No one to blame ila mimi mwenyewe

Nina maswali kadhaa hapa ambayo yanaambatana na hoja zangu.
1.Wewe ulitaka ndoa au ulitaka kupenda?maana hadithi yako inaonyesha kiu ya moyo wako siyo kupenda ila ni ndoa..
2.Uamuzi wakuolewa ulilazimishwa au ulikubali mwenyewe??maana inaonyesha maamuzi yako yametawaliwa na hasira na visasi kwa lengo lakumuumiza mtu/watu kama ilivyo ada ya wanawake wote dunian..
3.Unajuta kuingia ndani ya ndoa au unajuta kuwa na mahusiano na huyo mtu??maana inaonyesha hapa hoja yako siyo matatizo katika ndoa ila ni matatizo yako yakutokumpenda huyo jamaa kwa sababu ya maumivu uliyopewa hapo nyuma..
Hitimisho lako halina uhusiano na magumu ya kwenye ndoa ila lilitakiwa liwe na hoja yakuonya kutoanzisha mahusiano na mtu usiyempenda,maana story yako inaonyesha uchungu wa mahusiano ila hakuna uchungu wa ndani ya ndoa...hata waafrika wanafunga ndoa za mahakamani siyo wazungu pekee,ndiyo kusema UPENDO wako utaanza kustawi nakuonekana baada ya muda ikiwa utaweka akili yako ndani ya ndoa kuliko kupoteza muda kufikiria yaliyopita ambayo hayawezi badilika...
 
Mwanamke huwa anafikiria vitu vichache sana, vingine vilivyobakia huwa anatamani...
 
Watu kwa kupenda matatiizo...

Hivi husikii hata kale ka usemi "kosea yote usikosee kuoa/kuolewa???
 
Pole sana dada, siwezi kukulaumu kwa kuwa tayari umeshafunga pingu za maisha na huyo mtu. Muombe sana Mungu akufanye uwe na mapenzi na huyo mumeo. Jambo lingine wanawake huwa ni wagumu sana kutambua mwanaume mwenye mapenzi ya kweli nae hata ss wanaume n hvo pia inataka moyo na uvumilivu kuweza kumjua vizuri mtu.
 
shoga ulikuwa na hamu na ndoa duh! au kuna mtu ulitaka kumkomesha na "hayawi hayawi sasa yamekua ulisema siolewi"....ila wanawake huwa tunajifunza kupenda, pole ndo mmeo huyo jitahidi tu umpende!!!

point taken ntarudi baadae kumshauri
 
i feel your pain through your thread.
Tatizo letu tunapenda kumfurahisha kila mtu badala ya kujifurahisha wenyewe.
Im my life (i swear this) kama sitapata atakayenifanya moyo wangu upepesuke kwa kumpenda sidhani kama nitaoa na pia nikimpata na akanizingua kwa kweli sidhani kama ntang'ang'ania kuwa nae

I only live once and i want to live my life to the fullest
 
Nlifuatilia ndoa za wahindi....kuanzia hapo naamini You can build love with anyone....ni jinsi tu utavyoutune moyo wako....Moyo ni kama sponji ukilitia kwenye maji machafu ukikamua litatoa maji machafu, ukilitia kwenye maziwa ukikamua litatoa maziwa....

Just fill your heart with love....utampenda tu....
 
Kweli kabisa mkuu umenena mambo ya muhimu sana. Wanawake wengi sana siku hizi wanakimbilia ndoa ili kuwafurahisha ndugu jamaa na marafiki huku wakisaahau kuwa ndoa inajengwa na upendo kati ya mwanaume na mwanamke. Unaweza kukaa na msichana mda kidogo hata miaka 3 kila mara unamsisitiza kuwa utamuoa huku unajiandaa kweli serrious, anakuja mtu leo na kumdanganya atamuoa na kweli anatoa posa na kuoa ndani ya miezi miwili na kumuacha yule waliotoka nae mbali, matokeo yake ni majuto kwa huyo mwanamke.
 
Nlifuatilia ndoa za wahindi....kuanzia hapo naamini You can build love with anyone....ni jinsi tu utavyoutune moyo wako....Moyo ni kama sponji ukilitia kwenye maji machafu ukikamua litatoa maji machafu, ukilitia kwenye maziwa ukikamua litatoa maziwa....

Just fill your heart with love....utampenda tu....

ndo nilichotaka nimshauri mimi
japo we umetumia kiswahili murua
watu hujifunza kupenda na ukapenda kweli
 
Miaka 24 bado ni kabinti kabichi kabisa

Ila maji ukiyavulia nguo shurti uyaoge

Anza kum-accept mwenzio

Mazuri yake yapende na yakufanye umpende

La sivyo utaambulia hao walokudanganya jina............

Kumpa moyo wako na kujenga ndoa yako lipo mikononi mwako
 
Habar humu ndan,mimi ni mgeni humu ndan na ndio napost topic kwa mara ya kwanza,mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 24 sasa,lengo la kuandika hii poat nimehisi nikiitoa moyoni ntakua km nimetua mzigo fulani! Katika maisha yangu nimekua na wanaume watatu ambao wa kwanza nilikua nae A-level nilimpenda sana unfortunately akaniacha na sababu ilikua amerudiana na ex wake! Nilipofika form six nikapata mwingne nae tulipendana sana,ila tuu nilimvumilia sna nikashindwa kwasababu alikua ananicheat sana na kilichonikera sana ni kwamba wanawake ananicheat nao walikua wakinicall kunitukana!na mimi sipend gombana na mdada kisa mwanaume,nikasema sio kesi ngoja niachane nae japo niliumia sana yaan! Nilipoanza chuo 2009 nikampata mtu tena ila yy alikua mbali na mn yeye alikua anasoma iringa na mimi Dar,basi huyo tulikaa miaka mi tatu yaan mpk namaliza chuo bd nipo nae,tatizo likawa alikua ananitesa sana yaan,aliniahd kunioa na aliniambia nimwambie mama yangu kua analeta mahar,baai iliku

mm luckyline siku zote nasema staki kukosea mme wa kunioa bora nikosee nyumba maana nitachepuka. wakaka ninao wakataa munisamee sitaki kuchepuka ndoan so wadada tuwe makin,? poleee
 
Ulishafanya mabaya mengi, umetupa mimba, umetembea na wanaume wengi sasa ulitaka uolewe na malaika?
Shukuru huyo uliyempata maana kwa profile yako usingempata mwanaume wa kukuoa zaidi watakula papuchu na kutokomea.
 
shoga ulikuwa na hamu na ndoa duh! au kuna mtu ulitaka kumkomesha na "hayawi hayawi sasa yamekua ulisema siolewi"....ila wanawake huwa tunajifunza kupenda, pole ndo mmeo huyo jitahidi tu umpende!!!

Well said wanawake huweza kujifunza kupenda. Ukikosa unachokipenda jaribu kukipenda ulichokipata
 
......ningekuwa mie ningesepa, ya nn kukaa kwenye ndoa na wakati huna amani, furaha na upendo kwa mumeo? Napenda the way wazungu wanavyokuwa kwenye mahusiano, kama Im feels mtu anamwambia ukweli na kusepa.
Maisha mafupi haya, kama hupati raha, ya nini kuganda karaha.
 
Namuonea huruma sana huyo aliyekuoa, maana mtu mwenyewe profile yako mbaya then jamaa kakuoa tu sababu ni kabila moja pengine naye hakupendi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom