No one to blame ila mimi mwenyewe

No one to blame ila mimi mwenyewe

Habar humu ndan,mimi ni mgeni humu ndan na ndio napost topic kwa mara ya kwanza,mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 24 sasa,lengo la kuandika hii poat nimehisi nikiitoa moyoni ntakua km nimetua mzigo fulani.

Katika maisha yangu nimekua na wanaume watatu ambao wa kwanza nilikua nae A-level nilimpenda sana unfortunately akaniacha na sababu ilikua amerudiana na ex wake.

Nilipofika form six nikapata mwingne nae tulipendana sana,ila tuu nilimvumilia sna nikashindwa kwasababu alikua ananicheat sana na kilichonikera sana ni kwamba wanawake ananicheat nao walikua wakinicall kunitukana!na mimi sipend gombana na mdada kisa mwanaume,nikasema sio kesi ngoja niachane nae japo niliumia sana yaani.

Nilipoanza chuo 2009 nikampata mtu tena ila yy alikua mbali na mn yeye alikua anasoma iringa na mimi Dar,basi huyo tulikaa miaka mi tatu yaan mpk namaliza chuo bado nipo nae, tatizo likawa alikuwa ananitesa sana yaani, aliniahidi kunioa na aliniambia nimwambie mama yangu kua analeta mahari,baai ilikuwa kila nikikosea tuu kidg basi anasema mimi sio wife material na haez ntolea mahar,basi mimi na mbembelezwa na ukizingatia nilisha mwambia mama,mjomba wangu alinikataza sana kuhusu huyu mtu lakini nikawa sisikii.

Alitaka niachisha chuo kwa promise ya kunpeleka nje kusoma!na hio mahar amehairisha karibu mara tatu,alinipa ujauzto na kwa upande wangu nilifurah sana,ila yeye alinambia nitoe coz nilikua nalalamika tumbo kuuma so akasema nitoe,na akanipa namba ya document wake na huyo daktar alisema nitoe.baai nikatoa,ila kumbe alikua na girl mwingne ambae nae alikua mjamzito ndio maana alinicctizia nitoe,mwaka jana mwez wa nne nikaachana nae,na ulikua ni uamuzi mgumu nilioufanya!maana niligundua hata jina alinidanganya.

Basi zile stress yaan nikawa eager kuolewa nikiangalia home atleast mm ndio nimesoma na nina kazi,mama yangu ananiangalia mm,na nilishamwamvmbia natolewa mahar kwaio nilichanganyikiwa sana,sasa wiki moja baada ya kuachana na huyo wa tatu kuna rafiki yangu akaniambia ana kaka yake anahitaj mke maana kwao wamekataa wanawake aliowapeleka kwasababu ya kabila,kwaio kabila langu hawatalikataa,yaani nilisita sana,ila akanisisitizia basi nikamwambia ntaka kuonana nae,tukaonana na badae niliporud home akaniambia nimekupenda na mm nikamjibu nimekupenda(wakat deep down wala ckumpenda,na hio ndio first mistake),tumekaa miez miwili anaulizia ndoa mara akanipeleka kwao,mimi najipa moyo kua ntampenda tuu,haya mara mahar,mara ndoa.

Hapa sasa najilaumu kuchukua maamuzi ya haraka sana kuolewa maana nashindwa kumpenda kabisa kabisa yaan!sio kwamba namchukia hapana,ila no love and affection yaan!hata sijui nifanyaje nateseka sana,na kiukweli moyo wangu umeganda siwezi kumpenda mtu yoyote kabisa yaan!nipo ndoan am totally not happy yaani akienda job nawish asiwahi kurud hata unyumba imekua shida.

Sorry kwa story ndefu ila nimeona niandike atleast nitoe kitu moyoni!ushaur tuu tusikimbilie kuolewa mabinti jaman,na tusidanganyane kua utampenda ndoan haipo hio!hakuna kitu kizur km inner peace jamani.

Mimi nimejiharibia mwenyew kwaio the rest of my life is being unhappy,sometimes nataman ningekua mzungu kwasababu wao wanaweza kutengua ndoa km mtu hayupo happy!sasa sisi wabongo ni ngumu na nikifanya hivi nitamuumiza mara mia!dah ni hayo tuu jamani.

Tatizo umeweka ki2 moyoni, m mwenyew nilishakaa na mtu ambae sikumpenda hata kidog, ila badae nkaja kumpenda taratibu, ila sikuwa nimeolewa! jaribu kuangalia mazuri yake anayokufanyia, kama ni mchesh ndo utampenda zaidi, ila kama ndo mbumbumbu kaz unayo
 
Ni mpole kweli yaan
 
Nimekuhurumia tuu mpenzi maana najua adha ya kuwa na mtu usiyemfurahia .pole sana hakuna haja ya kulaumu hesabu mazuri yake uwe na mtizamo positive kwake.Kama kuna maumbile hayapo sawa kwake mkubali na uone kuwa yeye hajajiumba .
Umesema nae alioa kwa shinikizo la familia yake mfanye ajisikie furaha na hakukutana na wewe kimakosa .Tengeneza furaha yako dada fanya nyumba yako kuwa mbingu ndogo kila kitu kipo mikononi mwako
 
