejionea mwenyewe madhara makubwa, na akawa mkali kwa kufichwa na kudanganywa. Akasema sasa atapeleka taarifa kwa waziri mkuu. Maana yake viongozi wote aliofuatana nao katika ziara yake waliamua kumficha - kwanini? Buswelu analo jibu.

Leo anatoka waziri anayeshughulika na mazingira eti ataenda kufanya utafiti -why? its too late na ni upotezaji wa fedha za serikali. Kagasheki ameshaona na taarifa anapeleka kwa waziri mkuu. Wewe wa mazingira subiri waziri mkuu akuamrishe; au ndio unataka kwenda kuziba mashimo?
Sasa Buswelu, mkweli nani - wewe unayesema uko mbali na hivyo unazungumza nadharia tu au Naibu waziri aliyeenda kwenye site?
WATANZANIA TUACHE UTETEZI WA KIJINGA, WANAOKUFA NI NDUGU ZETU. HAO WAZUNGU WA BARRICK WALA HAWANYWI MAJI YA HAPO.
 
Last edited:
This is direct colonialism!Please mwenye namba za Tundu Lissu amakaribishe awe member humu we need to read from him as well.

This is una-aceptable!na inatia uchungu sana.
 
Hivi jaman waziri wa mazingira ana elimu gani? is she a minister? i am running crazy!!!!! namsikiliza hapa sina hata ham ya kuwapa live........

kulipwa fidia kwa utaratibu huu wetu, mh labda iwe ni shilingi moja and then go....
 
kapigiwa makofi baada ya kusema kuwa serikali ya ccm haina nia mbaya kwa wananchi ijapokuwa wanavutia wawekezaji... asante
 
Serikali yasema Barrick ilidanganya kuikana sumu toka mgodi North Mara

Exuper Kachenje na Claud Mshana

SERIKALI imesema kuwa, wamiliki wa mgodi wa North Mara walitoa maelezo ya uongo dhidi ya malalamiko ya wananchi kuwa mgodi huo unatiririsha maji ya sumu yaliyosababisha vifo vya watu, wanyama na kuathiri mazingira.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki alisema hayo juzi baada ya kutembelea mgodi huo kwa maagizo ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili kujionea hali halisi na kujua ukweli wa mambo.

Wananchi wa maeneo yanayozunguka mgodi huo wamekuwa wakieleza kuwa kumekuwepo na sumu inayovuja na kuingia kwenye Mto Tigite na kusababisha vifo vya viumbe walio kwenye mto huo, wanyama wao waliokunywa maji hayo na kukauka kwa mimea iliyo kandokando ya mto huo unaotegemewa na vijiji vitatu.

Picha za magazeti na televisheni zimekuwa zikionyesha watu walioathirika vibaya kwenye ngozi na ambao walieleza kuwa walipata athari hizo baada ya kutumia maji ya mto huo, huku ikielezwa kuwa ng'ombe zaidi ya 200 wamekufa baada ya kunywa maji hayo.

Hata hivyo, Barrick ilikanusha madai hayo na kusema kuwa, uchunguzi uliofanywa na mgodi huo kwa kushirikiana na watendaji wa serikali pamoja na mganga wa wilaya hiyo ulionyesha hakuna ukweli wowote katika malalamiko ya wananchi wa eneo hilo.

Hata hivyo, Balozi Kagasheki aliiambia TBC1 kuwa katika ziara yake kwenye mgodi huo unaomilikiwa na Barrick Gold ya Canada amebaini kuwepo na athari kubwa kwa viumbe na mazingira.

Alisema awali alitembezwa na uongozi wa Barrick kwenye maeneo kadhaa na ikaonekana kuwa hakuna tatizo, lakini alitokea mwananchi mmoja aliyemwelezea kuwa ni msamaria mwema ambaye alimshika mkono na kumwambia kuwa maeneo aliyoonyeshwa sio ambayo yanalalamikiwa na kumpeleka kwenye tatizo halisi.

