Nguvu ya tetemeko la ardhi lilikuwa limepimwa likiwa ni 6.3
Na uzito wa bomu hilo ni kiloton 100
Ni zaidi ya uzito wa bomu la nyuklia ambalo lilitupwa na Marekani mjini Nagasaki mwezi August mwaka 1945 na kumaliza vita vya pili vya dunia.
Hii ni ishara kwamba Korea Kaskazini hajaogopa vitishoi vya Marekani na washirika wake Japan na Korea Kusini ambao walikuwa wakifanya mazoezi ya kutisha katika ukanda wa Korea.
Njia ya kumaliza huu mgogoro ambao kwa kiasi kikubwa unachangiwa na kauli za raisi Donald Trump kama ile ya Korea Kaskazini kukumbana na hasira na moto wa Marekani kuishambulia Korea Kaskazini, ni mazungumzo na majadiliano.
Kim hatanii na sasa yupo tayari kukabiliana na nchi yoyote ile.