Dolby Atmos ndo nini Mkuu!?
Dolby Atmos ni audio decoding format ambayo imetolewa na Dolby Digital Laboratories, kampuni inayojihusisha na sound engineering. Ili kuelewa vizuri Dolby Atmos nitaanzia nyuma zaidi.
Dolby Digital Laboratories walianza na Dolby stereo ambayo ilihitaji spika 2 kimsingi kwa kuwa stereo ni 2 channel audio ila katika kumbi za sinema zilitumika spika 4 kwa kusambaza hizo 2 channels katika spika 4. Lengo ni kuhakikisha mziki unasambaa katika ukumbi mzima. Nyumbani spika 2 zilitosha. Mziki katika stereo ulikuwa mzuri zaidi ukilinganisha na ule wa spika moja yaani 1 channel audio (monaural au mono).
Kisha Dolby Laboratories walifanya maendeleo ya kitekinolojia na kuibuka na Dolby Digital Surround Sound decoding format. Hii format ilikuja na multichannel audio yaani channels zaidi ya 2. Na hii ikahusisha kuwepo spika maalum ya low frequency sounds ijulikanayo kama subwoofer. Kwa hiyo multichannel audio kimsingi inakuwa katika 5:1 channels. Wakati mwingine 2:1 au hata 7:1 channels. Hiyo namba ya kwanza inawakilisha idadi ya spika za kawaida na hiyo 1 ni subwoofer.
Kuna tofauti gani kati ya Dolby stereo na Dolby Digital Surround?
2. Mfano unaposikiliza mziki kwenye Dolby stereo system spika zote 4 zinatoa sauti zote kwenye mziki mfano sauti za gitaa,drums,trumpets ,saxaphone,organ na sauti za waimbaji. Kila spika inatoa sauti zote kwenye mziki kwa hiyo lengo la kuweka spika 2 au 4 ni kueneza mziki kwenye ukumbi ili usikike vizuri sehemu zote.
Sasa inapokuja upande wa Dolby Digital Surround sauti za muziki zinagawanywa katika mikondo (channels) mbali mbali na kila spika inapokea audio channel maalum na sio zote. Kwa mfano subwoofer ni kwa ajili ya low frequency sounds mfano bass sounds au mingurumo ya sauti nzito. Spika zingine zina handle sauti zingine za mziki au sauti za waimbaji. Kwa hiyo katika surround sound unaweza kusikia sauti ya trumpet au mwimbaji kwenye spika moja tu kati ya spika 6 au 8. Au kama kuna waimbaji 2 wanaimba kwa kupokezana/kujibizana unaweza kusikia sauti ya mwimbaji mmoja kwenye spika A na anayemjibu sauti inatokea spika B. Unaweza kuona hapa kuwa Digital Surround sound inavyoufanya mziki kuwa halisia zaidi yaani unajihisi kama vile uko kwenye live event na sio mziki uliorekodiwa tu. Ndio maana spika lazima ziwe nyingi katika Surround Sound ukifananisha na Stereo Sound. Kwa hiyo hawa Dolby Digital Technologies wameubadilisha(revolutionalized) mziki uliyorekodiwa kwa teknolojia yao ya Digital Surround sound.
Sasa je Dolby Atmos ndio nini?
Ukielewa Dolby Digital Surround ni rahisi kuelewa Dolby Atmos kwa sababu Dolby Atmos ni maboresho ya Dolby Digital Surround (=advanced Digital Surround).
Kama tulivyoona Dolby digital surround ina mikondo mingi ya sauti (multichannel audio) na spika zinapangwa mbele katikati na nyuma katika ukumbi na zinazunguka kote ukumbini ili kueneza sauti vizuri na kuongeza live experience. Standard channels ni hadi 8 (7:1).
Lakini unapokuja kwenye Dolby Atmos audio channels zimeongezeka sana kwa sababu licha ya spika za chini pia kuna za juu zinazofungwa kwenye dari. Sababu ya kuweka spika juu ni kushughulika na sauti ambazo kwa kawaida (naturally) hutokea juu kama mgurumo wa ndege, radi, nk. Kwa hiyo Dolby Atmos inaongezea uhalisia ( live experience) kwenye sauti unazosikiliza.
Sasa kuna tofauti gani kati ya Dolby Digital Surround na Dolby Atmos? Ili uelewe fikiria uko katika jumba la sinema unaangalia movie. Mbele yako kuna ndege inakuja. Kwenye Digital Surround utasikia mgurumo ukitokea kwenye spika za mbele, baada ya muda ndege inaposogea zaidi na kupita juu yako mgurumo unahamia spika za nyuma. Unakuwa kama uko kwenye tukio lenyewe.
Lakini kwenye Atmos utasikia mgurumo kwenye spika za mbele, jinsi ndege inavyosogea sauti inahamia spika za juu mbele, baadaye juu katikati kisha juu nyuma na hatimaye nyuma chini. Kwa hiyo utafuatatilia huo mgurumo hatua kwa hatua hadi ndege itakapopotea. Si utajiona kama uko nje na ni ndege halisi? Kwa kweli Dolby Atmos imeongeza sana uhalisia( live experience)
Sasa je kama Atmos inahitaji spika nyingi inawezekanaje kupata live experience kwenye spika 2 tu mfano headphones za simu, iPod, nk?
Tekinolojia ya Dolby inawezesha spika mbili kupata Surround sound na hata Atmos kwani utasikia sauti zikitoka direction tofauti tofauti mfano, mbele, nyuma,juu,kulia na.kushoto lakini sio kwa ufanisi kama vile unavyotumia spika nyingi.
Nimeeleza kifupi lakini natumaini umeelewa.