Alisema alimfuata msamaria huyo na kuonyeshwa hali halisi ambayo waziri huyo aliielezea kuwa "ni mbaya na ya kusikitisha" na akasema anashangazwa na kitendo cha uongozi wa mgodi huo kudanganya.

"Nasikitika sana uongozi wa mgodi kunidanganya. Niliyoyaona nitayapeleka kwa waziri mkuu... kwa kweli si nzuri, itabidi nifikishe ripoti kwa waziri mkuu," alisema naibu waziri huyo akionekana kukasirika.

Kagasheki, aliyekuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha TBC1, alisema inasikitisha zaidi kwa kuwa wakati mwingine inakuwa vigumu kuielewa serikali kwa matukio kama hayo na mimi kuwa naibu waziri wa wizara hiyo inayohusika na usalama wa watu na mali zao, atatekeleza wajibu wake katika kuhakikisha usalama wa wakazi wa eneo linalozunguka mgodi huo.

Katika wiki za hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti kutokea kwa vifo vya watu zaidi ya 21 na ng'ombe 200 huku wengine wakiathirika kutokana na kunywa maji ya Mto Tigithe unaopita katika Kata ya Kibasuka wilayani Tarime Mkoa wa Mara.

Diwani wa kata hiyo, ambaye aliibua malalamiko hayo, anashikiliwa na polisi na amefunguliwa mashtaka akidaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu vifo hivyo.

Wiki iliyopita Jumuiya ya Kikristo Tanzania pamoja wanaharakati wengine wa mazingira na haki za binadamu, walitoa tamko kutaka wahusika hao wachukuliwe hatua, ikiwa ni pamoja na kumtaka waziri mwenye dhamana ya mazingira, Batilda Buriani ajiuzulu kutokana na kashfa hiyo.

Walisema kuwa, upo ushahidi wa kutosha kuwa watu walikufa kutokana na kunywa maji ya sumu na kwamba wapo tayari kuchukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani iwapo jambo hilo halina ukweli ambapo pia walitaka kuundwa kwa tume huru kuchunguza kashfa hiyo.

Nao Wabunge waliochangia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Batilda Buriani walitaka serikali kulichukulia suala la Mgodi wa North Mara kwa uzito unaostahili na kuunda tume kuchunguza madhara yanayodaiwa kutokea kwa wananchi waliotumia maji yenye kemikali katika Mto Tigite.

Mbunge wa Tarime (Chadema), Charles Mwera alisema serikali inapaswa kuwawajibisha wote waliopima maji hayo na kusema kuwa, hayana kemikali hatari na kuongeza kuwa waziri atakapokuja kujibu hoja aeleze amefanya ziara ngapi katika maeneo hayo.

Mto huo wa Tigite unategemewa na zaidi ya familia 2,534 walio katika vijiji vya Kewanja, Nyangoto na Matongo ambazo zinaathirika moja kwa moja. Pia vijiji vya Wegita, Nyakurungu na Nyarwana wanaathirika na mto huo ambao unaungana na Mto Timbe unaopita kijiji cha Mtongo na baadaye kuelekea Ziwa Victoria.

Tangu mapema mwezi Mei, wakazi wa vijiji hivyo wamekuwa wakilalamika kuwa kumekuwepo na uvujaji wa takataka zenye sumu kutoka mgodi huo na kwamba mifugo yao ilifariki kutokana na kunywa maji ya mto huo. Pia walidai mimea iliyo pembezoni mwa mto huo inakauka na kwamba waliona samaki wengi wakiwa wamekufa.

