Kumekuwapo na madai mengi kuhusu radi ambayo mengine si ya kweli, yafuatayo ni madai 10 pamoja na uhalisia wake.
Dhana Potofu 1: Radi haipigi sehemu ileile mara mbili.
Uhalisia: Radi inaweza kupiga sehemu ileile mara nyingi, hasa ikiwa ni eneo lenye kitu kirefu, chenye ncha kali na kilichojitenga. Kwa mfano, jengo la Empire State Building hupigwa na radi takribani mara 25 kwa mwaka, na wakati mwingine zaidi ya mara 10 ndani ya dhoruba moja.
Dhana Potofu 2: Radi hupiga vitu virefu pekee.
Uhalisia: Radi inaweza kupiga popote. Inaweza kupiga ardhi, gari, maegesho ya magari au sehemu nyingine, si lazima kitu kiwe kirefu zaidi.
Dhana Potofu 3: Ukiwa nje wakati wa radi, ni salama kujikinga chini ya mti.
Uhalia: Hii ni mojawapo ya sehemu hatari zaidi. Radi ikipiga mti, umeme unaweza kusambaa ardhini na kumfikia mtu aliyeko chini yake. Kusimama chini ya mti ni sababu ya pili kwa wingi ya majeraha na vifo vinavyotokana na radi.
Dhana Potofu 4: Usipoona mvua au mawingu, uko salama.
Uhalisia: Radi inaweza kupiga umbali wa zaidi ya kilomita 5 kutoka kwenye dhoruba. Wakati mwingine inaweza kupiga hadi karibu kilomita 16 kutoka ilipoanzia, hata kama anga linaonekana kuwa wazi.
Dhana Potofu 5: Matairi ya mpira ya gari hulinda dhidi ya radi.
Uhalisia: Gari linaweza kukulinda, lakini si kwa sababu ya matairi yake. Kinga hutokana na mwili wa chuma wa gari unaoelekeza umeme nje. Magari ya wazi, pikipiki, baiskeli na magari yenye mwili wa plastiki au fiberglass hayatoi ulinzi wa kutosha.
Dhana Potofu 6: Ukiwa nje wakati wa radi, lala chini ili uwe salama.
Uhalisia: Kulala chini huongeza hatari ya kupigwa na umeme unaosambaa ardhini. Ni salama zaidi kutafuta makazi salama haraka iwezekanavyo.
Dhana Potofu 7: Ukimgusa mtu aliyepigwa na radi, nawe utapigwa na umeme.
Uhalisia: Mwili wa binadamu hauhifadhi umeme baada ya kupigwa na radi. Ni salama kumgusa mhanga na kumpa huduma ya kwanza mara moja.
Dhana Potofu 8: Kuvaa vitu vya chuma huvutia radi.
Uhalisia: Chuma mwilini hakivutii radi kwa kiwango kikubwa. Kinachoathiri zaidi ni urefu wa kitu, umbo lake na kama kimejitenga. Hata hivyo, kugusa vitu vya chuma wakati wa radi kunaweza kuwa hatari ikiwa umeme utapita kupitia hivyo.
Dhana Potofu 9: Ukiingia ndani ya nyumba, uko salama kabisa.
Uhalisia: Nyumba ni sehemu salama zaidi, lakini bado unapaswa kuepuka kutumia vifaa vya umeme, mabomba ya maji, nyaya, milango au madirisha ya chuma wakati wa radi.
Dhana Potofu #10: Surge suppressor pekee inaweza kulinda nyumba dhidi ya radi.
Uhalisia: Vifaa vya kuzuia mshtuko wa umeme (surge suppressors) husaidia kulinda vifaa vya umeme, lakini haviwezi kuilinda nyumba dhidi ya radi inayopiga moja kwa moja. Kinga kamili inahitaji mfumo wa ulinzi dhidi ya radi uliowekwa kitaalamu.
Makala za Rejea
Lighting safety: 10 myths-and the facts (Insurance Information Institute)
Lighting myths (National weather service)
Can Lighting strike the same place Twice (Britannica)