Pole sister kwa yakokukuta lkn usiwaze sana najua ni vigumu kukubaliana na hy hali lkn cha msingi angalia mbele ni vigumu sana kuulazimisha moyo umpende mtu usiyempenda coz love is something "emotional" lkn hakuna jinsi ndo mumeo huna budi kuvumilia naamini with time mtazoeana na hatimae utampenda,vema uwe na subra
 
miaka yote huwa nasemaga wanawake huwapenda wale wanaowadanganya danganya ila wale wenye nia ya dhati kama huyo jamaa aliyemuoa ndo wanakuwa hawapendwi,HAPO NDIPO MICHEPUKO INAPOANZIA KWA MWANAUME KUTOKA NJE YA NDOA.
 
hv si umuache km gundu ushatoa
mkato wa chumba ushauona
 
miaka yote huwa nasemaga wanawake huwapenda wale wanaowadanganya danganya ila wale wenye nia ya dhati kama huyo jamaa aliyemuoa ndo wanakuwa hawapendwi,HAPO NDIPO MICHEPUKO INAPOANZIA KWA MWANAUME KUTOKA NJE YA NDOA.
Safi kabisa mkuu umeongea jambo la msingi sana hua najiuliza kwa nini yule anaeonyesha kujali ndio wanamuona hafai ila akija jamaa dont care ndio wanaona hapo wamefika, at the end of the day matatizo kama hayo. wanawake jaribuni kusoma nyoyo za wanaume mpaka ndani sio kwa juu juu tu, pia ushauri wa watu wengine hata wazazi katika suala la mapenzi ni kuwa makini nalo sana, ukishauriwa utaendelea tena kuishi na wazazi? Pokea ushauri kisha upime na ufanye ucnguzi wa kina halafu ndio maamuzi baabdae.
 
Asanteni jamani!sina watoto,ila ndio tunatafuta,

POLE mdogo wangu....tulia tu kama jamaa hakufanyii vimbwanga jaribu ku-cool down na uconcentrate kutengeneza mtoto.....

trust me love takes time maadam umelogundua ilo jiwekee mazingira tu ya kumpenda......compare maumivu ya hao wanaume watatu vs huyu utaona ur in safe side...pls naomba usimuumize mumeo....hakuna cha ajabu san akwenye ndoa.....iyo love ipo kwenye boy n girlfriends mkishaoana mnakua kaka na dada...nimwendo wa kupambania maisha...mi ata sikumbuk siku ya mwisho kumwambia mke wangu nampenda....ni life on normal business.....usiyafanye maisha yako kuwa magumu dada....tulia na wala usichepuke...utampenda sooon nakwambia.......unajua kudeka?ndo ugonjwa wangu.....ebu mdekee kdogo mwambie beby plllz be romantic kdogo jamaniii...uone
 
Haahahaha asante kaka yangu,nashukuru sana!kila leo namwomba Mungu nimpende huyu mume wangu kwakweli
 
Haahahaha asante kaka yangu,nashukuru sana!kila leo namwomba Mungu nimpende huyu mume wangu kwakweli

fanya ivo mtoto mzuri sawa eeh?....usilalamike tena na umshukuru Mungu wenzio wanaumizwa wanaishia kurandaranda kwenye mabaa na makanisa kutwa kusaka ndoa na bado wanachezewa...wanaume wengine usiombe kukutanna nao
 
Asante sana
 
Usilaumu kudumbukia mtoni,laumu kwa nini hujui kuogelea,

jaribu kucheck kila kitu positive toka kwa mumeo, cherish it
 
You can learn to love...daaah ila nuonea huruma sana huyo husband wako.... kuishi na mtu asiyekupenda ni shida sana.
Unaweza kujifunza kupenda kama hujawahi kupenda. Ndo maana hata Wahindi wana arranged marriages ambazo ni lazima binti awe bikr. Tatizo kubwa la kutojifunza ni comparison. Otherwise Love Marriages ni muhimu kwa wale ambao walishapenda.
 
shoga ulikuwa na hamu na ndoa duh! au kuna mtu ulitaka kumkomesha na "hayawi hayawi sasa yamekua ulisema siolewi"....ila wanawake huwa tunajifunza kupenda, pole ndo mmeo huyo jitahidi tu umpende!!!

Niadisie......
 
miaka yote huwa nasemaga wanawake huwapenda wale wanaowadanganya danganya ila wale wenye nia ya dhati kama huyo jamaa aliyemuoa ndo wanakuwa hawapendwi,HAPO NDIPO MICHEPUKO INAPOANZIA KWA MWANAUME KUTOKA NJE YA NDOA.

dah! Umeongea ukweli mtu.
Hawa viumbe bado wanaendelea kudhihirisha kuwa wao ni waajabu.
Karibu wanawake wote wanapenda sana wanaowadanganya. Ila ukitaka kuwasikia redion na kuwasoma kwenye magazeti ww uwe mkweli kwao humpat hata mmoja.....
 
Back
Top Bottom