Barrick, ambayo inadai kuwa mgodi huo hautoi kabisa maji machafu yenye sumu, imeeleza kuwa kuvuja kwa takataka hizo zenye sumu kulitokana na vitendo vya wakazi wa vijiji hivyo kuharibu mabomba kwa lengo la kuhujumu. Mgodi huo umekuwa na matatizo na wananchi wa maeneo yanayouzunguka tangu ulipoanzishwa, baadhi yakitokana na wananchi kutoridhika na fidia waliyopewa kwa kuhamishwa eneo hilo, uchafuzi wa mazingira na mapigano ya mara kwa mara yanayotokana na wananchi kuvamia mgodini kila wakati miamba inapolipuliwa.

**********************************************
Labda huyu kwa kuwa ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani watamsikiliza.

Je, polisi waliomuweka ndani Diwani nao watachukuliwa hatua gani? Maana hapa kuna mambo mengi sana yanaingia.

Hao watendaji wa serikali walioshiriki kusafisha hiyo sumu ya Barrick watachukuliwa hatua gani?
 
Kwa wale ambao wanapenda kujua what is cyanide, types and its effects on environments wanaweza pitia document hii! Imeeleza kwa kifupi kidogo lakini inasaidia. I think kuna technical problem pale mgodini na kwa sababu we leave i a corrupt country ndo maana haya madhara yanazidi

Kwa uelewa wangu mdogo kuhusu Cyanides in Mines ni tatizo sugu. lakini haijaripotiwa duniani vifo vinavyotokana na direct contact with cyanide. Ni poisonous, toxic and volatile chemical. Survival time ni 7 haours after disposal unless kama kuna heavy metals (ukisoma documents strong cyanide ndo mgogoro) ndo kunaweza kuwa na matatizo.

Otherwise cyanides inaweza kuwa prevented isiharibu mazingira. Uzuri Barrick walishacyanide ile world Cyanide management agreements nashindwa kuelewa kwanini wanashindwa kucompliy na zile world Cyanide code. I think somewhere something is wrong!
 
Attachments

  • Cynidation Wastes of Gold-Silver.pdf
    602.6 KB · Views: 210
Hawa Barrick Bongo hatuwawezi, wameshainunua serikali. Kinachotakiwa sasa hivi ni kampeni ya kimataifa kuwaumbua katika world stage, liandaliwe dossier la mipicha na ushahidi mwingine wa maeneo yaliyoathirika halafu watu waanze kazi kwenye ma email, ma fax na ma snail mail, mnawashame huko huko kwa shareholders wao kwenye mi Green Peace

Tunaweza ku draft kitu, pamoja na development zote za kisiasa mpaka Cheyo kufukuzwa bungeni, na kuzisambaza kwenye most of these advocacy groups

NRDC: Environmental Groups

Reference/Links: Environmental Groups

Environmental Groups

African Wildlife Foundation works to conserve the wild animals of Africa and the land they inhabit.

The Alliance for Justice is a national association of environmental, civil rights, mental health, women's, children's and consumer advocacy organizations

The American Council for an Energy-Efficient Economy (ACEEE) is dedicated to advancing energy efficiency as a means of promoting both economic prosperity and environmental protection.

The Center for a Livable Future promotes policies to protect health, the environment and sustainable living.

Clean Water Network is an alliance of over 1000 organizations working to protect our nation's water resources.

Conservation International promotes biodiversity conservation in endangered ecosystems worldwide.

CREST provides information about energy efficiency, renewable energy and sustainable technology information and connections.

Defenders of Wildlife works to protect wild animals and plants in their natural communities.

Earth First! works to protect wilderness through radical means.

Earth Island Institute provides organizational support in developing projects to protect the global environment.

Go to Top

Earth Share manages workplace giving campaigns for its member charities.

Earthjustice Legal Defense Fund strives to protect people and natural resources by enforcing and strengthening environmental laws (formerly the Sierra Club Legal Defense Fund).

Earthwatch sponsors scientific field research to improve understanding of the planet and its inhabitants.

Energy & Environmental Research Center (EERC) provides multidisciplinary research and development of innovative energy and environmental technologies for the protection of air, water and soil.

Environmental Defense combines science, economics, and law to find economically sustainable solutions to environmental problems.

Environmental Literacy Council offers links to environmental resources on the web.

Environmental Working Group provides the public with locally relevant information on the environment.

Friends of the Earth USA focuses on the underlying social and economic causes of environmental problems.

Go to Top

Greenpeace uses non-violent, creative confrontation to expose global environmental problems and force solutions.

League of Conservation Voters is a bipartisan group working to educate voters and win elections on behalf of the environment.

National Audubon Society works through advocacy, policy, science, litigation, sanctuary management, grassroots outreach and education to protect birds and their habitats.

National Coalition for Marine Conservation is dedicated to conserving ocean fish, preventing overfishing, reducing bycatch and protecting habitat.

National Environmental Trust is a non-partisan organization dedicated to educating the American public on contemporary environmental issues.

National Parks and Conservation Association (NPCA) is dedicated to protecting, preserving and enhancing the U.S. National Park System.

National Religious Partnership for the Environment seeks to integrate commitment to global sustainability and environmental justice into all aspects of religious life.

National Wildlife Federation unites individuals, organizations, businesses and government to protect nature and wildlife.

Go to Top

Natural Resources Defense Council protects the environment and human health through advocacy, litigation, research and education. (And publishes this website!)

The Nature Conservancy preserves habitats and species by buying the lands and waters they need to survive.

Nuclear Control Institute monitors nuclear activities worldwide and pursues strategies to reverse the growth of nuclear arms.

Oceana works to protect and restore the world's oceans through advocacy, science, law and public education.

Public Agenda provides information on issues ranging from abortion to welfare.

Public Interest Research Group (PIRG) is an association of watchdog organizations dedicated to safeguarding the public interest and protecting the environment.

Rainforest Action Network protects rainforests through education, grassroots organizing and non-violent direct action.

Rainforest Alliance promotes research and education to conserve tropical rainforests.

Scenic America protects scenic roads, prevents billboards from trashing our highways and helps people create more attractive communities.

Sierra Club promotes environmental conservation by influencing public policy -- legislative, administrative, legal, and electoral.

Go to Top

Society of Environmental Journalists is a membership group of print and broadcast journalists as well as educators and students. SEJ's purpose is to enable journalists to better inform the public about critical issues concerning the environment.

Southern Environmental Law Center is the only environmental organization dedicated solely to protecting the natural resoures of the southeastern United States.

Southern Utah Wilderness Alliance works to protect the magnificent canyon country and unspoiled public lands surrounding Utah's prized national parks.

Union of Concerned Scientists is dedicated to advancing responsible public policies in areas where science and technology play a critical role.

The Wilderness Society protects wild places in the United States through public education, policy work and litigation.

Wildlife Conservation Society, headquartered at New York City's Bronx Zoo, works to save wildlife and wild lands throughout the world.

The Woods Hole Research Center addresses environmental issues through scientific research and education.

World Resources Institute helps governments and private organizations cope with environmental, resource and development challenges of global significance.

World Wide Fund for Nature (WWF) seeks to reverse degradation of the environment by promoting biodiversity and sustainability, while minimizing pollution and consumption.

World Wildlife Fund (U.S.) dedicated to protecting the world's wildlife and wildlands.
 
Hii kitu wangeiweka kitaalamu zaidi kwa kweli ingekuwa nzuri sana kama bwana bluray alivyo sema hapo...Inajulikana hawa jamaa hata PNG wana matatizo...Mexico..hata uko Elko nako ni hivyo hivyo.

Sumu ipo na kama walioangalia Tv wataona bwawa lile likuwa carpet lake likiwa limekatwa na maji kutulilika kwenye kwenye vyanzo vingine...lakini diwani kureport issue kama hii...kiasa siasa ndio maana limeleta mambo ya ajabu ajabu mpaka cheyo wamemkimbiza bungeni mzee wetu..shame on you speker sitta.
 
