Mi kitu cha kwanza napenda nikupe pole sana kwa kupenda alafu ukaishia kupewa ahadi zisizotekelezeka, hiyo ipo sana katika maisha mdada, lakini bado hujachelewa, kuolewa na huyo guy usijilaumu sana ukihisi umekosea nooooo, kinachokuponza ni kufanya comparison alafu inaonekana ulikuwa una kitu tunaita over expectations, hii ni sumu kwenye mapenzi mdada, utakuwa na tamaa bure make ulichohisi hukipati then utacheat alafu hiyo ndo itakuwa mbaya zaidi, nadhan huyo guy si rafiki yako kwa maelezo yako bali ni mmeo, hili ni kosa kubwa sana, mfanye awe rafiki alafu kaeni chini, mueleze ni jinsi gani unataka awe ili umpende zaidi, una nguvu na mamlaka ya kumfanya mtu awe kama unavyotaka wewe.
Ukifungua mdomo ndo utakuwa mlango wa furaha katika ndoa yako ila kwanza mlete karibu yako kwanza kwa kunfanya rafiki yako kwanza. hayo mambo yanatokea sana katika maisha ila unayo nafasi ya kufanya marekebisho.
Riser.