No one to blame ila mimi mwenyewe

tracy360

Member
Nov 24, 2014
27
12
Habari humu ndani, mimi ni mgeni humu ndani na ndio napost topic kwa mara ya kwanza, mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 24 sasa lengo la kuandika hii poat nimehisi nikiitoa moyoni nitakua kama nimetua mzigo fulani.

Katika maisha yangu nimekuwa na wanaume watatu ambao wa kwanza nilikua nae A-level nilimpenda sana unfortunately akaniacha na sababu ilikuwa amerudiana na ex wake.

Nilipofika form six nikapata mwingine nae tulipendana sana,ila tuu nilimvumilia sana nikashindwa kwasababu alikuwa ananicheat sana na kilichonikera sana ni kwamba wanawake ananicheat nao walikua wakinicall kunitukana!na mimi sipendi gombana na mdada kisa mwanaume, nikasema sio kesi ngoja niachane nae japo niliumia sana yaani.

Nilipoanza chuo 2009 nikampata mtu tena ila yeye alikuwa mbali na mimi yeye alikuwa anasoma Iringa na mimi Dar, basi huyo tulikaa miaka mitatu yaani mpaka namaliza chuo bado nipo nae, tatizo likawa alikuwa ananitesa sana yaani, aliniahidi kunioa na aliniambia nimwambie mama yangu kuwa analeta mahari,baai ilikuwa kila nikikosea tuu kidogo basi anasema mimi sio wife material na hawezi nitolea mahari, basi mimi na mbembelezwa na ukizingatia nilisha mwambia mama, mjomba wangu alinikataza sana kuhusu huyu mtu lakini nikawa sisikii.

Alitaka niachisha chuo kwa promise ya kunipeleka nje kusoma na hio mahari amehairisha karibu mara tatu, alinipa ujauzito na kwa upande wangu nilifurahi sana, ila yeye alinambia nitoe coz nilikuwa nalalamika tumbo kuuma so akasema nitoe,na akanipa namba ya document wake na huyo daktari alisema nitoe, ila kumbe alikuwa na girl mwingine ambae nae alikuwa mjamzito ndio maana alinisisitizia nitoe, mwaka jana mwezi wa nne nikaachana nae na ulikuwa ni uamuzi mgumu nilioufanya maana niligundua hata jina alinidanganya.

Basi zile stress yaani nikawa eager kuolewa nikiangalia home atleast mimi ndio nimesoma na nina kazi, mama yangu ananiangalia mimi na nilishamwambia natolewa mahari kwahiyo nilichanganyikiwa sana, sasa wiki moja baada ya kuachana na huyo wa tatu kuna rafiki yangu akaniambia ana kaka yake anahitaji mke maana kwao wamekataa wanawake aliowapeleka kwasababu ya kabila,kwahiyo kabila langu hawatalikataa, yaani nilisita sana, ila akanisisitizia basi nikamwambia nataka kuonana nae, tukaonana na baadae niliporudi home akaniambia nimekupenda na mimi nikamjibu nimekupenda(wakati deep down wala sikumpenda na hio ndio first mistake),tumekaa miezi miwili anaulizia ndoa mara akanipeleka kwao,mimi najipa moyo kua ntampenda tuu,haya mara mahari, mara ndoa.

Hapa sasa najilaumu kuchukua maamuzi ya haraka sana kuolewa maana nashindwa kumpenda kabisa kabisa yaani sio kwamba namchukia hapana, ila no love and affection yaani hata sijui nifanyaje nateseka sana na kiukweli moyo wangu umeganda siwezi kumpenda mtu yoyote kabisa yaan!nipo ndoa am totally not happy yaani akienda job nawish asiwahi kurudi hata unyumba imekua shida.

Sorry kwa story ndefu ila nimeona niandike atleast nitoe kitu moyoni!ushaur tuu tusikimbilie kuolewa mabinti jaman,na tusidanganyane kua utampenda ndoan haipo hio hakuna kitu kizur km inner peace jamani.

Mimi nimejiharibia mwenyewe kwahiyo the rest of my life is being unhappy, sometimes natamani ningekua mzungu kwasababu wao wanaweza kutengua ndoa kama mtu hayupo happy sasa sisi wabongo ni ngumu na nikifanya hivi nitamuumiza mara mia!dah ni hayo tuu jamani.
 
Mwandiko wako umenipa tabu ila nimekuelewa kuanzia unavyohisi sasa mpaka unavyojutia kuchukua uamuzi kama huo,pole sana dada, unajua hakuna kitu kibaya kama kuishi kwa kutegemea kitu amabcho hakipo tena hata picha yake huioni wala haiji akilini
 
Yaan kama ulikuwepo my dear nilotak kumkomeaha huyo mtu mana alinambia hakuna mwanaume atakae nioa!yaan nalia kila siku aisee basi tu
 
shoga ulikuwa na hamu na ndoa duh! au kuna mtu ulitaka kumkomesha na "hayawi hayawi sasa yamekua ulisema siolewi"....ila wanawake huwa tunajifunza kupenda, pole ndo mmeo huyo jitahidi tu umpende!!!
Mhurumie mwenzio wewe Evelyn
 
Yaan kama ulikuwepo my dear nilotak kumkomeaha huyo mtu mana alinambia hakuna mwanaume atakae nioa!yaan nalia kila siku aisee basi tu

Pole sana dada, ila unajua maneno ya watu nayo pia yanaunguza, ukicheki na strees basi ndio dah!!
 
Yaan acha tuu kaka yangu!maisha ninayo ishi yan ni ya tabu sana!naumia sana sana yaan
 
Kumbe haunipendi, kwa nini usiniambie mwenyewe mpaka uje kusemea humu Jf. Nimeumizwa sana, mm nimekuoa halafu unasema unajilazimisha kunipenda, leo hapa hapalaliki ngoja nikupe talaka
 
Kama humpendi mtu humpendi tu, hakuna cha mbele wala katikati.

Unadhani wamkomesha furani kumbe wajikomesha. Pole bidada maji umeyavulia nguo mwenyewe yaoge tu.
 
fungua moyo tu na umpe nafasi moyoni kwako.
Akifanya jambo zuri li-appreciate and jaribu kuweka romantic enviroments kati yenu mfano out goings etc.
Ni mumeo huyo, mkubali Mungu ndio amekupatia.
All the best mamie
 
Hapa kuchepuka hakukwepeki!Kama vp tafuta furaha kwa mchepuko tu ila ukikamatwa utajua mwenyewe irimladi furaha umepewa!
 
Pole sana dia..relationship r harder nwdays..usikate tamaa forget abt yo past na angalia mbele..usiangalie hyo mwingine alikutreat vp hyo kashakua wako wa maisha so jikaze tu..as long as anakuheshim wala.usihof hzo ndo changamoto zenyewe
 
Pole sana.
Kuna mmoja kafahamiana na Mtu mwezi wa tisa, jamaa taperi tu mwezi wa kumi jamaa akamwambia naleta posa. Umakini ni muhimu sana hali ni mbaya sio tu huku hata kule.
 
Dah...hiyo ya kuchoropoa tu ndio fungu langu la kukariri kwenyw habari yako...!!
 
Hivi kwani kuolewa ni lazima sana siku hizi mabinti. Una.miaka 24 hofu ya nini? Matokeo yake utaishi unhappy life hadi uione kaburi. Ndoa si mchezo.
 
Back
Top Bottom