Exuper Kachenje na Claud Mshana

SERIKALI imesema kuwa, wamiliki wa mgodi wa North Mara walitoa maelezo ya uongo dhidi ya malalamiko ya wananchi kuwa mgodi huo unatiririsha maji ya sumu yaliyosababisha vifo vya watu, wanyama na kuathiri mazingira.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki alisema hayo juzi baada ya kutembelea mgodi huo kwa maagizo ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili kujionea hali halisi na kujua ukweli wa mambo.

Wananchi wa maeneo yanayozunguka mgodi huo wamekuwa wakieleza kuwa kumekuwepo na sumu inayovuja na kuingia kwenye Mto Tigite na kusababisha vifo vya viumbe walio kwenye mto huo, wanyama wao waliokunywa maji hayo na kukauka kwa mimea iliyo kandokando ya mto huo unaotegemewa na vijiji vitatu.

Picha za magazeti na televisheni zimekuwa zikionyesha watu walioathirika vibaya kwenye ngozi na ambao walieleza kuwa walipata athari hizo baada ya kutumia maji ya mto huo, huku ikielezwa kuwa ng'ombe zaidi ya 200 wamekufa baada ya kunywa maji hayo.

Hata hivyo, Barrick ilikanusha madai hayo na kusema kuwa, uchunguzi uliofanywa na mgodi huo kwa kushirikiana na watendaji wa serikali pamoja na mganga wa wilaya hiyo ulionyesha hakuna ukweli wowote katika malalamiko ya wananchi wa eneo hilo.

Hata hivyo, Balozi Kagasheki aliiambia TBC1 kuwa katika ziara yake kwenye mgodi huo unaomilikiwa na Barrick Gold ya Canada amebaini kuwepo na athari kubwa kwa viumbe na mazingira.

Alisema awali alitembezwa na uongozi wa Barrick kwenye maeneo kadhaa na ikaonekana kuwa hakuna tatizo, lakini alitokea mwananchi mmoja aliyemwelezea kuwa ni msamaria mwema ambaye alimshika mkono na kumwambia kuwa maeneo aliyoonyeshwa sio ambayo yanalalamikiwa na kumpeleka kwenye tatizo halisi.

Alisema alimfuata msamaria huyo na kuonyeshwa hali halisi ambayo waziri huyo aliielezea kuwa "ni mbaya na ya kusikitisha" na akasema anashangazwa na kitendo cha uongozi wa mgodi huo kudanganya.

"Nasikitika sana uongozi wa mgodi kunidanganya. Niliyoyaona nitayapeleka kwa waziri mkuu... kwa kweli si nzuri, itabidi nifikishe ripoti kwa waziri mkuu," alisema naibu waziri huyo akionekana kukasirika.

Kagasheki, aliyekuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha TBC1, alisema inasikitisha zaidi kwa kuwa wakati mwingine inakuwa vigumu kuielewa serikali kwa matukio kama hayo na mimi kuwa naibu waziri wa wizara hiyo inayohusika na usalama wa watu na mali zao, atatekeleza wajibu wake katika kuhakikisha usalama wa wakazi wa eneo linalozunguka mgodi huo.

Katika wiki za hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti kutokea kwa vifo vya watu zaidi ya 21 na ng'ombe 200 huku wengine wakiathirika kutokana na kunywa maji ya Mto Tigithe unaopita katika Kata ya Kibasuka wilayani Tarime Mkoa wa Mara.

Diwani wa kata hiyo, ambaye aliibua malalamiko hayo, anashikiliwa na polisi na amefunguliwa mashtaka akidaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu vifo hivyo.

Wiki iliyopita Jumuiya ya Kikristo Tanzania pamoja wanaharakati wengine wa mazingira na haki za binadamu, walitoa tamko kutaka wahusika hao wachukuliwe hatua, ikiwa ni pamoja na kumtaka waziri mwenye dhamana ya mazingira, Batilda Buriani ajiuzulu kutokana na kashfa hiyo.

Walisema kuwa, upo ushahidi wa kutosha kuwa watu walikufa kutokana na kunywa maji ya sumu na kwamba wapo tayari kuchukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani iwapo jambo hilo halina ukweli ambapo pia walitaka kuundwa kwa tume huru kuchunguza kashfa hiyo.

Nao Wabunge waliochangia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Batilda Buriani walitaka serikali kulichukulia suala la Mgodi wa North Mara kwa uzito unaostahili na kuunda tume kuchunguza madhara yanayodaiwa kutokea kwa wananchi waliotumia maji yenye kemikali katika Mto Tigite.

Mbunge wa Tarime (Chadema), Charles Mwera alisema serikali inapaswa kuwawajibisha wote waliopima maji hayo na kusema kuwa, hayana kemikali hatari na kuongeza kuwa waziri atakapokuja kujibu hoja aeleze amefanya ziara ngapi katika maeneo hayo.

Mto huo wa Tigite unategemewa na zaidi ya familia 2,534 walio katika vijiji vya Kewanja, Nyangoto na Matongo ambazo zinaathirika moja kwa moja. Pia vijiji vya Wegita, Nyakurungu na Nyarwana wanaathirika na mto huo ambao unaungana na Mto Timbe unaopita kijiji cha Mtongo na baadaye kuelekea Ziwa Victoria.

Tangu mapema mwezi Mei, wakazi wa vijiji hivyo wamekuwa wakilalamika kuwa kumekuwepo na uvujaji wa takataka zenye sumu kutoka mgodi huo na kwamba mifugo yao ilifariki kutokana na kunywa maji ya mto huo. Pia walidai mimea iliyo pembezoni mwa mto huo inakauka na kwamba waliona samaki wengi wakiwa wamekufa.

Barrick, ambayo inadai kuwa mgodi huo hautoi kabisa maji machafu yenye sumu, imeeleza kuwa kuvuja kwa takataka hizo zenye sumu kulitokana na vitendo vya wakazi wa vijiji hivyo kuharibu mabomba kwa lengo la kuhujumu.

Mgodi huo umekuwa na matatizo na wananchi wa maeneo yanayouzunguka tangu ulipoanzishwa, baadhi yakitokana na wananchi kutoridhika na fidia waliyopewa kwa kuhamishwa eneo hilo, uchafuzi wa mazingira na mapigano ya mara kwa mara yanayotokana na wananchi kuvamia mgodini kila wakati miamba inapolipuliwa.

Source: Mwananchi
 
Ndiyo Barrick ya Gareth Taylor ilivyokuwa. I thought imebadilika kumbe bado mambo yaleyale. Ni aibu sana for a multination company to have substandard operations.Wavalishwe jukumu la kulipia fidia hasara yote kwa kosa la kizembe kama hili.Ingetokea Canada au USA ingelikuwaje?
 
Kuna haja ya kuwawajibisha baadhi ya watendaji wa Mkoa wa Mara waliokuwa wakitoa kauli za kukebehi madai ya wananchi walioathirika na kudai eti madai yao ni uzushi mtupu. Inasikitisha kiongozi mwenye dhamana ya kulinda na kutetea maslahi ya mwananchi anarubuniwa kwa vijisenti au ahadi ndogo ndogo. Uzalendo ulipotelea wapi???????????????
 
Hawa jamaa dawa yao ni kufunga mgodi huo maana maisha ya watu ni bora kuliko hata hizo pesa
 
Jamani inasikitisha sna. Ina maana serikali ya wilaya chini ya mkuu wa wilaya na ile ya mkoa chini ya mkuu wa mkoa hawajui hili, mpaka wasamalia ema wambonyeze waziri.

Wote waliohusika washitakiwe kwa kosa la mauaji na lazima fidia ya nguvu ilipwe kwa waathirika wote
 
Mpaka Tundu Lissu aseme ndio serikali isituke kwa nini watendaji wengine kama mkuu wa wilaya,mkoa na Mkuu wa polisi wote wamewasaliti wananchi hawa bwana wanatudanganya hawatachukua hatua yeyote hii ni danganya toto wanataka mjadala uishe kwa sababu limekuwa jambo la kitaifa na kila mtu anaongelea wewe unacheza na serikali ya CCM we utaona tuu mwisho wake
 
Cha ajabu na kushangaza kabisa ni kuwa shughuli za mgodi zinaendelea kama kawa kakuna kitu kilichotokea. Kungekuwa na serious government ingefunga mgodi mpaka watakapo hakikisha kuwa shughuli hizi hazitakuwa na madhara kwa binadamu na viumbe wengine
 
Exuper Kachenje na Claud Mshana
SERIKALI imesema kuwa, wamiliki wa mgodi wa North Mara walitoa maelezo ya uongo dhidi ya malalamiko ya wananchi kuwa mgodi huo unatiririsha maji ya sumu yaliyosababisha vifo vya watu, wanyama na kuathiri mazingira.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki alisema hayo juzi baada ya kutembelea mgodi huo kwa maagizo ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili kujionea hali halisi na kujua ukweli wa mambo.

Wananchi wa maeneo yanayozunguka mgodi huo wamekuwa wakieleza kuwa kumekuwepo na sumu inayovuja na kuingia kwenye Mto Tigite na kusababisha vifo vya viumbe walio kwenye mto huo, wanyama wao waliokunywa maji hayo na kukauka kwa mimea iliyo kandokando ya mto huo unaotegemewa na vijiji vitatu.

Picha za magazeti na televisheni zimekuwa zikionyesha watu walioathirika vibaya kwenye ngozi na ambao walieleza kuwa walipata athari hizo baada ya kutumia maji ya mto huo, huku ikielezwa kuwa ng'ombe zaidi ya 200 wamekufa baada ya kunywa maji hayo.

Hata hivyo, Barrick ilikanusha madai hayo na kusema kuwa, uchunguzi uliofanywa na mgodi huo kwa kushirikiana na watendaji wa serikali pamoja na mganga wa wilaya hiyo ulionyesha hakuna ukweli wowote katika malalamiko ya wananchi wa eneo hilo.

Hata hivyo, Balozi Kagasheki aliiambia TBC1 kuwa katika ziara yake kwenye mgodi huo unaomilikiwa na Barrick Gold ya Canada amebaini kuwepo na athari kubwa kwa viumbe na mazingira.

Alisema awali alitembezwa na uongozi wa Barrick kwenye maeneo kadhaa na ikaonekana kuwa hakuna tatizo, lakini alitokea mwananchi mmoja aliyemwelezea kuwa ni msamaria mwema ambaye alimshika mkono na kumwambia kuwa maeneo aliyoonyeshwa sio ambayo yanalalamikiwa na kumpeleka kwenye tatizo halisi.

Alisema alimfuata msamaria huyo na kuonyeshwa hali halisi ambayo waziri huyo aliielezea kuwa "ni mbaya na ya kusikitisha" na akasema anashangazwa na kitendo cha uongozi wa mgodi huo kudanganya.

"Nasikitika sana uongozi wa mgodi kunidanganya. Niliyoyaona nitayapeleka kwa waziri mkuu... kwa kweli si nzuri, itabidi nifikishe ripoti kwa waziri mkuu," alisema naibu waziri huyo akionekana kukasirika.

Kagasheki, aliyekuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha TBC1, alisema inasikitisha zaidi kwa kuwa wakati mwingine inakuwa vigumu kuielewa serikali kwa matukio kama hayo na mimi kuwa naibu waziri wa wizara hiyo inayohusika na usalama wa watu na mali zao, atatekeleza wajibu wake katika kuhakikisha usalama wa wakazi wa eneo linalozunguka mgodi huo.

Katika wiki za hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti kutokea kwa vifo vya watu zaidi ya 21 na ng'ombe 200 huku wengine wakiathirika kutokana na kunywa maji ya Mto Tigithe unaopita katika Kata ya Kibasuka wilayani Tarime Mkoa wa Mara.

Diwani wa kata hiyo, ambaye aliibua malalamiko hayo, anashikiliwa na polisi na amefunguliwa mashtaka akidaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu vifo hivyo.

Wiki iliyopita Jumuiya ya Kikristo Tanzania pamoja wanaharakati wengine wa mazingira na haki za binadamu, walitoa tamko kutaka wahusika hao wachukuliwe hatua, ikiwa ni pamoja na kumtaka waziri mwenye dhamana ya mazingira, Batilda Buriani ajiuzulu kutokana na kashfa hiyo.

Walisema kuwa, upo ushahidi wa kutosha kuwa watu walikufa kutokana na kunywa maji ya sumu na kwamba wapo tayari kuchukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani iwapo jambo hilo halina ukweli ambapo pia walitaka kuundwa kwa tume huru kuchunguza kashfa hiyo.

Nao Wabunge waliochangia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Batilda Buriani walitaka serikali kulichukulia suala la Mgodi wa North Mara kwa uzito unaostahili na kuunda tume kuchunguza madhara yanayodaiwa kutokea kwa wananchi waliotumia maji yenye kemikali katika Mto Tigite.

Mbunge wa Tarime (Chadema), Charles Mwera alisema serikali inapaswa kuwawajibisha wote waliopima maji hayo na kusema kuwa, hayana kemikali hatari na kuongeza kuwa waziri atakapokuja kujibu hoja aeleze amefanya ziara ngapi katika maeneo hayo.

Mto huo wa Tigite unategemewa na zaidi ya familia 2,534 walio katika vijiji vya Kewanja, Nyangoto na Matongo ambazo zinaathirika moja kwa moja. Pia vijiji vya Wegita, Nyakurungu na Nyarwana wanaathirika na mto huo ambao unaungana na Mto Timbe unaopita kijiji cha Mtongo na baadaye kuelekea Ziwa Victoria.

Tangu mapema mwezi Mei, wakazi wa vijiji hivyo wamekuwa wakilalamika kuwa kumekuwepo na uvujaji wa takataka zenye sumu kutoka mgodi huo na kwamba mifugo yao ilifariki kutokana na kunywa maji ya mto huo. Pia walidai mimea iliyo pembezoni mwa mto huo inakauka na kwamba waliona samaki wengi wakiwa wamekufa.

Barrick, ambayo inadai kuwa mgodi huo hautoi kabisa maji machafu yenye sumu, imeeleza kuwa kuvuja kwa takataka hizo zenye sumu kulitokana na vitendo vya wakazi wa vijiji hivyo kuharibu mabomba kwa lengo la kuhujumu.

Mgodi huo umekuwa na matatizo na wananchi wa maeneo yanayouzunguka tangu ulipoanzishwa, baadhi yakitokana na wananchi kutoridhika na fidia waliyopewa kwa kuhamishwa eneo hilo, uchafuzi wa mazingira na mapigano ya mara kwa mara yanayotokana na wananchi kuvamia mgodini kila wakati miamba inapolipuliwa.

Source: Mwananchi

-Kwanini Barriki isishitakiwe kwa kuidanganya serikali?

-kwanini isishitakiwe kwa kuwahonga baadhi ya watendaji wa serikali ili washirikiane nayo kuidanganya?

-Kwanini isishitakiwe kwa kusababisha madhara pamoja na vifo vya watu?

-----kwanini...? kwanini?....
 
Back
Top Bottom